Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

upo sahihi shin hye sun yupo vizuri sana.
mwaka huu kidogo KBS wamerudisha ubora wao wa kutengeneza project zenye muelekeo mzuri.
arthdal chronicles unaifuatilia?
Nimeangalia Episode 1 Nasubir Kuangalia Episode 2 Nikipata Wasaa, Ila Ukweli Watu Wanaiponda Sana.. Japo Kwangu Episode 1 Ni Nzuri Tu...
 
Kisa Chakutoweka Ni Nini!??

Wa Nane!? 😳
Sijaridhika!
umechukua likizo mwezi mzima kwa nini upande wangu iwe vibaya?
korean drama zinaelekea kunipotezea dira ya maisha yangu, nimeshakuwa addicted mpaka najionea aibu.

ndio maana nimepunguza dozi mwaka huu.
nimeanza kupunguza dozi ya kutembelea media zinazo ripoti korean entertainment.
kuna mwanadamu fulani alinambia siwezi kubadilika, kauli kama hizo nazichukulia ni kauli za kumkatisha adui yako tamaa.
nataka nijaribu kama naweza kuachana na ulevi wa thread hii.
 
upo sahihi shin hye sun yupo vizuri sana.
mwaka huu kidogo KBS wamerudisha ubora wao wa kutengeneza project zenye muelekeo mzuri.
arthdal chronicles unaifuatilia?
Ninachoipendea 1 Spring Night Ni Vile Wanavyotuonyesha ni Jinsi Gani Watu Wanahangaika Kumuacha Mtu Ulokua Nae Kwa Muda Mrefu Japo Mapesi Yashaisha Siku Mingi!

Yaani Yule Dada Naenda Nae Maumivu Anayopitia (Kimaigizo) Naenda Nae Kabisaa..

Ila Mule Ndani Napo Muna Hisia Sana Lol!
 
umechukua likizo mwezi mzima kwa nini upande wangu iwe vibaya?
korean drama zinaelekea kunipotezea dira ya maisha yangu, nimeshakuwa addicted mpaka najionea aibu.

ndio maana nimepunguza dozi mwaka huu.
nimeanza kupunguza dozi ya kutembelea media zinazo ripoti korean entertainment.
kuna mwanadamu fulani alinambia siwezi kubadilika, kauli kama hizo nazichukulia ni kauli za kumkatisha adui yako tamaa.
nataka nijaribu kama naweza kuachana na ulevi wa thread hii.
Jamaniii 😔...Mi Sababu Ya Swaum Ndomna Nikapotea!

Huyo Alokuambia Ivyo Niii Wiii...

Kupunguza Ni Sahihi Kabisaa Kabisaa Apo Wala Hatukinzani!

Ila Siyo Kupotea Umu Eti!?
 
Ninachoipendea 1 Spring Night Ni Vile Wanavyotuonyesha ni Jinsi Gani Watu Wanahangaika Kumuacha Mtu Ulokua Nae Kwa Muda Mrefu Japo Mapesi Yashaisha Siku Mingi!
Yaani Yule Dada Naenda Nae Maumivu Anayopitia (Kimaigizo) Naenda Nae Kabisaa..
Ila Mule Ndani Napo Muna Hisia Sana Lol!
pole sana
unadhani yupo sahihi bidada kuomba kwake kuvunja mahusiano na boy friend wake?
episode ya 6 sijaiangalia hivyo basi sijui kilichoendelea mbeleni.
sijaona udhaifu wa yule mwanamume hata ifikie hatua bidada alazimishe kuvunja mahusiano kwa kutumia kigezo cha familia ya mwanamume.

halafu cha kuvutia baba yake binti ni muajiriwa wa shule ilio chini ya usimamizi wa baba yake mwanaume
 
Ina bidi nikutafute unipe hizo series kaka
EMPEROR WANG GUHN DRAMA
imenichukua miaka takribani mitatu kuiangalia hii drama and finally usiku wa jana nimeimaliza, drama kama hizi zinaangaliwa zaidi na wale binadamu wabishi, watemi na vichwa maji kama damushin ambao kwa kiasi kikubwa muda wao mkubwa huutumia kwa ajili ya kuangalia televisheni kuliko kufanya kazi mpaka anayaletea athari macho yake aliyopewa na muweza wa yote ulimwenguni.

jumla ya episode 200 na kila episode inachukua wastani wa dakika 48- 53, kilichonivutia ni kwamba 85% ya matukio yalioigizwa humu ndani yamerikodiwa kwenye vitabu vya historia na kwa kuwa washindi walikuwa ni goryeo basi kivyovyote maandishi ya kihistoria yaliorekodiwa yatakuwa upande wa kuisifu Goryeo.
Neno goryeo(koryeo) ndio msingi wa neno korea.
  1. wang gun amezaliwa na kufariki (31 January 877 – 4 July 943)
  2. ni mzaliwa wa shilla lakini chimbuko la ukoo wao ni watu kutoka goguryeo ya zamani, ukoo wao ulikuwa na heshima kubwa sana na utajiri uliotokana zaidi na biashara walizokuwa wakizifanya kwa njia ya bahari.
  3. kwa mujibu wa drama na maandishi ya kihistoria aliwahi kuwepo muhadhiri wa imani ya buddhism aliyeitwa dosun ambaye aliwahi kutabiri ya kwamba wang guhn atakuja kuwa mtawala mwenye nguvu kwenye hizi nchi tatu za baadae (laer goryeo+ later baekje +shilla)
  4. wang guhn alitawala goryeo kwa miaka 25,ndipo madaraka yake yakarithiwa na mtoto wake wa kwanza ambaye ni wang mu lakini alifariki baada ya miaka miwili ya kuwa madarakani
  5. wang guhn alioa wanawake takribani 30, kwa kiasi kikubwa alifunga ndoa zaidi za kisiasa kwa dhumuni la kuunganisha damu dhidi ya koo tofauti ambazo ziliamua kujisalimisha kwa wang guhn.
  6. upande wa pili alikuwepo jamaa anayeitwa gong ye ambaye alizaliwa na mfalme wa shilla lakini kupitia kwa mwanamama amabye ni concubine, huyu jamaa alikutana na mitihani mingi sana uddogoni mwake alipokuwa shilla ikiwemo kupoteza jicho lake na alishuhudia kifo cha mama yake jambo lililopelekea aikimbie nchi yake na kuwa MONK.
  7. Gong yae baadae alipata nguvu kubwa sana na kufanikiwa kuanzisha taifa lake ni kulipa jina la Taebong, ukoo wa wang guhn waliamua kujisalimisha kwa gong yae na hatimaye akapewa cheo cha general, mfalme gong yae alivutiwa sana na wang guhn kiasi ambacho alifikia hatua ya kumtangaza wang guhn kama ni mdogo wake.
  8. miaka ilizidi kusogea huyu jamaa akawa na chembe chembe za kidikteta, miongoni mwa vitendo vyake vya ovyo ni kuisambaratisha familia yake mbele ya hadhara, baadae gong yae akamua kulibadilisha jina la taifa lake kutoka Taebong kuelekea Majin.
  9. mwaka 918 takribani wanajeshi wanne wenye nguvu nchini Taebong waliamua kumfuata wang guhn nyumbani kwake kwa dhumuni la kumshauri ashiriki kwenye kampeni yao ya kutaka kumpindua mfalme gong yae ambaye alikwisha vuka mipaka kwa matendo yake maovu, wang guhn alikataa mpango huo lakini baadae baada ya kubembelezwa na mke wake hatimaye akaongoza kampeni ya kumuondoa madarakani mfalme gong yae kwa njia ya mapinduzi.
  10. mfalme gong yae aliuawa pamoja na wafuasi wake na hatimaye wang guhn akabeba ufalme na kutangaza rasmi utawala wa goryeo(goguryeo mpya).
  11. alikuwepo general aliyeitwa kyu hwon kutoka shilla, huyu general nayeye alifanya mapinduzi kwa kuivamia shilla maeneo ya mujinju na hatimaye baadae akaanzisha taifa lake ambalo ni HUBAEKJE ( baekje mpya)
  12. wenye lugha yao wanadai ya kwamba kama utashindwa kuiongoza familia yako haijalishi wewe ni shujaa unayeogopeka basi pia utashindwa kuiongoza tawala yako kwa amani na ndicho kilichomkuta huyu mfalme.
  13. alitokezea kumpenda sana sana mtoto wake wa mwisho huku akimchukia mnoo mtoto wake wa mwanzoni kupitia kwa mke wa mwanzoni, jamaa aliipa mafanikio makubwa sana hubaekje ikiwemo kampeni yake ya kuivamia shilla na kumuua mfalme wa shilla huku akimweka mfalme mwengine aliyekuwa akiendana na maamuzi yake lakini vita ya familia ilipelekea anguko la nchi yake.
  14. mtoto wake wa kwanza aliitwa shin guhm ambaye aliamua kufanya mapinduzi kwa kumuondoa madarakani baba yake na pia aliamua kumuua ndugu yake wa kambo aliyeitwa keum gang na hatimaye akawa mfalme wa pili baekje.
  15. kyu hwon hatimaye akaamua kukimbilia goryeo ili apate hifadhi kutoka kwa wang guhn ambaye ni adui wake wa muda mfrefu ambaye wameshakutana mara kwa mara vitani, mzee aliona ni bora ajisalimishe kwa wang guhn kuliko kumuunga mtoto wake wa kumzaa awe mfalme.
  16. vita ya mwisho hatimaye hubaekje wakajisalimisha kwa goryeo na baadae shilla pia wakajisalimisha kwa goryeo, bila ya kusahau taifa la balhae ambalo lilianzishwa na general daejoyong kutoka goguryeo nao pia walijisalimisha kwa goryeo.
  17. hawa balhae utawala wao uliangushwa na wahuni wanaoitwa KHITAN, hatimaye goryeo wakafanikiwa kuziunganisha kingdom tatu na wang guhn kupewa heshima ya emperor.
  18. shilla waliziunganisha tawala tatu kwa kutumia msaada zaidi kutoka nchi za kigeni hususani Tang.
  19. wang guhn hakutegemea nguvu za nchi za kigeni kuziunganisha three kingdom za baadae.
maisha ya emperor wang guhn na baadhi ya watoto wake pia yameelezewa kupitia drama zifuatazo
scarlet heart ryeo
shin or go crazy

huyu wang guhn kwa vipindi tofauti alizungukwa na wanadamu wenye akili zaidi kuliko binadamu wengineo kama mimi.

choi ung= aliingia madarakani akiwa na miaka 14 nyakati za utawala wa gong yae, alikuwa ni zaidi ya genius na alifariki akiwa na miaka 35
choi jimong = huyu jamaa alibobea mnoo kwenye elimu ya nyota
View attachment 1098969
 
pole sana
unadhani yupo sahihi bidada kuomba kwake kuvunja mahusiano na boy friend wake?
episode ya 6 sijaiangalia hivyo basi sijui kilichoendelea mbeleni.
sijaona udhaifu wa yule mwanamume hata ifikie hatua bidada alazimishe kuvunja mahusiano kwa kutumia kigezo cha familia ya mwanamume.

halafu cha kuvutia baba yake binti ni muajiriwa wa shule ilio chini ya usimamizi wa baba yake mwanaume
Pole Nawe

Yupo Sahihi Kabisa! Unavyowaona Unahisi Wana Uhusiano Wakimahaba Wale!?

Kilichobakia kwao Ni Mazoea kwakua Wamekua Pamoja Mda Mrefu Lakini Hakuna Ile Hisia Yakuwafanya Wazidi Kua Pamoja Kwa Muda Mrefu Zaidi.

Yule Bint Kapata Mtu Wa Tofauti (Apa Wanaume Mnafeli Sana) Anamuonyesha Maisha Ya Tofauti Na Yale Ambayo Hayaoni kwa Mtu Wake! Lazima Dada Akili Iruke..

Iyo Familia ya Mwanaume, Dada Anatafuta Sababu Tu Ila Ukweli Dada Ana Hisia Na Jamaa
 
atakubali kulea mtoto wa mwanamke mwengine?
ikitokezea mama mtoto amerudi kitatokezea kitu gani?
 
atakubali kulea mtoto wa mwanamke mwengine?
ikitokezea mama mtoto amerudi kitatokezea kitu gani?
Mpaka Pale Tayari Kashakubari

Huyo Mama Mtoto Hatausikaje Na Maisha Yao!
Ye akirudi akitaka Mtoto Amchukue, Awaache Ye Miaka yote alikua Wapi Mpaka Akamtelekeza Mtoto Bado Mdogo Vile!
 
Great Conqueror tafadhali kuja hapa mara moja my rafiki, hivi ile barua yangu niliyoiwasilisha kwako ya kuchukua likizo ya muda usiojulikana kuanzia mwezi JUNE ndani ya hii thread umeisambaza kwa wanachama wa hiki kijiwe na kama hujaisambaza labda ulidhani nipo kwenye utani?

gwenchanah gwenchanah nitachukulia kama umesahau ombi langu mwenyekiti mpya wa hiki kijiwe kwa upande wa jinsia ya meeee.

my dongsaeng chuma96 ukweli ni kwamba mwaka 2019 nimejiwekea malengo ya kupunguza kuangalia korean drama kwa takribani 45% ukilinganisha na mwaka uliopita, hivyo basi unaponiambia nikuwekee list ya top 5 korean drama zilizofanya vizuri za mwaka huu utakuwa umenipa adhabu nzito sana, kwa drama zilizokuwa compeleted mpaka muda huu nimeangalia sita tu.

drama sita bora za kwangu mimi ambazo ndio nimeziangalia kwa mwaka huu ni hizi hapa:-
  1. doctor prisoner drama
  2. the fiery priest drama
  3. touch your heart drama
  4. romance is a bonus book drama
  5. haechi drama
  6. the banker drama
her private life drama sikubahatika kuiangalia lakini majorities ya walioiangalia wameisifia sana hususani love chemistry kati ya park min young noona pamoja na kim jae wook sunbaenim.

View attachment 1121993
================================================================================================
================================================================================================

scalethat noona hujaniambia wewe ni mpenzi wa drama za aina gani na nimeshasahau ladha uzipendazo. lakini jaribu kuchagua kati ya drama zifuatazo kwa kusoma kwanza drama details:-
  1. money flower drama + bad papa drama = kwa heshima ya bae wako jang hyuk
  2. secret forest (best drama kwa mwaka 2017) = criminal, law, investigation
  3. because this is my first life (best drama kwa mwaka 2017)
  4. signal (best drama kwa mwaka 2015) = criminal, investigation, time travel
  5. tunnel drama = criminal, investigation, time travel
  6. my mister (best drama kwa mwaka 2018)
  7. mr sunshine (best drama kwa mwaka 2018)
  8. incomplete life drama or misaeng drama (best drama kwa mwaka 2014) = inanihusu kwenye maisha ninayoishi
  9. replay 1988 (best drama kwa mwaka 2016)
  10. misty drama
  11. sky castle (best drama kwa mwaka 2018)
  12. whats wrong with secretary kim drama
  13. prison playbook drama
  14. encounter drama
  15. lawless lawyer drama
  16. life on mars = criminal, investigation, time travel
  17. hwayugi
  18. the last empress drama
  19. the smile has left your eyes drama
  20. come and hug me drama
95% ya list ya hapo juu ni drama zilizoonyeshwa na cable tv, nimepunguza sana kufuatilia drama zinazoonyeshwa na public broadcasting kama SBS, KBS na MBC
View attachment 1121991
Aigooooo nashukuru sana opah (sijui km nimepatia) yaaan apo nimeona moja tu ya Mr sunshine.zote mi naangalia siko selective Sana kwa Hawa ndugu zangu wakorea.
asante sanaaaa ngoja nianze na za bae wng then nije moja baada ya nyingine.........uzidi kubarikiwa na sorry kwa usumbufu kumbe umejipa likizo.
 
hamuna tatizo wala hujanisumbua kihivyo, ni makosa yangu nimeshindwa kuweka taarifa rasmi kwa muda mrefu.
nasumbuliwa na ugonjwa wa kuandika comment na kuifuta baada ya muda mchache.
ugonjwa huu kitaalamu unaitwa comment diagnosis kolomijee.

mungu ametutofautisha binadamu na viumbe wengine kwa kutuzawadiwa maarifa lakini si binadamu wote tunaotumia maarifa yetu ipasavyo kwa dhumuni la kuyakabili maisha yetu ya kila siku.
kang pil joo ni miongoni mwa viumbe hai wanaotufundisha jinsi gani mwanadamu anapaswa kuyatumia maarifa aliyopewa na muumba wake kwa ajili ya kutimiza malengo yake ya maisha aliyojiwekea.

itafute kwanza money flower drama naamini hutojutia maamuzi yako.
nitalipa fidia ya bando lako na mwengine yeyote kama atachukizwa na hii project.
mchana mwema.
1122570

Pole Nawe
Yupo Sahihi Kabisa! Unavyowaona Unahisi Wana Uhusiano Wakimahaba Wale!?
Kilichobakia kwao Ni Mazoea kwakua Wamekua Pamoja Mda Mrefu Lakini Hakuna Ile Hisia Yakuwafanya Wazidi Kua Pamoja Kwa Muda Mrefu Zaidi.
Yule Bint Kapata Mtu Wa Tofauti (Apa Wanaume Mnafeli Sana) Anamuonyesha Maisha Ya Tofauti Na Yale Ambayo Hayaoni kwa Mtu Wake! Lazima Dada Akili Iruke..

Iyo Familia ya Mwanaume, Dada Anatafuta Sababu Tu Ila Ukweli Dada Ana Hisia Na Jamaa
jeongin ameshajifunza kupitia kwa dada yake ambaye ameolewa kwa ndoa ya kulazimishwa na baba yake (ndoa za siasa), angalia matatizo anayoyapitia dada yake ndani ya ndoa yake, tuachane na maigizo kwenye dunia hii tunayoishi wapo wengi sana wanaopitia maisha ya ndoa yenye manyanyaso makubwa sana kutoka kwa wenza wao lakini wakashindwa kutoa taarifa kwa sababu tofauti ikiwemo kuogopa kudhihakiwa na kuitwa wahuni wanaokimbia ndoa kwa visingizio dhaifu.

matokeo yake wanasubiri kumeshakucha ndio wanajifanya kujifunika shuka, unakuta mwanamke ameshavunjwa viungo na mwenza wake kwa vipigo, mara mwanamume ametiliwa sumu na mke wake ndio anatafuta ushauri nasaha.
kadri unavyoshindwa kutafuta msaada mapema ndio unazidi kuchochea moto wa mateso ya ndoa yako.
kuna kesi moja niliwahi kusoma stori ilitokezea nchi za amerika ambapo mwanamama alipeleka malalamiko ya kunyanyaswa na mume wake kwenye vyombo vya sheria(polisi), kibaya zaidi mume wake alikuwa ni miongoni mwa polisi wenye nyadhifa kubwa sana hali iliopelekea kesi yake ionekane ni ujinga (haikufuatiliwa) na mwisho wa siku yule baba aliamua kumuua mke wake.

unajua baadhi ya nyakati wanawake munasumbuliwa na tatizo la kuiogopa zaidi jamii kuliko munavyojiogopa wenyewe, unakuta msichana hana amani na mahusiano yake lakini kutokana umaarufu wake au umaarufu na ushawishi wa mume wake anaona tabu kutoka hadharani na kuelezea yanayomkabili.

"dah hivi kweli nitojitokeze mbele ya jamii na umaarufu wangu wote huu niilalamikie ndoa yangu, hivi jamii itanichukuliaje nitakaposema mume wangu ambaye ni waziri wa njaa na shibe wa serikali ya awamu ya 10 anachepuka si nitaonekana chanzo ni mimi nashindwa kumpa huduma bora"
 
Kwa bahati mbaya siwafahamu hata mmoja maana miye ni mzee wa Historical drama.

TOP 7 Male Idols With The Best Visuals, As Chosen By Korean Press
Here are the top 7 chosen “face geniuses”!
mwcpnHQCMsMwFynZ4_XK3uFaVJ1Cp-CBznl1bY0SH5avEw2eM7MIOaxpxY6nDXKraHj3VKxbMY3PDFC2j9RGMH0h2kJzRCsbpA=w720

STORIES
Yesterday
Korean media named the 7 male idols as the most handsome “face geniuses”, thanks to their deep gazes, perfect proportions, sweep-you-off-your-feet smiles and more!

7. Ong Seongwoo
most handsome visuals kpop 14

most handsome visuals kpop 15

4-D visual, Ong-(da)vid.
Unbelievably perfect, tall body proportions.
— Sporbiz

6. Vernon (SEVENTEEN)
most handsome visuals kpop 13

most handsome visuals kpop 12

Dicaprio doppelgänger.
Visual member of SEVENTEEN, Ver-caprio.
— Sporbiz

5. Suho (EXO)
1111
most handsome visuals kpop 11

His nickname is literally Jun-chael (Junmyeon and Saint Michael).
Are you human or an angel?
— Sporbiz

4. Jaehyun (NCT)
most handsome visuals kpop 9

most handsome visuals kpop 16

Visuals fit for the SM standard.
The ideal SM visual.
— Sporbiz

3. Kim Jinwoo (WINNER)
most handsome visuals kpop 6

most handsome visuals kpop 7

YG’s most handsome visual idol.
God-sent visuals.
 
Kwa bahati mbaya siwafahamu hata mmoja maana miye ni mzee wa Historical drama.

TOP 7 Male Idols With The Best Visuals, As Chosen By Korean Press
Here are the top 7 chosen “face geniuses”!
mwcpnHQCMsMwFynZ4_XK3uFaVJ1Cp-CBznl1bY0SH5avEw2eM7MIOaxpxY6nDXKraHj3VKxbMY3PDFC2j9RGMH0h2kJzRCsbpA=w720

STORIES
Yesterday
Korean media named the 7 male idols as the most handsome “face geniuses”, thanks to their deep gazes, perfect proportions, sweep-you-off-your-feet smiles and more!

7. Ong Seongwoo
most handsome visuals kpop 14

most handsome visuals kpop 15

6. Vernon (SEVENTEEN)
most handsome visuals kpop 13

most handsome visuals kpop 12

5. Suho (EXO)
1111
most handsome visuals kpop 11

4. Jaehyun (NCT)
most handsome visuals kpop 9

most handsome visuals kpop 16

3. Kim Jinwoo (WINNER)
most handsome visuals kpop 6

most handsome visuals kpop 7
Huyu no moja kabla sijaona uko juu nikajua ni demu.daaah wakorea hatari sana
 
Back
Top Bottom