kwa wasio na ajira walio Dar es salaam inatuhusu.

Blessed

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
3,663
2,000
ajira ni haba sana mjini.nimekuwa na wazo kama tukijikusanya watu 100 na kutengeneza kitu kama ushirika/shirikisho/company kwa mchanganuo ufuatao.pamoja na ugumu wa ajira;tunaweza kupata 25,000tsh kila mwezi inaleta 2,500,000 kwa mwezi. miezi mitatu 7,500,000. na kuanza biashara yoyote kwa manufaa yetu.lengo hapa ni kujenga mtandao wa kukusanya raslimali zetu.si deci ni shirika kwa mtindo huo.tunatafuta watu 100 tu.tutaunda comapany kwa kufuata companies Act,tutakuwa na Memoranduma of Association na article of association ,ndo vitaongoza daily routine ya company,refer mchanganuo hapa chini.
kila member atakuwa anachangia 25,000/= kwa mwezi kusudi tupate mtaji.
100 members @ 25,000/= 2,500,000/=mwezi mmoja
miezi 3 7,500,000/=capital ya kuanzia biashara
miezi 6 15,000,000/=
miezi 9 22,500,000/=
miezi 12 30,000,000/=
mwaka 1 30,000,000/=
miaka 3 90,000,000/
miaka 5 150,000,000/=
miaka 10 300,000,000/=
miaka 20 600,000,000/=

tarehe za kuzingatia
28th/12/12 kufunga zoezi la usajili
7th/01/13 kikao cha kwanza
interested people watume private message(PM)wapewe namba ya usajili,na wenyue maswali pia,tunakusanya rasilinmali zetu kupata mtaji wa biashara,

www.daryouthinitiative.wordpress.com
 

DALA

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
1,266
2,000
Good idea! Count me in! Its better to take action than to talk! Hata tukiwa wawili
 

kisoda

Senior Member
Dec 4, 2012
168
0
ajira ni haba sana mjini.nimekuwa na wazo kama tukijikusanya watu 100 na kutengeneza kitu kama ushirika/shirikisho kwa mchanganuo ufuatao.pamoja na ugumu wa ajira tunaweza kupata 25,000tsh inaleta 2,500,000 kwa mwezi mmoja,baada ya miezi mitatu tunapata 7,500,000 na kuanza biashara yoyote kwa manufaa yetu.lango hapa ni kujenga mtandao wa kukusanya raslimali zetu.si deci ni shirika kwa mtindo huo.tunatafuta watu 100 tu.tutaunda muongozo utaotuongoza hadi 31 dec.tuwe watu 100 tayr tukutane physically.
wazo zuri!,nachangia wazo la biashara,kuanzisha bookshops tz nzima na kupiga kampeni tz nzima watz waache uvivu wa kujisomea!inawezekana,mbn kila baada ya nyumba kuna bar?tunaweza anza kwa faida yetu na kizazi kijacho!
 

aloycev

Member
Aug 6, 2011
22
0
Watu 100 ni wengi sana, lazima kutatokea kutofautiana kwa kiasi kikubwa, ni hulka ya mwanadamu
 

hekimatele

JF-Expert Member
May 31, 2011
9,891
2,000
Gilo una wazo zuri sanaaaaaa.
However, ningekusihi wewe na timu yako kabla hata ya kuchanga hizo pesa mnaweza ku brainstorm na kujua ni biashara gani 'exactly' mnayotaka ku venture into to be specific rather than being excited with the idea. Mkipata jibu la hilo swali mtengeneze a simple structured business plan itakayowaongoza ili msije jikuta mnaenda kiholela holela. I know few people ambao ni matajiri wakubwa sasa hivi duniani ambao walianza na idea kama hii ya kwako lakini walijitengenezea muongozo ambao waliufata na kuuheshimu collectively.
Swali langu la msingi ni je, hao wanachama wengine wataweza kuwa na uwezo wa kuchangia hicho kiwango kwa kila mwezi?
Kingine msijifungie sana kwa ambao hamna kazi. Wapo watu wengine ambao wako makazini na wanaweza kujiunga na kuchangia kwa kiasi kikubwa ukiacha tu pesa hata professional consultancy. Wafungulieni mlango na m-sail pamoja.
It will be worth a try and efforts.
 

Kitanga

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
361
250
Juzi Waziri Mkuu aliyejiuzulu alikuwa katika harambee kuko Akheri- Meru. Aliambatana na mtoto wa Sumari (Sioi). Kwa matambo alisema kijana huyo anatekeleza ahadi za baba yake akitolea mfano ukosefu za ajira kwa vijana. Swali ni je, kanisani ni mahala pa kampeni? Na toka lini tukaanza kujenga tabia ya kurithishaan vyeo vya kisiasa? Suala lilikuwa harambee kwa ajili ya ujenzi wa kanisa lakini ndani yake kumekuwa ni kunadi mtu ambaye alishindwa uchaguzi dogo wa ARUMERU MASHARIKI! Na katika suala la AJIRA , waziri huyu huwa hatoi jawabu ili ni mafumbo, atatoa jawabu ni nani?
 

Executivesister

JF-Expert Member
Aug 7, 2012
494
1,000
Watu 100 ni wengi sana, lazima kutatokea kutofautiana kwa kiasi kikubwa, ni hulka ya mwanadamu
Mbona umekuwa negative thinker sana,kwa nini usiwaze kwanza mafanikio alafu kutofautiana kuwe kama challenge,me naona ni wazo zuri hata mie ntajiunga
 

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,122
2,000
Kwa usahauri wangu kweli watu 100 ni wengi sana, kikubwa ni kukusanyana ambao tiyali mnafahamiana tabia na kazalika either mmesoma chuo, pamoja na kazalika, kwa watu 100 huwezi jua tabia za wengine, na return itachukua mda mrefu kiasi kwamba wengi watakata tamaa,

Mnaweza anzisha hata kikundi cha cha kuweka na kukopa GSL groups saving and loan kutoka hapo ndo mnaweza anza kukusanya mitaji ya nyie kufanya biashara, na mara nyingi ni bora mkaanza na kila mtu na muradi wake na then mkisha somana vya kutosha ndo mnafanya mradi wa pamoja, ila kuanza tu na muradi wa pamoja ni ngumu sana, GSL huwa na wanachama kati ya 15- 30 na kikundi hukutana weakely kununua hisa na kila baada ya mwezi hutoa mikopo kwa wanachama wake.

Hivi vikundi ni vizuri sana endapo mtaanza na share ya juu angalau 5000 kwa share moja na kwa wiki limit ni share 5 so ukiweza unaweza nunua share 5 kwa sh 25000 ukishindwa hata 1, 2,3 au 4,

Kwenye mikopo kila mtu hukopa kulingana na kiwango cha share zake na mwanachama hukopa mpaka mara 3 ya thamani ya share zake, so kama unashare za Tsh 500000 unaweza kopa hadi 1500000,

Na kikundi huwa na riba yake na vingi hutoza 5%
 
May 22, 2012
28
20
count on me hapo i need people like u hakuna kuongea bila kuja na wazo mbadala lazima tujue hakuna kazi hilikuja bila mtu kuanzisha lazima kuwepo na haja yakucreate kazi wenyewe
 

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,435
2,000
Approaches ziko mbili,

1) Unapata hela/mtaji ndio unafikiri biashara gani ya kufanya.

2) Unafikiri biashara kwanza kisha ndio unaitafutia mtaji

Wewe umeamua kutumia approach ya kwanza!!

Biashara ya mtaji wa Tshs 7.5Mil inaweza kutoa faida ya kuwatosheleza watu 100 wote??

Alternatively ingeweza kua watu 50 kwa Tshs 50,00/=.
 

Blessed

JF-Expert Member
Nov 16, 2011
3,663
2,000
Approaches ziko mbili,

1) Unapata hela/mtaji ndio unafikiri biashara gani ya kufanya.

2) Unafikiri biashara kwanza kisha ndio unaitafutia mtaji

Wewe umeamua kutumia approach ya kwanza!!

Biashara ya mtaji wa Tshs 7.5Mil inaweza kutoa faida ya kuwatosheleza watu 100 wote??

Alternatively ingeweza kua watu 50 kwa Tshs 50,00/=.


mawazo yako ni mazuri,tunatengeneza entinty(business entinty)ambayo inakuwa loanable/fundable na mashirika kama ILO,UNDP ,etc no other financial institution,ni vigumu kufanya hivyo kwa individuals,lakini tukiwa na hiyo entinty tunapata funds/loans......
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom