Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako! | Page 64 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Discussion in 'Entertainment' started by Kazz0, Mar 22, 2015.

 1. Kazz0

  Kazz0 Member

  #1
  Mar 22, 2015
  Joined: Mar 15, 2015
  Messages: 48
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 15
  Kama wewe ni mpenzi wa Korean Dramas, karibu katika thread hii tupate ku share kuhusu kazi hizo hatari za mkorea.

  Tuambiane;

  - Ipi ni drama yako bora ya kila wakati kwako?

  - Ni ya aina gani? (Wengi tumezoea kusema za 'mjini' na 'vijijini')

  -Nini kinakuvutia sana katika hiyo Drama?

  Pia:

  - Nani ni Msanii wako Bora wa kiume na wa kike na baadhi ya drama alizoigiza?

  - Nani ni sexiest Actor au Actress kwa maoni yako?

  - Ipi ilikua Drama yako ya kwanza ya kikorea kuiona?

  - Ni Drama gani ya kikorea unaitafuta sana na unapata wakati mgumu kuipata? (Unaweza ukasaidiwa kuipata na mashabiki wengine)

  *Pia tumia thread hii kufahamishana kuhusu drama mpya zilizotoka au unayohisi ni nzuri ila haijapata umaarufu sana!!

  Karibu tujumuike! Saraghae! Kumooyo!!

  =========

  Baadhi ya Links za Dramas mbali mbali za Korea...;

  Be Strong Geum Soon

  Princess Ja Myung Go

  THREE DAYS (2014)

  Swallow the Sun

  Jumong

  King Guenchoggo

  =====

  Links za ku-download drama za Kikorea;

  - Watch Drama Online | Korean Drama | Japanese Drama | Taiwanese Drama | Hong Kong Drama | Chinese Drama
  - GoodDrama.Net


  ======

  Updated: Kwa mjadala na kubadilishana uzoefu kuhusu series za jumla za movies mbalimbali, za zamani na mpya, Unaweza pia kufuatilia UZI HUU hapa Series (Special thread)
  ..

  Kazi kwako.. Enjoy!
   
 2. komba05

  komba05 JF-Expert Member

  #1261
  Oct 27, 2016
  Joined: Jan 8, 2016
  Messages: 369
  Likes Received: 274
  Trophy Points: 80
  Umenena vema kabisaaaaa
   
 3. George Betram

  George Betram JF-Expert Member

  #1262
  Oct 27, 2016
  Joined: Oct 10, 2015
  Messages: 1,972
  Likes Received: 1,554
  Trophy Points: 280
  Dae Jo Yeong
  Me nilitumia link hiyo mkuu..!
   
 4. juan moses

  juan moses JF-Expert Member

  #1263
  Oct 27, 2016
  Joined: Feb 16, 2014
  Messages: 2,129
  Likes Received: 1,812
  Trophy Points: 280
  Naona Now Websites Nyingi Zimeanxa Kuiweka Mm Niliiangaliaga Zamani.
  Nilihaha.
  Good For You.
   
 5. Damushin

  Damushin JF-Expert Member

  #1264
  Oct 27, 2016
  Joined: Dec 15, 2015
  Messages: 1,251
  Likes Received: 4,902
  Trophy Points: 280
  wasifu wake naomba najua utakua umeiangalia
   
 6. Damushin

  Damushin JF-Expert Member

  #1265
  Oct 28, 2016
  Joined: Dec 15, 2015
  Messages: 1,251
  Likes Received: 4,902
  Trophy Points: 280
  mwengeso aliuliza swali ni yupi muigizaji bora wa historical drama kati ya CHOI SOO JANG na SONG IL KOOK, maana yake ya kwamba alitaka wachangiaji watoe hoja zao kwa kuangalia historical drama ambazo hawa waigizaji wamecheza na mimi nikawa ni miongoni mwa waliotoa mawazo yangu na nakumbuka sikutoa hata hoja moja au mfano hata mmoja unaohusu modern drama kama vile PRESIDENT, COMRADE, LOBBYIST, A MAN CALLED A GOD, TERMS OF ENDEARMENT,FERMENTATION FAMILY (kimchi family) kwa sababu hazihusiani na mjadala wetu.
  Pia hakuna umuhimu wowote wa mimi kurejea mawazo yangu niliyoandika huko nyuma,na pia nalazimika kuheshimu mawazo ya wenzangu hata kama tunatofautiana kimtazamo ila na wao pia wanapaswa kuheshimu mawazo ya wenzao.
  kwa ufahamu wangu mimi unaposhindanisha watu wawili au vitu viwili unatakiwa utoe tofauti zao (differentiation) ulizozigundua na mimi nilijaribu kuweka tofauti zao nilizozigundua kati ya hawa wawili choi oppa na il kook oppa kwenye post iliyopita.

  Mimi nilipotoa tofauti kati ya CHOI SOO JANG na SONG IL KOOK sikugusia kabisa suala la sura zao kwa sababu siamini kama sura ina nafasi kubwa sana unapowalinganisha wanaume. Pia mimi siamini kabisa ya kwamba eti song il kook amekuwa maarufu sana kuliko choi soo jang kwa sababu ndiye wa kwanza kumuona kwenye TV drama na pia kwa sababu ni handsome kuliko choi soo jang. nakumbuka niliandika ya kwamba wakati choi soo jang ni maarufu nchini korea mwenzake song il kook bado alikuwa ni rookie actor nchini mwao na hakuna mtu yoyote aliyefikiri kuwa song il kook atakuja kuwa ni muigizaji mkubwa tu,na uthibitisho wa hoja hii ni mwaka 2002 wakati choi soo jang alipata ofa ya kuigiza historical drama ya EMPEROR WAN GUN yenye episode 200 kwa sababu team ya ma director kwa muda mrefu walikwisha vutiwa na uwezo wa choi soo jang tufahamu hizi historical drama hususan zinazozungumzia three kingdom zinataka maandalizi na uzoefu mkubwa kwa muigizaji, sihitajiki kuandika ya kwamba choi soo jang alishinda tunzo ngapi kupitia drama hii na wala sihitaji kuzungumzia rate ya kila episode ilikuwa ni wastani wa asilimia ngapi kuangaliwa korea nzima.
  Emperor of the sea (haeshin 2004): mi naona tuanzie tena hapa hapa ambapo hii ilikuwa ni sageuk drama ya pili mfululizo kwa choi soo jang kuigiza kama muigizaji mkuu wa drama na pia ndio historical drama yenye episode kidogo kati ya drama zote alizocheza choi soo jang , pia hii ilikuwa ni historical drama ya kwanza kwa song il kook tena akiwa ni muigizaji msaidizi tena ni mpinzani wa muigizaji mkuu. huu ulikuwa ni mtihani tosha kwa song il kook kuwathibitishia madirector wa korea kuwa tayari anaweza na yeye kusimama kama muigizaji mkuu.
  Swali tunalopaswa kujiuliza:

  je ina maana song il kook ambaye alicheza kama ni mpinzani wa starring wa drama hii alishinda tunzo tatu tena ikiwa ni historical drama yake ya kwanza ni kwa sababu alikuwa ni handsome kuliko staring, je kwa sababu alipigiwa kura nyingi na wanawake, je alikuwa ni maarufu zaidi nchini mwao na duniani kuliko choi soo jang hali yakuwa mpaka 2004 hakuna drama hata moja aliyocheza kama muigizaji mkuu (starring) tena tayari akiwa na miaka 34?

  Kwa mtazamo wangu mimi nahisi hoja hizo hazihusiani kabisa ila nilicho kiona mimi ni kwamba song il kook alimfunika sana choi soo jang kwenye emperor of the sea licha ya nafasi yake kuwa ni serial killer na ndio hapo umaarufu wake ulipoanzia na ndio sababu ya kupata nafasi ya kucheza kwenye jumong.

  Nakumbuka hivi karibuni nilisoma post moja ilianzishwa kwenye jukwaa fulani hapa jamiiforums muanzilishi wa ile post akaandika ya kwamba choi soo jang na kim nam gil yule jamaa aliyecheza kama bidam kwenye queen seondeok ndio waigizaji wake bora wa drama,bahati nzuri nikazisoma comment zote za wachangiaji ili kuona hoja zao nilichokingundua wengi wao hoja zao ni zile zile ya kwamba hawa jamaa wawili ni wakali kwa martial arts(mapigano) na pia uyo jamaa aliyecheza kama bidam hafikishi hata historical drama mbili alizosimama kama muigizaji sasa sijui utapimaje ubora wa muigizaji kwa kuangalia drama moja tu tena kwa kigezo cha martial arts. ila kilichonivutia zaidi ni kwamba kuna mchangiaji mmoja anaitwa PRINCESS ARIANA ni mwanamke na yeye akaandika kuwa ni mshabiki mkubwa wa choi soo jang hata kwenye emperor of the sea kwa sababu yeye anapenda action kuliko mapenzi jambo ambalo liliwashangaza wachangiaji wengi wa kiume na nilipoendelea kumchunguza kwenye comment nyengine nikagundua kweli anapenda drama za mapigano kuliko urembo kwa hivyo si kila mwanamke ni mpenzi wa song il kook kama walivyosema wengine.

  Hii hoja ya martial arts tayari nilishaizungumzia na nilitoa mawazo yangu na nikasema hapa kwenye martial arts inategemea na director walivyoamua kuzitengeneza kwa mfano mimi siku moja nilikuwa naangalia behind the scene za six fly dragons na slave hunter jinsi wanavyopigana ni tofauti kabisa unavyoona kwenye drama, nakumbuka mwisho nilikubali kuwa choi soo jang anafiti zaidi kwenye zile drama zenye mapigano mengi kuliko song il kook.
  Swali la kujiuliza

  tunapowalinganisha choi soo jang na song il kook kwa kuangalia historical drama, je ina maana tuangalie tofauti moja tu ya martial arts ?
  kwa mtazamo wangu mimi nahisi hapana kwa sababu tofauti moja haitoshi kwa kuwalinganishia ndio maana nilijaribu kuweka na tofauti nyengine nilizozigundua mimi kati yao wawili,

  kwa mfano niligusia suala la maumbile yao na jinsi wanvyoweza kutumika katika sehemu tofauti, hapa nakumbuka nilisema kuna baadhi ya maeneo choi soo jang anamzidi song il kook na kuna baadhi ya maeneo song il kook anamzidi choi soo jang.nikatolea mfano choi soo jang anazitendea haki zaidi zile nafasi ambazo anaigiza kama ni mtu dhalili na baadae akapigania haki za wanyonge mpaka akawa ni mtu mwenye kuheshimika zaidi,pia nikasema maumbile yake na uzungumzaji wake ni wa kihisia zaidi jambo ambalo linamfanya avutie zaidi anapohamasisha jambo. Naamini kama utaiangalia vizuri DAE JO YOUNG naamini utakubaliana na mimi.


  Song il kook baada ya emperor of the sea alipata ofa ya jumong hii ilikuwa ni historical drama ya pili kwa song il kook kuigiza na ilikuwa ni drama ya kwanza kwa yeye kuigiza kama ni muigizaji mkuu,sasa naomba tujiulize tena kwanini drama hii ilikuwa ni maarufu dunia nzima,je ni kwa sababu song il kook alikuwa tayari ni maarufu nchini korea na dunia nzima, drama ya jumong ni dalili tosha ya kuonesha song il kook ni hodari si rahisi kwa mtu ambaye hakuwahi kuigiza kama muigizaji mkuu halafu kazi yake ya kwanza kama muigizaji mkuu ikaangaliwa na takribani 50% ya wakorea kila episode.

  Naamini ya kwamba tungelishuhudia tofauti kubwa sana kutokana na maumbile yao,uzungumzaji wao,na uigizaji wao kama

  1. Choi soo jang angelicheza kama yeom mun na song il koo angelicheza kama jang bogo

  2. Pia tungelishuhudia choi soo jang akipigwa na song il kook kama kigezo kitaendelea kuwa ni martial arts

  3. Pia tungeshuhudia tofauti kubwa kama Choi soo jang angelicheza kama prince jumong na song il kook angelicheza kama dae jo yeong.
  4. pia tungelishuihudia tofauti kubwa sana kama choi soo jang angelicheza kama prince muhyool
  Nakumbuka hoja nyengine nilisema ya kwamba choi soo jang si hodari linapokuja suala la romantic ukimlinganisha na song il kook, ila sijui kwa nini tofauti hii team choi soo jang hawaipendi., Korean drama awards zote zinazofanyika lazima pawepo kipengele cha best couples kama romantic si muhimu basi kipengele hiki kingeondolewa.
  Nikatoa na mfano kwenye emperor of the sea love triangle kati ya jang bogo,lady jung hwa na yeom mun.
  Mimi naamini bila ya muigizaji bora historical drama huwa hazivutii na ndio maana drama zote walizocheza choi soo jang na song il kook zimefanya vizuri kutokana na kuwa wote ni mahodari.
   
 7. buret-moses

  buret-moses Member

  #1266
  Oct 28, 2016
  Joined: Jan 12, 2013
  Messages: 6
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
 8. sojobizzy

  sojobizzy Member

  #1267
  Oct 28, 2016
  Joined: Oct 18, 2016
  Messages: 47
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 25
  Mkuu nichek 0787489392 tubadilishane madin kama hautakuwa nayo niliyonayo hapo chn
   

  Attached Files:

 9. sojobizzy

  sojobizzy Member

  #1268
  Oct 28, 2016
  Joined: Oct 18, 2016
  Messages: 47
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 25
  Mkuu nichek 0787489392 tubadilishane madin kama hautakuwa nayo hapo chn 1477675113575.jpg 1477675125627.jpg
   
 10. fansureboy

  fansureboy JF-Expert Member

  #1269
  Oct 28, 2016
  Joined: Mar 16, 2015
  Messages: 275
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 80
  Namba yng imeishia 99
   
 11. sojobizzy

  sojobizzy Member

  #1270
  Oct 28, 2016
  Joined: Oct 18, 2016
  Messages: 47
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 25
  Ungeniflash kwa hyo no coz sijaipata no yko
   
 12. baraka muyabi

  baraka muyabi Senior Member

  #1271
  Oct 28, 2016
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Mkuu mbona haina eng subtitles. .nime download episode 1..au mbele kuna eng subtitles
   
 13. George Betram

  George Betram JF-Expert Member

  #1272
  Oct 28, 2016
  Joined: Oct 10, 2015
  Messages: 1,972
  Likes Received: 1,554
  Trophy Points: 280
  Ina English subtitle kaka...
  Labda kama wamefanya madudu yao...
  Lakini mimi kipindi ninaicheki ilikua na subtitle..!
   
 14. baraka muyabi

  baraka muyabi Senior Member

  #1273
  Oct 28, 2016
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Washafanya yao ila nkiangalia online inakua na subtitle niki download haiji na subtitles
   
 15. mkorea

  mkorea JF-Expert Member

  #1274
  Oct 29, 2016
  Joined: Aug 16, 2016
  Messages: 279
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 80
  song il gook haihitaji drama nyingi kujua kama jamaa ni fundi chek emperor of the sea,jumong utaelewa namaanisha nini ila huyu bwana mdogo choi soo jang inahitaji mpenzi wa drama na kumuangalia kwa muda mrefu ili kujua kujua ukali wake. ata hyo martial arts mnayo yazungumzia ukiangalia mapigano ya song il gook katika jumong na emperor of the sea alipoigiza kama pirates utakubali show zake. ukiachana na uhandsome general appearance ya choi soo jang ni mtu mmoja wa kawaida ambae anafanya uigizaji ila kwa song il gook mim naamin ni uwezo wake bnafsi wa maisha yake halisi wa kila siku. kwa sis wapenzi wa korea drama za kijijin zenye fighting za kutosha song il gook katuanguasha ila ukitoka mzigo wake lazima ukae. thats why watu tunafanya kuziludia emperor of the sea, kingdom of wind na jumong ili tu :Dkama mmenielewa lakin
   
 16. barnabas masoko

  barnabas masoko JF-Expert Member

  #1275
  Oct 29, 2016
  Joined: Aug 8, 2016
  Messages: 907
  Likes Received: 399
  Trophy Points: 80
  Into the badland
   
 17. B

  Baba yenu JF-Expert Member

  #1276
  Oct 29, 2016
  Joined: Jun 17, 2016
  Messages: 1,058
  Likes Received: 1,393
  Trophy Points: 280
  Me siamin kama kuna series ya korea sijaangalia sahiz nafatilia current zinazotoka eps moja moja kama K2 wamefika eps 10
   
 18. sumuni samson

  sumuni samson JF-Expert Member

  #1277
  Oct 29, 2016
  Joined: Nov 27, 2015
  Messages: 380
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  Hivi imetoka nyingine ya mwenderezo
   
 19. cc12

  cc12 JF-Expert Member

  #1278
  Oct 29, 2016
  Joined: Jan 26, 2013
  Messages: 970
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 60
  hii ni ya kikorea kwan mkuuu
   
 20. Khantwe

  Khantwe JF-Expert Member

  #1279
  Oct 30, 2016
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 21,035
  Likes Received: 7,270
  Trophy Points: 280
  Si ndo hapo na mimi nimeshangaa khaaa. Maana mimi zinazotajwa hapa asilimia kubwa ni mpya kwangu na zile nilizoangalia zimetajwa chache sana
   
 21. B

  Baba yenu JF-Expert Member

  #1280
  Oct 30, 2016
  Joined: Jun 17, 2016
  Messages: 1,058
  Likes Received: 1,393
  Trophy Points: 280
  Nitajie ambayo unahisi sijaona? Nikupe mbinu ya kuzimaliza! Nenda kwa dramafire.com wao wamezipost kuanzia herufi A mpaka Z hivyo anza kuangalia kwa kuanzia herufu A within a year utamaliza mbona! Sasa mimi nimeanza ziangalia 2013 mpk leo unadhan nimefikia wap? Na mimi huu ndo ulev wangu! Muda wote naokuwa free kazi yangu ni drama
   
Loading...