Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kazz0

Member
Joined
Mar 15, 2015
Messages
48
Points
95

Kazz0

Member
Joined Mar 15, 2015
48 95
Kama wewe ni mpenzi wa Korean Dramas, karibu katika thread hii tupate ku share kuhusu kazi hizo hatari za mkorea.

Tuambiane;

- Ipi ni drama yako bora ya kila wakati kwako?

- Ni ya aina gani? (Wengi tumezoea kusema za 'mjini' na 'vijijini')

-Nini kinakuvutia sana katika hiyo Drama?

Pia:

- Nani ni Msanii wako Bora wa kiume na wa kike na baadhi ya drama alizoigiza?

- Nani ni sexiest Actor au Actress kwa maoni yako?

- Ipi ilikua Drama yako ya kwanza ya kikorea kuiona?

- Ni Drama gani ya kikorea unaitafuta sana na unapata wakati mgumu kuipata? (Unaweza ukasaidiwa kuipata na mashabiki wengine)

*Pia tumia thread hii kufahamishana kuhusu drama mpya zilizotoka au unayohisi ni nzuri ila haijapata umaarufu sana!!

Karibu tujumuike! Saraghae! Kumooyo!!

=========

Baadhi ya Links za Dramas mbali mbali za Korea...;

Be Strong Geum Soon

Princess Ja Myung Go

THREE DAYS (2014)

Swallow the Sun

Jumong

King Guenchoggo

=====

Links za ku-download drama za Kikorea;

- Watch Drama Online | Korean Drama | Japanese Drama | Taiwanese Drama | Hong Kong Drama | Chinese Drama
- GoodDrama.Net


======

Updated: Kwa mjadala na kubadilishana uzoefu kuhusu series za jumla za movies mbalimbali, za zamani na mpya, Unaweza pia kufuatilia UZI HUU hapa Series (Special thread)
..

Kazi kwako.. Enjoy!
 

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
2,033
Points
2,000

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
2,033 2,000
Mpo wapendwa katika Tasnia!!!

Baada ya mapumziko ya muda mrefu nadhani ni muda muafaka wa kurejesha ari na nguvu bila kusahau kasi ya ule upepo maarufu ili kufuatilia Projects mbalimbali za Kikorea hususani zinazoendelea.

Miaka ya zamani huko siku za nyuma, enzi hizo karne na karne, robo milenia, nusu milenia ama milenia nzima, enzi za mababu bila kusahau mabibi waliwahi kusema;

"Nyota njema huonekana asubuhi."

Ukijaribu kuutumia msemo huu hususani kupitia hizi Drama zetu pendwa pale ambapo unakutana na Project yenye Episodes mathalani 60 na kuendelea alafu unajaribu kuusoma mchezo kupitia Episodes chache za kwanza ama niziite "Episodes za asubuhi" ili zikupe hamasa au ari ya kuitazama Project nzima mpaka mwisho.

Hilo laweza kuwa jambo la kawaida kabisa kwa watazamaji wengi hasa pale ambapo soko likiwa limetawaliwa na 'utitiri' wa Drama ambazo kila mtazamaji angependa kuutumia muda wake kutazama kazi zilizo na ubora wa hali ya juu katika viwango vya kimataifa.

Lakini je, kuna ukweli wowote kuwa Episodes za mwanzo mwanzo au mwanzoni huwa ni kielelezo tosha kuwa Project nzima ni nzuri ama la?
 

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
2,033
Points
2,000

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
2,033 2,000
Hivi? cheo cha Mishil( Seju) kilikuwa kipi Haswa. ( Queen SeonDeok Drama).
Kuhusiana na huyo 'Mishil' kumekuwa na kautata fulani ambapo maswali mengi yameibuliwa na Wanahistoria kwamba kweli ali-Exist ama la.

Sababu mojawapo ni kukosekana kwa jina hilo kutamkwa katika nyaraka muhimu za kihistoria za 'Falme Tatu' za Korea, hapa nazungumzia Samguk Sagi bila kusahau Samguk Yusa. Mishil anatajwa ama historia yake inapatikana kikamilifu katika nyaraka za Hwarang almaarufu kama Hwarang Segi.

Kwa mujibu wa nyaraka za kihistoria za Hwarang, Mishil alikuwa ni 'Royal Concubine' na alikitumikia cheo hicho kwa awamu tatu tofauti, yaani kwa Wafalme watatu tofauti. Hapa nawazungumzia Wafalme wa Silla; Jinheung, Jinji na Jinpyeong. 

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
2,033
Points
2,000

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
2,033 2,000

Forum statistics

Threads 1,364,458
Members 520,742
Posts 33,317,106
Top