Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kazz0

Member
Joined
Mar 15, 2015
Messages
48
Points
95

Kazz0

Member
Joined Mar 15, 2015
48 95
Kama wewe ni mpenzi wa Korean Dramas, karibu katika thread hii tupate ku share kuhusu kazi hizo hatari za mkorea.

Tuambiane;

- Ipi ni drama yako bora ya kila wakati kwako?

- Ni ya aina gani? (Wengi tumezoea kusema za 'mjini' na 'vijijini')

-Nini kinakuvutia sana katika hiyo Drama?

Pia:

- Nani ni Msanii wako Bora wa kiume na wa kike na baadhi ya drama alizoigiza?

- Nani ni sexiest Actor au Actress kwa maoni yako?

- Ipi ilikua Drama yako ya kwanza ya kikorea kuiona?

- Ni Drama gani ya kikorea unaitafuta sana na unapata wakati mgumu kuipata? (Unaweza ukasaidiwa kuipata na mashabiki wengine)

*Pia tumia thread hii kufahamishana kuhusu drama mpya zilizotoka au unayohisi ni nzuri ila haijapata umaarufu sana!!

Karibu tujumuike! Saraghae! Kumooyo!!

=========

Baadhi ya Links za Dramas mbali mbali za Korea...;

Be Strong Geum Soon

Princess Ja Myung Go

THREE DAYS (2014)

Swallow the Sun

Jumong

King Guenchoggo

=====

Links za ku-download drama za Kikorea;

- Watch Drama Online | Korean Drama | Japanese Drama | Taiwanese Drama | Hong Kong Drama | Chinese Drama
- GoodDrama.Net


======

Updated: Kwa mjadala na kubadilishana uzoefu kuhusu series za jumla za movies mbalimbali, za zamani na mpya, Unaweza pia kufuatilia UZI HUU hapa Series (Special thread)
..

Kazi kwako.. Enjoy!
 

Daemusin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
7,069
Points
2,000

Daemusin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
7,069 2,000
Mungu ametupa uwezo wa kuweza kutambua hisia tulizonazo na hata zile hisia za wenzetu wanazokumbana nazo kila siku, kadiri ninapoiangalia when the camellia blooms mawazo mengi hunijia kichwani mwangu (mawazo hasi na chanya).

hisia za kimapenzi zimebeba maajabu makubwa sana, unaweza kuwa na uhusiano wa muda mrefu na mwenza wako lakini akashindwa kukupa furaha ndani ya nafsi yako na ukamuona si chochote kwako, ajabu zaidi kwa muda mchache unaweza kujikuta unaanza kuvutiwa na mr/ mrs x ambaye ameanza kukufanya uwe na amani ya nafsi ulioikosa kwa bwana / bibi yule kwa muda mfupi muliofahamiana.

sitoshangaa tena kuwaona wadau humu ndani wanaanzisha mahusiano ya kimapenzi japokuwa wanafahamiana kwa njia ya keyboard, hisia za mapenzi ni zaidi ya biashara ya kujichua inayopumbaza na kulemaza (nimekusudia kujichua mgongo jamani)

daemusin na gong hyo jin ni marafiki kuanzia leo, utakapomuona daemusin ndio umemuona gong hyo jin.
wanaojipendekeza kwa daemusin / gong hyo jin wakome na wachakae.
nataka niachane na imani ya buddha kumbe mapenzi yana raha na utamu kuliko pilau la krismasiaaa nililoalikwa na Khantwe ahjummaaaa.

kang ha neul humu ndani amebeba uhusika wa ajabu sana, jamaa ni mwehu mnooooo.

sielewi ni sababu ipi inayowafanya wazazi waliotelekezwa kimahusiano wawe ni wagumu sana kuzipokea hisia mpya za
kimapenzi kutoka kwa wengineo iwe ni mwanamke au mwanamme, nafahamu kuna uoga fulani huja pindi unapopitia ugumu kutelekezwa kihisia na mwenza wako wa mwanzo lakini binadamu hatufanani bwanaaaaa.
hivyo basi si sahihi hata kidogo kutuangushia nyumba ya lawama wengineo tusiohusika na breakup zenu pindi tunapoamua kuwatokea kwa lengo jema la kuanzisha mahusiano.

jamani bongo movies mpaka stori nyepesi kama hii munashindwa kutengeneza, location za uswahilini, mavazi ya ushwahilini, maisha ya uswahilini, mpaka vyakula vya uswahilini.
mdogo mdogo tumeshagonga 10% kwa kuangaliwa kila siku ya jumatano na alhamisi.

single mother oyeee = when the camellia blooms drama.
single father oyeee = one night spring drama.
1570549294014.png
 

Daemusin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
7,069
Points
2,000

Daemusin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
7,069 2,000
Lee Byung Hun, Han Ji Min, Nam Joo Hyuk, Shin Min Ah, And More Confirmed For New Drama
On October 8, Lee Byung Hun, Han Ji Min, Shin Min Ah, Bae Sung Woo, and Nam Joo Hyuk were confirmed for “HERE” (working title).

It is reported to tell the story of an international NGO (non-governmental organization), but additional details have not yet been revealed publicly. However, viewers are already anticipating the collaboration of top actors and Noh Hee Kyung, who is known for hit dramas such as “Live,” “It’s Okay, That’s Love,” and “That Winter, The Wind Blows.”

“HERE” is scheduled to begin filming in 2020..
=========================================================
nimebaki najiuliza hii ni drama au variety show?
nimezoea kuona variety show ndio zinawakutanisha celebrities maarufu kwa wakati mmoja na sio drama.

han ji min = si muigizaji mwepesi hivyo basi kivyovyote dau lake ni kubwa
shin min ah = dau lake pia ni kubwa.
nam joo hyuk = bwana mdogo pia anafanya vizuri kivyovyote dau lake ni kubwa kiupande fulani.

lee byung hun ndio usisemee, mwaka 2009 kupitia IRIS DRAMA season 1 inasemekana alilipwa bonus ya dolla millioni 1 na producer kutoka japan, miaka 9 baadae kupitia MR SUNSHINE DRAMA inasemekana alilipwa takribani $3.2 million kwa episode 24 alizoshiriki.

bila ya kusahau kuna gharama nyengine za uzalishaji.
1570559426617.png
 

Great Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2018
Messages
430
Points
1,000

Great Conqueror

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2018
430 1,000
wewe muhuni kutoka pyongyang unapaswa uwe na heshima mbele ya wazee wako wa kambo.
huyo babu director lee byung heon amezaliwa miaka 74 iliopita.
ameanza kufanya kazi tokea mwanzoni mwa miaka ya 70 na project zake takribani zote amefanya ndani ya shirika la MBC.
kuna project moja ameisimamia inaitwa 500 Years of Joseon (kuanzia mwaka 1983 hadi 1990) inajaribu kuzungumzia mtiririko wa matukio yaliotokezea ndani ya joseon kwa takribani miaka 500 ya kuanzishwa kwake.

kusimamia project kwaa miaka 8 si jambo la masihara hata kidogo.
View attachment 1226844
Pumbavu zake Huyu muhuni.
Anatuzo ngapi?!, na Hiyo Project ya miaka 500 ya Joseon ina episode ngapi?!
 

Daemusin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
7,069
Points
2,000

Daemusin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
7,069 2,000
BTW acha tabia yako yakufuta quotes zako kwangu dogo, nilikaa kimya zile nyingine ila ile ya juzi kwenye mabeki visiki nimesema hapana! Lazima nikuambie kama hivi
teh teh teh
tokea urudi kwa mara nyengine JF baada ya likizo ndefu umekuwa tofauti na ulivyokuwa mwanzoni na sababu za kuwa hivyo naomba ziendelee kubaki kwenye kiwiliwili chako (kiukweli hazinihusu), bahati nzuri hayo mabadiliko si peke yangu ninayoyashuhudia bali hata wadau wengine kupitia majukwaa tofauti wameuona utofauti wako (ule mzuka wa kuchangia umekuwa ni mdogo sana kiupande wako).

ndio maana hata kiupande wangu imenibidi nibadilishe mdundo wa muziki kama ulivyobadili wewe ili niendane na kasi yako na sifanyi hivyo kwa nia mbaya inayoongozwa na wivu, chuki zinazoambatana na hasira za kijinga.

ndio maana nimekuwa mzito wa kunukuu comment zako, kumention jina lako na hata niki replay sichukui muda nazifuta.

mawazo ya kijinga hunitawala kwa kiasi kikubwa sana (labda hii comment hata nikinukuu itakuwa namzingua huyu mwandamu hivyo basi bora niifute kabla hajaiona, nikimention jina lake pia itakuwa namzingua n.k)

dah! sikujua kama hali hiyo huwa haikufahishi ndio maana nimekuwa nikiendeleza hiyo tabia mbaya kwa zaidi ya mara moja.


samahani sana kwa hayo matendo yote ya kijinga jinga nilioyatenda huko nyuma, nafahamu wanadamu inatuwia vigumu sana kusamehe yaliopita kwa sababu ya maumivu kama alivyofanya prezidaaa japo kwa njia ya maigizo, pia naamini kuomba kwangu msamaha itakuwa ni sababu tosha ya kuitanua barabara yetu ya mahusiano kuanzia sasa, hakuna umuhimu wa kuifuta home page ya tovuti kwa sababu ya errors zinazotokana na server haliyakuwa button ya refresh ipo hapo juu.

Niruhusu niurefresh urafiki wetu unaoendelea kudumu kwa mwaka wa nne huu tokea nijiunge na JF haijalishi ni urafiki unaoongozwa zaidi kwa njia ya keyboard
 

Daemusin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
7,069
Points
2,000

Daemusin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
7,069 2,000
Nikuambiaje Upate Faraja!?
njia pekee ya kunipa faraja itakulazimu umwambie bwana jurgen klopp atupunguzie maumivu wiki mbili zijazo pale old trafford.
teh teh teh
========================================================
umekuwa ukinipa faraja kwa muda mrefu sana hivyo basi itakuwa unaendeleza tu tabia yako njema uliojaaliwa na muumba ,kwa hilo acha niendelee kukushukuru na kumuomba Mungu akutimizie haja zako zote ikiwemo ile ya kukupa mwanaume atakayezifahamu hisia zako zote za kimwili na kihuduma na si kukupa mwanamume atakayeongozwa zaidi na ashki za kimapenzi pekee (haja za kimwili).

usiku mwema mpendwa japokuwa sisi makapuku tunashindwa hata kuzitimiza ndoto zetu tunapokuwa usingizini ndio maana nimesita kulala mpaka muda huu japokuwa mvua inanyesha ikiambatana na upepo mzuri kama nipo maeneo ya Busan.
wengine wanaota usingizini wanatengeneza fedha za ukweli kwa kufanya biashara cha ajabu sisi wengine tukilala tunaota tunakojoa kitandani kama watoto wadogo.
teh teh teh siruhusa kucheka​
 

Daemusin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
7,069
Points
2,000

Daemusin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
7,069 2,000
My country inahusiana na Nini nipe kidogo story yake
takribani mwezi mmoja uliopita niliziona baadhi ya comment zako ukiwa unaulizia six flying dragons drama na je umeshaiangalia?

kama hujaiangalia nahisi utakuwa unajizingua pindi utakapoiangalia hiyo my country kwa sababu nahofia itakuacha na maswali mengi yasiokuwa na majibu kwako.

ili uendane na hadithi ya my country itapendeza zaidi uwe na ufahamu wa taifa la goryeo pamoja na baadhi ya characters kama vile yi seong gye, yi bang won, yi ban sok n.k
na huwezi kuzifahamu characters za hao wahusika kiundani zaidi kwa kurukia moja kwa moja kuiangalia my coutry drama bila ya kuangalia six flying dragons au jung do jeon drama.

nitatoa mifano kwa faida yako:
  1. kuna ishu iliopelekea vita ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya goryeo, vita hiyo ndio ilibadilisha muelekeo mzima wa dynasty ya goryeo, ukiangalia hiyo drama ya my country humo ndani utaona chenga nyingi kama huna uelewa nalo hili tukio ila kiupande wangu nafahamu kinacho na kitakachoendelea huko mbele kwa sababu ya uzoefu wangu haijalishi hadithi ya my country drama ni tofauti,
  2. nafahamu fika yi seong gye atabadilisha upepo wa vita na atakataa kuishambulia liaodong na hatimaye atageuza jeshi lake kurudi mji mkuu (it means that yi seong gye atakataa amri ya mfalme na kumpinga mfalme ni uasi, ili yi seong ye aepukane na kifo alilazimika apambane na jeshi la serikali likiongozwa na general mashuhuri anayeitwa choi young.
  3. Choi young anashindwa na hatimaye yi seong ye anabaki kuwa mtemi pekee anayeogopeka ndani ya goryeo
  4. kuna ishu ya mgogoro wa kurithi madaraka kati ya maprince wakiongozwa na yi bang won dhidi ya wenzake na bahati nzuri hiyo drama ya my country imeanzia hapo kwenye mapinduzi japokuwa hiyo drama imekosa characters muhimu sana kama vile sambong na poeun.

huo ndio ushauri wangu wa bure ninaokupa ila usisahau unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako ila ni faida kwa serikali kwa sababu kodi ya vilevi inaongezeka mara kwa mara.
==================================================
heshima kwake huyu mzee kim young chul, hajawahi kuniangusha hata mara moja tokea nianze kumfahamu kupitia IRIS 1,2 drama, wala hahitaji kupewa screen time kubwa ili athibitishe uwezo wake.

emperor wang guhn
the great king sejong
father is strange
iris drama and movies
jang yeong sil
criminal minds
sword and flower
princess man
seoul 1945
the innocent man
1570569034346.png
 

Nifah

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2014
Messages
26,641
Points
2,000

Nifah

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2014
26,641 2,000
teh teh teh
tokea urudi kwa mara nyengine JF baada ya likizo ndefu umekuwa tofauti na ulivyokuwa mwanzoni na sababu za kuwa hivyo naomba ziendelee kubaki kwenye kiwiliwili chako (kiukweli hazinihusu), bahati nzuri hayo mabadiliko si peke yangu ninayoyashuhudia bali hata wadau wengine kupitia majukwaa tofauti wameuona utofauti wako (ule mzuka wa kuchangia umekuwa ni mdogo sana kiupande wako).

ndio maana hata kiupande wangu imenibidi nibadilishe mdundo wa muziki kama ulivyobadili wewe ili niendane na kasi yako na sifanyi hivyo kwa nia mbaya inayoongozwa na wivu, chuki zinazoambatana na hasira za kijinga.

ndio maana nimekuwa mzito wa kunukuu comment zako, kumention jina lako na hata niki replay sichukui muda nazifuta.

mawazo ya kijinga hunitawala kwa kiasi kikubwa sana (labda hii comment hata nikinukuu itakuwa namzingua huyu mwandamu hivyo basi bora niifute kabla hajaiona, nikimention jina lake pia itakuwa namzingua n.k)

dah! sikujua kama hali hiyo huwa haikufahishi ndio maana nimekuwa nikiendeleza hiyo tabia mbaya kwa zaidi ya mara moja.


samahani sana kwa hayo matendo yote ya kijinga jinga nilioyatenda huko nyuma, nafahamu wanadamu inatuwia vigumu sana kusamehe yaliopita kwa sababu ya maumivu kama alivyofanya prezidaaa japo kwa njia ya maigizo, pia naamini kuomba kwangu msamaha itakuwa ni sababu tosha ya kuitanua barabara yetu ya mahusiano kuanzia sasa, hakuna umuhimu wa kuifuta home page ya tovuti kwa sababu ya errors zinazotokana na server haliyakuwa button ya refresh ipo hapo juu.

Niruhusu niurefresh urafiki wetu unaoendelea kudumu kwa mwaka wa nne huu tokea nijiunge na JF haijalishi ni urafiki unaoongozwa zaidi kwa njia ya keyboard

nazidi kuomba radhi kwa njia ya sanaa ya muziki, I hope kesho tutaamka vizuri tukiwa tumezungukwa na taswira ya tabasamu kupitia nyuso zetu na hata mioyo yetu.
Dear Young Broh, mbona hili suala nimekuwa nikilitolea ufafanuzi kila mara? Miaka imesogea mambo yamebadilika ikiwemo wingi wa majukumu ya kikazi na kifamilia yameongezeka kiasi ni ngumu kuendelea na ‘mzuka’ uleule wa kuchangia humu.

Ukitaka kujua mambo yamebadilika wako wapi akina Honey Faith, Mrembo By Nature, Ms. Lincoln, Heaven Sent,Brenda18 n.k?
Hao wote ndio tulikuwa kizazi kimoja ila kila mmoja kapotea na wachache waliopo wanachangia kwa uchache sana.

Wakati najiunga JF mwanzoni mwa 2014 nilikutana na nyuzi nyingi za members kuulizia wenzao, niliwashangaa sana waliokuwa wakiuliziwa like “Unawezaje kuacha kuitumia JF?” Lakini sasa nawaelewa, kila jambo lina wakati.
Hata wewe utafika wakati utatafutwa na kuuliziwa humu vilevile.

Anyways, sikuwa serious sana wakati naongelea suala la kufuta japo nilikuwa namaanisha.
Otherwise, bado nipo japo kwa kujikongoja ila nipo
 

Forum statistics

Threads 1,343,525
Members 515,078
Posts 32,787,439
Top