Kwa Wasomi na Wahenga Afrika: Je, ni kweli mizimu ya kiafrika ni dhaifu na duni mbele ya wazungu? Kwanini mizimu yetu haikututetea walipotutawala?

Blueface

Member
May 2, 2020
46
47
Kuna baadhi ya mambo nikiyafikiria nakosa majibu.Kabla ya wakoloni wa kizungu na kiarabu kuja Afrika tulikua na mpaka leo tunayo mizimu yetu. Waafrika tangu wakiwa wadogo walifundishwa kuiheshimu mizimu. Mtu yoyote aliyeenda kinyume na mafundisho hayo aliadhibiwa vikali ikiwa ni pamoja na adhabu ya kuuliwa kama kosa ni kubwa.Mizimu ilikuwa na nguvu sana kiasi cha kuiamrisha nvua kunyesha hata kama sio majira ya nvua.Pamoja na hili,

Afrika pia kulikua na waganga hodari waliotisha kwa nguvu zao.Walikua na uwezo wa kuamrisha radi, mamba au hata simba kwenda kumdhuru mtu muovu hapo kijijini.Jambo la ajabu, wazungu walipokuja walituteka, kutudhalilisha, wakiua waafrika wenzetu kwa vifo vya kikatili kwa kuwapiga risasi au kuwanyonga. Tena kwa dharau waliwanyongea kwenye miti ileile waliyokua wakitambikia mizimu yao. Sasa nauliza; Wakati wazungu wanafanya hizi dharau mizimu na hao waganga walikua wapi?Hivi mtu akisema waafrika na mizimu yao hawana akili atakua amekosea?

Fikiria mtu kama Mwanamalundi aliyekua anaogopwa kwa miujiza yake kule usukumani akiweza kukausha msitu mbichi na kuugeuza kua kuni lakini alishindwa kuua hata mzungu mmoja?Mwanamalundi alishindwaje kuwakomboa wasukuma akawaacha wananyongwa kwa dharau chini ya mti mkubwa wa matambiko pale mwanza ilipo round about ya kwenda Airport?

Hii mizimu alishindwaje kuua hata muarabu au mzungu mmoja lakini ikaua mamia ya waafrika waliokosea masharti? Tafadhalini wahenga na wasomi majibu yenu yanahitajika.Wale wa PhD na masters fanyeni utafiti hili eneo majibu yanatakiwa.!
 
Hata zile dawa za mvuto wa mapenzi zinafanya kazi kwa watu weusi tuu lakin kwa mzungu hazipandi
Whites are not human they are hybrid of demons and human
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom