Kwa wapenzi wa muziki wa DRC, upi muziki wako pendwa, ambao huuchoki kusikiliza.

Nyingi sana...

  • Ya jean - Madilu System
  • Mamou - Franco Luambo Makiadi
  • Kokola - Tshala Muana
  • Fatimata - Sam Mangwana
  • Nadina - Mbilia Bel
    - Muzina - Tabu ley
 
Gallup ipupa-oloko yo
Koffi olomide-loi
Pepe kale-hidaya
Aurlis Mabele- Everlyne (sijuh kama ni mkongo)
 
Fally Ipupa 1~Canne sucre 2~Maria PM
Tshala Muana ~Karibu yangu
Lady Issa ~ Tama (ni heri kufa masikini kuliko kusimangiwa)
Samba Mapangala ~Dunia Tunapita heee, kila kitu kitabakiya, binadamu ni mchangaaaa! (Huu wimbo japo ni wa zamani nimeufahamu mwaka huu na ninaupenda sana naupiga kila siku, una funzo la msingi sana!)
 
Kaka nikiwa sumbawanga 1980s, Mzee wangu km wako, mfanyakazi serikalini. Alikuwa na collection ya kutosha ya nuimbo za Franco! Aisee zile nyimbo mpaka leo ukisikiliza recording quality yake ni balaa! Kuna nyimbo Kama mbawu na recuperer, peuch del sol, muzi, aisee hizi nyimbo huwa zinaniliza, zinanikumbusha Kaka yangu marehemu(RIP) alikuwa Kaka na rafiki yangu mkubwa, alinifundisha vitu vingi Sana! Alinifundisha kucheza football, dah so painful wadau rest in power brother! .Sasa hizo nyimbo jioni Mzee anaweka sie tupo nje tunacheza chandimu! Life was so good!
Hiyo ni Rumba, kulikuwa na Kavasha akina Nzaya Nzayadio na kibao kinaitwa Na seki zenge, Motoba, my best song kwenye Kavasha ilitoka kwa Orch Kiam Kamiki daaah naupenda Sana huu wimbo.

Mid 80s kulikuwa na akina Mbilia bell, faya Tess, Chicco Chikaya fujo zilianza ilipokuja soukouss akina Pepe kale, Diblo dibala yankomba, late 80s hapa Sasa ndio Moto bin faya! Akina Yondo sister, Shimmita, pappy Tex na ile nyimbo tamu kabisa Kanda ya Nini (chuki ya Nini?) Sakiss! Hapa ilikuwa mauno kwa kwenda mbele! Baadaye ndo wakaja akina Koffi, Wenge bcbg na wengineo! Bana Congo iko talented Sana! Music, soccer wapo mbele yetu ingawa wana Vita kila siku
Wenzetu walifanikiwa sana kwenye suala la muziki,yaaan kama wangelijuwa na mfumo mzuri basi nchi yao ingelikuwa mbali sana
 
CONGO si mchezo,mie napenda instrumental yao ingawa lugha sielewi,bt nakumbuka ukimwi ulisambaa kwa kasi sana kupitia nyimbo za wakongo Man miaka ya 1990's
 
Hayati AURLIS MABELE alikuwa anatokea congo Brazzaville!! Alikuwa fundi sana, zile staili zake za kushitua kama amejikwaa anadondoka chini kuna rafiki yangu hadi leo hana meno mawili ya barazani!!alidondoka mazima!!!
Ahahhahaha kibongo ni kustua kijoti
 
Ferre Golla- Maboko Pamba/100 kilos/primiere classe/pakadjuma/court circuit/kipelekise/regarde moi/azalaki awa remix
Koffi- Micko/Mon Armour/Efrakata/
Fally ipupa-Tokoos2 album/a flye/bircabonet/mawa/libre parcous/kiname/mannequin/tout le monde dance/animation/allo telephone
Extra musica&roga roga/ Moyini mbote/etet major/sissi/elanga

siku inaenda vizuri nikisikiliza vibao hivyo
Hapo Kwa Ferre Gola umesahau
Kamasutra
Vita Imana Remix
 
Koffi Olomide
1. Effevercent (Yuko na Fally Ipupa)
2. Etoile d'Etat (Yuko na Mkewe Cindi)

Meje30
1. Fumbo ya Bakandja
2. Doukou Doukou

Madilu System
1. Frere Eduard
2. Si je savais ca
3. Nzele

Mbilia Bel
1. Beyanga
2. Tikabazuwa
3. Eswiyo wapi

Pepe Kale & Empire Bakuba
1. Moyibi (Yuko na Nyboma Mwandido)
2. Amour Perdu
3. Nina
4. Ibetibi

Franco
1. Masu
2. Azda
3. Mamou
4. Makambo Ezali
5. Mario

Ntarudi baadae kuongeza nyingine nikikumbuka
 
Kwakweli nimekuwa mpenzi wa muziki sana wa DRC na majirani zake, kiasi kwamba kwa umri nilio nao na hasa vijana wenzangu wananishangaa sana na kujiuliza maswali mengi.

Tokea nikiwa mdogo baba yangu MZAZI alikuwa mtumishi wa serikali huko morogoro mvuha, hivyo basi anapokwenda kupokea mshahara hununua kanda na kurudi nazo, hivyo sisi na majirani zetu tunapata burudani na huku kushangaa makava ya TAPE.

Kwako wewe ipi nyimbo bora mbayo unaisikiliza na haichoshi kabisa, mimi kwangu kuna wale WENGE Musica wananyimbo yao moja hivi inaitwa SOLOLA BIE, hii nyimbo kwakweli tokea iachiwe miaka ya 1999 mpaka leo kwangu ndio nyimbo bora kabisa kuwahi kutokea upande wa CONGO.

"" WEWE UNAKUMBUKA, AU IPI CHAGUO LAKO INAPOPIGWA BASI TABASAMU LINARUDI"""
PENALTY ya Mzee wa Fimbu na Fimbu (Felix Wazekwa)
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom