Kwa Wataalam wa magari

Yale yale mambo ya shule za msingi kuwa kilo 1 ya mawe na kilo 1 ya manyoya ya kuku ipi nzito? Ukimwuliza mtoto atasema kilo 1 ya mawe ni nzito kuliko kilo 1 ya manyoya (which makes sense kwa mtoto ingawa si kweli). 80km/hr ya starlet na 80km/hr ya basi na 80 km/hr ya ndege ziko sawa kabisa. Si kweli kuwa starlet ikiwa kwenye 80km/hr itapitwa na bus iliyo katika mwendo huohuo unless kuwa na uchakachuaji kwenye speedometer. Yaani isome ndivyo sivyo
 
hapa pointi sio turbo..pointi hapa ni speed....ukisikia 80km/h ina maanisha umbali wa 80km utakua covered within 1 hour, hiyo staplet iliokua ina soma 100km/h ikapitwa na basi ambalo lina 80km/h sikweli, either speed mita ya staplet ilikua mbovu au ya basi ndiombovu...other wise hakuna standard maalum, kwasababu ukisikia upepo ulikua na speed 80km/h basi ujue upepo huo ulikua na uwezo wa kufika umbali wa 80km ndani ya lisaa limoja...upepo hauna tairi kubwa wala ndogo wala turbo...au la wanasayansi niwaongo kutuambia maswaala ya standards...
 
Ukitaka kujua mabasi yanaenda speed kiasi gani jaribu kwenda nalo sambamba siku moja katika highway za mikoani ukiwa na gari ndogo...
 
iyo experiment umeifanya vipi? under what conditions? ...
There is no such a thing as a speed of 80km/hr could be faster than a speed of 100km/hr...whatever the types of vehicles you can talk about.
 
Napata picha ni jinsi gani lile swali la darasa la tatu/ nne lilivyowasumbua baadhi yenu humu. Kilo kumi za pamba na kilo kumi za mawe zipi nzito? hahaha ahahaha ahahah! with our subject in question kilo 10 za pamba na kilo nane za mawe zipi nzito????????? And am wondering the discusion still goes on and on!!!!!!
 
YES nyambala science haina majibu mawili kwa swali moja labda siasa tu!!!!!!!!!!!! bunge limefungwa.
 
Hivi mwenye Starlet akiwa speed 100km/hr anapitwa kama amesimama na mwenye Prado?
 
Tafakarini vizuri haya mambo iwe tairi kubwa au ndogo chassis sijui ikoje unit per hour ndio inakutanisha gari kubwa na dogo kitakacho tokea hapo ni kwamba tairi za starlet zitagharimika kuzunguka mara nyingi ukilinganisha na basi ila kama zote zinasoma 80km/hrs basi zitakua sambamba isipokuwa tairi za basi zitakua na mizunguko michache zaidi. Ila zipo gari pia zina speedometer ya mile/hr sasa kwa hizo gari mile ni kubwa kwa km . Na 80mile/hrs haiwezi kulingana na 80km/hr

Kweli mkuu, kwenye bold hapo...
1mile=1.6km
 
Wakuu,

Haya ni sawa na kuchukua machungwa kuyafananisha na ndimu!!! Definitely ladha ni tofauti; misingi ya kushindanisha inahitaji uwe na washindani wawili wenye vigezo sawa.

Hatuwezi kukaa na kubishana kushindanisha Toyota Starlet na Scania. Haya ni magari mawili tofauti!!!
Engine ya starlet ni less than 1200cc wakati ya scania ni zaidi ya 5000cc; starlet inatumia petrol na scania dielsel. Hizi ni injini tofauti sana!!! Wachilia mbali chassis zake, matairi, distance covered in a meter, performernces zake, power produced kwa kila combustion, transimission performances etc.

Vipimo vya speed vinabaki kuwa sawa tu!! Ila huwezi kuzishindanisha hizi gari mbili kamwe!!!
 
Unanikumbusha swali la kilo moja ya pamba na kilo moja ya sukari - ipi nzito zaidi.

Mwendo kasi wa 80km/h ni mdogo kuliko ule wa 100km/h daima dumu. Tatizo bila shaka ni kwenye usahihi wa vipimio mwendo kasi katika magari uliyoyaona.
 
Ukitaka kujua mabasi yanaenda speed kiasi gani jaribu kwenda nalo sambamba siku moja katika highway za mikoani ukiwa na gari ndogo...

Lets be scientific, kinachofanya kitu kiwe kasi ni speed(mwendokasi) yake na speed=distance/time sasa kama unaweza leta uhusiano wa distance na uzito au ukubwa wa gari au tairi ndio nitakubali kuwa basi linakuwa na advantage. Speed haina uhusiano wowote na ukubwa wa gari. Kama callibration ya magari yote ni sawa wakiwa na spidi sawa lazima watakaa stationary with repect to each other ,hakuna kupitana. Tatizo hasa Tanzania mabasi mengi yamechakachuliwa speedometer zake au yanamaliza speed zote za kwenye meter na kukopa zaidi.

Halafu gari zenye kasi zaidi duniani ni gari ndogo , angalia mfano gari za fomular one na sio mabasi au malori. Kama mabasi au malori yangekuwa yana uwezo wa kwenda kasi zaidi basi tungekuwa tumeshaelezwa zamani au kungekuwa na fomula one ya mabasi ambayo ingekuwa maarufu zaidi ya sasa.

Halafu wewe umesema eti uende sambamba na basi uone yalivyo na speed. Hiyo haiwezi kukupa picha yeyote mpaka ujue kwa uhakika linakimbia kiasi gani na wewe unakimbia kiasi gani . Njia pekee ya kujua speed yako ya uhakika ni kutumia GPS kama alivyosema mtu mmoja hapo juu. Kama mwenye basi atakuwa na GPS na wewe ukawa na GPS mkakubaliana kuenda 100Km/hr na akakuacha hapo sasa itakuwa issue ya kukabili air resistance kutokana na umbo au uzito ndio vitaipa gari moja advantage na wala si vinginevyo. Callibration ya speed inapofanywa inakuwa imeshatilia maanani kila kitu hata ukubwa wa matairi. Gari ndogo inapokuwa katika 100km/hr matairi yake yakuwa yanazunguka kwa kasi zaidi ya gari kubwa kwenye speed hiyo hiyo ya 100km/hr (hii inaitwa angular velocity, V=rw, v=velocity, r=radius,w=angular velocity)
. Kwa hiyo usidhanie kuwa tairi za gari kubwa zitakuwa zinazunguka sawasawa na tairi za gari ndogo katika speed moja.

Sehemu nzuri amabayo unaweza pima haya mambo ni kama kwenye highway za USA ukiwa kwenye cruise control ukaweka maximum speed allowed huwezi ona malori au mabasi au gari yeyote yanakupita ovyo kwani na wao wanakuwa speed hiyohiyo na uchakachuaji hakuna kwani huwa wanaogopa tiketi.
 
Wakuu,

Haya ni sawa na kuchukua machungwa kuyafananisha na ndimu!!! Definitely ladha ni tofauti; misingi ya kushindanisha inahitaji uwe na washindani wawili wenye vigezo sawa.

Hatuwezi kukaa na kubishana kushindanisha Toyota Starlet na Scania. Haya ni magari mawili tofauti!!!
Engine ya starlet ni less than 1200cc wakati ya scania ni zaidi ya 5000cc; starlet inatumia petrol na scania dielsel. Hizi ni injini tofauti sana!!! Wachilia mbali chassis zake, matairi, distance covered in a meter, performernces zake, power produced kwa kila combustion, transimission performances etc.

Vipimo vya speed vinabaki kuwa sawa tu!! Ila huwezi kuzishindanisha hizi gari mbili kamwe!!!

Mkuu baada ya hayo yote,,nakuja kwenye swali langu kwanin speed zitofautiane?
kwanini wasinge equate tu,,kumbuka mi siongelei kushindanisha hayo magari,bali naungelea outcome.

Ka ishu hapa ni cc, kunamagari ya ujenzi na migodi yana cc kubwa lakini hayana speed.

Pikipiki ya cc 2600 mfano nadhani inaweza kuipita hiyo scania yako ya cc 5000.

Kwa hiyo usiongelee cc wala matairi, ama la sivyo matrekta nayo yangekua na speed.

Weka ceteris peribus mkuu.
 
Tuchukulie hakuna uchakachuaji katika speedomiter,, kiukweli gari ndogo huwa inapitwa tu hata kama tofauti ni ndogo, mfano moja kubwa speed 120 afu dogo likiwa 125km/h.
 
Hii ni physics
unaweza kusoma soma mambo ya Acceleration na Momentum na Force

  • Gari yenye uzito mdogo ina accelerate/de celerate upesi kuliko gari yenye uzito mkubwa
  • Lakini gari yenye uzito mkubwa haipotezi momentum kirahisi sababu ya uzito uliyonayo kama gari ndogo

So at the same speed gari ndogo inaweza kutangulia gari kubwa but ile gari klubwa iki gain momentum then theoretically mwedo kasi wa gari zote utakuwa sawa
 
Ivi inakuaje spidi ya gari mfano starlet ikiwa kwenye 100km/h inapitwa na basi kubwa ambalo lipo 80km/h.

Kama ishu ni gear box revolution,,sasa speed ipi ndo correct?

kaka jambazi , could you take time to read bellow literature as quoted from Average vs. Instantaneous Speed

Average vs. Instantaneous Speed

During a typical trip to school, your car will undergo a series of changes in its speed. If you were to inspect the speedometer readings at regular intervals, you would notice that it changes often. The speedometer of a car reveals information about the instantaneous speed of your car. It shows your speed at a particular instant in time.

trip.gif

The instantaneous speed of an object is not to be confused with the average speed. Average speed is a measure of the distance traveled in a given period of time; it is sometimes referred to as the distance per time ratio. Suppose that during your trip to school, you traveled a distance of 5 miles and the trip lasted 0.2 hours (12 minutes). The average speed of your car could be determined as
trip1.gif

On the average, your car was moving with a speed of 25 miles per hour. During your trip, there may have been times that you were stopped and other times that your speedometer was reading 50 miles per hour. Yet, on average, you were moving with a speed of 25 miles per hour.

it should be known that the car /truck gets its energy from the engine through the gearbox. so the engine size have great influence on the instantaneous velosity as follows.: 1. the higher the engine size the larger the calories transfered to the traansmission system
2. the larger the quantity of energy involved in transmission, the longer the period the car can do at one transmission level -eventually one can drive longer before changing from one transmission level to another , indee this gives stabilised higher instantaneous speed.

based on the above explanation, one may agree that instantaneous speed of a car with1800cc varies greately with a 7000cc engine
 
Do u agree that 10Kg of stone is heavier than 20kg of wool?????????????? Think...................
 
Hii ni physics
unaweza kusoma soma mambo ya Acceleration na Momentum na Force

  • Gari yenye uzito mdogo ina accelerate/de celerate upesi kuliko gari yenye uzito mkubwa
  • Lakini gari yenye uzito mkubwa haipotezi momentum kirahisi sababu ya uzito uliyonayo kama gari ndogo

So at the same speed gari ndogo inaweza kutangulia gari kubwa but ile gari klubwa iki gain momentum then theoretically mwedo kasi wa gari zote utakuwa sawa
Momentum haihusiki na gari kubwa kuipita gari ndogo ila momentum utaiona kazi yake kwenye kuondoka na kusimama, hasa ule umbali wa kusimama ambapo gari kubwa litahitaji umbali mrefu zaidi kusimama kuliko dogo. Tunachosema hapa ni kama yakiwa kwenye barabara isiyo na vikwazo yakiwa yaongozana then muulizaji anasema gari kubwa linalipita dogo kitu ambacho nimekielezea kwa undani hapo juu kuwa kinawezekana tuu kwa sababu ya air resistance.
 
Kwa kweli watu wengine waendelee kuchangia siasa tu kwa kuwa huko huongo na ukweli havina tofauti ili mradi ujue tu kupaza sauti. Tukiwa kwenye sayansi ukweli unabaki kuwa ukweli na uongo unabaki kuwa uongo. Kwangu mimi hii mada ni ya aina yake na majibu yamedhihirisha hali hiyo
 
Momentum haihusiki na gari kubwa kuipita gari ndogo ila momentum utaiona kazi yake kwenye kuondoka na kusimama, hasa ule umbali wa kusimama ambapo gari kubwa litahitaji umbali mrefu zaidi kusimama kuliko dogo. Tunachosema hapa ni kama yakiwa kwenye barabara isiyo na vikwazo yakiwa yaongozana then muulizaji anasema gari kubwa linalipita dogo kitu ambacho nimekielezea kwa undani hapo juu kuwa kinawezekana tuu kwa sababu ya air resistance.

malezo unayotoa ni sahihi kabisa ila ukinisoma nilichoandika mwanzao mpaka mwisho nadhani Au nielimishe ni statement gani niliyonadika ambayo si sahihi.
 
Back
Top Bottom