Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Ni kweli lilikuwa tukio baya sana lakini mimi naona zilikuwa akili za utoto tu na kama alivyofanikiwa kumshape katika mengine angeweza kumuelimisha na hilo pia na kwa vile alikuwa bado mdogo angerekebika tu
Hapana ile hali haikuwa ya kawaida, ushiruhusu mahaba yakupofushe ili ushindwe kuutazama ukweli. Ingawa nakubaliana na wewe binadamu anapaswa kupewa nafasi ya pili.
 
Mimi nimeanalia Drama nyingi mno ivyo sina drama moja ninayoipenda zaidi bali nina msululu wa drama nizipendazo kuzipitia mara kwa mara.

1.Drama Zangu bora za kila wakati ni Dong Yi ikifuatiwa na Horse Doctor na Road No 1 .:canada:
2.Zote ni historical (za kijijini)

3.Drama za malovee nilizozipenda ni Be Strong Geum soon,Angel eyes, Princess Man na Jang Ok Jung
wa
4.Za kichawi ni Jeon Woo Chi na Arrang and the Magistrate

5.Za Action Iris, City Hunter, The Fugitive Plan B,3days,A man called God na Swallow the Sun

Wasanii ninaowakubali:
1.Ji Sung (Swallow the Sun, Kim Soo Ro)
2.Song II Gook (Aman called God)

Sexiest actress ni Gu Hye Sun (Angel eyes)

Msanii anayenivunjaga mbavu ni Sung Dong Il (Jang Ok Jung,The Fugitive Plan B, Jeon Woo chi

Drama ya kwanza ni Iris
Hiyo Drama ya Dong Yi ni Hatari.
 
Ngoja nikimaliza Personal taste na hii Kim So Roo nitaitafuta.
Wewe hunizidi mimi tena naona wewe bado mwanafunzi kwangu.
Mimi hizi drama/Korean movies nimeanza kuziangalia serious since 2010 na hadi leo hii nimeshaangalia zaidi ya 100!
Kama juzikati nimemaliza Hotel King, My loveable girl,na Hong Gil Dong.Ni juzi tu hata wiki 2 hazijaisha.
Sorry hiyo Hong Gil Dong ni nzuri?!
Maana ni drama niliyoifahamu tangu 2011, lkn sikuwahi kuitazama
 
Shikamoo dada, lo! Unastahiki kuwa malkia wa humu ndani.

Hahaaaaa yani kama ubalozi wa Korea ungetoa ofa kwa wanaoipenda Korea Wallah nisingeikosa nafasi ya kwenda kutalii kisiwani Jeju na jijini Seoul.

Nawapenda kitambo na mpaka nimeiambukiza familia yangu, mdogo wangu nae kawa mlevi wa drama za Kikorea siku hizi sihangaiki kudownload drama kila weekend naletewa mzigo wa wiki nzima.
Viva Korean Drama
 
Naomba unigawie
 
Hi Unnie...
Unaangalia drama gani? Nilipoimaliza Hwarang nikaanza kuicheki Korean Odyssey ambayo naona inanivuruga tu nimefika ep 10 nimestop nimeanza Strong Woman Bong Soo nikiimaliza nianze kukicheki chuma Six Flying Dragons huhuuuuuu
Hello darling, unnie hana mali mpya na wewe uko kny mgomo baridi wa kutoniwezesha umeamua kunitambishia sijui nifanyeje! Wk end nilirudia kidogo empress ki maana niliwamiss sasa naendelea na American series ya Power...mpaka utakaponikumbuka.
Six flying dragons naitamani sana unayo soft copy? Vipi hiyo strong woman imetulia? :)
 
Jamani si ndio kama hivi nimekukumbuka Unnie? Of course ninazo ktk PC, kwa sasa ninazo drama 5 na movie moja.
Ngoja nikifikisha walau 10 nikucheki nikupatie...
Hii strong woman ni nzuri comedy kibao na ina crime pia.
Make sure huangalii hizi ninazokuambia, nakuhifadhia...
 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom