Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hutaki kuitwa Mkuuu Eeenh!

Arthdal Mbona Haijarudi Kama Nilivyoitegemea...!
kuna uwezekano kabila la white mountain ndio chanzo kikuu cha matatizo yanayojiri kwenye ardhi ya arthdal, inavyosemekana aramun haesulla (aliyeunganisha makabila ndani ya ardhi ya arthdal) asili yake pia alikuwa ni igutus ila cha kushangaza hiki kizazi cha bibi Asa sin wakiongozwa na Asa Ron wanakwenda kinyume na uhalisia wa mambo kwa kuficha ukweli tokea kuondoka kwa huyu bibi takribani miaka mingi iliopita.

season 1 and 2 tumepata kushuhudia nguvu ya damu ya huyu bibi Asa sin jinsi ilivyoweza kutapakaa mpaka kwenye ardhi ya Iark linakopatikana kabila la wahan(wahan tribe) na hatimaye imegundulikana ya kwamba Tanya ndiye mrithi halali wa kizazi cha Asa sin mwishoni mwa season 2.

kama aramun haesulla asili yake ilikuwa ni igutus basi hakuna ubaya wowote endapo kama atajitokeza mwanadamu mwengine mwenye asili ya igutus kuitawala ardhi ya arthdal, bahati mbaya sana Asa Ron na wenzake kwa kutumia nguvu ya kabila lao pamoja na ushawishi wao kidini kama tunavyofahamu dini hubeba nguvu kubwa sana pindi inapotumiwa kwenye siasa either kwa nia njema au kinyume chake wamewaaminisha wananchi wote wanaounda makabila ndani ya arthdal ya kwamba igutus na binadamu jamii ya neanthal ni wanadamu hatari na wanapaswa kusambaratishwa.

khofu hii walioijenga kwenye mioyo ya wananchi ndio iliopelekea hata baba yake tagon atumie kila njia ikiwemo kutoa uhai kwa wasiokuwa na hatia ili aifiche asili ya mtoto wake ili asijulikane kama ni igutus, khofu hii pia ilimwingia tagon mwenyewe ndio maana na yeye ameendelea kuificha asili yake na hata kuficha asili ya mtoto wa kumlea ambaye ni Saya.

kama ingeliwekwa wazi historia ya aramun haesulla basi tagon angelistahili kupewa heshima ya reincarnation ya aramun haesulla bila hata ya kumwaga damu kama itakavyotokezea episode ijayo kwa sababu na yeye asili yake ni igutus japokuwa hajawahi kuendesha farasi wa kanmoreu kama alivyofanya eunseom.

ningelipenda tagon pindi atakapofanikiwa mapinduzi yake ya umwagaji damu dhidi ya kabila la white mountain na wafuasi wao wakiongozwa na Asa Ron atatangaza hadharani ya kwamba yeye ni igutus na atathibitisha hata aramun haesulla mwenyewe alikuwa ni igutus hivyo basi hakuna ubaya wowote kwa igutus kuchanganyika na saram (binadamu wa kawaida)
1568405521685.png
 
Nimependa Saya Anavyomuaangalia Tanya.. (Siri Yako Usiseme)
saya afanana na popo kwa sababu hajulikani upande upi aliyoelekea kitabia (wema au uovu), ila jambo kubwa linalomuathiri ni malezi alioyapata tokea utotoni kupitia kwa wanadamu wawili waliojawa na tamaa za kimadaraka na ubinafsi, hatimaye na yeye amerithi tabia zile zile za wazazi wake ila tofauti kubwa ni kwamba uovu wake umezidi zaidi kwa sababu ya elimu alionayo ambayo mara kwa mara amekuwa akiitumia vibaya.

unaweza kujiuliza kwa nini aliamua kumwekea sumu kaka yake tagon?
je ni kweli ana mapenzi ya dhati kwa Tanya au ndio anataka kumtumia ili afanikishe malengo yake na baba yake?
hayo yote anayoyafanya na kuyapanga je ni kweli dhumuni lake kuu ni kuwathibitishia wananchi ya kwamba hata igutus wana haki ya kuheshimiwa au ana lengo jengine ambalo ni kupata madaraka pindi atakapoondoka tagon?
1568410510139.png
tofauti kubwa iliopo kati ya saya na eunseom ni kwamba eunseom ni mwanadamu ambaye yupo tayari kutoa msaada kwa anayeuhitaji muda wowote bila hata ya kutegemea kulipwa ujira wowote baadae ndio maana baadhi ya watu wanamshangaa kwa ihsani na wema alionao. ndio maana hata momo tribe wakiongozwa na mwanadada mwenye asili ya kijapani (erika karata) anayetumia jina la xabara ndani ya drama ameanzisha kampeni ya kumtafuta eunseom baaada ya kuwapa msaada na kusepa (nafikiri watataka awe kiongozi wao)

episode ya 14 nimeona tagon na taelha wameshaandaa mikakati ya kwenda kubeba makabila mengineo kwa njia ya upanga ila sidhani kama watafanikiwa kwa sababu namuona eunseom akichaguliwa kuwa kiongozi wa makabila mbali mbali ikiwemo ago tribe na wale jamaa wanaoogopewa wanaojipaka rangi (momo tribe), hii inamaanisha ya kwamba hatimaye eunseom anakwenda kukusanya nguvu itakayomsaidia kuiangusha nchi ya arthdal inayotawaliwa na tagon.

eunseom amebarikiwa kuwa na sifa za kuwa kiongozi kwa sababu ya tabia zake za kupenda haki na usawa kwa jamii na pia kupenda kwake kutoa msaada kwa wanaohitaji tofauti na tagon na mwanawe saya ambao wote kwa pamoja wanajaribu kutumia reference ya maisha yao magumu waliopitia kama ni kigezo tosha cha kuwafanya wayapambanie maisha kuelekea njia ya peponi hata kwa kumwaga damu isiyokuwa na ulazima.
rejea mauaji ya neanthal species pia rejea uvamizi dhidi ya wahan tribe.
tagon alitekeleza mission zote mbili kwa sababu apate kuendelea kuishi mjini kwa sababu baba alishamwambia aondoke mji mkuu ili asije akamletea balaa ndipo tagon akamwambia baba yake nipo tayari kukupa zawadi ya ardhi ya neanthal na watumwa kutoka wahan tribe ili nipate kuendelea kuishi makao makuu.
kilichotokezea baadae tagon pia alimuua baba yake mzazi.​

kama ni shida basi aliyepata shida zaidi ni eunseom lakini bado hajakata tamaa na wala hajawahi kutumia kipaji chake na uwezo alionao kwa ajili ya kuwaonea wengineo ili afanikishe malengo.

hivi kwa akili ya kawaida tagon angeliweza kumsaidia yule jamaa aliyewauza eunseom na wenzake kwenye kambi ya utumwa, dah! yule fala aliwatesa mnoo lakini eunseom akaona acha nimsaidie na mwisho alimwambia.
"naomba ukumbuke leo hii umesaidiwa na igutus (uliyekuwa ukimtukana na kumtesa kama mnyama)"​

igutus = binadamu aliyezaliwa na mzazi mmoja akiwa ni neanthal na mwengine ni saram (binadamu wa kawaida) kwa mujibu wa drama lakini a.k.a mixed race
1568410074449.png
 
Hahahhahaa. Kama Yule Muhuni Aloongozana Na Eunseom Kwenda Kwa Hao Mabaharia Yaani Yule Ndo Baharia Kabisaa.
kadri anavyoendelea kujiweka karibu na eunseom naamini ipsaeng atabadilika kitabia na atakuwa mtu muhimu sana kwa eunseom hususan kwenye safari yake ya kutafuta power kupitia makabila tofauti na yeye ndiye atakayeshuhudia mara kwa mara tabia njema alizonazo eunseom pamoja na ungwaji mkono atakaupata kupitia jamii tofauti
wenyewe wanasema ukikaa na mlevi na wewe utakuwa mlevi hivyo hivyo ukikaa na mtu mwema kama eunseom utaadilika kimatendo japo kwa 80%.

kuna uwezekano ipsaeng anatokea kwenye makabila yenye nguvu lakini yaliyomtokezea huko nyuma ndio yamemfanya awe na tabia za ajabu ajabu ikiwemo tamaa na usaliti. yaliyomkuta huko nyuma huenda ndio yamempelekea asiwaamini binadamu hata kwa sekunde 10

pia nina wasiwasi huenda anatokea ago tribe kabila ambalo kwa muda mrefu limekuwa kwenye vita zisizokwisha, kama utavuta kumbu kumbu season 1 episode 2 mwanzoni kabisa kuna nyakati tagon alikuwa anawambia wafuasi wake
"nimesikia kabila la ago wamerudisha amani na utulivu lakini muda wowote huenda wakatwangana tena"

kuna nyakati walipokuwa wamelala kwenye barafu alikuwa anamtaja inaishigi, moja kati ya legend god wanaoheshimiwa sana na kabila analotokea na inasemekana jamaa aliwahi kuokoka kwenye maporomoko ya maji na akaendelea kuwa hai, kama umeangalia preview ile yenye dakika 5 kuna nyakati eunseom anapewa mtihani wa kutupwa kwenye maji ina maana kama atasalimika huenda lile kabila lile watamchukulia eunseom kama ndiye reincarnation ya inaishigi.

momo tribe + ago tribe + wahan tribe + neanthal + white peak tribe + mubaek = eunseom
tagon na wafuasi wake kazi wanayo hapo mbeleni.

1568412469172.png
 
nimeota ndani ya ardhi yenu mutatoana roho wenyewe kwa wenyewe - ragaz
hatimaye utabiri wa ragaz unakwenda kutimia kwenye episode 15, tagon atawasambaratisha wale wote waliofanikiwa kuifahamu siri yake ya kwamba yeye ni igutus na pia ndiye aliyemuua baba yake mzazi.
mwenyewe anasema hapendi kumwaga damu ya wasiokuwa na hatia na alitamani kuwa mtawala atakayeleta usawa kwa makabila yote lakini sidhani kama itawezekana tena.

sijui ni lini tagon ataiweka siri yake hadharani ya kwamba yeye ni igutus.
kwa nini anaogopa na yeye ndiye aliyeshikilia makali ya kisu.
heshima kwake jang dong gun ahjussi kwa zawadi aliotupa mwaka huu baada ya suit drama.

kuna taarifa zisizo rasmi kwa asilimia 100 zinadai ya kwamba kuna uwezekano arthdal chronicles tukashuhudia tena muendelezo wake mnamo mwaka 2020, pia upo uwezekano wa hii drama kutengenezewa character games.
1568413644459.png
 
General Wang Gun nimekuona unamnyapianyapia huyu binti, halafu General Park Sulhee anakwambia umemlavu huyo binti unakanusha haya!.

Msimulizi nae hacheleweshi mambo kanipasha kuwa huyo binti atakuwa mke wa 3 wa Emperor Wang Gun pia yasemekana ndiye atakuwa mkewe kipenzi.

Hiyo drama Emperor Wang Gun nimefikia episode ya 80/200 unaambiwa ukitaka kwenda haraka nenda mwenyewe, ila ukitaka kufika mbali nenda mwenzio.
kwahiyo hapa nasindikizwa na

The Book of Correction: Tayari kina Konishi na Kato washaanza kufanya yao hapa Joseon. Ndo kwanza episode 15/50.
 
nimeota ndani ya ardhi yenu mutatoana roho wenyewe kwa wenyewe - ragaz
hatimaye utabiri wa ragaz unakwenda kutimia kwenye episode 15, tagon atawasambaratisha wale wote waliofanikiwa kuifahamu siri yake ya kwamba yeye ni igutus na pia ndiye aliyemuua baba yake mzazi.
mwenyewe anasema hapendi kumwaga damu ya wasiokuwa na hatia na alitamani kuwa mtawala atakayeleta usawa kwa makabila yote lakini sidhani kama itawezekana tena.

sijui ni lini tagon ataiweka siri yake hadharani ya kwamba yeye ni igutus.
kwa nini anaogopa na yeye ndiye aliyeshikilia makali ya kisu.
heshima kwake jang dong gun ahjussi kwa zawadi aliotupa mwaka huu baada ya suit drama.

kuna taarifa zisizo rasmi kwa asilimia 100 zinadai ya kwamba kuna uwezekano arthdal chronicles tukashuhudia tena muendelezo wake mnamo mwaka 2020, pia upo uwezekano wa hii drama kutengenezewa character games.
View attachment 1206725
Yani episode 15 ni moto jana imebid niangalie ikiwa raw saiv ndio nairudia ikiwa na subs. Nimependa true love aliyonayo taealha kwa tagon.
 
Yani episode 15 ni moto jana imebid niangalie ikiwa raw saiv ndio nairudia ikiwa na subs. Nimependa true love aliyonayo taealha kwa tagon.
yes wote wanapendana kwa dhati, kila mmoja anazifahamu hisia za mwenzake kiundani na kubwa zaidi kila mmoja anaifahamu siri ya mwenzake na yupo tayari kuificha siri hiyo kwa uhai wake ndio maana uhusiano wao umekuwa imara zaidi ya jiwe la msingi lililojengwa na fundi maico.

kuna preview fulani nilibahatika kuiona inajaribu kuonyesha matukio yatakayojiri season 3 na miongoni mwa matukio hayo ni kitendo cha tagon kujitangaza kuwa mfalme na malikia wake kivyovyote atakuwa ni Taelha kwa sababu yule binti aliyemuoa kutoka ASA clan amehusika na mapinduzi yalioongozwa na ASA HON.

sifahamu hii drama itamaliza vipi cause nikiangalia hadithi ndio kwanza inazidi kuchangamka na episode zilizobaki ni mbili tu ila kwa kuangalia hayo mahusiano imara ya kimapenzi kati ya Tagon na Taelha kunajizalisha swali moja muhimu sana.

je Taelha ataridhika na heshima ya umalikia peke yake?
mara nyingi tumeshuhudia pindi panapozaliwa mahusiano kati ya wanadamu wawili khususan wenye afya njema tukio muhimu linalosubiriwa na pande zote mbili zilizounga mahusiano hayo ni tendo la kutafuta kizazi kitakachoendeleza muungano wa familia mbili hizo zilizoungana kwa njia ya damu.

nikimuangalia Tagon na changamoto zake alizozipitia kimaisha hususan kitendo chake cha kuificha asili yake ya igutus kwa kutumia upanga sidhani kama atakuwa tayari kutafuta mtoto haliyakuwa tayari anaye mwengine wa kulea (adopted son) ambaye ni Saya na tayari alikwisha muahidi ya kwamba yeye ndiye atakayekuwa mrithi wake pindi atakapoondoka madarakani.

Hilo ndio tatizo atakalokutana nalo Taelha na atajutia maamuzi yake ya kujipendekeza na kumuamini Tagon kwa maisha yake yote na kumdharau baba yake, kwa kutegemea kupata mtoto atakayeliwezesha kabila lake lake la Hae kuwa na nguvu baadae ndani ya arthdal pindi mwanawe wa kumzaa atakaporithi madaraka atakapoondoka Tagon.

Tukumbuke sababu kubwa inayomfanya Taelha atofautiane na baba yake kwa muda wote ni ile hali ya kutokubalina kimtazamo wa njia gani sahihi itumike ili kabila lao la Hae liwe na nguvu kuliko kabila la sanyeok na mengineo.

je ikitokezea Saya amerithi madaraka ya Tagon atampa heshima ya queen dowager Taelha?
Hakuna binadamu muhuni, kahaba, muuaji na msomi wa kuzaliwa bali yote hayo yanatokana na mazingira aliyokulia na ukimuangalia Saya amekulia kwenye mikono ya wanadamu ambao mikono yao imejaaa damu ya wasiokuwa na hatia kama neanthal species na wenye hatia kama Asa hon na baadhi ya wafuasi wake.

Saya bado ana machungu ya kumpoteza mchumba wake ambaye aliuliwa na Hae Too Ak kwa amri yaTaelha hivyo basi siku atakayopata nguvu ya madaraka atahakikisha analipiza kisasi kwa Taelha na Hae Too Ak a.k.a bibi bonge.

Taelha atahitaji mtoto ili ajiokoe na kifo kutoka kwa Saya na Tagon hatohitaji mtoto kwa sababu wanaye Saya.

ngoja tuone itakavyokuwa ila mara nyingi stori za korea historical drama ndivyo zinavyokuwa.
1568732604373.png

Lee Seung Gi, Suzy, And More Discuss High Budget For “Vagabond” And Goal To Break 30 Percent Viewership Ratings
“Vagabond” tells the story of a stuntman named Cha Dal Gun (played by Lee Seung Gi), who stumbles upon a massive corruption scandal while trying to uncover the hidden truth behind a mysterious plane crash. He ends up investigating the case alongside National Intelligence Service (NIS) secret agent Go Hae Ri (played by Suzy).

On September 16, the cast and producing director Yoo In Shik held a press conference ahead of the drama’s premiere. Yoo In Shik raised anticipation for “Vagabond” and complimented the actors’ close teamwork, saying,
We shot in Morocco for two months, and not only was the flight long, but the food and environment might not have suited the cast. They also must have been nervous because of the action scenes. [Despite these factors,] it was great while we were there. We got to know each other through morning shoots and evening drinking parties. Even when the drama ends, I think these friend

When Lee Seung Gi was asked whether the 25 billion won (approximately $21.1 million) budget put pressure on him, the actor said,
“The producers prepared so perfectly that I didn’t feel any pressure. Because they filmed in a way that didn’t disrupt the drama and was more fun than the script, I never felt burdened. It was a place where I could safely focus on my acting.”ships will last.”

Suzy also shared a bit about her character, Go Hae Ri. She explained,
“Go Hae Ri is a multidimensional figure who comes to investigate a plane crash with Cha Dal Gun while dispatched to Morocco. I hope that viewers will be able to see my own growth through the development of Go Hae Ri.”

Shin Sung Rok, who will play brilliant NIS agent Ki Tae Woong, closed the press conference by expressing his confidence in the drama. He said,

“I think this project will do really well. I experienced a lot of things I’ve never done before, and while I was on set, I thought to myself that this drama will be on a whole new level. Our goal for viewership ratings is 30 percent. If we get 30 percent, the actors will discuss and come up with a special event.”

“Vagabond” premieres September 20 at 10 p.m. KST.​
1568734490950.png

nimemuona mchumba wangu Hwang bo ra kwenye picha wa pili kutoka upande wa kulia, wapo wanaoniuliza nimependa nini kwa huyo binti ila nabaki kuwacheka hi hi hi kama jiwe wenye wivu wa kishamba.

hata kama ingelikuwa maneno yake ni sumu huyu dada basi kwangu mimi yangelikuwa ni zaidi panadol yenye kutibu maumivu, nikiuguwa kidogo tu namtafuta yeye amwage porojo lake la maneno kama yule mzungu kichaa na kelele zake zisizoumiza.

tukutane ijumaa inshaallah panapo uhai, jamani hii drama ilikuwa kwenye ratiba zangu tokea mwaka 2019 ulipoanza, imepelekwa mbele weeeeeeee kutoka May mpaka september hatimaye imefika paap.

tatizo si pesa bali uhai ndio muhimu zaidi hapa duniani, mengi na kidogo wamekufa ila daemusin yupo hai japokuwa hana mbwa mfukoni.
shikamoo uhai.​
 
Gong Hyo Jin, Kang Ha Neul, And Kim Ji Suk Talk About Working Together For “When The Camellia Blooms”

The cast of KBS’s upcoming romantic comedy drama “When the Camellia Blooms” has shared what it’s like to work together on set.

On September 17, a press conference for “When the Camellia Blooms” took place. Attending the event were Gong Hyo Jin, Kang Ha Neul, Kim Ji Suk, and director Cha Young Hoon.

“When the Camellia Blooms” will tell the stories of three couples in different stages of love. Moreover, the drama will focus on the romance that blossoms between Dong Baek (Gong Hyo Jin), a woman who is trapped in a certain perception about love, and Yong Shik (Kang Ha Neul), who shows undying support and love for her.

During the press conference, the actors talked about working with each other. Gong Hyo Jin said, “I’ve heard great stories about how Kang Ha Neul is kind and works hard, so I went to the set with high expectations. Just like I’ve heard, he works really hard and is full of energy, and it was great to see his positivity. I’ve told my friends, ‘Yong Shik is really great.'”

Gong Hyo Jin also talked about working with Kim Ji Suk. The actress said, “I feel comfortable with him because we are in the same age group. We worked together a few years back in the drama ‘Let’s Go To School, Sang Doo.’ He was a supporting character who sat at the very far end of a classroom. I thought he was great at the time, but when I saw him a couple years later in a variety show, I realized that he is actually very silly. I’m glad to have met him again over 10 years later. We have many scenes that are set in the past, and I’m thankful that he helps me act while feeling as if he were my actual first love.”

Kang Ha Neul responded, “The script was the reason I joined this drama. I read until episode 4, and I realized it wasn’t a script that I could see anywhere else. It became more clear when I got to talk to the director and the writer. I chose the drama because I trusted them to lead us to pull off this script with depth. Gong Hyo Jin’s influence also played a huge role. I’m a big fan. There is a part of me that chose the drama because I’m a fan.”

Kim Ji Suk added, “Kang Ha Neul is full of energy. Gong Hyo Jin takes care of us as if we were her sons and she is our mother. She also looks after things outside of acting, so it feels like she’s taking care of us.”

“When the Camellia Blooms” will premiere on September 18 at 10:00 p.m. KST.
1568740439309.png
 
Lee Seung Gi, Suzy, And More Discuss High Budget For “Vagabond” And Goal To Break 30 Percent Viewership Ratings
“Vagabond” tells the story of a stuntman named Cha Dal Gun (played by Lee Seung Gi), who stumbles upon a massive corruption scandal while trying to uncover the hidden truth behind a mysterious plane crash. He ends up investigating the case alongside National Intelligence Service (NIS) secret agent Go Hae Ri (played by Suzy).

On September 16, the cast and producing director Yoo In Shik held a press conference ahead of the drama’s premiere. Yoo In Shik raised anticipation for “Vagabond” and complimented the actors’ close teamwork, saying,
We shot in Morocco for two months, and not only was the flight long, but the food and environment might not have suited the cast. They also must have been nervous because of the action scenes. [Despite these factors,] it was great while we were there. We got to know each other through morning shoots and evening drinking parties. Even when the drama ends, I think these friend

When Lee Seung Gi was asked whether the 25 billion won (approximately $21.1 million) budget put pressure on him, the actor said,
“The producers prepared so perfectly that I didn’t feel any pressure. Because they filmed in a way that didn’t disrupt the drama and was more fun than the script, I never felt burdened. It was a place where I could safely focus on my acting.”ships will last.”

Suzy also shared a bit about her character, Go Hae Ri. She explained,
“Go Hae Ri is a multidimensional figure who comes to investigate a plane crash with Cha Dal Gun while dispatched to Morocco. I hope that viewers will be able to see my own growth through the development of Go Hae Ri.”

Shin Sung Rok, who will play brilliant NIS agent Ki Tae Woong, closed the press conference by expressing his confidence in the drama. He said,

“I think this project will do really well. I experienced a lot of things I’ve never done before, and while I was on set, I thought to myself that this drama will be on a whole new level. Our goal for viewership ratings is 30 percent. If we get 30 percent, the actors will discuss and come up with a special event.”

“Vagabond” premieres September 20 at 10 p.m. KST.​
View attachment 1209928

nimemuona mchumba wangu Hwang bo ra kwenye picha wa pili kutoka upande wa kulia, wapo wanaoniuliza nimependa nini kwa huyo binti ila nabaki kuwacheka hi hi hi kama jiwe wenye wivu wa kishamba.

hata kama ingelikuwa maneno yake ni sumu huyu dada basi kwangu mimi yangelikuwa ni zaidi panadol yenye kutibu maumivu, nikiuguwa kidogo tu namtafuta yeye amwage porojo lake la maneno kama yule mzungu kichaa na kelele zake zisizoumiza.

tukutane ijumaa inshaallah panapo uhai, jamani hii drama ilikuwa kwenye ratiba zangu tokea mwaka 2019 ulipoanza, imepelekwa mbele weeeeeeee kutoka May mpaka september hatimaye imefika paap.

tatizo si pesa bali uhai ndio muhimu zaidi hapa duniani, mengi na kidogo wamekufa ila daemusin yupo hai japokuwa hana mbwa mfukoni.
shikamoo uhai.​
Duh eti mengi na kidogo wamekufa ila daemusin yupo hai
 
Profile

Drama: Flower Crew: Joseon Marriage Agency (English title)

Revised romanization: Kkotpadang: Joseonhondamgongjakso
Hangul: 꽃파당 : 조선혼담공작소
Director: Kim Ga-Ram
Writer: Kim Yi-Rang (novel), Kim Yi-Rang
Network: JTBC
Episodes:
Release Date: September 16, 2019 --
Runtime: Mon & Tue 21:30
Language: Korean
Country: South Korea
 
yes wote wanapendana kwa dhati, kila mmoja anazifahamu hisia za mwenzake kiundani na kubwa zaidi kila mmoja anaifahamu siri ya mwenzake na yupo tayari kuificha siri hiyo kwa uhai wake ndio maana uhusiano wao umekuwa imara zaidi ya jiwe la msingi lililojengwa na fundi maico.

kuna preview fulani nilibahatika kuiona inajaribu kuonyesha matukio yatakayojiri season 3 na miongoni mwa matukio hayo ni kitendo cha tagon kujitangaza kuwa mfalme na malikia wake kivyovyote atakuwa ni Taelha kwa sababu yule binti aliyemuoa kutoka ASA clan amehusika na mapinduzi yalioongozwa na ASA HON.

sifahamu hii drama itamaliza vipi cause nikiangalia hadithi ndio kwanza inazidi kuchangamka na episode zilizobaki ni mbili tu ila kwa kuangalia hayo mahusiano imara ya kimapenzi kati ya Tagon na Taelha kunajizalisha swali moja muhimu sana.

je Taelha ataridhika na heshima ya umalikia peke yake?
mara nyingi tumeshuhudia pindi panapozaliwa mahusiano kati ya wanadamu wawili khususan wenye afya njema tukio muhimu linalosubiriwa na pande zote mbili zilizounga mahusiano hayo ni tendo la kutafuta kizazi kitakachoendeleza muungano wa familia mbili hizo zilizoungana kwa njia ya damu.

nikimuangalia Tagon na changamoto zake alizozipitia kimaisha hususan kitendo chake cha kuificha asili yake ya igutus kwa kutumia upanga sidhani kama atakuwa tayari kutafuta mtoto haliyakuwa tayari anaye mwengine wa kulea (adopted son) ambaye ni Saya na tayari alikwisha muahidi ya kwamba yeye ndiye atakayekuwa mrithi wake pindi atakapoondoka madarakani.

Hilo ndio tatizo atakalokutana nalo Taelha na atajutia maamuzi yake ya kujipendekeza na kumuamini Tagon kwa maisha yake yote na kumdharau baba yake, kwa kutegemea kupata mtoto atakayeliwezesha kabila lake lake la Hae kuwa na nguvu baadae ndani ya arthdal pindi mwanawe wa kumzaa atakaporithi madaraka atakapoondoka Tagon.

Tukumbuke sababu kubwa inayomfanya Taelha atofautiane na baba yake kwa muda wote ni ile hali ya kutokubalina kimtazamo wa njia gani sahihi itumike ili kabila lao la Hae liwe na nguvu kuliko kabila la sanyeok na mengineo.

je ikitokezea Saya amerithi madaraka ya Tagon atampa heshima ya queen dowager Taelha?
Hakuna binadamu muhuni, kahaba, muuaji na msomi wa kuzaliwa bali yote hayo yanatokana na mazingira aliyokulia na ukimuangalia Saya amekulia kwenye mikono ya wanadamu ambao mikono yao imejaaa damu ya wasiokuwa na hatia kama neanthal species na wenye hatia kama Asa hon na baadhi ya wafuasi wake.

Saya bado ana machungu ya kumpoteza mchumba wake ambaye aliuliwa na Hae Too Ak kwa amri yaTaelha hivyo basi siku atakayopata nguvu ya madaraka atahakikisha analipiza kisasi kwa Taelha na Hae Too Ak a.k.a bibi bonge.

Taelha atahitaji mtoto ili ajiokoe na kifo kutoka kwa Saya na Tagon hatohitaji mtoto kwa sababu wanaye Saya.

ngoja tuone itakavyokuwa ila mara nyingi stori za korea historical drama ndivyo zinavyokuwa.
View attachment 1209911
Na huku kwa eunseom mambo yanapamba moto. Hii drama sijui kwanini wengine hawajaielewa wakati ni moto wa kuotea mbali. Ya 17 tagon ndio atajitangaza king naona
 
Na huku kwa eunseom mambo yanapamba moto. Hii drama sijui kwanini wengine hawajaielewa wakati ni moto wa kuotea mbali. Ya 17 tagon ndio atajitangaza king naona
hata mimi nashangaaa wakati hadithi yake ukiifuatilia kwa umakini utafanikiwa kuielewa.
nakumbuka episode 1 ndio iliniwia vigumu zaidi ukilinganisha na episode zilizofuata.

cha kushangaza hata korea haiangaliwi kwa kiwango kikubwa sana wakati ilitarajiwa hii drama iwe na rates kubwa sana kwa jinsi ilivyocontains gharama nyingi na waigizaji wote kuwa na umaarufu.

tetesi za muendelezo wake zimezidi kushamiri.​
 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom