Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

😂😂😂😂aah kumbe nimekukatishia uhondo nikajua ushaimaliza. Naona unaufaidi mzimu wa dokta shin kutwa kukodolea macho warembo. Mzimu unaenda kuogelea swimming pool,mzimu unadowea ice cream
Hahahaha Usiniambie.....mwenzio nimejivuta vuta nisimalize haraka nikujua ikiisha imeishaa kumbee laaah.....Tumepatikana😂😂
 
Duh!, Huyo mzee kumbe ni konki kiasi hicho, ndio maana series zake, zinastori nzuri na hazichoshi.
So Hur Jun na Dae Jang Geum hawa watu walikuwepo historically au mmoja wapo alikuwepo, na huyo wapili ni nyongeza ya Producer?
historia ya uwepo wa heo jun haina tatizo lolote kwa sababu rekodi zote zinakubaliana na uwepo wake, kwa mfano ukisema heo jun hakuwepo tafsiri yake ni kwamba unapingana na uwepo wa kitabu cha tiba kinachotambuliwa na UNESCO alichokiandika mwenyewe kinachoitwa Dongui Bogam kikiwa na maana ya kiengereza Mirror of Eastern Medicine
heo jun alikuwepo nyakati za utawala wa mfalme seonjo (mfalme wa 14 wa Joseon) na chini ya utawala wake ndipo ulipotokezea uvamizi wa Japan (Imjin war).

Annals of the Joseon Dynasty ilifanikiwa kumtaja mara 10 dae jang geum kwa matukio aliohusika nayo, hivyo upo uwezekano naye jang geum alikuwepo kweli japokuwa kuna uhaba wa maandishi yanayomuhusu yeye kuanzia kuzaliwa kwake, mafanikio yake mpaka kifo chake.
rekodi za Annals of the Joseon Dynasty zinaonyesha uwepo wa jang geum chini ya utawala wa mfalme Jungjong (mfalme wa 11 wa Joseon)
 
Yan kuna ka feeling hata ikitajwa vipi unasikia raha kufahamika

Mask singer mmoja alivaa mask ya Serengeti tiger nikasema weuwee
wakorea siku wanayochafukwa utawachukia, wana ujinga wa kuwajumuisha waafrika wote dhidi ya changamoto wanayotaka kuiwasilisha kwa njia ya sanaaa.

"mwanangu unataka kwenda Afrika, kuna majini wakitaka kuvuka barabara mpaka waangalie kushoto na kulia"
masikini kumbe majini wenyewe wanapatikana nchi ya bongo movies pekee.
 
Anaeweza kunisaidia kuipata Sound track ya THE VEIL, inaitwa "Reason" aliyeimba anaitwa Yoari. Nimeitafuta Youtube nimeipata ila sijui namna ya kuidownload, anaeyejua namna ya kuipakua anielekeze.

bila ya impactful soundtrack kwenye drama husika, hiyo project inakuwa utopolo bwanaaa (kwa mtazamo wangu, nikiwa kama muathirika wa soundtrack)....

soundtrack sio tu zinatuletea hisia fulani kwa mujibu wa tukio labda huzuni, furaha, upendo, breakup, lakini baadhi ya nyakati pia huweza kutusaidia kuyakumbuka matukio yaliokwisha pita,

unaweza kuwa umelisahau tukio la drama husika labda ni kwa sababu umeangalia siku nyingi nyuma lakini soundtrack yake kama ipo kwenye kumbukumbu zako inaweza kukuletea miujiza usiyoitegemea kwa kuyakumbuka matukio hayo kana kwamba umewekewa screen mbele yako.

nikiusikiliza huo wimbo hunirudisha mwishoni mwa episode 2, namgoong alipokuwa anafukuzana na wauza madawa ya kulevya baada ya kufanikiwa kumtoa bosi wao kituo cha polisi, kuna mzuka fulani (goosebumps) hujizalisha nakujihisi ndiye mtendaji mkuu wa scene (uraibu ni mbaya sana). :D:D:D
=========================
 
Reflection of You / Person Who Looks Like You drama: episode 1 imenivutia sana licha ya pace yake kuwa ni ndogo, ni aina ya zile drama unazoangalia kwa nusu saa baadae unatafuta kitanda, sports au chakula kilipo. Lengo kuu ni kuitafuta nguvu mpya itakayoshajihisha au kukuhamasisha kuendelea tena kuingalia project husika. Ni drama zinazohitaji uvumilivu kwa sababu ya upungufu wa matukio yatakayokufanya muda wote utamani kuyashuhudia.
Ngoja niisubirie episode 2, kwa masikitiko hii drama sijafanikiwa kuiona kwenye tovuti ya nkiri (imenibidi nirudi dramanice)
====================
Niwakumbushe tu huyu gong hyu jung ana miaka 50, wakorea walivyo na maajabu yanayochangizwa zaidi na matunzo yao ya ngozi pamoja na ulaji wao mwanamke mwenye miaka 50 unaweza kumwita dada (binti), huku kwetu upembani na ungujani mwanamke mwenye miaka 50 anaitwa bibi (kashaozesha mwanawe, keshajukuu).
ngozi imeshakunjana kama chapati ya bifatuma kibuno kwa sababu ya ukosefu wa matunzo ya mwili wake kwa kuanzia na lishe yake (kushiba hashibi, atapata nguvu ya kununua vipodozi), na mwanaume mwenyewe mfano wa daemushin muda wote yupo kibarazani anakunywa supu ya pweza lakini fedha ya kununua lotion kwa mkewe hana.
====================

Gyeoul (shin hyun bin) where are you?
nakuona humu ndani jinsi unavyomtambisha dada mkubwa (mishil), inaonekana kuna mkasa mkubwa sana unaowahusu wawili kati yenu uliotokea miaka ya nyuma.
=====================

Jeong Hui-Ju (Ko Hyun-Jung) had a poor and fierce time during her youthful days. She is now a successful painter and essayist. Her husband is the successor of a hospital and they have two children. Her family life seems enviable, but Jeong Hui-Ju feels like she spends her time meaninglessly. At that time, Jeong Hui-Ju meets a woman. The woman is poor, just like Jeong Hui-Ju in her younger days, but she still shines.
20211013509091.jpg

Anayejua muendelezo wa hizi series anisaidie nilianza kuangalia root of the throne nikapata muendelezo wake kwenye deep tree rooted inayofuata ndiyo nimeshindwa kuijua anayeifahamu anisaidie

Ila pia nahitaji historical korean drama nzuri maana hizi ndiyo nazikubali
kwa uelewa wangu kwa hiyo kesi yako sidhani kama ni sahihi kutumia neno muendelezo (naruhusu masahihisho), nafahamu drama zote mbili zimeandikwa na muandishi mmoja na zimesimamiwa na director mmoja, pia nafahamu baadhi ya characters wanapatikana kwenye hizo drama zote mbili lakini bado haihalalishi kusema project B ni muendelezo wa project A.

ngoja nijaribu kukusaidia hicho ulichokikusudia, unachohitaji wewe ni drama zilizobeba wahusika uliowaona humo ndani kupitia drama ulizozitaja pamoja na muendelezo wa hadithi zao bila ya kujali uhalisia wa maandiko ya hao waandishi.

kuanguka kwa goryeo na kuzaliwa joseon pamoja na mtiririko wa maisha ya taejo (yi seong gye) , taejong (yi bang won) na sambong (jung do jeon)
  1. six flying dragons (root of the throne) drama - umeshawafahamu watu sita waliozungumzwa humo ndani na maisha yao
  2. jung do jeon drama - utamfahamu huyo sambong na maisha yake (mchango wake)
  3. the great seer drama
  4. my country: the new age drama
Maisha ya Taejong baada ya kutawazwa ufalme pamoja na mrithi wake sejong (Yi Do)
  1. the great king sejong drama
  2. tree with deep roots drama
  3. jeong yeong sil drama
  4. Taejong yi bang won drama: tuombe uhai mpaka mwezi December ndipo tutakapoanza kuishuhudia hii drama
ukimaliza hizo dozi ikiwa kama bado unasumbuliwa na uraibu wa Joseon, njoo tena utafute tiba.
 
Asante mamie kwa ile app ulionipa najipakulia manyama ile mbaya nilichogundua ile tatizo la subtitle niliyokueleza ilikuwa ipo kwenye The veil pekee hasa episode ya 4.Hii app kiboko unapata mb ndogo na ina quality kubwa tofauti na ya server ile ya chini kabisa ya kisaasian.Yaani ningekuwa tupo face to face ningekukiss bibie kwa hii zawadi ulionipa mpaka najiuliza nilikuwapi kutoijua hii app basi chukua hiyo na hii
Numbisa
App gani hiyo mkuu na mie naomba connection
 
View attachment 1974675
bila ya impactful soundtrack kwenye drama husika, hiyo project inakuwa utopolo bwanaaa (kwa mtazamo wangu, nikiwa kama muathirika wa soundtrack)....

soundtrack sio tu zinatuletea hisia fulani kwa mujibu wa tukio labda huzuni, furaha, upendo, breakup, lakini baadhi ya nyakati pia huweza kutusaidia kuyakumbuka matukio yaliokwisha pita,

unaweza kuwa umelisahau tukio la drama husika labda ni kwa sababu umeangalia siku nyingi nyuma lakini soundtrack yake kama ipo kwenye kumbukumbu zako inaweza kukuletea miujiza usiyoitegemea kwa kuyakumbuka matukio hayo kana kwamba umewekewa screen mbele yako.

nikiusikiliza huo wimbo hunirudisha mwishoni mwa episode 2, namgoong alipokuwa anafukuzana na wauza madawa ya kulevya baada ya kufanikiwa kumtoa bosi wao kituo cha polisi, kuna mzuka fulani (goosebumps) hujizalisha nakujihisi ndiye mtendaji mkuu wa scene (uraibu ni mbaya sana). :D:D:D
=========================
Mkuu nakushukuru sana kwa kunipandishia hii OST hapa, aiseeh wakorea ni hatari sana linapokuja swala la kuteka hisia za mtazamaji.Hii OST iliendana kwa 100% na tukio la mwishoni mwa episode 2,mwanzo nilifikiri ni kwangu tu ila nimeiona ni wengi sana wamekuwa na mtazamo kama wangu.

Huyu Namkoong Min na Kim ji-eun wamefit sana uhusika wao,jamaa ni underrated ila ana uwezo mkubwa sana.
 
Reflection of You / Person Who Looks Like You drama: episode 1 imenivutia sana licha ya pace yake kuwa ni ndogo, ni aina ya zile drama unazoangalia kwa nusu saa baadae unatafuta kitanda, sports au chakula kilipo. Lengo kuu ni kuitafuta nguvu mpya itakayoshajihisha au kukuhamasisha kuendelea tena kuingalia project husika. Ni drama zinazohitaji uvumilivu kwa sababu ya upungufu wa matukio yatakayokufanya muda wote utamani kuyashuhudia.
Ngoja niisubirie episode 2, kwa masikitiko hii drama sijafanikiwa kuiona kwenye tovuti ya nkiri (imenibidi nirudi dramanice)
====================
Niwakumbushe tu huyu gong hyu jung ana miaka 50, wakorea walivyo na maajabu yanayochangizwa zaidi na matunzo yao ya ngozi pamoja na ulaji wao mwanamke mwenye miaka 50 unaweza kumwita dada (binti), huku kwetu upembani na ungujani mwanamke mwenye miaka 50 anaitwa bibi (kashaozesha mwanawe, keshajukuu).
ngozi imeshakunjana kama chapati ya bifatuma kibuno kwa sababu ya ukosefu wa matunzo ya mwili wake kwa kuanzia na lishe yake (kushiba hashibi, atapata nguvu ya kununua vipodozi), na mwanaume mwenyewe mfano wa daemushin muda wote yupo kibarazani anakunywa supu ya pweza lakini fedha ya kununua lotion kwa mkewe hana.
====================

Gyeoul (shin hyun bin) where are you?
nakuona humu ndani jinsi unavyomtambisha dada mkubwa (mishil), inaonekana kuna mkasa mkubwa sana unaowahusu wawili kati yenu uliotokea miaka ya nyuma.
=====================

Jeong Hui-Ju (Ko Hyun-Jung) had a poor and fierce time during her youthful days. She is now a successful painter and essayist. Her husband is the successor of a hospital and they have two children. Her family life seems enviable, but Jeong Hui-Ju feels like she spends her time meaninglessly. At that time, Jeong Hui-Ju meets a woman. The woman is poor, just like Jeong Hui-Ju in her younger days, but she still shines.
20211013509091.jpg

Hivi wanafanya nini Ili kuendelea kuwa na muonekano wa vijana ilhali ni wazee? Na hili sio tu kwa wadada,nimeliona hata kwa wanaume. Utakuta mtu anapewa role ya usichana (na ni kweli anaonekana mdogo) ila ukifatila unakuta ana miaka 28-35 wakati huku kwetu watu wenye umri huo ni ma-mama kabisa.

Jang Yang-Nam ni moja Kati ya wadada nilishangaa kujua kwamba amezaliwa 1973.Kwa korea, ukimuona mtu amekuwa na muonekano wa kizee kabisa usiojificha basi ujue amekula age sana miaka 70-onwards.

Namkoong Min, ni mtu wa 1978 ila ukimcheki ni sawa na watoto wa 1991 huku.
 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom