Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Ukiona hivyo ujue ni tabia yake halisi ndo maana anaiwezea sana
:p :p :p :p
sipendi kutoa hukumu kwa kitabu ambacho sijakisoma.
waigizaji pornography ndio celebrities pekee wanaoigiza uhalisia wa maisha yao 🏇🏇
1111141


1111143
 
Hivi wadau kuna mtu ambaye drama ya Yi San mwishoni haikumuumiza kiasi cha chozi kulenga?

Wiki iliyopita nimeimaliza inaisha kihuzuni sana hata maji nilishindwa kunywa!!
 
Itafute pia na Movie yake ambayo Storyline yake ndio imetumika kwenye hiyo Drama uliyoitazama.

Movie inaitwa Masquerade ya mwaka 2012.
hii movie imechangia kwa kiasi kikubwa sana niachane na mpango wa kuiendeleza the crowned clown drama.
gwanghae alikuwa ni mfalme aliyepitia maisha ya ovyo sana ya kiutawala.
gwanghae pia alikuwa ni mfalme aliyefanya baadhi ya matukio ya kishujaa yanayopaswa kukumbukwa.
aliondolewa madarakani kwa njia ya mapinduzi yakiongozwa na watu wa magharibi.
ni miongoni mwa wafalme waliopita kwenye tawala za korea wasipewe jina la heshima.
kama ni mtihani gwanghae amepata 5/10
 
hii movie imechangia kwa kiasi kikubwa sana niachane na mpango wa kuiendeleza the crowned clown drama.
gwanghae alikuwa ni mfalme aliyepitia maisha ya ovyo sana ya kiutawala.
gwanghae pia alikuwa ni mfalme aliyefanya baadhi ya matukio ya kishujaa yanayopaswa kukumbukwa.
aliondolewa madarakani kwa njia ya mapinduzi yakiongozwa na watu wa magharibi.
ni miongoni mwa wafalme waliopita kwenye tawala za korea wasipewe jina la heshima.
kama ni mtihani gwanghae amepata 5/10
Inashangaza sana kwakweli kutompa Gwanghae temple name wakati mfalme aliyerithi utawala baada yake, Injo alipewa temple name pamoja na kwamba aliboronga zaidi ya Gwanghae.

Kama ni kuwanyima heshima hiyo ingetakiwa wanyimwe wote na si kumtosa Gwanghae na kumpa Injo.
 
Inashangaza sana kwakweli kutompa Gwanghae temple name wakati mfalme aliyerithi utawala baada yake, Injo alipewa temple name pamoja na kwamba aliboronga zaidi ya Gwanghae.

Kama ni kuwanyima heshima hiyo ingetakiwa wanyimwe wote na si kumtosa Gwanghae na kumpa Injo.
labda ni kwa sababu aliondolewa madarakani kwa njia ya mapinduzi ndio maana hakupewa heshima.
si unajua tena maisha yote aliyeshinda vita ndiye mwenye haki ya kuandika historia atakavyo, inawezekana watu wa mgaharibi (western faction) walimwenkea ngumu asipewe heshima
 
chukua assignment nyengine itakayokusaidia kufikisha angalau alama 16 za kufanyia mtihani wa mwisho.
AGE OF WARRIORS DRAMA
kwa taarifa zilizothibitishwa na daemusin bin makinikiyya bin koroshow bin vipigo kwa shangazi zenu ni kwamba ndani ya drama hii hamuna muigizaji mwenye sura ya mvuto haijalishi ni mwanamke. :) :) :p :p .
hii drama episode 11 za mwanzoni ni mwendo wa kuchinjana kwa mapanga, shoka, iron ball n.k,
View attachment 1111637

kwa nini ikaitwa age of warriors?
kutoka mwaka 1170 hadi mwaka 1270 taifa la goryeo lilijikuta likiendeshwa kwa nguvu za kijeshi (goryeo millitary regime).
walikuwepo watemi watatu wakiongozwa na yi ui bang ambao ndio waliongoza mapinduzi ya kumuondoa mfalme aliyechaguliwa kwa nguvu za wananchi anayeitwa Uijong na hatimaye wakamweka madarakani mdogo wake aliyeitwa Myeongjong.

kwa takribani miaka 100 goryeo ilijikuta ikiendeshwa kwa njia hiyo, mfalme anakuwepo kama kawaida lakini nguvu ya kimaamuzi inabaki kwa mwanajeshi aliye na nguvu pamoja na ukoo wake.
kwa ufupi ilikuwa ni mwendo wa kupinduana mwanzo mwisho, si unajua nyakati hizo kila mwenye nguvu alikuwa na jeshi lake.
ujinga huu uliisha baada ya goryeo kukaliwa kimabavu na MONGOLIA.​

  1. yi ui bang na wenzake waliongoza mapinduzi na kumweka madarakani mfalme myeongjong​
  2. baadae siku za mbeleni mnamo mwaka 1174 jeong jung bu ambaye pia alishiriki mapinduzi ya mwanzo pamoja na yi ui bang alimuondoa madarakani mwenzake na kutoa amri ya kunyongwa kwa general yi ui bang (hakuna rafiki wa kudumu kwenye madaraka),​
  3. mwaka 1179 general gyeong dae seung ikawa ni zamu yake kutamba, huyu alimuondoa madarakani jeong jung bu huku akitoa amri ya kunyongwa kwa familia nzima ya general jeong bung ju (karma is bitch).huyu jamaa yeye akataka kurudisha serikali itakayoongozwa kwa sauti za wananchi lakini ikashindikana​
  4. mnamo mwaka 1183 nguvu za utawala zikahamia kwa yi ui min baada ya kifo cha gyeong.​
mfumo wa utawala ukaendelea hivyo hivyo kwa miaka mingi sana mpaka kuuliwa kwa Kim Jun (ukiangalia god of war drama imejaribu kuzungumzia maisha yake kutoka kuwa mtumwa hadi kuwa kiongozi mwenye nguvu wa goryeo).
kifo chake kilipelekea madaraka yarithiwe na kiongozi mwengine lakini hakudumu sana kwa sababu goryeo ilijikuta ikiwa chini ya himaya ya mongolia kwa miaka takribani 80.

ukifuatilia hali ilivyokuwa utagundua ya kwamba goryeo karne ya mwishoni ilikuwa inapumulia mashine kwa sababu royal family (wang clan) walikosa nguvu na ushawishi mbele ya koo nyengine zenye nguvu
View attachment 1111639
bado namtafuta hand some boy mtoto mwenye sura nyepesi kama makonda.
drama ime contained episode 158
Dah! Umeiandika kibabe!! Loo! Kweli nimeamini usipokuwa mshapu kwenye kufanya maswali assignment zitakuua maana zinakuja zimepangana.
Ndo kwanza Emperor wang nipo sehemu ya 4.
Sijakaa sawa unanipa hii.
 
Kweli, hata yule mshikaji wao aliyekuwa General.
Kwa taarifa yako.
Yi san anatajwa kama mfalme bora wa Joseon.
1. Yi do ( Sejong the Great)
2. Yi san ( JeongJo)
Hao best Kings wa Joseon.
Yeah wote nimewasoma hadi huyo Sejong ndo aliyegundua lugha na maandishi ya Hangul
Kuna hadi mji umepewa jina Sejong City na wizara karibu zote zimehamishiwa huko.
Walikuwa na mpango wa kuufanya mji mkuu badala ya Seoul
 
Yeah wote nimewasoma hadi huyo Sejong ndo aliyegundua lugha na maandishi ya Hangul
Kuna hadi mji umepewa jina Sejong City na wizara karibu zote zimehamishiwa huko.
Walikuwa na mpango wa kuufanya mji mkuu badala ya Seoul
Cha kushangaza wamelelewa na Wafalme wenye akili nyingi halafu na madikteta:

Sejong tewang, yeye alichukua nchi kutoka kwa Baba yake Taejong, Taejong aliamini kuwa Nchi inapaswa kuongozwa kwa mkono wa chuma, ikiwa kama ngao ya kuepusha migongano ya ndani, na kwa ajili ya ustawi wa taifa. Taejong aliwauwa Ndugu zake wa damu, pia kina Jeong Mong-Ju ( Poeun), Jeong Do-Jeon ( Sambong) n.k

JeongJo: alichukua nchi kutoka kwa Babu yake YeongJo( mwana wa Dong Yi), YeongJo pia aliongoza kwa mkono wa chuma, pia alikuwa ana wajali wananchi wake. na moja ya tukio la kukumbukwa alitoa amri kali na kupewa adhabu ya kifo mtoto wake Crown Prince( Yi sado) kwa kosa la kutakata kufanya mapinduzi.Ingawa jambo hili halipo clear sana, wengine wanadai Yi sado alisingiziwa na wengine wanasema yaweza kuwa kweli.
 
Daemusin : ttok ttok nugu eopso = Knock knock anyone there?
aminas : Knock knock i'm here, knock knock right there.

kuna yoyote aliye tayari kunishikilia (kuwa pamoja nami)
nahitaji kuwa na mtu, nahitaji kuondoa upweke
kila ninapoangazia kila pande za jf,
sioni mtu wote wamekimbia amebakia great conquer
nashindwa kuvumilia, tafadhali rudi (njoo) kwangu
sihitaji tena kuwa mpweke
kiukweli hata sifahamu mjinga wewe umekwenda wapi
idon't care about shit


where are you chingu?
ndio nini kwenda likizo bila ya kunipa taarifa ahjummaaa au nimegeuka maua ya msituni (wild flower)?

nimekuwa lonely kwa takribani wiki tatu lakini ok baada ya miaka mitatu my crown princess lee hi amekuja kuniondolea upweke siku ya leo.
 
Back
Top Bottom