M Z A N Z I B A R I
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 21,648
- 116,865
kuondoka kwa mtakatifu jumong kuliifanya kwanza Goguryeo ipoteze nguvu kwa Buyeo ambayo bado mfalme Daeso alikuwa ndio mtawala, tokea mwanzoni Buyeo haikupendelea kuona taifa changa la Goguryeo linakuwa na nguvu kubwa zaidi yao, hivyo basi kugawanyika kwa Goguryeo pia ulikuwa ni mwiba kwa ustawi wa Goguryeo mbele ya Buyeo, Han dynasty na makabila mengineo ukiiondoa Baekje ambayo isingelikuwa na nguvu ya kuivamia Gogoryeo kwa miaka ya mwanzoni.Baada ya kifo cha Jumong Gogryeo ilipoteza ushupavu wake hasa kwa Bakje ambayo ilianzishwa na Sosono.
Lakini baada ya mfalme Yuri kumkabidhi madaraka mtoto wake wa kiume aliyeitwa Muhyool taifa la goguryeo lilirudisha tena nguvu zake za mwanzoni, huyu muhyool alikuwa ni mjukuu wa nne wa jumong na alitunukiwa cheo cha crown prince akiwa na umri mdogo na hii ilitokana zaidi na kifo cha kaka yake Dojeol, pia alikuwa na kaka yake anaitwa hamyeong ambaye alivuliwa cheo cha crown prince na baba yake.
huyu muhyool ndiye aliongoza kampeni ya kuivamia buyeo ambayo ilikuwa onfire nyakati hizo chini utawala wa babu yake wa pili ambaye ni Daeso na kufanikiwa kumuua mfalme daeso, tukumbuke mama yake jumong aliolewa na baba yake daeso ambaye ni geumwa hivyo basi muhyool alimchukulia daeso kama ni babu yake.
huyu muhuni hakuishia hapo tu bali mataifa mengi ya jirani aliyabeba na kuitanua tawala ya goguryeo mpaka kufikia kubeba maeneno ya han china pamoja na naklang.
muhyool kama walivyo baadhi ya wafalme wengineo alipewa heshima ya DAEMUSIN (damushin = mungu wa vita).
mpaka hapa utaona ya kwamba baekje hawakuwa na nguvu ya kusimama na Goguryeo nyakati za mwanzoni.
kutoka jumong wa goguryeo hadi geunchogo wa baekje ni miaka takribani 300 imepita.