Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

kwangu mimi naweza nikasema hii ndo best Historical drama 2019 so far!!kuna ile scene bwana mdogo yule clown,kajifanya mfalme yupo na malkia nje palace wakaenda "kwa mama ntilie" malkia anashangaa mfalme kapajuaje hapa?wakati wanarudi usiku jamaa akapita sehemu wanauza zile compass,jamaa mfalme anajua ku negotiate bei vibaya mnoimefika wamekubaliana kulipa jamaa hela hana anamcheki queen!!View attachment 1291381View attachment 1291382

Sent using Jamii Forums mobile app
clowned Crown kama sijakosea
Ila kuna kuna single movie inaitwa masquerade nadhani iliyochezwa na lee byun hun ni same story na hiyo series
Kitu kilichonishangaza katika hii Drama ni jinsi Waandaaji walivyojaribu kuitofautisha na Masquerade Movie hususani kadri Storyline ilivyokuwa ikiendelea na utofauti ulizidi kuonekana.

Moja ya tofauti hizo ni hasa pale ambapo Mfalme wa kweli Lee Hun alipouawa hivyo kumfanya 'Mchekeshaji' Bw. Ha Sun kukichukua mazima kiti cha Ufalme kitu ambacho ni tofauti na kwenye filamu ya Masquerade.

Utofauti mwingine ni katika uhusika. Katika Movie ya Masquerade tunaona likitumika jina la Gwanghae wa Joseon kama Character ya Mfalme wa kweli kitu ambacho kilikuwa ni tofauti katika The Crowned Clown.

Scenes za kuchekesha na wakati mwingine kuhuzunisha zimesheheni humo ingawa kwa muono wangu naweza kusema kuwa Masquerade Movie imejaa vituko lukuki vya kukufanya ucheke ndani ya muda wa masaa mawili tu na dakika kadhaa.

Yote kwa yote, zote mbili yaani Drama pamoja na Movie, kila moja ilikuwa na uzuri wake wa kipekee.
 
Kwa wale wapenzi wa Projects mbalimbali kutoka TVN ama tvN basi kaa tayari kupokea kazi mpya kabisa inayokwenda kwa jina la 'BLACK DOG'.

Hii Project (Black Dog) inahusu maisha ya vijana wadogo ambao kwa jina maarufu hujulikana kama 'Teenagers' pamoja na maisha ya walimu wa shule katika harakati zao za kuwapatia hawa 'Teenagers' elimu iwapasayo.

Drama hii itakutoa hapo ulipo kama ni nyumbani, ofisini ama popote pale utakapokuwa ukiitazama na kukupeleka katika shule mojawapo ambapo utaweza kuona pia maisha ya walimu na mambo kadha wa kadha wanayoyapitia wakiwa shuleni.

Ndani ya Drama hii utakutana na mwanamke kijana ambaye anapata nafasi ya kuwa mwalimu kwa muda mfupi yaani 'Short-term' na anafanya vizuri sana kupigania wanafunzi waweze kuzifikia ndoto zao wakiwa shuleni.

Kwa waliopata kutazama Projects chache nyinginezo kama vile; The Beauty Inside ya mwaka 2018, Another Miss Oh pamoja na Dr. Romantic zote mbili za mwaka 2016 bila kusahau King's Daughter, Soo Baek-Hyang ya mwaka 2013, utakuwa ukimfahamu hata kwa muonekano tu mwanadada ajulikanaye kama Seo Hyun Jin ambaye utapata kumuona katika hii Project mpya ya 'Black Dog' kama muhusika mkuu ambaye ndiye huyo mwalimu mwenye bidii na juhudi kubwa niliyemzungumzia hapo awali.

Vilevile utakutana na wasanii wengineo wenye vipaji vya kipekee kama vile; Mwanamke wa makamo, Ra Mi Ran. Uwezo wake katika tasnia sihitaji kuusimulia sana, nadhani kwa waliowahi kutazama kazi nyinginezo kama vile; Reply 1988, Come Back Mister, The Miracle We Met, Avengers Social Club, The Heirs n.k. mtakuwa mkiufahamu vizuri uwezo wake.

Pia wapo wengine kama; Ha Joon, Lee Chang Hoon, Mzee wa makamo,Jung Hae Kyun na wengine wengi.

Project hii itaanza kuruka hewani panapo Desemba 16 mwaka huu yaani siku chache tu zijazo (wiki ijayo) ikipatikana mara mbili kwa wiki yaani Jumatatu na Jumanne kupitia kituo chako pendwa kabisa cha tvN.

Kaa chonjo!

1576328552546.png

1576329053646.png
 
ngoja niitafute movie yake niichek
Kitu kilichonishangaza katika hii Drama ni jinsi Waandaaji walivyojaribu kuitofautisha na Masquerade Movie hususani kadri Storyline ilivyokuwa ikiendelea na utofauti ulizidi kuonekana.

Moja ya tofauti hizo ni hasa pale ambapo Mfalme wa kweli Lee Hun alipouawa hivyo kumfanya 'Mchekeshaji' Bw. Ha Sun kukichukua mazima kiti cha Ufalme kitu ambacho ni tofauti na kwenye filamu ya Masquerade.

Utofauti mwingine ni katika uhusika. Katika Movie ya Masquerade tunaona likitumika jina la Gwanghae wa Joseon kama Character ya Mfalme wa kweli kitu ambacho kilikuwa ni tofauti katika The Crowned Clown.

Scenes za kuchekesha na wakati mwingine kuhuzunisha zimesheheni humo ingawa kwa muono wangu naweza kusema kuwa Masquerade Movie imejaa vituko lukuki vya kukufanya ucheke ndani ya muda wa masaa mawili tu na dakika kadhaa.

Yote kwa yote, zote mbili yaani Drama pamoja na Movie, kila moja ilikuwa na uzuri wake wa kipekee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu kilichonishangaza katika hii Drama ni jinsi Waandaaji walivyojaribu kuitofautisha na Masquerade Movie hususani kadri Storyline ilivyokuwa ikiendelea na utofauti ulizidi kuonekana.

Moja ya tofauti hizo ni hasa pale ambapo Mfalme wa kweli Lee Hun alipouawa hivyo kumfanya 'Mchekeshaji' Bw. Ha Sun kukichukua mazima kiti cha Ufalme kitu ambacho ni tofauti na kwenye filamu ya Masquerade.

Utofauti mwingine ni katika uhusika. Katika Movie ya Masquerade tunaona likitumika jina la Gwanghae wa Joseon kama Character ya Mfalme wa kweli kitu ambacho kilikuwa ni tofauti katika The Crowned Clown.

Scenes za kuchekesha na wakati mwingine kuhuzunisha zimesheheni humo ingawa kwa muono wangu naweza kusema kuwa Masquerade Movie imejaa vituko lukuki vya kukufanya ucheke ndani ya muda wa masaa mawili tu na dakika kadhaa.

Yote kwa yote, zote mbili yaani Drama pamoja na Movie, kila moja ilikuwa na uzuri wake wa kipekee.
mkuu mbna story inataka kufanana na “ruler, master of the mask" au ndio hio hio?

nmezmss sn historical drama nataka wknd hii niichek hata1..km unaijua hata moja kali share nami asee

地那天刚才妇产科☆
 
mkuu mbna story inataka kufanana na “ruler, master of the mask" au ndio hio hio?

nmezmss sn historical drama nataka wknd hii niichek hata1..km unaijua hata moja kali share nami asee

地那天刚才妇产科☆
Hapana mkuu, hiyo si Ruler, Master of the Mask.

Sifahamu ni Historical Drama zipi ambazo wewe umezitazama maana naweza kukutajia ambayo kumbe tayari umekwisha kuiona.

Mfano, umeshawahi kuiona hii hapo chini?
  • Rebel: Thief Who Stole the People
 
Habri zenu,

Hatimaye nimeweza kuimaliza Empress Chun Chu Drama
Ilikuwa na Episode 78.
@Daemusin mbona huyu Empress Chunchu Uhodari wake haujaelezwa kwenye Wikipedia?, Halafu, Huyu General Gang Jo pia rekodi ( wikipidia) zinaeleza moja kwa moja kuwa ndiye alihusika na kifo cha Mfalme Mokjong( Goryeo) wakati zile zilikuwa tetesi tu, lakini Gang Jo kutokana na Drama inaonyesha hakuhusika na mauaji ya Mokjong. Kwahiyo njoo na majibu kama utapa sosi nyingine vilevile.
huyu Gang Jo according to wikipidia, ina mtaja kama moja kati ya ma- General wa muda wote wa huko Korea.

Kwako mchangiaji mwingine katika hili.
 
hiyo drama nilifika episode 8.
hayo maswali yako tafadhali kaonane na watunza kumbukumbu waliopo maeneo ya pyongyang naamini watakusaidia.
ikiwa nashindwa kumfahamu demu wa kwanza wa baba yangu nitaweza kuyafahamu maisha ya empress chunchu?

hebu nipishe bwana weeee.
long timeeee noo siiii burazaaaa.
 
Wapi Nikutengee Au Si Ahjumma Mimi!?
umeshasahau kama ulimwita dada yako prishaz humu ndani kwa sababu nilikuita ahjumma....

ninaye ahjumma mwengine nimpendaye
mwenye macho makubwa kama maandazi ya bihalima kibuno.
mwenye miguu mipana kama chupa ya chai.
mwenye nywele nyingi kama mtoto wa sanamu.
meno meupeee kama chumvi ya unga.

anipendae kuliko ukuta wa ikulu...
anidekezae kama mtoto wa kuku.
anajua kupika chapati na urojo kuliko mwanamke wa kihindi.
 
Crash Landing On You Ni Moto Mzee Baba.

Nimetoka Kuimalizia Now Episode 2 Ni Cheche.
yes, nilikuwa kwenye likizo ya muda mfupi ila nimerudia tena ulevi wangu
nimeiangalia muda mchache uliopita kama wewe
mwanzoni nilitaka kushangaa inakuwaje hyun bin anaigiza uhusika wa mwanajeshi mlalahoi, nimeshamzoea kumuona kwenye drama anaigiza kama mtoto wa kitajiri (chaebol) anayesimamia kampuni kubwa.

daebak, kumbe ni mtoto wa generali mwenye nguvu ndani ya ardhi ya korea ya kaskazini.
 
Back
Top Bottom