Kwa wasiojua kupika wali, watoa bokoboko hii ni njia rahisi kwao

Njia nayotumia kupika wali
1. Naandaa maji Mara 2 ya mchele. Kama mchele ni kikombe kimoja maji naweka viwili
2. Nachemsha maji, yakichemka naweka chumvi hadi iyeyuke.
3. Naweka mafuta nakoroga vizuri ili mafuta yasishikane.
4. Naweka mchele ila sifuniki sufuria. Nahakikisha kiasi cha moto sio kikubwa. Maji yakianza kukaukia nafunika sufuria hadi wali uive.
Uwezekano wa kupata wali mzuri ni 60%
 
Binafsi sipendagi wali wa kuchambuka sana na mlevi,
nauona kama haujaiva vile,
Pia naona kama mchele wa VIP au kitumbo
Hata upikeje haukai sawa,
Napenda wali wa kuinama ,

I mean sipendagi wali wa kuchambuka chambuka sana na mkavu!
Naonaga kama haujaiva vizuri vile,

Unakuwa kama wali utokanao na Mchele wa kitumbo au VIP,

Mimi napendaga wali wa kuinama.
 
Dah...njia ndefu Sana kwa Karne hii... kirahisi kabisa...Osha mchele...weka ndani ya rice cooker...weka mafuta na chumvi kwa kipimo....nenda bas ya jirani...ukirudi wali tayari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom