Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kwa maana kwamba imeshindikana kupata link?
Korean wakishailisha maneno ya kiswahili kwangu ni sawa na supu iliyotiwa Nazi!!
😀😀😀😀
King dae jo yeoung kuipata online ni inshu sana. We kama unataka uone maudhui ya mule, huda budi ya kukutana na madj wa arusha. Utainjoi tu, japo kuwa ladha/ uhondo kamili utaukosa
 
hili neno akulaani lina maana gani huko upande wa pili?
kwetu sisi maana yake ni pesa au utajiri.
:p:p:p

kama maandishi yangu yalivuka mipaka nakuomba radhi ila na wewe unadhani huyu Khantwe anaweza kuangalia drama yenye episode 60 bila ya kuiba mchumba?
ngoja tumuulize amefika episode ya ngapi tokea aweke nia ya kutaka kuifuatilia queen seondeok.

umemuonaje mfalme gwanggaeto?
ahsante Mungu kwa kumuondoa go damdeok duniani akiwa bado na umri wa miaka 38, kwa balaa alilokuwa nalo kama angelifikisha miaka 60 huenda angelitembeza kipigo mpaka huku kwetu kwa waarabu koko.
pengine leo hii damushin angelikuwa ni uzao wa general komu wa goguryeo.
:D:D:D
Mimi kama Raia wa Gogryeo niliyezaliwa Yodongsong tunajivunia Emperor wetu wa kwanza Dam doek.

Huwa najiuliza sana wale wafalme ambao ni wakali wa kivita walikuwa hawaishi muda mrefu mfano Gwanggaetto alitawala kwa miaka ishirini akafa 39 . King Genghis khan wa Mongolia alitawala miaka 27, Alexernder miaka 13 akafa..
 
Download movie na Season buree
Download Seasons&Movies SD&HD Quality In Your Android Phone For Free

https://t.co/JDzeaDLSXu
IMG_20190227_095559_705.jpeg
images(21).jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani jamani Khantwe achana na Bidam
Wewe chagua kati ya Archeon au Kim Yushin
Japo Bidam alinikera sana kwa kukosa imani juu ya Deokman iliyopelekea adanganywe kirahisi ila bado ni my favorite ktk hii series pendwa.

Ila Mishil kiboko jamani, halafu kazuriiiiii na ana akiliiii dah. Sio kwa kuichanganya kule mibaba, alijua kuutumia uzuri wake haswaaa.
Mimi yule kaka yake mjingamjinga ananiachaga hoi

Hakuna drama ambayo nimewahi kuvunjika mbavu kama hii kwenye scene za comedy
Jukbang na Godo niliwapenda sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
'Jukbang' Huyo Mzee Namkubali Sana. Anafahamika Kama Lee Moon-Sik. Ameigiza Pia Drama Kama Vile Empress Ki, Rooftop Prince. Kwa Vichekesho Vyake HuweziChoka Kumtizama!
 
yes upo sahihi, mwili wa lee tae gon ulikuwa ni zawadi tosha ya kumfanya aweze kuutendea haki uhusika wa mfalme gwanggaeto.

ukiniuliza ni muigizaji gani aliyenivutia mule ndani basi jibu langu ni kim jung hwa.

drama ilikuwa na episode takribani 90 lakini cha kushangaza tumeonyeshwa upande mmoja tu wa maisha ya damdeok akiwa kama ni mtawala wa goguryeo nao ni upande wa harakati zake za kuitanua kingdom yake mpaka kuwa empereror.

je raia wa goguryeo walifaidika vipi na kampeni zake za vita zisizokwisha?
kama tunavyofahamu unaweza ukawa na himaya kubwa kama ilivyo Tanzania lakini raia wako wakakosa huduma muhimu za kila siku, cha ajabu sijawahi kukutana na historia ya gwanggaeto inayoangazia hali halisi ya maisha kwa raia wake, vita inataka
maandalizi ya ya chakula na mtoaji chakula cha jeshi ni raia wa kawaida kwa sababu ndiye mlimaji mkuu kwa msaada wa land owner.

utawala wake wa ndani ulikuwaje kwa wale ambao walikuwa na mawazo tofauti na yakwake?

ndio maana kiupande wangu SEJONG anabaki kuwa mfalme bora kwa sababu utawala wake ulielemea pande zote.
Kwa Kipindi Cha Goguryeo, Mfalme Bora Wa Kipindi Hicho Anaweza Kuwa Ni Gwanggaeto Ukimtoa Jumong Ambaye Ndiye Baba Wa Taifa Hilo. Lakini Ukija Kipindi Cha Joseon, Sejong The Great Anasimama Kama Mfalme Bora Zaidi Wa Muda Wote Katika Joseon Dynasty!
 
Mpya Hiyo! Kama Uliwahi Kuitazama Korean Movie Inayoitwa MASQUARADE Ya Mwaka 2012 Basi Hii Drama Ni Kama Remake Yake! Inakwenda Kwa Jina La THE CROWNED CLOWN Yenye Episodes 16 Kwa Hisani Ya tvN.

Kwa Kifupi Tu Inahusu Mfalme Mmoja Ambaye Alikuwa Akiandamwa Sana Na Majaribio Mengi Sana Ya Kutaka Kuuawa 'Assassination Attempts'. Alichofanya Akatafutwa Mtu Wa Kufanana Naye 'Double' Ambaye Hapo Kabla Alikuwa Akivaa Vinyago Na Kuchekesha Watu Masokoni Huko Joseon. Balaa Linaanza Pale Ambapo Watu Mbalimbali Ndani Ya Palace Wanapoanza Kuhisi Tabia Za Mfalme Zimebadilika Kutokana Na Uwepo Wa Huyo Jamaa 'Clown'. Ghafla Tu Watu Wanashangaa Mfalme Kaanza Kuwa Mpole, Alafu Kaanza Kumpenda Queen Wake Kuliko Awali.

=>> Aliyeigiza Kama Mfalme Kwenye Hii Drama Ni Yeo Jin-Goo. Ameigiza Pia Drama Kama Vile:
  • The Royal Gambler,
  • The Moon That Embraces The Sun,
  • Warrior Baek Dong-Soo,
  • Tree With Deep Roots,
  • Princess Ja-myung,
  • Swallow The Sun,
  • Iljimae n.k.
==========
Kwa Wale Waliyoitazama Movie Yake (Masquarade) Basi Hii Drama Utaipenda Sana!

The Crowned Clown (2019)
1551629299082.png
 
mukinichagua niwe balozi wa nyumba 10 wa korean drama club nitawaleteeni BTS uwanja wa CCM kirumba:p:p:p

BTS wanakwenda kuushangaza ulimwengu na vilivyomo ndani yake.
BTS watasababisha show iwe repeatition kwa wale watakaokosa tiketi,naamini siku ya kwanza ya mauzo ya tiketi zitamalizwa zote

muda huu kwenye mitandao stori kubwa ni BTS.
kwa mara ya kwanza nimeamua nijinukuu mwenyewe ili kurudisha kumbukumbu ya maneno niliyoyazungumza siku ya February 19 kwa saa za kitanzania ambayo ilikuwa ni sawa na february 20 kwa saa za korea.

sijui kwa nini nilishindwa kutabiri kurudi kwa lowassa ndani ya CCM akiwa na mkia uliokatika japokuwa utaungwa kwa siku chache zijazo.

rasmi tarehe 1/03 nchi zote za ulaya ikiwemo marekani ambazo BTS watafanya show ya love your self kumeshuhudiwa kuuzwa kwa tiketi zote siku moja.

fikiria uwanja wa wembley uliopo uingereza ambao unachukua mashabiki 90000 tiketi zote zimeuzwa kwa dakika 90 tu, Tottenham hotspur ambao ndio wanatumia uwanja wa wembley kipindi hiki naamini hawajawahi kujaza mashabiki 90000 kwa mechi moja.

ndio maana navutiwa zaidi na lugha ya muziki kwa sababu ni nyepesi kuifahamu na kukujaza hisia, unaimba lugha ya kikorea lakini wasikilizaji wanazungumza kiingereza na lugha nyenginezo lakini bado huoni tofauti yoyote.

hmmmmmm! nilidhani wale wote wanaojipa cheo cha ARMY wana mapenzi ya uongo (fake love) kumbe nilikuwa najidanganya.
 
Attachments

  • 1551642873268.png
    1551642873268.png
    9.9 KB · Views: 39
Tumalize Utata Bidam rang Vs Dang sae(Lee bang ji)

Gukseon Muno vs Chuk sagwa
Chilsuk vs Giltae mi

nipe mshindi hapo.
zamani nilikuwa ni mpenzi mkubwa sana wa martial arts kiasi ambacho nilifika hatua ya kuacha kuangalia drama za mjini hususani zile zenye maudhui ya rom- comedy.

baadae nilijifunza ya kwamba nachukua maamuzi ya kijinga kwa sababu ubora wa muigizaji na drama haupaswi kupimwa kwa martial arts pekee ambazo zinapangwa kutokana na matukio husika kwa ushirikiano wa timu nzima ya uzalishaji (production).

lakini tukirudi kwenye hoja yako kiupande wangu mimi kwenye historical drama muigizaji bora kwa upande wa martial arts kwa upande wa veterani nitamchagua choi soo jong ahjussi, licha ya umri kumtupa mkono lakini hakuacha kuonyesha uwezo wake kupitia longest period historical drama zenye mapambano makali na harakati za kuendesha farasi mara kwa mara.
emperor wang guhn, emperor of the sea, dae jo young, dream of emperor zote hizi ameigiza huku umri wake ukianzia miaka 42 mpaka 47 lakini shughuli yake aliyokuwa akituonyesha ilikuwa ni kubwa kuliko ya vijanadume wa SEOUL.
Cha ajabu zaidi drama pekee yenye episode chache ambayo ameshiriki kwa upande wa historical drama ni emperor of the sea yenye episode 51 hivyo basi kivyovyote screen time inakuwa ni kubwa kwa sababu yeye ndiye muongozaji mkuu.

kwa upande wa modern drama na short historical drama nitamchagua jang hyuk linapokuja suala la martial arts kwa hawa waigizaji wenye umri wa miaka 40 kwenda juu, jamaa ni mpiganaji wa ukweli na anaendelea kujifunza mapigano hususani ngumi za ulingo mara kwa mara.

kwa upande wa mabishoo wa seoul nitamchagua lee joon gi, sijamuona muigizaji mwenye uwezo wa kusimama na bwana yule kwenye ishu ya martial arts kuanzia historical drama hadi modern drama.

1551698150082.png
 
Lee Jong Suk’s Enlistment Date Confirmed
Actor Lee Jong Suk will be enlisting for his mandatory national service on March 8 as a public service agent.
Lee Jong Suk, who suffered a ruptured ACL (anterior cruciate ligament) from a car accident when he was 16, was deemed unfit for service as an active duty soldier. He will instead be assigned to a location by the Military Manpower Administration, where he will be a reservist working as a public service agent.

Lee Jong Suk will be discharged on January 2, 2021.
1551698488093.png
 
Kwa Kipindi Cha Goguryeo, Mfalme Bora Wa Kipindi Hicho Anaweza Kuwa Ni Gwanggaeto Ukimtoa Jumong Ambaye Ndiye Baba Wa Taifa Hilo. Lakini Ukija Kipindi Cha Joseon, Sejong The Great Anasimama Kama Mfalme Bora Zaidi Wa Muda Wote Katika Joseon Dynasty!
niwe mkweli kama watatafutwa wanadamu 100 wasiopenda kutafuta maarifa kupitia fasihi ya uandishi basi nitashika nafasi ya pili kutoka juu,na uvivu wangu katika kufuatilia kwangu kote historia ya maisha ya mfalme gwanggaeto nimejifunza ya kwamba maisha yake yameelezewa zaidi upande mmoja tu ambao ni wa kampeni zake za kijeshi.

kwa mukhtadha huu nitaendelea kuamini ya kwamba ubora wa gwanggaeto unapimwa zaidi na mafanikio yake ya kijeshi kuliko siasa yake ya ndani ukilinganisha na mfalme sejong licha ya kwamba watu hawa wawili wametawala karne tofauti.

  • kama gwanggaetto alikuwa ni kiongozi bora wa kupigiwa mfano mbona historia yake haituonyeshi harakati zake za siasa ya ndani ya nchi kama sejong?
  • ukiondoa upanuzi wa kingdom yake mpaka kuwa emperor ni mafanikio yepi mengine ya kukumbukwa aliyoyakamilisha nyakati za utawala wake ambayo wewe umebahatika kujifunza?
  • historia ya mfalme sejong ipo wazi kuanzia harakati zake za kuhakikisha nchi yake inaongozwa kidemokrasia mpaka kampeni zake za kijeshi dhidi ya japan, sasa kwa nini upande wa gwanggaeto historia yake haionyeshi harakati hizo?
  1. chini ya sejong joseon kwa mara ya kwanza walitumia kalenda yao
  2. aliwapa nafasi watu wenye vipaji haijalishi ni watumwa, mfano jang young sil, combination ya sejong na genius jang young sil waliifanya joseon iwe nchi imara kwa kila nyanja.
  3. chini ya sejong joseon aliweza kupromoted research za kiuchumi, sayansi, astronomy, musical nakadhalika
  4. chini ya sejong joseon waliweza kuwa na ramani yenye kuonyesha mipaka ya nchi
  5. chini ya sejong joseon walifanikiwa kutengeneza ala za muziki na hatimaye joseon kuwa na muziki wao kwa msaada wa scholar park na jang youngsil
  6. ugunduzi wa lugha ya kikorea licha ya wapinzani wake kumpinga hadharani lakini alijibizana nao kwa hoja.
  7. tanzania tulishangaa mwalimu nyerere kwa matendo yake ya kuweka mijadala huru na baadhi wapinzani wa sera zake, sejong alifanya hayo mnamo karne ya 14, alikuwa na uwezo wa kuwachinja wapinzani wake kama alivyofanya baba yake lakini aliona nchi inapaswa iongozwe huku pakiwepo haki ya kutoa mawazo na kuwepo kiunganishi kati ya kiongozi na watumishi. alifikia kumpa nafasi hwang hui awe waziri mkuu wake licha ya kuwa mwanzoni jamaa alikuwa anamuunga mkono kaka yake arithi madaraka.
kwa dunia hii ya sasa hivi kama atawekwa sejong na gwanggaeto utamchagua kiongozi yupi?
kwa ardhi ya goguryeo ilivyokuwa ni ya milima naamini kampeni za kijeshi za mara kwa mara hazikuwafurahisha wananchi wa goguryeo ila hawakuwa la kufanya.
 
Wakati ni mjenzi bora wa Mabadiliko kuanzia kwa binadamu mpka mazingira yanayowazungua watu hao, ndiyo maana katika evolution of man, Nyani walikuwa wanatumia miguu minne na walipata chakula kupitia miti, Lakini kutokana na Mabadiliko ya Nyakati Nyani walilazimika kubadili mtindo wao wa maisha kwani mazingira yao yaliwataka wawe hivyo sababu wakati ulibadilisha Climate kutoka Equatorial to Savana Glass land maana yake miti ili anza kuwa adhimu hivyo walilazimika kusimama ili wapate riziki. Kama ungalienda mwanzoni ukawauliza nyani kama wanapenda kusimama na kutembea kwa miguu miwili ili wapate riziki bila shaka jibu lao lingekuwa hapana.
Mfalme Gwanggaetto aliishi kipindi ambacho alipaswa kukabiliana na hali halisi ya Mazingira na wakati, wakati ule wa Three Kingdom ulikuwa ni wakati wa Vita sana karibia kila Nchi ilitaka ku-expand territory yake, Mataifa kam.a Baekje yalikuwa yanaishambulia sana Gogryeo,Ni vigumu kujiremba wakati unasikia nje ya Nyumba yako unasikia kuna Majambazi, maana yake akili yako itajiseti namna gani ya kujihami kama ni kupambana nao au kuwakimbia. Naamini Sejong angeishi zama zile pia angejiandaa kukabiliana na Mazingira yanavyotaka awe.
 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom