Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Park Hyo Shin announcing that his 20th anniversary solo concert will take place this coming June

collaborations kati ya the king of ballad park hyo shin na composer jung jae il inakufanya usahau machungu yote ya kukosa top 4.
achana na mafundi wengine wa piano kama vile yiruma huyu jung jae il ni balaa na wameanza kufanya kazi kwa pamoja kuanzia wild flower nyakati hizo wanatoka jeshini, mwanzoni inasemekana jamaaa alimkatalia park hyo shin kufanya kazi pamoja kwa sababu alihofia park atafeli.

naweza kufuta nyimbo za waimbaji wote ila si gwiji park hyo shin, nimeshakuwa mgonjwa wa sauti yake..

Na Top 4 Ushaikosaa..

Hii Nyimbo Ilinipungizia Machungu Jana!
 
Son Ye Jin And Hyun Bin In Talks For New Drama From “The Legend Of The Blue Sea” Writer
Son Ye Jin’s agency MS Team Entertainment : ni kweli son ye jin amepata offer ya kushiriki kwenye drama lakini mpaka sasa hajatoa uamuzi wowote

Hyun Bin’s agency VAST Entertainment : ni kweli mteja wetu amepata offer lakini bado anafanya review ili kuangalia whether ashiriki au akatae offer hiyo.

muandishi Park Ji Eun ameshaandika project tofauti kama vile my love from another star, the producer pamoja na the legend of blue sea.

director Lee Jung Hyo ndiye atakayeongoza project hiyo inayotarajiwa kuonekanwa second half ya mwaka 2019, director ndiye aliyesimamia project ya romance is a bonus book drama.

mnamo january 2019 wawili hao walivumishiwa kuwa wana mahusiano ya kimapenzi lakini wamekuwa wakikataa mara kwa mara.
kituo cha tvN ndio watakaokuwa na haki ya kuonyesha project hiyo.
1062267

https://www.soompi.com/article/1296687wpp/son-ye-jins-agency-clarifies-dating-rumors-hyun-bin
 
Exclusive: “Her Private Life” Cast Talks About Personal Fangirl Experiences, Previous Dramas, And Real-Life Chemistry
kwa ufupi:

PD Hong Jong Chan
: hii ni drama inayomzungumzia mwanadada anayevutiwa sana na idols haijalishi amepitia changamoto ngumu za kimaisha, pia inajaribu kuangazia hadithi ya wanaume wawili wanaovutiwa na mwanamke mmoja, wakati naandaa project hii niligundua ya kwamba hii ni hadithi inayotuhusu wanadamu wote duniani na hii ni kwa sababu kwa nyakati tofauti tunajikuta tunavutiwa zaidi na maisha ya wengine.

park min young: nilikuwa ni mshabiki mkubwa sana wa H.O.T (first idol group created by SM Entertainment in 1996), baada ya kwa sasa nimepata bahati ya kuwa mshabiki(fangirl) kupitia drama kiukweli najisikia furaha sana kushiriki ndani ya drama hii, vile vile navutiwa sana na kahawa pamoja na mbwa wangu.

Kim Jae Wook: ni mara yangu ya kwanza kuigiza uhusika mkuu ndani ya rom comedy, project zangu nyingi zilizopita nimekuwa nikishiriki nafasi ngumu sana kiasi ambacho watu wengi wanaogopa kufuatilia drama zangu.
tukutane april 10 inshaallah.
1062272
 
On April 3, the actress’s agency, E&T Story Entertainment, confirmed that Kim So Hyun would be appearing in the KBS drama “Mung Bean Chronicles” (working title)

Mung Bean Chronicles ni webtoon drama inayozungumzia hadithi ya mvulana anayeitwa Jeon Nok Du ambaye hakuvutiwa kabisa na habari za kufunga ndoa, Jeon Nok Du alifikia hatua za kuigiza kama mwanamke ili apate nafasi ya kuwa karibu na wasichana.

pia inazungumzia maisha ya msichana anayeitwa Dong Dong Joo nyakati za joseon aliyekuwa havutiwi kabisa na mila za ukahaba, ni msichana ambaye alikuwa na uwezo wa kutengeneza vitu tofauti kwa kipaji alichokuwa nacho hadi kufikia kupewa jina la jang young sil
1062276

https://www.soompi.com/article/1314...n-talks-to-join-kim-so-hyun-in-upcoming-drama
 
SBS Responds To Reports Of Delay Of Lee Seung Gi And Suzy’s Drama “Vagabond”

mpaka sasa hatujafahmu ni drama gani itakayofuata pindi itakapomaliza big issue drama kati ya vagabond au Absolute Boyfriend.
mwanzoni kampuni ya Apollo Pictures ambao ndio wasimamiaji wakuu wa absolute boyfriend drama walitoa taarifa inayodai ya kwamba drama hiyo ndio itakayofuata pindi itakapomaliza big issue.
https://www.soompi.com/article/1314...suzys-spy-drama-vagabond-delayed-to-september

Vagabond” is a 25 billion won (approximately $22 million) production.
1062285
 
Kim Hyun Joo In Talks For New Drama With Seo Kang Joon And Han Suk Kyu
On April 3, a source from the drama industry stated that Kim Hyun Joo is confirmed for the female lead role in OCN’s upcoming Saturday-Sunday drama “Watcher,” which is set to premiere in July.

Watcher ni thriller drama itakayozungumzia hadithi ya watu watatu wanaokumbwa na matukio ya hatari kwenye maisha yao, hatimaye wanaamua kufanya kazi kwa pamoja kwa dhumuni la kufichua maovu ya jeshi la polisi pamoja na watu wenye nguvu(matajiri)
1062287
 
upo sahihi, hayakuwa maamuzi sahihi kiupande fulani labda alichukua maamuzi kutokana na hasira alizokuwa nazo baada ya kumpoteza baba yake aliyeamua kukatisha uhai wake kutokana na depression. laiti kama wanadamu tungelikuwa na uwezo wa kutabiri kitakachojiri mbeleni kwa usahihi basi mke wake angelikuwa na haki ya kudai talaka kwa mume wake kwa kushindwa kwake kuzuia kifo cha mkwe wake.

taarifa ya habari ilielezea tukio lililoitikisa dunia kiuchumi baada ya taasisi kubwa ya kifedha ya lehman brother iliopo marekani kufilisika, sio tu marekani hata soko la hisa linalopatikana london pia lilikumbwa na athari bila ya kusahau nchi za Asia nazo zilikumbwa na mtikisiko wa kiuchumi ikiwemo japan.

mtikisiko wa uchumi ulioikumbuka ulaya na marekani ndio ulipelekea taasisi nyingi za kifedha nchini korea zikiwemo benki za biashara kukumbwa na athari ndio maana mzee alishindwa kupata msaada kwa muda muafaka kutoka benki.

hivyo basi hata mimi sijaliona kosa la mzee noh kwa sababu yeye si aliyepelekea dunia kukumbwa na mtikisiko wa kiuchumi mnamo mwaka 2008.

ni matumaini yangu kabla ya kufariki dunia kwa mwanamama ambaye kwa sasa ni mgonjwa atarudisha tena moyo wake kwa bwana assad wa the banker drama.
sidhani kama ndani ya dunia hii tunayoishi wanafika angalau wanaume 100 ambao wako tayari kuwasaidia kifedha wanawake ambao walikwisha kuachana pindi wanapokutwa au kukumbwa na mitihani ikiwemo maradhi, auditor noh nafsi yake imejawa na ubinadamu uliovuka mipaka.

Halafu drama alizoigiza nilizoiona Auditor Noh huwa anaigiza roho nzuri (utu) i.e City Hunter, Jing Birok na hii ya sasa. Sijui atakuwa ana utu kweli? Ananivutia sana anavyoigiza vile...

Jamani jamani The Great Seer ni motoooo. Hatari fire
Niliianza kama utani naona imenivutia kuliko nilivyodhani! Hiyo Ja Mi Won inatoa watu roho, yule head priest ananikera kama nini.

BTW Banker umeshaone ep ya jana? Naona KissAssian hawajaweka bado, ndio maana huwa sipendi haya mambo ya ongoing 🤦🏽‍♀️


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Jamani jamani The Great Seer ni motoooo. Hatari fire
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png

Niliianza kama utani naona imenivutia kuliko nilivyodhani! Hiyo Ja Mi Won inatoa watu roho, yule head priest ananikera ka
Nimeanza na Sambong japo sijaikamilisha episode 1 sababu nilijisikia hovyo kiafya ila natumai nikiendelea vizuri huenda nikaimalizia na kujiunga episode 2, ni nzuri sana ila kwa kuitazama kwa dk 40 nimeona mfalme ni mzinguaji mno. Mzee Komu Hwanghoe wapo humu ndani basi ni utamu tu.
 
dah hii drama ya empress ki niliishia episode 11.
mkuu kwani ni china au korea?

kwa mujibu wa stori ila sina uhakika ni kwamba jamii ya wakorea wengi wao hawavutiwi na historia ya empress ki kutokana na mambo aliyoyafanya wakati alipokuwa na cheo kwenye serikali ya YUAN (mongolia).

Mongolia waliivamia goryeo kwenye vita iliodumu kwa miaka 30 na kufanikiwa kuyachukua maeneo mengi ya kaskazini na kuyafanya himaya yao kwa takribani miaka 80.

kitendo cha kuwapa madaraka jamaa zake kwenye serikali ya yuan kilileta athari kubwa sana kwa serikali ya goryeo kwa sababu ilifika wakati kabila lao ndio lilikuwa na nguvu ya kufanya maamuzi kwenye serikali ya goryeo kwa kutumia nguvu ya yuan dynasty.

kaka yake aliwahi kufanya jaribio la kutaka kumuondoa madarakani mfalme lakini jaribio hilo lilishindikana na mfalme kuamua kulipa kisasi kwa kuangamiza koo ya GI.

empress ki akaamua kutuma wanajeshi wa mongolia ili wamuondoe madarakani mfalme gong min ambaye kwenye utawala wake alifanya jitihada kubwa sana ili kuinusuru goryeo isiendelee kutawaliwa na mongolia ila kabla ya jeshi halijafika korea wanajeshi watiifu waliwazuia mongolia kwenye border ya goryeo.

empress ki alitumia nguvu yake ili kuifanya familia yake iwe na nguvu ya utawala kwenye nchi ya goryeo kwa kutumia nguvu za utawala wa mongolia.

nakumbuka aminas aliwahi kuandika hadithi yake humu ndani.
Alaa kumbe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Empress Ki kali bhana, au labda sababu sisi wanawake ndio tunaona fahari kwa jinsi Ki alivyoweza kusimama imara tofauti na drama nyingi ambazo wanaume ndio wanaofanya aliyoyafanya yeye.

Jang Yeong Sil niliipenda sababu tu humo kacheza kipenzi zangu Song ila sikuvutiwa nayo kivile,enjoy.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Empress Ki bonge moja la drama aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom