Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kuna Kitu Nakuwa sikielewi, Drama Ipi Iko Sawa King's Dream( Dream Empire) au The Great Queen SeonDeok.
Hizi Drama zote zinaeleza Nyakati za Queen SeonDeok.
Queen SoenDeok Drama inaeleza Kuwa Bidam alikufa nyakati za Queen SeonDeok kwa Uhasi while King's Dream drama inasema jamaa alikufa Nyakati za Queen JinDeok tena Bidam alikuwa General huko Mipakani na alinyongwa kwa Uhaini.
Ipi iko saww?
Hata Uhusika wa Chunchu unachanganya.
Vyanzo vingi vya kihistoria vinakielezea kifo cha Bidam nyakati ambazo Queen Seondeok alikwisha kufa, mapema sana wakati uasi unaanza rasmi.

Na baada ya kifo cha Seondeok, kiti cha Ufalme kilichukuliwa na binamu yake ambaye ndiye huyo Jindeok ambaye alikipokea kijiti na kuendeleza mapambano dhidi ya waasi (akina Bidam) mpaka pale uasi huo ulipofutiliwa mbali.

Kwa maana hiyo nadhani, King's Dream Drama imefuata mtiririko huo tofauti na Queen Seondeok Drama ingawa kwa upande wangu Queen Seondeok Drama inasimama vizuri zaidi.

Pia, waandaaji wa Projects husika huwa wanajaribu kuipangilia 'Storyline' ili iweze kumuwakilisha zaidi mhusika mkuu katika Project hiyo. Na ukitazama Drama hizo zote mbili zinaelezea maisha ya watawala wawili tofauti katika nyakati tofauti hivyo basi kunakuwa na ulazima wa Project husika kujikita zaidi katika maisha yao mpaka mwisho.
 
Episode za mwanzo ni kama reception, pale ndio mahala pa kukufanya upate hamu ya kuendelea na Drama, nikitumia uzoefu wangu Historical Drama, Maranyingi sana huwa mtindo wa kuanzia mwisho kurudi mwanzo ili uende mwisho( Nadhani hii ndo waswahili mwaita MSAGO), huu mtundo huumpa kiu mtazamaji kuona kipi kilichotokea. Zile Drama zinazoenda moja kwa moja zinahitaji nguvu kubwa ya akili ya mtayarishaji ili akushawishi ili msafiri wote ki- Fikra mpaka mwisho.
 
sijui ndio hii uliokusudia

Naam... shukrani!!
 
Back
Top Bottom