Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Eeeh bwana eeeh...
Ngoja niicheki hii nione je ndio konki drama kuliko zote kama mnavyosema?
Kama itaweza kuizidi Jumong basi nitanyanyua mikono juu.

Kwa maana hiyo basi Jumong alikuwa emperor bora ila aliangushwa na waliomfuata, sad!

Sent from my iPhone using JamiiForums[/QUOTE
Eeeh bwana eeeh...
Ngoja niicheki hii nione je ndio konki drama kuliko zote kama mnavyosema?
Kama itaweza kuizidi Jumong basi nitanyanyua mikono juu.

Kwa maana hiyo basi Jumong alikuwa emperor bora ila aliangushwa na waliomfuata, sad!

Sent from my iPhone using JamiiForums
Jumong inachoizidi hii ni utamu wa stori ila kwa Vita humu ndo kwao
 
kuna Drama naitafuta inaitwa Winter Sonata, nakumbuka ilikuwa inarushwa na ITV mwaka 2006. sikuweza kukaa na kuifuatilia nilikuja kupata nafasi na kuangalia episode kama 2 za mwisho. sijui nawezaipata wapi, kariakoo nimewauliza wauzaji wengi hawana kwanza nahisi hata hawaijui nikiwaulizaga wanaishia kunikodolea macho tu hahah. Wapi naeza ipata wadau
 
Hahahahahahahahahahahahhahaha!

Kama Kawaida Yako.

Ninafungua Mwaka Kwa Tabasamuu.

Ndomna Saraghaeyo My Lovely Chinguya...

Hahahaha! Uaga Unawaza Nini! lilikuwa Linakufurukuta Ila Ulimtafutia Muda.
gwenchanah gwenchanah.
nilijua atashindwa kunijnibu kwa sababu yale maandishi ukiyasoma kwa umakini utagundua ya kwamba ameyaiba halafu akayaweka humu ndani bila ya kuongeza au kupunguza chochote, na mara nyingi unapochukua idea ya mwenzako bila ya kuifanyia uchunguzi wa kina basi pindi unapokumbana na changamoto ndogo unakimbia pambano na ndicho alichokifanya yule mdau.
maisha yangu ya uhalisia siwezi kumtamkia hadharani maneno kama yale hata kama utaniwekea dau kubwa na ndio maana nilisita kwa takribani wiki nzima kutokujibu chochote.
ok yameshapita na sikupaswa kuyakumbushia nyakati hizi.
 
kuna Drama naitafuta inaitwa Winter Sonata, nakumbuka ilikuwa inarushwa na ITV mwaka 2006. sikuweza kukaa na kuifuatilia nilikuja kupata nafasi na kuangalia episode kama 2 za mwisho. sijui nawezaipata wapi, kariakoo nimewauliza wauzaji wengi hawana kwanza nahisi hata hawaijui nikiwaulizaga wanaishia kunikodolea macho tu hahah. Wapi naeza ipata wadau
Winter Sonata - Episode 20 English subtitles | Watch online and Download free on FastDrama

Ingia hapo cheki kama ni yenyew afu ipakue kama sio nenda kwenye menu hapo juu kwenye website itafute upya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pale Kwenye Misosi Mingii Panaitwaje!? Zenji
forodhani Gardens.
wabahili kama mimi tunaishia vibanda vya chipsi kwa sababu hatujazoea kununua mishikaki, pweza, kachori na vyenginevyo kwa kiingilishi, nadhani unafahamu fika bidhaa zinazouzwa kwa kiingilishi zinakuwa ni gharama ukilinganisha na zile zinazouzwa kwa lugha ya upembani na ujambiani.
1547072608664.png

Aigooooo, mbona like nilikupa?

Sikuweza kujibu wakati ule maana ningejibu nini? Umenipa suggestions ilibidi niangalie kwanza ndio nije na feedback kama hivi.

Nilianza kuangalia ile ya yule Dr kupitia link ya drama cool uliyoiweka mwishoni mwa ile post ila ilikuwa balaa, nimekutana na matangazo ya ajabu sipati kusema.
Nikaachia kwenye ep ya 3.
naomba unisamehe dada yangu kwa kukosa kwangu umakini, ile project niliichukua kupitia PC ya rafiki na sikukutana na matangazo ya ajabu nilipokuwa naiangalia sasa sijui kiupande wake aliichukua kupitia tovuti ipi.
DR heo jun alikuwa daktari wa mfalme seonjo na familia nzima ya kifalme, kwenye post zako za mbele unaonekana kuchukizwa sana na matendo ya mfalme seonjo wakati wa dhiki ndani ya nchi yake.
 
Consort sook choe(Dong Yi) alikuwa mwanamke bright kuliko hata Lady Ki wa Empress Ki Consort sook naweza kumuweka Chungu Kimoja na Daek Man(Queen Seon deok) Consort Hui(Jang ook Jang) aliambiwa atakuwa Kivuli hakuamini Mwisho wa siku akaomba poo si kwa Consort Hui alikuwa hajiwezi bali alikutana na mtu wa kutisha
ukimuondoa SOSEONO kiupande wangu mimi shujaa wangu wa pili kwa upande wa wanawake ni Empress Myeongseong (1851-1895), Wajapani walimuua baada ya kuzidi kuwa kikwazo kwao.
Empress Myeongseong - Wikipedia
 
Hii Last Empress inaonekana ni nzuri sana, nipo katika episode ya 5. Japo sipendelei kutazama drama ambazo hazijakamilika hii itanifanya nivunje huu mwiko hahahaah.
the last empress mpaka muda huu sijaona faida ya kuwa na episode 24. Sijaona mantiki yoyote ya malikia oh sunny kurudi tena ikulu kwa dhumuni la kuishi na mume wake ambaye alishamfanyia kitendo cha kishenzi.
episode 20 zingependeza zaidi.
 
kuna Drama naitafuta inaitwa Winter Sonata, nakumbuka ilikuwa inarushwa na ITV mwaka 2006. sikuweza kukaa na kuifuatilia nilikuja kupata nafasi na kuangalia episode kama 2 za mwisho. sijui nawezaipata wapi, kariakoo nimewauliza wauzaji wengi hawana kwanza nahisi hata hawaijui nikiwaulizaga wanaishia kunikodolea macho tu hahah. Wapi naeza ipata wadau
hii drama wajapani waliinunua kama bwana yule anavyonunua kunguru kwa ajili ya kusafirishia kitoweo, mhhhhhhhhh na kunguru alivyo mroho, mamamamaaaaaaaaa mara kitoweo chote atakula njiani.
mwaka 2004 utamaduni wa korea kupitia sanaa mizizi yake ilikuwa inaanza kwenda mbali zaidi, kupitia drama hii economic impact yake inakadiriwa kufikia 3 trillion won (S$3.7 billion).

nyakati zile unaambiwa kama bae yong joon angelikuwa na tabia kama za yule muimbaji wetu pendwa asiyeweza kuimba live na kudance muda huo huo basi nusu ya wasichana wa kijapan angelilala nao mbele (nimemnukuu mkuu wa nchi ya palestina alipowazungumzia mafisadi)
kuna stori fulani inadai ya kwamba mnamo mwaka wa 2004 jamaa alitembelea japani basi alipofika uwanja wa kunguru takribani wanawake 3000 wa kijapani walikuwa wanamsubria kwa ajili ya mapokezi.
waziri mkuu wa japan nyakati zile bwana JUNICHIRO KOIZUMI alinukuliwa akisema ya kwamba bae yong joon amekuwa maarufu ndani ya nchi yake kuliko yeye mwenyewe.
  1. Winter Sonata at Dramanice
  2. https://kissasian.es/Drama/Winter-Sonata/
tumuache bae aendelee na biashara zake huku pia akiendelea kuwa karibu na mama watoto wake.
1547076952185.png
 
Huyu nimekwisha kumuona kwenye Jing Birock sasa najiuliza hiyo drama yake itakuwa na jipya kweli?

Of course niliwahi kuisoma kiasi inaelezea maisha yake yote tokea kuzaliwa ila nimekosa hamasa kabisa ya kuiangalia.

Vipi ikoje Mkuu? Naona ina ep 104!
Hatari sana

Kama hutojali nipe list ya drama za kibabe za historical ukiachana na
Jumong
Dae Jo Young (Niliangalia hadi episode ya 30/40 hivi mwaka 2013 nikaiacha)
King Geunchoggo
Chunno

Napenda drama za kibabe zenye kutumia akili nyingi, thanks.

Sent from my iPhone using JamiiForums
hakuna umuhimu wa kuitafuta admiral yi soon shin kwa sababu utajikuta unarudia hadithi uliokwisha isoma ila imebadilishwa gamba la nje.
halafu huenda ikakukera kwa sababu video quality yake ni ya kiwango cha barabara ya mavumbi na project ilikuwa ni ya mwaka 2004
admiral yi soon shin bahati mbaya kila siku nazungumza humu ndani ya kwamba laiti kama angelizaliwa nchi za wazungu basi tungelilazimishwa kumsoma kupitia somo la historia tena kwa bakora kama mwalimu wa madrassa.

admiral anatufundisha ya kwamba mshindi wa vita hapatikani kwa resource nyingi alizonazo bali ni mipango imara ya kuweza kuzitumia resource ulizonazo haijalishi ni chache, baada ya kupewa msamaha na mfalme kuna vita fulani za mwishoni mwa uhai wake alipigana huku joseon wakiwa na meli 12 lakini jamaaa aliwachapa wajapani.

mwenzako ninapojisikia natamani kuona vurugu la yi soon shin basi hukipasha moto kiporo changu, nimefika episode ya 61 ambapo jamaa ndio anaongoza vita yake ya kwanza ya okpo akishirikiana na mpinzani wake general kyun won.

unamkumbuka yule general aliyeambiwa na konishi kwa usalama wake afungue njia ili japani wasonge mbele, hahahahaaaa alijibu
"kwangu mimi ni rahisi zaidi kupambana kuliko kufungua njia"​
nafasi ile ikinikuta mimi nitamwita konishi bwana mtakatifu usiye na dhambi naomba upite uelekee huko unakokwenda (chezea bunduki ya mjapani)
sasa lile tukio pia ukiiangalia admiral yi soon shin utaliona tena na mengineo mengii mpaka utaboeka kwa sababu stori umeshaifahamu.

shikamooo mzimu wa baharini admiral yi soon shin.
1547078225779.png
 
Ryu
Huyu ndiye muandishi mwenyewe wa Jing Birock hivyo ameweza kutendea haki na nimehasika sana na ujasiri wake wa kumkosoa mfalme bila kujali mfalme atachukua hatua gani dhidi yake!

Mfalme alikuwa mdogo mbele ya Ryu kiasi muda mwingi analia tu maana nyakati zote Ryu aliibuka mshindi wa mijadala na matokeo baada ya mijadala.
nilichompendea huyu great thinker ni kwamba licha ya kutokea upande wa "Eastern faction" lakini lilipokuja suala lenye maslahi na nchi hakuona tabu kuachana na siasa za kimatabaka na kuungana na "western faction" kwa lengo la kuipigania nchi yake tofauti na wanasiasa wengineo kama mzee yeon du su
wanasiasa wa sasa wanaposema mapambano ya kupigania maendeleo na maslahi ya nchi dhidi ya wanyonyaji hayana chama wala ukabila basi waonyeshe matendo yao ya ukweli kama alivyofanya ryu seong ryeon mnamo karne ya 16.
 
King Seonjo
Huyu mfalme amenifanya nitamani kuingia ktk drama mara nyingi nimtandike vibao! Ni mfalme mpuuzi na muoga ambaye sijawahi kuona drama yenye mfalme dhaifu kama yeye.
Nimeshangaa tuzo aliyopewa na MBC mwaka 2015 ya Best Actor... Au ni vile kaweza kuigiza kama mfalme goigoi? Lol

T
seonjo alikuwa anakwenda na mdundo wa muziki na ndio jambo lililopelekea kwa kiasi kikubwa joseon kuwa dhaifu, baadhi ya nyakati alikuwa karibu na wamagharibi na baadhi ya nyakati alikuwa karibu na wa mashariki. Joseon kwa nyakati zile ilimuhitaji mfalme mwenye sifa za ryu seong ryeong na si mfalme mwenye tabia za seonjo.
hivyo basi mara nyingi unakutia maamuzi anayofikia yanatokana na mawazo ya wanasiasa kuliko mawazo ya kwake yeye ndio maana alifikia hatua ya kudharau vitisho vya wajapani kwa sababu ya kuwasikiliza wanasiasa eti hawakuona dalili ya vita ijapokua ryu seong ryeong alikwisha toa maono yake ya nini kifanyike.
alikuwa ni mfalme wa ovyo kiupande fulani na pia ilichangiwa zaidi na kumsikiliza zaidi concubine wake kuliko wengineo.
 
Best drama ever if you like political/war drama I’ll highly recommend you this
unajua kwa nini leo nimeitembelea hii thread baada ya takribani siku 10 kupita?
jibu ni rahisi, nahitaji nikusaidie drama nyengine ya kuangalia kwa sababu nimeshaona dalili za uanaharakati kutoka kwako, ila tu chonde chonde karata zako zichange vizuri dada yangu yasije yakakutokezea ya bwana jung do jeon a.k.a sambong.
Kabla hujaanza kuifuatilia historical drama nyengineyo basi itafute hii lakini bahati mbaya kissasian haipo.

JUNG DO JEON (SAMBONG) : 2014 project
1547080408656.png

  1. Jeong Do Jeon at Dramanice
ukiiangalia hii picha kwa macho yote mawili utakutana na veterani actor watupu ambao wanafahamu maana halisi ya kuigiza historical drama. kama ilivyo jing bi rok drama na humu ndani vile vile hamuna muda wa mapenzi bali ni ubabe wa wanasiasa.
kama umewahi kuiangalia six flying dragons drama na ukaiangalia na hii itakuwa unatembea mule mule ila kwa asiyefahamu six flying dragons ni project ya mwaka 2015 wakati hii ni project ya mwaka 2014.

mwandishi wa six flying dragons kwa kiasi kikubwa anatulazimisha tuamini ya kwamba shujaa aliyefanikiwa kuiangusha goryeo na kuzaliwa joseon alikuwa ni yi bang won ambaye baadaye anakuwa mfalme wa tatu wa joseon (taejong) baada ya kufanya mapinduzi ya damu kwa ndugu zake na wapinzani wake, lakini shujaa wa ukweli ni huyu jamaa anayeitwa jung do jeon(sambong)
humu ndani utaona jinsi gani sambong alivyoweza kupambana kutoka mwanasiasa asiyekuwa na nguvu hadi akafanikiwa kumshinda waziri mkuu wa goryeo na mpaka kufikia hatua ya kuiangusha Goryeo kingdom na kuzaliwa Joseon akishirikiana na general yi seong gye. Kuna tabu nyingi sana alizipitia ikiwemo kugombana na rafiki yake kipenzi jung moong jo
best historical drama na hutojutia kuitazama nakuahidi.

  1. Jeong Do-jeon alizaliwa na kufariki (1337-1398), alikuwa ni mwanasiasa na mwanamapinduzi wa ukweli nyakati hizo za goryeo hadi joseon.
  2. ndiye alikuwa bwana mipango wa general yi seong gye ambaye ndiye mfalme wa kwanza wa joseon (taejo).Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1383 maeneo ya hamgyeong.
  3. walipofanikiwa kuiangusha goryeo alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa kwanza wa joseon.
  4. wakati joseon makao makuu yake yalipojengwa hanyang, sambong ndiye aliyependekeza ikulu ipewe jina la Gyeong bokgung.
sambong alijikuta akiingia kwenye mgogoro na Yi Bang-won kwa sababu ya vita ya urithi wa madaraka ambapo sambong kiupande wake hakuvutiwa na mtazamo wa kiuongozi aliyokuwa nao yi bang won.
  1. sambong aliamini ya kwamba serikali bora ni ile inayoongozwa na watu wote wakiwa na uhuru wa kutoa mawazo yao mbele ya kiongozi mkuu, sambong aliamini ya kwamba pindi kiongozi mkuu wa nchi anapoongoza nchi kwa ushirikiano wa watumishi bora aliowachagua basi hata kama mfalme ni mediocre basi siasa ataiweza. Dhana hii kiupande fulani ilipingwa na wapinzani wake ambao waliamini ya kwamba sambong alikuwa na mpango wa kujimilikisha madaraka kwa kumtumia mtoto mdogo wa yi seong gye. lakini hoja zao alizijibu ya kwamba mfalme ndiye mwenye mamlaka ya kunichagua mimi na pia ana mamlaka ya kuniondoa mimi hivyo basi kama ataniona ni tishio basi atakuwa na haki ya kuniondoa madarakani.hivyo basi aliamini kama yi bang won atashika madaraka ataongoza kwa mkono wa chuma.
  2. yi bang won na washirika wake waliamini ya kwamba kwa kuwa joseon bado ni taifa changa basi linamhitaji zaidi kiongozi atakayekuwa na msimamo ili aweze kulivukisha mbali taifa hilo kwa sababu bado waliendelea kujitokeza wanaharakati waliotaka kuirudisha goryeo. Vita ya watu hawa wawili wenye akili nyingi ilimalizwa kwa mapinduzi ambapo yi bang won aliwaua ndugu zake ambao walikuwa hawakubaliani kimtazamo na vile vile alimuua sambong na watu wake na kumtangaza kama ni msaliti wa nchi. yale aliyoyahofia sambong ndiye yaliotokezea wakati wa utawala wa mfalme taejong kwa miaka 18 ya utawala wake kwa sababu alitawala kidikteta, japokuwa alifanikiwa kuifanya joseon kuwa taifa imara kabla hajamuachia madaraka yote mtoto wake yi do (sejong the great). Nilichowapendelea zaidi wanasiasa hawa wawili ni kwamba wote walitaka kuyapigania maslahi ya wananchi na si matumbo yao

great thinker jeong mong ju na jung do jeon walikuwa ni marafiki sana nyakati hizo wanasoma pamoja mpaka kujiingiza kwenye siasa nyakati za goryeo. wawili hao kwa pamoja walikuwa na ndoto ya kuleta mageuzi kwenye utawala wa goryeo ambao uligubikwa na rushwa na ubadhirifu wa rasilimali nyakati za mwishoni.
bahati mbaya sana wawili hao walipoteana njia baada ya sambong kubadili msimamo wake wa kutaka kuirudishi heshima goryeo hadi kufikia hatua ya kuizamisha goryeo na kuanzisha joseon.
  1. sambong aliamini ya kwamba kwa hatua iliofikia goryeo hakuna uwezekano wa kuirudisha katika njia ilionyooka kama ndoto zao zinavyowaaminisha, bali njia pekee ni kuizamisha goryeo iliotawaliwa na ukoo wa WANG ( from emperoe wangun to.....). sambong aliamini ya kwamba taifa jipya chini ya kiongozi mpya atakayekuwa chini ya wanasiasa wanaokwenda na wakati ndiyo ukombozi wa wananchi.
  2. great thinker jeong mong ju aliamini ya kwamba kubadilisha jina la taifa kusingeliondoa uhalisia wa dhiki wanazokumbana nazo wananchi, kiupande wake aliamini goryeo hii inayoonekana kuchoka kama atapatikana kiongozi bora basi wananchi watayafurahi maisha, hivyo basi alikataa maoni ya sambong na wafuasi wake mpaka kufa kwake, bwana yule aliamini ya kwamba Tanzania kuipa jina jipya la Dubai haimaanishi chochote kiuhalisia kama viongozi wake hawaendani na jina la Dubai. msimamo wa bwana huyu ulikuwa ni mwiba mchungu sana kwa upande wa sambong na wafuasi wake kwa sababu yeye aliyekuwa ndio nguzo ya mwisho ya goryeo, hivyo basi kama jeong mong jo angeliachana na mkakati wa kuipigania goryeo na kuungana na sambong basi urafiki wao ungeliendelea kuwepo kama mwanzoni.
hatimaye Jeong Mong-ju aliuliwa mnamo mwaka 1392 kwenye daraja la sonjuk na aliyeongoza mauaji hayo ni yi bang won, nyakati hizo sambong alikuwa kifungoni kutokana na harakati zake za kuiangusha goryeo.
historia hadi leo inamtaja Jeong Mong-ju kama ni mzalendo wa ukweli aliyeamua kufa kwa ajili ya nchi yake ya Goryeo. kifo chake ndio ulikuwa mwisho wa taifa la goryeo kuendelea kuwepo kwani mwaka huo ndio taifa la joseon lilipoanzishwa.

siku chache kabla ya kifo chake vita ya maneno kati ya pande mbili hizo ilizuka ila kwa njia ya ushairi

yi bang won aliandika shairi lifuatalo
What shall it be: this or that?
The walls behind the temple of the city's deity* has fallen - shall it be this?
Or if we survive together nonetheless - shall it be that?

jeong mong ju naye akajibu
Though I die and die again a hundred times,
That my bones turn to dust, whether my soul remains or not,
Ever loyal to my Lord, how can this red heart ever fade away?

KBS DRAMA AWARDS:2014

  1. Daesang awards (muigizaji bora wa mwaka) : Yoo Dong Geun ambaye pia mwaka huu amebeba tunzo hii
  2. High Excellence Award in Acting :Jo Jae Hyun
  3. Excellence Award in Acting park Young Gyu
  4. Best Screenwriter :Jeong Hyun Min
ina maana hii drama ndio ilibeba tunzo ya ubora kwa mwaka 2014, mwaka 2015 drama ya jing bi rok the memoir of imjin war ndio ilibeba drama bora ya mwaka.
kwa maelezo zaidi tembelea tovuti hii
anyeong
 
Hizo nilizozibold zote nimeziona Chief, na kweli ni moto kwelikweli.
Drama ambazo zilinipa uchizi hapo sikuwa natamani kula wala kulala ni Jumong, Dong Yi na Queen Seondeok.

Hiyo King Gwanggaetto nitaipataje wajameni? Kwenye site yangu pendwa KissAsian hakuna!

Sent from my iPhone using JamiiForums
Jaribu kucheck na hizi
Shine or go crazy
Jackpot
Hwarang
Rebel
Flower in prison
Moon lovers
Ruler master of mask

King gwanggaetto unaweza kuidownload kupitia drama cool au dramafire

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unajua kwa nini leo nimeitembelea hii thread baada ya takribani siku 10 kupita?
jibu ni rahisi, nahitaji nikusaidie drama nyengine ya kuangalia kwa sababu nimeshaona dalili za uanaharakati kutoka kwako, ila tu chonde chonde karata zako zichange vizuri dada yangu yasije yakakutokezea ya bwana jung do jeon a.k.a sambong.
Kabla hujaanza kuifuatilia historical drama nyengineyo basi itafute hii lakini bahati mbaya kissasian haipo.

JUNG DO JEON (SAMBONG) : 2014 project
View attachment 991270

  1. Jeong Do Jeon at Dramanice
ukiiangalia hii picha kwa macho yote mawili utakutana na veterani actor watupu ambao wanafahamu maana halisi ya kuigiza historical drama. kama ilivyo jing bi rok drama na humu ndani vile vile hamuna muda wa mapenzi bali ni ubabe wa wanasiasa.
kama umewahi kuiangalia six flying dragons drama na ukaiangalia na hii itakuwa unatembea mule mule ila kwa asiyefahamu six flying dragons ni project ya mwaka 2015 wakati hii ni project ya mwaka 2014.

mwandishi wa six flying dragons kwa kiasi kikubwa anatulazimisha tuamini ya kwamba shujaa aliyefanikiwa kuiangusha goryeo na kuzaliwa joseon alikuwa ni yi bang won ambaye baadaye anakuwa mfalme wa tatu wa joseon (taejong) baada ya kufanya mapinduzi ya damu kwa ndugu zake na wapinzani wake, lakini shujaa wa ukweli ni huyu jamaa anayeitwa jung do jeon(sambong)
humu ndani utaona jinsi gani sambong alivyoweza kupambana kutoka mwanasiasa asiyekuwa na nguvu hadi akafanikiwa kumshinda waziri mkuu wa goryeo na mpaka kufikia hatua ya kuiangusha Goryeo kingdom na kuzaliwa Joseon akishirikiana na general yi seong gye. Kuna tabu nyingi sana alizipitia ikiwemo kugombana na rafiki yake kipenzi jung moong jo
best historical drama na hutojutia kuitazama nakuahidi.

  1. Jeong Do-jeon alizaliwa na kufariki (1337-1398), alikuwa ni mwanasiasa na mwanamapinduzi wa ukweli nyakati hizo za goryeo hadi joseon.
  2. ndiye alikuwa bwana mipango wa general yi seong gye ambaye ndiye mfalme wa kwanza wa joseon (taejo).Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1383 maeneo ya hamgyeong.
  3. walipofanikiwa kuiangusha goryeo alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa kwanza wa joseon.
  4. wakati joseon makao makuu yake yalipojengwa hanyang, sambong ndiye aliyependekeza ikulu ipewe jina la Gyeong bokgung.
sambong alijikuta akiingia kwenye mgogoro na Yi Bang-won kwa sababu ya vita ya urithi wa madaraka ambapo sambong kiupande wake hakuvutiwa na mtazamo wa kiuongozi aliyokuwa nao yi bang won.
  1. sambong aliamini ya kwamba serikali bora ni ile inayoongozwa na watu wote wakiwa na uhuru wa kutoa mawazo yao mbele ya kiongozi mkuu, sambong aliamini ya kwamba pindi kiongozi mkuu wa nchi anapoongoza nchi kwa ushirikiano wa watumishi bora aliowachagua basi hata kama mfalme ni mediocre basi siasa ataiweza. Dhana hii kiupande fulani ilipingwa na wapinzani wake ambao waliamini ya kwamba sambong alikuwa na mpango wa kujimilikisha madaraka kwa kumtumia mtoto mdogo wa yi seong gye. lakini hoja zao alizijibu ya kwamba mfalme ndiye mwenye mamlaka ya kunichagua mimi na pia ana mamlaka ya kuniondoa mimi hivyo basi kama ataniona ni tishio basi atakuwa na haki ya kuniondoa madarakani.hivyo basi aliamini kama yi bang won atashika madaraka ataongoza kwa mkono wa chuma.
  2. yi bang won na washirika wake waliamini ya kwamba kwa kuwa joseon bado ni taifa changa basi linamhitaji zaidi kiongozi atakayekuwa na msimamo ili aweze kulivukisha mbali taifa hilo kwa sababu bado waliendelea kujitokeza wanaharakati waliotaka kuirudisha goryeo. Vita ya watu hawa wawili wenye akili nyingi ilimalizwa kwa mapinduzi ambapo yi bang won aliwaua ndugu zake ambao walikuwa hawakubaliani kimtazamo na vile vile alimuua sambong na watu wake na kumtangaza kama ni msaliti wa nchi. yale aliyoyahofia sambong ndiye yaliotokezea wakati wa utawala wa mfalme taejong kwa miaka 18 ya utawala wake kwa sababu alitawala kidikteta, japokuwa alifanikiwa kuifanya joseon kuwa taifa imara kabla hajamuachia madaraka yote mtoto wake yi do (sejong the great). Nilichowapendelea zaidi wanasiasa hawa wawili ni kwamba wote walitaka kuyapigania maslahi ya wananchi na si matumbo yao

great thinker jeong mong ju na jung do jeon walikuwa ni marafiki sana nyakati hizo wanasoma pamoja mpaka kujiingiza kwenye siasa nyakati za goryeo. wawili hao kwa pamoja walikuwa na ndoto ya kuleta mageuzi kwenye utawala wa goryeo ambao uligubikwa na rushwa na ubadhirifu wa rasilimali nyakati za mwishoni.
bahati mbaya sana wawili hao walipoteana njia baada ya sambong kubadili msimamo wake wa kutaka kuirudishi heshima goryeo hadi kufikia hatua ya kuizamisha goryeo na kuanzisha joseon.
  1. sambong aliamini ya kwamba kwa hatua iliofikia goryeo hakuna uwezekano wa kuirudisha katika njia ilionyooka kama ndoto zao zinavyowaaminisha, bali njia pekee ni kuizamisha goryeo iliotawaliwa na ukoo wa WANG ( from emperoe wangun to.....). sambong aliamini ya kwamba taifa jipya chini ya kiongozi mpya atakayekuwa chini ya wanasiasa wanaokwenda na wakati ndiyo ukombozi wa wananchi.
  2. great thinker jeong mong ju aliamini ya kwamba kubadilisha jina la taifa kusingeliondoa uhalisia wa dhiki wanazokumbana nazo wananchi, kiupande wake aliamini goryeo hii inayoonekana kuchoka kama atapatikana kiongozi bora basi wananchi watayafurahi maisha, hivyo basi alikataa maoni ya sambong na wafuasi wake mpaka kufa kwake, bwana yule aliamini ya kwamba Tanzania kuipa jina jipya la Dubai haimaanishi chochote kiuhalisia kama viongozi wake hawaendani na jina la Dubai. msimamo wa bwana huyu ulikuwa ni mwiba mchungu sana kwa upande wa sambong na wafuasi wake kwa sababu yeye aliyekuwa ndio nguzo ya mwisho ya goryeo, hivyo basi kama jeong mong jo angeliachana na mkakati wa kuipigania goryeo na kuungana na sambong basi urafiki wao ungeliendelea kuwepo kama mwanzoni.
hatimaye Jeong Mong-ju aliuliwa mnamo mwaka 1392 kwenye daraja la sonjuk na aliyeongoza mauaji hayo ni yi bang won, nyakati hizo sambong alikuwa kifungoni kutokana na harakati zake za kuiangusha goryeo.
historia hadi leo inamtaja Jeong Mong-ju kama ni mzalendo wa ukweli aliyeamua kufa kwa ajili ya nchi yake ya Goryeo. kifo chake ndio ulikuwa mwisho wa taifa la goryeo kuendelea kuwepo kwani mwaka huo ndio taifa la joseon lilipoanzishwa.

siku chache kabla ya kifo chake vita ya maneno kati ya pande mbili hizo ilizuka ila kwa njia ya ushairi

yi bang won aliandika shairi lifuatalo
What shall it be: this or that?
The walls behind the temple of the city's deity* has fallen - shall it be this?
Or if we survive together nonetheless - shall it be that?

jeong mong ju naye akajibu
Though I die and die again a hundred times,
That my bones turn to dust, whether my soul remains or not,
Ever loyal to my Lord, how can this red heart ever fade away?

KBS DRAMA AWARDS:2014

  1. Daesang awards (muigizaji bora wa mwaka) : Yoo Dong Geun ambaye pia mwaka huu amebeba tunzo hii
  2. High Excellence Award in Acting :Jo Jae Hyun
  3. Excellence Award in Acting park Young Gyu
  4. Best Screenwriter :Jeong Hyun Min
ina maana hii drama ndio ilibeba tunzo ya ubora kwa mwaka 2014, mwaka 2015 drama ya jing bi rok the memoir of imjin war ndio ilibeba drama bora ya mwaka.
kwa maelezo zaidi tembelea tovuti hii
anyeong

Aigooooo!
Hivi mdogo wangu unafanya nini Bongo? Si uende tu huko kwa Wakorea wenzio?
Seriously unajua haya mambo kiasi cha kushangaza, wewe ni jembe la hii thread.

Bahati mbaya nimeshaanza kuangalia King Gwanggaetto, baada ya kumaliza kuangalia Jing Birock nilikuwa idle nikaona niicheki hiyo baada ya ushawishi kuwa mwingi.
Nikimalizana na hii nitaicheki hii, sina shaka na suggestions zako.

Yes, ninayo hiyo passion ya uwanaharakati ila tatizo ni ile nchi yetu mdogo wangu! Bora nibaki kujifunza na kuwa ‘admire’ akina Ryu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom