Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Akina nani aliwatupa? Mimi najua alimtelekeza Bidam
Bidam huyu apa kwenye the pirates vs bandit,naitafuta Sana wadau,jamaa ni noma
qYvO2c.jpeg
 
Mpo wapendwa katika Tasnia!!!

Baada ya mapumziko ya muda mrefu nadhani ni muda muafaka wa kurejesha ari na nguvu bila kusahau kasi ya ule upepo maarufu ili kufuatilia Projects mbalimbali za Kikorea hususani zinazoendelea.

Miaka ya zamani huko siku za nyuma, enzi hizo karne na karne, robo milenia, nusu milenia ama milenia nzima, enzi za mababu bila kusahau mabibi waliwahi kusema;

"Nyota njema huonekana asubuhi."

Ukijaribu kuutumia msemo huu hususani kupitia hizi Drama zetu pendwa pale ambapo unakutana na Project yenye Episodes mathalani 60 na kuendelea alafu unajaribu kuusoma mchezo kupitia Episodes chache za kwanza ama niziite "Episodes za asubuhi" ili zikupe hamasa au ari ya kuitazama Project nzima mpaka mwisho.

Hilo laweza kuwa jambo la kawaida kabisa kwa watazamaji wengi hasa pale ambapo soko likiwa limetawaliwa na 'utitiri' wa Drama ambazo kila mtazamaji angependa kuutumia muda wake kutazama kazi zilizo na ubora wa hali ya juu katika viwango vya kimataifa.

Lakini je, kuna ukweli wowote kuwa Episodes za mwanzo mwanzo au mwanzoni huwa ni kielelezo tosha kuwa Project nzima ni nzuri ama la?
 
Hivi? cheo cha Mishil( Seju) kilikuwa kipi Haswa. ( Queen SeonDeok Drama).
Kuhusiana na huyo 'Mishil' kumekuwa na kautata fulani ambapo maswali mengi yameibuliwa na Wanahistoria kwamba kweli ali-Exist ama la.

Sababu mojawapo ni kukosekana kwa jina hilo kutamkwa katika nyaraka muhimu za kihistoria za 'Falme Tatu' za Korea, hapa nazungumzia Samguk Sagi bila kusahau Samguk Yusa. Mishil anatajwa ama historia yake inapatikana kikamilifu katika nyaraka za Hwarang almaarufu kama Hwarang Segi.

Kwa mujibu wa nyaraka za kihistoria za Hwarang, Mishil alikuwa ni 'Royal Concubine' na alikitumikia cheo hicho kwa awamu tatu tofauti, yaani kwa Wafalme watatu tofauti. Hapa nawazungumzia Wafalme wa Silla; Jinheung, Jinji na Jinpyeong.



 
Si alikuwa King's consort, halafu watu walikuwa wanaamini ana nguvu za kiroho hivyo ikamuongezea influence. Mimi ndio najua hivyo
Mishil alitumia Sayansi kuwahadaa wananchi ambao kwao Sayansi ilikuwa ni miujiza ya kutetemekewa.

Ndiyo maana Deokman alipotaka kui-Publicize Sayansi Mishil alihuzunika na alimsikitikia sana Deokman.
 
Back
Top Bottom