Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

😂😂😂😂😂dada mtu anaogopwa mtaa mzima. Anafokea woote na kutishia kasoro kajamaa kamoja tu
reply 1988 drama nimesogea mpaka episode 7, kuna pambano la kibabe ilikuwa nalimalizia usiku na mchana hatimaye ikanilazimu nichukue likizo ya kuangalia wakorea. Alhamdulillah (shukurani kwa Mwenyezi Mungu) leo dae ni raia huru na nimeyaanza rasmi maisha ya uraiani.

sitakiwi kuwa na huzuni kwa sababu ya matukio yaliyokwisha pita, (kuna uzembe mmoja unaoepukika niliufanya ambao najiaminisha umechangia kurudi nyuma kiupande fulani japo sina uhakika), acha nisahau kwani napaswa kupambana na yajayo.
=================
episode 6 na 7 zimenivutia sana kwa sababu zimeanza kututoa rasmi kwenye huu ulimwengu wa kiurafiki, kifamilia, kiuwanafunzi, ujirani mwema mpaka kwenye ulimwengu wa kimahusiano na kwa sasa nachezeshwa mchezo wa unrequited love kwa kila angles (upendo wa upande mmoja).

  • binti anapenda yule na yule anampenda dada yake binti
  • dada yake binti anamtolea nje yule.
  • wewe unampenda binti na binti bado hampendi wewe
  • wao na binti bado hawaelewi kipi kinaendelea nafsini mwao, wao atafahamu fika si kila wakati atacheza baduk (kuna muda wa kuanzisha mahusiano)
===================
mapenzi ya upande mmoja si mapenzi bali na mateso: wasubiria jambo ambalo ni vigumu kujitokeza, wajitahidi kumtafuta mwanadamu asiyetaka kujionyesha kwako, masaa 24 unamfikiria mwanadamu ambaye hajawahi kukuwazia hata kwa sekunde moja (hana muda wa kufikiria bwana/ bibi yule anaendeleaje), wabaki ukijipa matumaini hewa kama mashairi ya wimbo wa jide commando (umepika chakula huli, usijigambe eti wampenda blah blah blah).

mapenzi ya upande mmoja ni zaidi ya vita: muda wote unajikuta ukipigana vita ya peke yako ya kihisia, kibaya zaidi vita hiyo huipiganii ukiwa ndotoni bali ni muda ule una fikra timamu, ni vita ambayo ni ngumu sana kushinda hadi pale adui yako atakapokufahamu na kuridhia ukitakacho, ni vita ambayo ni ngumu sana kumalizika (mpaka pale mpinzani wako atakaporidhia kujisalimisha kwako).

mapenzi ya upande mmoja ni zaidi ya kuvunjana moyo: mmoja anatoa na mwengine anapokea, mmoja anapenda na mwengine haonyeshi dalili ya kupokea upendo huo, mmoja anategemea muda wowote atapokea jambo fulani huku mwengine akilipotezea jambo hilo (either bila ya kujua au kwa kukusudia), mmoja yupo tayari kufanya lolote ili mradi atimize azma yake huku mwengine akiwa hana habari ya kinachoendelea.
hatimaye mmoja anabaki kulia kama mtoto aliyekosa maziwa huku mwengine ni mwendo wa kucheka, kutabasamu (kutuonyesha dimples kama vishimo vya kuchezea gololi).

=================================
acha niendelee kujichekea, niwaachie wenye mapenzi yao ya upande mmoja....
wewe endelea kuteseka kimya kimya kihisia (baridi yakuandama wewe, upepo wakuandama wewe) kama maiti wa baharini
1600431835809.png
 
Waaow welcome back uchambuzi mzuri zaidi.

Pole kwa changamoto zoote ulizopitia. Kila mtu alikumiss humu.

Doh! Kumbe ulikuwa huku na hukunitaarifu dada yako? Zawadi utazionea kny picha. Mie mzima sana salaams kwa Amina na Numbisa.
nitakutaarifu vipi haliyakuwa mpaka mawasiliano ya kimtandao yalikatwa na malaika corona.
Tafadhali uwe unapita Itaewon japo mara moja (kuna mgahawa fulani nilisahau chupa yangu ya maji, wakorea ni wakarimu sana huenda bado wamenihifadhia)
------------------------
Numbisa analea wajukuu
Amina ameolewa (sijui anaendeleaje)
 
images.jpeg-1.jpg

Hatimaye nimeimaliza HONG GIL DONG ilikuwa Drama nzuri sana, yaani inakupa hamu ya kuifuatilia tangu episode ya kwanza mpaka ya mwisho.
Uhusika wa binti Heo Yi nok kwenye hii drama umenikumbusha uhusika wa binti Sujin kwenye Drama ya LEGEND OF FOUR GODS, character zao zimefanana mno mpaka kujiuliza kuwa nani alitisha zaidi kwenye Drama yake aliyocheza.

Nimeianza INSPIRING GENERATION humu ndani ni mwendo wa mkong'onto tu.
japokuwa drama inaelezea ugumu wa maisha watu waliokuwa wakipitia wakati wa Korea Empire. ambapo kutokana na ugumu wa maisha watu walijiingiza kwenye biashara halamu, ili waweze kupata mahitaji muhimu.
images.jpeg-1.jpg
 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom