Kwa wataalamu wa Afya: Naomba majibu ya maswali haya kuhusu virusi vya corona

Butiyangu

Senior Member
May 19, 2018
123
167
Kwa wale wataalam wa afya, nina maswali naomba nipatiwe majibu.

1. Je, ni kweli wanapopima virusi vya Covid-19 huwa wanachukua damu?

2. Kama jibu ni ndio, kwa hiyo hawa virusi wapo kwenye damu?

3. Kama wapo kwenye damu, wanawezaje kufa kwa kujifukiza mvuke?

4. Kipi kinacho wasabisha waishi kwa muda mrefu? Chakula chao ni nini?

5. Je, hawa virusi wanaosababisha mafua ya kawaida ni aina gani ya virusi? Wanatofauti gani na hawa?
 
Butiyangu, 1. Hawachukui sample ya damu. Sample inayotumika ni mate/ute kutoka kooni au ndani ya pua.

2. Hapana. Mara nyingi virusi wanaoshambulia njia ya hewa huwa hawaambukizi na wala hawafiki kwenye damu.. Ni kirusi mpya na research bado zinaendelea.

3. Kujifukiza ni njia ya asili tuu. Haijathibitishwa kisayansi kama ni kweli inatibu ama laa. Jifukize at your own risk.

4. Virusi hawali. Wanachofanya wakiingia kwenye mwili wanautumia kuzaliana kwa wingi. Kuzaliana huko ndiko kunafanya mwili upate reactions na hatimaye unajisikia kuumwa.

5. Wanaitwa Influenza virus au kwa jina maarufu "the flu". Wapo aina A,B,C,D. Aina D huwa hawaambukizi binadamu.

Unforgetable

Manners Maketh Man
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom