Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

mqaxy

Senior Member
Jul 10, 2018
166
250
Niko najivuta vuta na voice season 4 niimalize mara nasikia tena wana mpango wa season 5.

Hivi aliyewafundisha wakorea huu ujinga wa season ni nan?
Voice profiler center director Kang anajuaπŸ‘πŸ‘
Kama uliipenda Tell me what u saw "yule bidada alikuwa ni visual profiler"

Sasa kwenye voice unakutana na bidada ambaye ni "voice profiler"
Voice ipo poa twist zakutosha recommended kwa wapendaji wa SERIAL KILLER .
 

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
198,948
2,000
Kupitia google download application inaitwa vidmate kisha tumia hio app kuingia youtube usearch hio song utaivuta vizuri tu
Huyu Namgoong Min ni actor mmoja mzuri sana.

Anaeweza kunisaidia kuipata Sound track ya THE VEIL, inaitwa "Reason" aliyeimba anaitwa Yoari. Nimeitafuta Youtube nimeipata ila sijui namna ya kuidownload, anaeyejua namna ya kuipakua anielekeze.
 

The Happiness

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
6,838
2,000
Auntie tukimkamata aliyewafundisha wakorea mambo ya season tumchape viboko vikali sana shuain zake

Ulipoitaja marriage(love and divorce) nikasema aah wacha nimalizie hii season 2 aisee kumbe wao wana mipango mingine kama naiona season 3 ileeeeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Hahahaha Usiniambie.....mwenzio nimejivuta vuta nisimalize haraka nikujua ikiisha imeishaa kumbee laaah.....TumepatikanaπŸ˜‚πŸ˜‚
 

Papaa Gx

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
8,316
2,000
So unataka niwafuate wao wanavyo taka.!!!?? Hao watu wote nani kawatoa akili? Ama ni ww mwenyewe.

Mimi nimesema Squid Game no overrated full stop, hayo mengine utajua ww. Ama umekurupuka ku reply kwa mtu mwingine.
Acha mambo ya ajabu...watu wote wanaoisifia hawana akili ila wewe peke yako ndio unazo? Sema wewe hujaipenda sio eti utopolo.
 

Papaa Gx

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
8,316
2,000
Nkiri kama Nkiri
Aiseeeh hii THE VEIL ni moto bwana, zile promo za Innocent hazikuwa za uongo.Lakini pia nisiache kumshukuru aliyetuletea habari za Nkiri.Com humu, nimepinga mahesabu kupitia hiyo tovuti unaweza kudownload episode zaidi ya sita kwa GB moja tu, alafu Sasa zote ni Quality.

Mtiririko wa matukio kwenye hii drama ni wa kusisimua sana, watu walikuwa wanaifananisha na VAGABOND yes kwa upande wa genre ni sawa ila kwa ukali wa scenes THE VEIL remains at the top.Wahusika wamekaa vizuri kwenye nafasi zao.

Kinacho niumiza ni kuanza kuitazama hii drama ikiwa bado haijaisha (ongoing), nina tabia ya kutokuwa mvumilivu nikishaanza kutazama series.Ile Vagabond nilijitahidi kuisubiria mpaka iishe ila hii nimeshindwa kwa sababu ya mjinga mmoja Innocent dependent .


Hivi wabongo tutafikia lini level za wakorea kwenye kuigiza?
 

3 Angels message

JF-Expert Member
Aug 3, 2017
3,559
2,000
Anayejua muendelezo wa hizi series anisaidie nilianza kuangalia root of the throne nikapata muendelezo wake kwenye deep tree rooted inayofuata ndiyo nimeshindwa kuijua anayeifahamu anisaidie

Ila pia nahitaji historical korean drama nzuri maana hizi ndiyo nazikubali
 

DAEMUSHIN

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
16,067
2,000
Duh!, Huyo mzee kumbe ni konki kiasi hicho, ndio maana series zake, zinastori nzuri na hazichoshi.
So Hur Jun na Dae Jang Geum hawa watu walikuwepo historically au mmoja wapo alikuwepo, na huyo wapili ni nyongeza ya Producer?
historia ya uwepo wa heo jun haina tatizo lolote kwa sababu rekodi zote zinakubaliana na uwepo wake, kwa mfano ukisema heo jun hakuwepo tafsiri yake ni kwamba unapingana na uwepo wa kitabu cha tiba kinachotambuliwa na UNESCO alichokiandika mwenyewe kinachoitwa Dongui Bogam kikiwa na maana ya kiengereza Mirror of Eastern Medicine
heo jun alikuwepo nyakati za utawala wa mfalme seonjo (mfalme wa 14 wa Joseon) na chini ya utawala wake ndipo ulipotokezea uvamizi wa Japan (Imjin war).

Annals of the Joseon Dynasty ilifanikiwa kumtaja mara 10 dae jang geum kwa matukio aliohusika nayo, hivyo upo uwezekano naye jang geum alikuwepo kweli japokuwa kuna uhaba wa maandishi yanayomuhusu yeye kuanzia kuzaliwa kwake, mafanikio yake mpaka kifo chake.
rekodi za Annals of the Joseon Dynasty zinaonyesha uwepo wa jang geum chini ya utawala wa mfalme Jungjong (mfalme wa 11 wa Joseon)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom