Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hii ameigiza pia huyu mwaba hapo chiniView attachment 1182368
Pia naomba kujua filamu kadhaa alizoigiza huyu jamaa..namkubali sana aisee..move zake nyingi ni akili sana..hakurupuki
Huyo ni Mzee wa makamo Jun Kwang-ryul.

Kama unahitaji "ya kifalme" basi bila shaka utakuwa unahitaji Historical Drama na katika Historical Drama alizoigiza huyo mzee nguli kabisa katika Tasnia ni kama zifuatavyo;
  • Jumong (2006)
  • Warrior Baek Dong Soo (2011)
  • Jang Hee-Bin / Royal Story (2003)
  • King and I (2007)
  • Royal Gambler (2016)
  • Flower in Prison (2016)
  • Jung-Yi, Goddess of Fire (2013)
  • Heo Joon (1999)

Kati ya hizo nilizokutajia, alizoigiza kama 'Mfalme' ni mbili nazo ni;
  • Jumong (2006): Aliigiza kama Mfalme Geumwa wa Buyeo
  • Jang Hee-Bin / Royal Story (2003): Aliigiza kama Mfalme Sukjong wa Joseon

Kazi nyinginezo alizofanya huyo mzee wa makamo ni kama ifuatavyo;
  • Swallow the Sun
  • The Man in the Mask
  • Witch at Court
  • You Are Too Much
  • Sign n.k.

Mpaka hapo nadhani tutakuwa tumekula ng'ombe mzima kasoro mkia ambao bado tunautafuta.
 
Pia kama kuna anayejua kazi kadhaa za huyu mwamba hapo chini anipe nizijue..ama aniambie yuko wapi nije kuzifuata..

View attachment 1182371
Hapa unamzungumzia Ji Sung.

Kazi alizofanya Ji Sung hususani Drama zipo nyingi tu na zifuatazo ni baadhi tu:
  • Defendant (2017)
  • Kim Su-Ro, The Iron King (2010)
  • Kill Me, Heal Me (2015)
  • Royal Family (2011)
  • The Great Seer (2012)
  • Swallow the Sun (2009)
  • Protect The Boss (2011)
  • Secret Love (2013)
  • Entertainer (2016)
  • Doctor John (2019)
  • Familiar Wife (2018) n.k.
 
Episode ya 9 tu nimeikinai
Duh! Hilo pengine ni kutokana na 'Role' ya Ji Chang-wook.

Lakini, sidhani kama Ji Chang-wook alifeli sana kwa sababu ndivyo 'Storyline' ilivyokuwa inamtaka afanye. Maana hata katika Historia inaelezwa kuwa Toghon Temur aliyumbishwa na akayumba sana katika utawala wake kipindi cha mwanzoni. Alikuwa 'Very Weak'.

Alikuwa akiendeshwa sana na Warlords kama akina Bayan n.k. lakini alivyokuwa akizidi kukua (Mature), alibadilika sana na ule woga na udhaifu wa mwanzoni ulipungua kwa kiasi kikubwa kama si kuisha kabisa.

Na kwa upande wa Ji Chang-wook mwenyewe nadhani hii Empress Ki ni moja ya Drama ambazo jamaa amecheza vizuri sana kuliko baadhi ambazo alicheza pia kama vile Historical Drama: Warrior Baek Dong Soo n.k.
 
Hapa unamzungumzia Ji Sung.

Kazi alizofanya Ji Sung hususani Drama zipo nyingi tu na zifuatazo ni baadhi tu:
  • Defendant (2017)
  • Kim Su-Ro, The Iron King (2010)
  • Kill Me, Heal Me (2015)
  • Royal Family (2011)
  • The Great Seer (2012)
  • Swallow the Sun (2009)
  • Protect The Boss (2011)
  • Secret Love (2013)
  • Entertainer (2016)
  • Doctor John (2019)
  • Familiar Wife (2018) n.k.
Nimeona mbili tu za defendant na swallow the sun..jamaa namkubali sana katika kazi zake..vipi naweza pata kwenye flash hizo kazo zake kama unazo mkuu??
 
Huyo ni Mzee wa makamo Jun Kwang-ryul.

Kama unahitaji "ya kifalme" basi bila shaka utakuwa unahitaji Historical Drama na katika Historical Drama alizoigiza huyo mzee nguli kabisa katika Tasnia ni kama zifuatavyo;
  • Jumong (2006)
  • Warrior Baek Dong Soo (2011)
  • Jang Hee-Bin / Royal Story (2003)
  • King and I (2007)
  • Royal Gambler (2016)
  • Flower in Prison (2016)
  • Jung-Yi, Goddess of Fire (2013)
  • Heo Joon (1999)

Kati ya hizo nilizokutajia, alizoigiza kama 'Mfalme' ni mbili nazo ni;
  • Jumong (2006): Aliigiza kama Mfalme Geumwa wa Buyeo
  • Jang Hee-Bin / Royal Story (2003): Aliigiza kama Mfalme Sukjong wa Joseon

Kazi nyinginezo alizofanya huyo mzee wa makamo ni kama ifuatavyo;
  • Swallow the Sun
  • The Man in the Mask
  • Witch at Court
  • You Are Too Much
  • Sign n.k.

Mpaka hapo nadhani tutakuwa tumekula ng'ombe mzima kasoro mkia ambao bado tunautafuta.
Katika hizo za kifalme ipi ameigiza kama head of enuch derpartment ?? Ambapo anakuwa mlinzi mkuu wa familia ya kifalme pamoja na kuasili mtoto ili awe mwanawe??
 
Nimeona mbili tu za defendant na swallow the sun..jamaa namkubali sana katika kazi zake..vipi naweza pata kwenye flash hizo kazo zake kama unazo mkuu??
Mara nyingi huwa natumia njia ya kuzitazama katika tovuti ama 'Online' kama wadau wengine pia wafanyavyo humu ambayo ni njia nzuri tu kwa sababu popote utakapokuwepo na Smartphone yako tu yenye kifurushi cha 'Internet' cha kutosha ama sehemu yenye Wi-Fi, unaweza kuzitazama.

Hizo kazi zinapatikana sehemu mbalimbali ila kwa upande wangu mimi sina hizo kazi zake pia bado kuna nyingi sijazitazama. Kuna wavuti nyingi tu mojawapo ni Dramacool ambayo imesheheni hizo Drama bila kusahau Movies pia.

Huko unaweza kuzipakua (Download) kama una nafasi ya kuziweka kuendana na kifaa chako unachotumia ama unaweza kutumia ile njia niliyosema mwanzo ya kuzitazama mtandaoni, njia ambayo haitohitaji uwe na nafasi ama 'Drive' ya kuhifadhia.
 
Katika hizo za kifalme ipi ameigiza kama head of enuch derpartment ?? Ambapo anakuwa mlinzi mkuu wa familia ya kifalme pamoja na kuasili mtoto ili awe mwanawe??
Kwa maelezo hayo uliyoyatoa nadhani utakuwa ukizunguzia Drama ya mwaka 2007-2008 inayokwenda kwa jina la The King and I. Kama ndiyo hiyo unayozungumzia ambayo ndiyo hii hapa pichani, basi 'Link' ya kuipata ipo hapo chini:

1565960616922.png

[LINK] Korean Drama: The King and I
 
No jaman hawa ndo mastaa pekee waliobakia na ndoa imara duh kumbe nao wanaelekea shimoni daah
Huyo dada ni yule main cast wa kwenye boys over flowers na huyo kaka yupo zaid kwenye supporting casts kama a man from another star. Waliigiza pamoja drama ya blood ndio kupendana mpaka kufunga ndoa.
 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom