Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Nimepatwa Na Hisia Kali (Emotion) Baada Ya Episode ya Jana/Leo ya One Spring Night

Hii Drama Inanifunza Sana! Kati ya Drama Chache Zinazoacha Mafunzo Baada ya Kuziangalia

Kudos Kwa Producer and Director Na Writer Pia Maana Kazi si Ya Kitoto.
giseok ni mwanamme mwenzangu lakini baadhi ya nyakati huniudhi kutokana na kauli zake za kujifanya ndiye muathirika mkuu wa mahusiano ya kimapenzi dhidi ya Jae In.

Dunia ya sasa inamhitaji mwanamke mfano wa Jae in asiyekubali kuendeshwa kifikra mfu na mwanamme asiyekuwa na muelekeo, sielewi kwa nini wanawake munajishusha sana mbele ya wanaume mpaka kwenye masuala yale ambayo munapaswa mutoe maamuzi wenyewe, si ajabu kumkuta mwanamke anafikia hatua anamuuliza rafiki wa kiume
"nikanunue nguo gani ya ndani kwa hii pesa ulionipa?"

kauli za giseok nazo ni za kushangaza sana anapokuwa karibu na mwenza wake, hajui kutumia maneno ya kubembeleza ni mwendo wa command kama yupo jeshini, maneno yenye hekima yanachangia kwa kiasi kikubwa sana kurudisha amani kwenye mahusiano yaliopinda
ingia kwenye gari
njoo tuongee ndani ya gari
shuka kwenye gari
tunapaswa tufunge ndoa
siwezi kukuacha
nipo tayari kusahau yaliopita na wewe unapaswa usahau
come to your sense
mwanamme/ mwanamke anayechukulia maneno yake kuwa ni sheria ya kumuongozea mwenzake ni kirusi hatari zaidi ya ugonjwa wa ebola,hakikisha unamuepuka mwenye sifa hizo awe ni meee au keeee haijalishi maisha yake ni mboga 7.
hatokufikisha popote kimalengo uliojiwekea
one night spring drama kwa mara ya kwanza imeshika nafasi ya kwanza wiki hii kwa kuangaliwa nchini korea.​
 
Nimepatwa Na Hisia Kali (Emotion) Baada Ya Episode ya Jana/Leo ya One Spring Night
chengine nimevutiwa na kiss scene :p :p , tendo lake limefanywa kwa nidhamu ya juu sana kwa kuangalia zaidi character ya upole ya jiho na jung in.
kwa wale waliozoea kiss za kibabe kama za ji chang wook na park bogum wanaweza kudharau kitendo cha Ji-Ho, kiupande wangu nimevutiwa na first kiss.

haipendezi siku ya kwanza kujaribu tendo hilo munatumia nguvu kubwa mpaka munafikia hatua ya kutaka kuvuana nguo hadharani kwa uchu, ya nini kupapatuana utadhani munapeana ujumbe wa kukumbukana pindi munapozama kwenye TITANIC wakati kumbe ndio kwanza munaanza kufahamiana kwa kutumia viungo vyenu.

yule ni wa kwako nenda naye taratibu kama ulivyokwenda naye taratibu ulipokuwa ukimtongoza awe wa kwako, unakuta mee na keee wanafanya tendo la kiss mpaka inafikia hatua wanang'oana ulimi (pumbavuuu)
1135826
 
M

Maneno mazuri hayo
 
Apo Kwenye Kupapatuana 😂
Yaani we Si Mzima.
 
Ndomana Naipenda Sana Hii Drama! Ina Uhalisia Wa Hali ya Juu..

Vile Ji Ho Anavyomuonea Aibu Ji Min Yaani!
 
giseok ni mwanamme mwenzangu lakini baadhi ya nyakati huniudhi kutokana na kauli zake za kujifanya ndiye muathirika mkuu wa mahusiano ya kimapenzi dhidi ya Jae In.

Dunia ya sasa inamhitaji mwanamke mfano wa Jae in asiyekubali kuendeshwa kifikra mfu na mwanamme asiyekuwa na muelekeo, sielewi kwa nini wanawake munajishusha sana mbele ya wanaume mpaka kwenye masuala yale ambayo munapaswa mutoe maamuzi wenyewe, si ajabu kumkuta mwanamke anafikia hatua anamuuliza rafiki wa kiume
"nikanunue nguo gani ya ndani kwa hii pesa ulionipa?"

kauli za giseok nazo ni za kushangaza sana anapokuwa karibu na mwenza wake, hajui kutumia maneno ya kubembeleza ni mwendo wa command kama yupo jeshini, maneno yenye hekima yanachangia kwa kiasi kikubwa sana kurudisha amani kwenye mahusiano yaliopinda
ingia kwenye gari
njoo tuongee ndani ya gari
shuka kwenye gari
tunapaswa tufunge ndoa
siwezi kukuacha
nipo tayari kusahau yaliopita na wewe unapaswa usahau
come to your sense
mwanamme/ mwanamke anayechukulia maneno yake kuwa ni sheria ya kumuongozea mwenzake ni kirusi hatari zaidi ya ugonjwa wa ebola,hakikisha unamuepuka mwenye sifa hizo awe ni meee au keeee haijalishi maisha yake ni mboga 7.
hatokufikisha popote kimalengo uliojiwekea
one night spring drama kwa mara ya kwanza imeshika nafasi ya kwanza wiki hii kwa kuangaliwa nchini korea.​
Then Anajitia Kama Sijuh Mtu Gani Ambaye Ji Min Hawezi Muacha! Anachukua Udhaifu wa Ji ho Japo Si Udhaifu kama Akili yake Inavyomtuma Kuwatenganisha!

Maneno yake Muda Wote ya Kujikweza! Ndomna Hata Baba Ake Alimwambia Kua Ji Min Ni Yupo Vizuri Kukushinda Na Wala Huendani Nae.
 
wale watu wanajitahidi kuwasaidia watazamaji wasioelewa kiingereza lakini baadhi ya nyakati ni waongo.
vile vile wanajifanya too much know huku wakifikiria wateja wao wote hawafutilii maisha ya korean celebrities.

unaweza kumuongopea mdogo wangu kwa sababu hana muda wa kufuatilia korean media lakini huwezi kunidanganya mimi.

one day nilikuwa naangalia IRIS 2 miaka mingi iliopita basi nikamsikia mtangazaji anadai ya kwamba Jang hyuk na lee da hae ni wachumba na wameshatangaza ndoa.

jang hyuk ameoa takribani mwaka 2008, ina maana jang hyuk ameoa kabla ya tamthilia ya slave hunter haijatengenezwa.
jang hyuk ameoa kabla ya IRIS 1 haijatengenezwa sembuse IRIS 2.
mkewe jang hyuk si celebrity​
View attachment 1136096
lazima uchoke
 
Then Anajitia Kama Sijuh Mtu Gani Ambaye Ji Min Hawezi Muacha! Anachukua Udhaifu wa Ji ho Japo Si Udhaifu kama Akili yake Inavyomtuma Kuwatenganisha!

Maneno yake Muda Wote ya Kujikweza! Ndomna Hata Baba Ake Alimwambia Kua Ji Min Ni Yupo Vizuri Kukushinda Na Wala Huendani Nae.
one night spring drama inataka kufanana kwa kiasi fulani na terms of endearment drama ya mwaka 2004,
  • familia zote zimebarikiwa kupata watoto wa jinsia ya kike
  • zote zinajaribu kuonyesha udhaifu wa baba mzazi kwa matendo yake ya kujigeuza muuzaji wa watoto wake ili apate urahisi wa kuyaendesha maisha yake.
gi seok pamoja na shi hoon ni ndege wawili wenye kufanana kimatendo na wanastahili kuwa marafiki wa kudumu wapate kudumisha fikra zao mfu za kuwa mwanamke ni chombo kinachopaswa kutii amri ya muwekaji mafuta.
gi seok amekuwa ni bingwa wa kuwadanganya watu wake wa karibu kuwa mahusiano yake na jung in yanazidi kunawiri kama maua wakati wa kipupwe.

shin hoon ni mjanja mjanja anayetaka kuwaaminisha watu ya kwamba endapo atakapofanikiwa kuiongezea sehemu dispensary yake basi kuna uwezekano mkubwa wa kujiongezea kipato haliyakuwa anafahamu fika bila ya kujirekebisha kimatendo na kuzidisha uwajibikaji hata kama atajenga hospitali ya meno yenye ukubwa kama john hopkins ni kazi bure.

wote ni mabingwa wa kuweka ahadi za uongo kwa wenza wao, mara nyingi muongopeaji watu huwa na tabia ya kujisahaulisha kila dakika lile alilozungumza
nitabadilika, nitakuwa uwe mwanamke mwenye furaha duniani: ni maneno haya ni mepesi mno kutamkwa kwenye vinywa vya wahuni wale wawili.

If the rain no longer fell
And the flowers wasted to the ground
If the stars no longer shone
And the breeze died down
You and I, we could still be happy

If the writers lost their words
And the blue fell from the sky
And the dreamers lost their nerve
And the seas went dry
You and I, we could still be happy

If the world forgot to turn around again
And the winter never knew to change to spring
And the birds forgot to sing
We could still be happy

If I lost my memory and forgot my name
If the road that led back home could not be found again
If the fires burned out
And we could not stay warm
If the world forgot to turn around again
And the winter never knew to change to spring
And the birds forgot to sing
We could still be happy

The fallen rain may wash our home away
But we remain protected just the same
Always
We won't want for anything
 
Ndomana Naipenda Sana Hii Drama! Ina Uhalisia Wa Hali ya Juu..

Vile Ji Ho Anavyomuonea Aibu Ji Min Yaani!
anajaribu kumuonyesha jinsi gani anamheshimu, nataka nione mbeleni itatokezea kitu gani pindi familia jung in watakapogundua ji ho ni single father.
tumezoea sana kuona love story ya single mother
 
Arthdal chronicles ep 7

Tagon ni mwanadamu mwenye tabia na mipango ya kishetani ndio maana si ajabu kukuta baba yake alitamani kumuua ili jinamizi la kumzaa muhuni atakayeleta mtafaruku kwenye ardhi ya arthdal limuondokee, kinyume chake tagon kwa mara nyengine alimaliza uhai wa mzee wake mwengine baada ya kumuua mama yake hapo mwanzoni.

moja kati ya sifa kubwa ya igutu ni uwezo wao wa kujifunza kwa haraka sana pamoja na kuyazoea mazingira mageni kwa muda mfupi ndio maana si ajabu kumuona eunseom (song joong ki) anaweza kupigana kwa kutumia zana zilizotengenezwa kwa chuma eg panga, shoka haliyakuwa kwa miaka 20 ya kuzaliwa kwake hajawahi kuzishuhudia machoni mwake, si hivyo tu eunseom pia ana uwezo mkubwa wa kuendesha farasi haliyakuwa watu wa kabila la wahan kiupande wao wanamchukulia farasi kama ni kiumbe mfano wa kuku (hawamtumii kwa usafiri).
1136289

ndio maana pia si ajabu kumshuhudia saya (song joong ki) na yeye akiwa na chembe chembe za ukatili ambazo amejifunzia kutoka kwa Tagon anayemchukulia kama ni baba yake pamoja na Tanya ambaye anamchukulia ni kama mlezi wake (mama)
wote wawili hawaoni tabia kutoa uhai wa mtu anayewaekea kikwazo kwenye njia zao za kuyatafuta mafanikio yao ya kuitawala ardhi ya arthdal.

ninachokiona ni kitendo cha sanya kutaka kumtumia mwanadada tanya ili atimize malengo yake kama ilivyo tagon anavyomtumia taelha, na wakati huo huo tanya atataka kumtumia sanya kwa sababu tanya anamfahamu sanya kupitia ndoto alizokuwa anaziota eunseom (sijajua kama sanya na yeye ana uwezo wa kuona matukio ya mbeleni kwa njia ya ndoto kama ilivyo kwa mdogo wake eunseom)

sanya ndio kikoo kilichotabiriwa so that sijui kioo hicho kitatumika vipi:
je atakuwa kioo kwa kumsaidia tagon atimize ndoto yake ya kuiendesha dunia atakavyo huku akimsubiria baba yake amrithishe madaraka pindi tagon atakapochoka au kioo hicho kitabeba sifa ya mapinduzi ya kumuondoa nguvuni tagon na hatimaye sanya kujimilikisha madaraka ya arthdal.
si tunafahamu karma is bitch,
kama ilivyo tagon alivyomtoa uhai baba yake je na sanya atamtoa uhai bwana tagon?
tusisahau tagon ndiye aliongoza kampeni ya kumuua ragaz ambaye ni baba mzazi wa eunseom na sanya pamoja na mauaji ya kizazi kizima cha neandthal species.

sifikirii kama mapacha eunseom na sanya wataungana kwa pamoja kwa sababu ni watu waliokuzwa mazingira tofauti ya kitabia, mmoja anawajali wananchi wanaonyanyaswa na mmoja amekulia nyumba ya shetani mwenye kupenda harufu ya damu ya wanaonyanyaswa.

kongole kwa song joong ki kwa kutuonyesha sura mbili zenye kutofautiana kimatendo kwenye kiwiliwili kimoja.
1136291

  1. https://www2.ondramanice.tv/drama/the-chronicles-of-aseudal-detail
  2. https://kissasian.sh/Drama/Arthdal-Chronicles
 
Back
Top Bottom