Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Park Bo Young And Ahn Hyo Seop Talk About How They Approached Their Characters For “Abyss”
View attachment 1087964

ko se yeon ni msichana mrembo ambaye ni prosecutor, siku moja anapata ajali inayopelekea kifo chake lakini kwa maajabu ya jiwe (bead) fulani linaloitwa Abyss anajikuta anarudisha tena uhai wake huku akiwa na muonekano tofauti.

cha min ni mvulana anayeendesha kampuni inayojishughulisha na maswala ya uzalishaji na mauzo ya vipodozi, ni mcheshi, mchangamfu na pia ni kajanadume cha seoul, naye pia siku moja anapata ajali inayopelekea kifo chake na hatimaye pia anarudisha tena uhai wake kwa maajabu ya jiwe la abyss akiwa na umbile tofauti na la mwanzoni.

ko se yeon baadae anaajiriwa ofisi inayojishughulisha na utoaji wa huduma za kisheria huku cha min naye anaishia kuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo hiyo ya sheria.

kwa tafsiri isiyo rasmi:
Park Bo Young: nilikuwa nina wasiwasi mkubwa sana juu ya baadhi ya lines (mazungumzo) yatawafanya watazamaji wasijisikie furaha, hivyo basi niliamua kuzungumza na director ili baadhi ya lines zibadilishwe, drama yetu baadhi ya nyakati ni mwendo wa kuwa serious lakini pia wakati mwengine ni maudhui ya vichekesho (comical) zaidi.

ahn hyon seop: niwe mkweli muda wote nimekuwa katika hali ya kuwa na khofu zaidi inayotokanwa na uhusika wangu ndani ya drama hii (handsome and humble man). nafahamu itakuwa ni kichekesho ndani ya drama hii pindi utakaposhuhudia mabadiliko kati ya park bo young pamoja na uhusika wangu.

kwa mujibu wa mtandao wa asianwiki mwanzoni uhusika wa ko se yeon ameigiza mwanadada kim sa rang, uhusika wa cha min ameigiza an se ha a.k.a mzee wa vituko.

100 days my prince ndio drama yangu ya mwisho kuiangalia kwa drama zote zinazoonyeshwa siku ya jumatatu kupitia kituo cha Tvn, sijui kama na hii itafuata nyayo za 100 days my prince au itaingia kwenye mkumbo wa kuwekwa kwenye dustbin

mama fairy and the wood cutter drama
the crowned clown drama
he is psychometric

niliupenda uhusika wa ahn hyon seop kupitia drama inayoitwa 30 but 17 drama, nadhani ndio iliomfanya apate offer ya kuwa muigizaji mkuu kwa mara ya kwanza kupitia abyss drama.
Sunbae kuna kituo cha televisheni kinachoonesha kdrama?
 
Ilikuwa Capital na ITV zamani TBC nao wakajaribu 2014 siku hizi hata sijui maana si tumeondolewa channel za kwetu? (Local channels)

DSTV nilishawapa maoni mara nyingi lakini hawafanyakii kazi, wana kazi ya kutujazia machaneli ya hovyo ya Kichina ilhali wangeweka hata channel 1 tu ya Kikorea inayoonesha drama ingewabust sana maana watu wameamka sana na drama zetu hizi pendwa.
 
Basi juzi kuna mtu nimebishana nae alikuwa anaangalia wachina kwenye king'amuzi cha startimes ye kakomaa ni wakorea, nikamwambia hawa sio wakorea ni wachina akakomaa ni wakorea nikasema ok
 
Basi juzi kuna mtu nimebishana nae alikuwa anaangalia wachina kwenye king'amuzi cha startimes ye kakomaa ni wakorea, nikamwambia hawa sio wakorea ni wachina akakomaa ni wakorea nikasema ok

Huyo hawajui Wakorea, ukiwajua Wakorea wanavyoongea unaweza kabisa kuwatofautisha na Wachina.
Hata hivyo hawafanani sana...poleeee
 
Huyo hawajui Wakorea, ukiwajua Wakorea wanavyoongea unaweza kabisa kuwatofautisha na Wachina.
Hata hivyo hawafanani sana...poleeee
Mimi drama yoyote nikitupia tu macho hivi hasa historical najua tu hii ni Korean au sio. Alikuwa anaangalia zile walizowekewa maneno ya kiingereza sio kichina chenyewe
 
Mimi drama yoyote nikitupia tu macho hivi hasa historical najua tu hii ni Korean au sio. Alikuwa anaangalia zile walizowekewa maneno ya kiingereza sio kichina chenyewe

Yeah, siku hizi nao wana series zao kama Wakorea tena zinafanana sana.
Wewe uko kama mimi, sichukui hata dakika 1 najua ni Wachina.
Ila sasa sizipendi hizo series zao maana hazina uhalisia michosho tu.
 
kama yupo msulihishi wa migogoro tunaomba ajitokeze na mapemaa kabla ya hawa watu wawili hawajatoana roho, mimi kazi yangu itakuwa ni kurithi kizuka haijalishi ameachwa na spika wa bunge au professor Assad.
bado sijaoa mwanamke hata mmoja, nataka niache harakati za kuwa baba mchungaji.
View attachment 1088950
Hawa wana nini? Kuna drama wamecheza pamoja? Nampenda sana huyo baba mkwe jamani
 
kama yupo msulihishi wa migogoro tunaomba ajitokeze na mapemaa kabla ya hawa watu wawili hawajatoana roho, mimi kazi yangu itakuwa ni kurithi kizuka haijalishi ameachwa na spika wa bunge au professor Assad.
bado sijaoa mwanamke hata mmoja, nataka niache harakati za kuwa baba mchungaji.
View attachment 1088950

Mimi nimepumzika kuicheki, nataka siku nikiiangalia naiangalia wiki nzima.
 
Yeah, siku hizi nao wana series zao kama Wakorea tena zinafanana sana.
Wewe uko kama mimi, sichukui hata dakika 1 najua ni Wachina.
Ila sasa sizipendi hizo series zao maana hazina uhalisia michosho tu.
Wa-Thailand pia niliona drama yao moja inaita Brothers ipo quality sana.
Miye drama za awali za kichina nilizowahi kuziona ni Master of Tai chi, 7 swordsmen, Stranger hero, Lift in the sky, Destiny to love,Arrow n.k but drama yao niliyoona iko poa zaidi ni A fist within Four walls kwngu hii niliipa *5 na ilikuwa drama bora ya mwaka 2016.
Hahaha mwambie huyo kuna tofauti kati Jeoun Achimieyo na Zhang xhang hao.
 
kama yupo msulihishi wa migogoro tunaomba ajitokeze na mapemaa kabla ya hawa watu wawili hawajatoana roho, mimi kazi yangu itakuwa ni kurithi kizuka haijalishi ameachwa na spika wa bunge au professor Assad.
bado sijaoa mwanamke hata mmoja, nataka niache harakati za kuwa baba mchungaji.
View attachment 1088950
Huyo mzee upande wa kushoto si alitunzwa kama mwigizaji bora wa Drama ya Jeong do jeon. Alichorwa kama Lee Songgye.
 
aminas our captain,
the legendary god of vocals
the king of ballad amerudi tena mchana wa leo
GoodBye
You were on the corner of memory, Maybe this is the last Goodbye
I loved all the days I was together,
In the screen that has already stopped , You smile like summer.

Huu wimbo leo nitausikiliza mpaka maneno yote ya kikorea yajihifadhi kwenye ubongo wangu,
kuna hadithi fulani ya mpemba aliwahi kumuuza mbuzi wake kwa faida kubwa, furaha yake ikampelekea apande basi la abiria haliyakuwa hana safari muhimu.
Basi kondakta akawa anamuuliza "mzee unashuka wapi kwa sababu muda wote upo garini"
mzee akajibu " wewe jua bili yako tu ninaposhuka hapakuhusu, leo nataka nilikomoe hili gari lako"

sasa sijui nani alikomolewa siku hiyo kati ya gari au bwana mbuzi na fedha zake, kwa mujibu wa hadithi inasemekana mzee alirudi nyumbani na zawadi ya halua pekee

ramadhan kareem mpendwa
hivi tuende likizo ya muda mfupi?

Ramadhan Kareem Kwako Pia Chingu....

Inabidi Twende Lakini Sidhani!
 
Hivi kwanini Unamaneno Ivyiii.
 
Back
Top Bottom