Superman
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 5,693
- 1,700
Wadau;
Nimekuwa ni kija mara kwa mara hapa kwa watani wa jadi na in particular Nairobi kwa shughuli za kikazi siku za hivi karibuni. Hivyo nina makazi DSM na NRB. Haya ndiyo niliyoyaona na kuyashuhudia:
1. City Centre mji ni msafi sana, bustani za kupendeza na majengo mazuri
2. Ujenzi wa majengo makubwa na ya kuvutia unaendelea sehemu mbali mbali na kwa kasi ya ajabu
3. Kenyatta Airport iko busy sana. wastani wa ndege kuruka au kutua ni kila baada ya dakika 15. Counter za uhamiaji ni nyingi na average unagongewa passport yako si zaidi ya dakika 5.
4. Dereva wa ofisi anapaki gari kwangu na kuacha funguo kwangu, anafika nusu saa kabla ya muda asubuhi na kufanya usafi wa gari mwenyewe. Anaongea kiingereza kizuri tu. Hii ni kwa madereva wote.
5. Daladala (Matatu) hazisimamishi watu. Kama unapenda Lupango au faini au kunyang'anywa leseni jaribu kusimamisha.
6. Fly-Overs si suala la kisiasa. Nimeona baadhi ya sehemu wanazijenga.
7. Ofisini watu wanafanya kazi, hakuna vigenge vya story za Simba na yanga, wala uchaguzi wala bongo fleva wala stories zozote. Ni kazi tu, moto juu moto chini.
8. Vijana wadogo sana wanashikilia position nyingi sana za juu level ya managers na wakurugenzi. Na wanajua wanachofanya inside out.
9. Kuna magari mengi kuliko DSM, lakini kila mahali traffic light zilipo zinafanya kazi, ambako hakuna pana traffic full time yuko kazini na si pembeni. So, que inatembea pamoja na kuwa magari ni mengi.
10. Maji ni mengi sana na hajawahi kukatika wala sijaona mgao na same kwa umeme.
12. Supermarket kubwa ziko kwenye vitongoji vingi.
13. Bei ya nyumba si ghali kama DSM: Mfano ninalipa $ 400 kwa apartment ya 1 bedroom, Dining Room, Sitting Room; Kitechen; Choo na bafu ikiwa full furnished including TV yenye 100 Channels, Internet na Simu. Serviced Apartment.
14. Watu wanaheshimu utawala wa sheria. Siku za hivi karibuni mawaziri walijiuzulu ili kupisha uchunguzi.
15. Wana moyo wa Utaifa kuliko kawaida.
16. Wamachinga wa Barabarani wapo wa kike na wa kiume
17. Huduma zao katika Mahoteli ni nzuri sana na wana uchangamfu wa hali ya juu.
18. Wanaofanya baishara, kazi ni kazi tu, hakuna kuchanganya biashara na mambo mengine.
19. Makampuni ya biashara na huduma yako serious kutoa huduma bora
20. Wako so strict kuhusu miadi au appointments
Hata hivyo, watani wa jadi bado wana kasumba ya ukabila kwa mbali na hata kupenda ukubwa na kujionyesha wao ni nani. Kura ya maoni hivi karibuni juu ya katiba inaonyesha kuwa Wakikuyu ambao ndiyo wengi wana-own land kubwa walipiga kura ya NO where as makabila mengine kura ya YES.
Piga picha kwa hayo machache hapo juu, na toa maoni yako. Kisha changanua nini kitatokea na watanzania itakuwa vipi wakati wa jumuiya ya Afrika mashariki watakapounganisha Nchi.
QED