Kwa wataalam wa Afya: Mwenzi mmoja kukutwa na UKIMWI na mwingine kutokuwa nao naomba ufafanuzi

mkumbwa junior

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
493
1,000
Kuna Rafiki yangu amegombana hadi kafikia kumpa talaka mkewe kisa tu ana maambukizi ya VVU.

Ilivokuwa:

Rafiki yangu ananisimulia kuwa mke wake wakati ana Mimba aligundulika ana VVU mimba ilipokuwa na miezi saba ila yeye alipimwa hana, walirudia kupima sehemu tofauti na ile majibu yakaja vile vile, jamaa akasubiri mtoto amezaliwa amefanana kila kitu na huyo rafiki yangu na kwa bahati mbaya mtoto nae alipata maambukizi.

Mke anaapa hadi kwa kuruka msahafu hajawah chepuka hajui kapataje Ukimwi, mume hataki kashindwa kuelewa akamtimua.

Hichi kisa kikanirudisha miaka kama 20 nyuma wakati tunaishi Moshi kuna bwana mmoja mke wake na watoto wake wawili walikufa kwa gonjwa la UKIMWI ajabu yeye hakuwa nao, akaoa mwingine nae vile vile akapata maambukizi akafa jamaa akaenda hadi KCMC kupimwa hana, 2007 alioa tenaa mambo yakawa yale yale bahati ikawa ni kuwa teknolojia imekuwa mtoto hakuwa na maambukizi ila mke aliathirika, yule jaama hadi leo yupo na hajawahi kukutwa na mambikizi ya VVU.

NAOMBA KUJUA HILI LINAWEZEKANAJE KITAALAMU? NA JE MTU WA HIVO INAWEZA MCHUKUA MUDA GANI HADI APATE MADHARA AU AGUNDULIKE ANA VVU?
 

Goddess

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
7,365
2,000
Jamaaa ni carrier
Haviwezi mdhuru yeye ila anauwezo wa kuambukiza kama kawaida
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom