Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

yes binafsi nimeshangaa sana kushuhudia Tagon kuwa ni igutu na alizaliwa nje ya ndoa (mzee sanung nirung alichepuka) kwa sababu mama yake ni species ya neanthal na aliyekuwa akifahamu siri hiyo ni baba yake, kwa sasa ameongezeka eunseom ndio maana kwa khofu ya kuwekwa wazi udhaifu wake amekubali kutekeleza baadhi ya makubaliano waliowekeana na eunseom ya kutokuwadhuru watu wa kabila la Wahan (wahan tribe).

ndio maana si ajabu kukuta ep1 tagon ndiye aliyekuja na best idea ya kuwamaliza watu wa neanthal kwa sababu anafahamu udhaifu wao, si hivyo tu tagon alishatabiriwa kuwa ni mtoto atakayempindua baba yake ndio maana mzee kwa kulifahamu hilo alihakikisha mwanawe haishi mara kwa mara mji mkuu kwa kuhofia mtoto wake atazidi kujiongezea nguvu na umaarufu kutoka kwa viongozi wa makabila mengine wanaounda nchi ya Arthdal.

Tagon, Taealha na Giseon kwa muda mrefu wamekuwa wakiandaa mipango ya kuwaondoa madarakani wazee wao ili warithi madaraka ndio maana si ajabu kuona taelha ndiye aliyetengeneza barua feki ili mzazi wake aonekane ni mfitinishaji wa makabila aliyejawa na wivu kwa tagon, na pia tagon ndiye aliyemuua baba yake mzazi (sanung nirun) japokuwa mzee na yeye alikuwa anamuwinda mwanawe.

kama umefuatilia kwa umakini majadiliano kati ya mubaek na yule bibi Asa Sakan utajifunza ya kwamba tagon alikuwa anataka kupambana na mipango ya Mungu kwa mujibu wa prophecy of Daraburu ni kwamba tagon ataleta balaa kwenye ardhi ya arthdal. bibi akaendelea kusema vitakapojitokeza vitu vitatu vilivyozaliwa miaka 20 iliopita (kengele, upanga, kioo) tagon atazidisha mipango yake ya kuitawala dunia, ndipo mzeee sijui kwa bahati mbaya au maybe bibi amepangwa na tagon akamwambia mubaek amsaidie tagon atimize ndoto yake ya kuiongoza dunia kuiletea amani haliyakuwa anafahamu fika utabiri haupo hivyo.

ninachokiona mbeleni ni uaminifu atakaouonyesha Mubaek kwa kumsaidia eunseom japokuwa hawajakutana uso kwa uso mpaka muda huu, mubaek ni muumini mkubwa sana wa aramun haesulla halafu anafahamu dalili atakazokuja nazo mrithi wa aramun haesulla ikiwemo dalili ya kuendesha farasi ya kanmoreu, alama ya maua mwilini mwake pamoja na necklace iliokuwa ya mwanamama asa hon ambaye ndiye mama mzazi wa eunseom pamoja na pacha mwengine (hammer of the wind, lonicera flower, kanmoreu )

Tagon ni igutu na yeye ndiye aliyeanzisha kampeni ya kuwamaliza species wenzake huku akimuacha hai kaka yake eunseom kwa dhumuni la kutaka kumtumia huko mbeleni, asichokifahamu tagon ni kwamba eunseom na yeye pia ni igutu
kitakochomuangusha Tagon huko mbeleni ni ujinga wake wa kuamini yeye pekee ndiye mtu sahihi anayepaswa kuwa kiongozi wa ardhi ya Arthdal.

3 objects kwa mujibu wa tabiri
belly (mfano wa kengele) =mwanadada tanya
sword (upanga) = eunseom
mirror (kioo) = saya/ kaka yake eunseom

ina maana song joong ki ameigiza nafasi mbili kwa wakati mmoja.
part 1 imemaliza na jumamosi inaanza part 2
View attachment 1131333
Mi Taelha Nimempenda! Kujiamini Kwake tu..
 
Kipi Kikunukishacho Chingu!?
huwezi amini huu utani wa kunipa heshima ya ugenius bado haujanivutia my friends, hii heshima ulionipa ni kubwa sana na nisingependa uendelee kunipa heshima hiyo (nitafutie heshima nyengine).

genius: an exceptionally intelligent person or one with exceptional skill in a particular area of activity.
synonyms: brilliant person, mental giant, mastermind, Einstein, intellectual, intellect, brain, highbrow, expert, master, artist, polymath; More
=============================================================================================
hizi sifa zote hapo juu najiona sina labda ni kwa sababu baadhi ya binadamu hatujioni ubora wetu, kama ni hivyo pengine upo sahihi waniona ni genius from kolomije.

ila nimependa haya maneno yako "Ila U Genius Ni Mbali na Kuishia Kidato Cha Nne"
teh teh teh sijachukia mpendwa wangu usije ukajibebesha wasiwasi bureeee nafsini mwako.

mimi ni miongoni mwa wanadamu wanaochelewa kuchukizwa na jambo, hivyo basi nitanie mpaka uchoke wala sitopandishi presha
 
Apo Kwenye “Nitania Mpaka Uchoke” 😂 Naona Umenipa Rungu Na Kichwani Umenyoa Lol!

Pokea Sifa Izo! Ukue Nazo, Zinaweza Ongeza Kitu..
 
Siku Izi Ninavyoipenda J5 Hatari!
yes jumatano imekuwa ni motoo kwa walevi wa korean drama.
  1. angels last mission dram
  2. one spring night drama
  3. search WWW drama
1131540
 
anafanana na wewe kisifa?
Ye Mzuri Sana..

Kisifa Sidhani! Labda Anaeniona Aniambie

Huwa Napenda Mwanmke Anaesimamia Msimamo Wake! Hayumbishwi! Kila Anachoona Kwake na Kwa Wanaomzunguka Kina Tija Ndo Hufanya, Hua Namfurahia Sana!

Kwa Taelha Nimekubari Misimamo Yako Japo Haijaoneshwa Sana!

Ila Ji-Min ndo Ananikosha Sana
 
Iyo Search Bado Sijaiona!

Ila Izo Mbili Acha Kabisaa. Usiku Wa j5 Hua Nakesha
itafute hutojutia humo ndani, stori yake ni ushindani wa makampuni mawili makubwa yanayojishughulisha na utoaji wa huduma za mtandaoni (search engine) kama vile google, bing n.k

waigizaji wakuu ni wanadada watatu pamoja na jang ki yong
1131547

Back
Top Bottom