Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Habari wakuu naomba link ya kudawnload drama ya age of warriors. Nimejitahidi kuitafuta siipati.
jaribu link hii:,
 
Ndio Nimtoroshe We Han Ji Min Wa Nini!?
  1. anajua udhaifu wangu na mimi pia nafahamu udhaifu wake kupitia maisha yetu halisi.
  2. sifahamu udhaifu wako wala hufahamu udhaifu wangu kupitia maisha yetu halisi (without keyboard)
:p:p:p
sababu ya kwanza nimeshakupa, kadri nikipata muda nitakuwa nakuwekea sababu nyenginezo
 
Niliona trailer yake ni noma yaani mambo kama hayo ndio huwa yanaukeep ubongo wangu busy. Mapinduzi sifanyi ila nitaenjoy. Na nimeipata naanza utaratibu wa kuipakua
 
  1. anajua udhaifu wangu na mimi pia nafahamu udhaifu wake kupitia maisha yetu halisi.
  2. sifahamu udhaifu wako wala hufahamu udhaifu wangu kupitia maisha yetu halisi (without keyboard)
:p:p:p
sababu ya kwanza nimeshakupa, kadri nikipata muda nitakuwa nakuwekea sababu nyenginezo
Apo Kwenye Udhaifu Sidhani kama Unamsemea Ji Min, Labda Ni Yule Mwengine Wa Kuvuka Bahari,Huyo Ntakuelewa....🙂

Iyo Namba 2 Ipo Kindani Zaidi Lol!
 
na wewe pia Blessed bosi wangu.
mpaka muda huu sijafahamu maana ya neno blessed ndio maana nikalirudisha kwako hivyo hivyo.
kama ulinitukana na mimi pia nimeshakurudishia
kama ulinishukuru na mimi pia nimekushukuru.
karibu tena kwenye kijiwe cha wasiokuwa na kazi ya kufanya​

Blessed ni (Worth of Worship) or holy Boss wangu wala sikukutukana au ubarikiwe kwa namna nyingine.
 
Naona Arthdal Chronicles Ina Twist Za Khatari!

Uku Saya Uku Eunseum Twin Tena

Tagon Nae Ni Igutu How!?

Njoo Unielekeze Basi.
yes binafsi nimeshangaa sana kushuhudia Tagon kuwa ni igutu na alizaliwa nje ya ndoa (mzee sanung nirung alichepuka) kwa sababu mama yake ni species ya neanthal na aliyekuwa akifahamu siri hiyo ni baba yake, kwa sasa ameongezeka eunseom ndio maana kwa khofu ya kuwekwa wazi udhaifu wake amekubali kutekeleza baadhi ya makubaliano waliowekeana na eunseom ya kutokuwadhuru watu wa kabila la Wahan (wahan tribe).

ndio maana si ajabu kukuta ep1 tagon ndiye aliyekuja na best idea ya kuwamaliza watu wa neanthal kwa sababu anafahamu udhaifu wao, si hivyo tu tagon alishatabiriwa kuwa ni mtoto atakayempindua baba yake ndio maana mzee kwa kulifahamu hilo alihakikisha mwanawe haishi mara kwa mara mji mkuu kwa kuhofia mtoto wake atazidi kujiongezea nguvu na umaarufu kutoka kwa viongozi wa makabila mengine wanaounda nchi ya Arthdal.

Tagon, Taealha na Giseon kwa muda mrefu wamekuwa wakiandaa mipango ya kuwaondoa madarakani wazee wao ili warithi madaraka ndio maana si ajabu kuona taelha ndiye aliyetengeneza barua feki ili mzazi wake aonekane ni mfitinishaji wa makabila aliyejawa na wivu kwa tagon, na pia tagon ndiye aliyemuua baba yake mzazi (sanung nirun) japokuwa mzee na yeye alikuwa anamuwinda mwanawe.

kama umefuatilia kwa umakini majadiliano kati ya mubaek na yule bibi Asa Sakan utajifunza ya kwamba tagon alikuwa anataka kupambana na mipango ya Mungu kwa mujibu wa prophecy of Daraburu ni kwamba tagon ataleta balaa kwenye ardhi ya arthdal. bibi akaendelea kusema vitakapojitokeza vitu vitatu vilivyozaliwa miaka 20 iliopita (kengele, upanga, kioo) tagon atazidisha mipango yake ya kuitawala dunia, ndipo mzeee sijui kwa bahati mbaya au maybe bibi amepangwa na tagon akamwambia mubaek amsaidie tagon atimize ndoto yake ya kuiongoza dunia kuiletea amani haliyakuwa anafahamu fika utabiri haupo hivyo.

ninachokiona mbeleni ni uaminifu atakaouonyesha Mubaek kwa kumsaidia eunseom japokuwa hawajakutana uso kwa uso mpaka muda huu, mubaek ni muumini mkubwa sana wa aramun haesulla halafu anafahamu dalili atakazokuja nazo mrithi wa aramun haesulla ikiwemo dalili ya kuendesha farasi ya kanmoreu, alama ya maua mwilini mwake pamoja na necklace iliokuwa ya mwanamama asa hon ambaye ndiye mama mzazi wa eunseom pamoja na pacha mwengine (hammer of the wind, lonicera flower, kanmoreu )

Tagon ni igutu na yeye ndiye aliyeanzisha kampeni ya kuwamaliza species wenzake huku akimuacha hai kaka yake eunseom kwa dhumuni la kutaka kumtumia huko mbeleni, asichokifahamu tagon ni kwamba eunseom na yeye pia ni igutu
kitakochomuangusha Tagon huko mbeleni ni ujinga wake wa kuamini yeye pekee ndiye mtu sahihi anayepaswa kuwa kiongozi wa ardhi ya Arthdal.

3 objects kwa mujibu wa tabiri
belly (mfano wa kengele) =mwanadada tanya
sword (upanga) = eunseom
mirror (kioo) = saya/ kaka yake eunseom

ina maana song joong ki ameigiza nafasi mbili kwa wakati mmoja.
part 1 imemaliza na jumamosi inaanza part 2
1131333
 
Arthdal the chronicle, bonge la series
upo sahihi
director Kim Won-Suk, muandishi Park Sang-Yeon na mwanamama Kim Young-Hyun hakuna asiyefahamu ubora wao.
arthdal chronicle
six flying dragons
tree with deep roots
the great queen seondeok
signal
misaeng
jewel in the palace
the great king sejong

 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom