Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kazz0

Kazz0

Member
Joined
Mar 15, 2015
Messages
48
Likes
157
Points
15
Kazz0

Kazz0

Member
Joined Mar 15, 2015
48 157 15
Kama wewe ni mpenzi wa Korean Dramas, karibu katika thread hii tupate ku share kuhusu kazi hizo hatari za mkorea.

Tuambiane;

- Ipi ni drama yako bora ya kila wakati kwako?

- Ni ya aina gani? (Wengi tumezoea kusema za 'mjini' na 'vijijini')

-Nini kinakuvutia sana katika hiyo Drama?

Pia:

- Nani ni Msanii wako Bora wa kiume na wa kike na baadhi ya drama alizoigiza?

- Nani ni sexiest Actor au Actress kwa maoni yako?

- Ipi ilikua Drama yako ya kwanza ya kikorea kuiona?

- Ni Drama gani ya kikorea unaitafuta sana na unapata wakati mgumu kuipata? (Unaweza ukasaidiwa kuipata na mashabiki wengine)

*Pia tumia thread hii kufahamishana kuhusu drama mpya zilizotoka au unayohisi ni nzuri ila haijapata umaarufu sana!!

Karibu tujumuike! Saraghae! Kumooyo!!

=========

Baadhi ya Links za Dramas mbali mbali za Korea...;

Be Strong Geum Soon

Princess Ja Myung Go

THREE DAYS (2014)

Swallow the Sun

Jumong

King Guenchoggo

=====

Links za ku-download drama za Kikorea;

- Watch Drama Online | Korean Drama | Japanese Drama | Taiwanese Drama | Hong Kong Drama | Chinese Drama
- GoodDrama.Net

======

Updated: Kwa mjadala na kubadilishana uzoefu kuhusu series za jumla za movies mbalimbali, za zamani na mpya, Unaweza pia kufuatilia UZI HUU hapa Series (Special thread)
..

Kazi kwako.. Enjoy!
 
Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined
Apr 14, 2018
Messages
116
Likes
164
Points
60
Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined Apr 14, 2018
116 164 60
unajua kwa nini leo nimeitembelea hii thread baada ya takribani siku 10 kupita?
jibu ni rahisi, nahitaji nikusaidie drama nyengine ya kuangalia kwa sababu nimeshaona dalili za uanaharakati kutoka kwako, ila tu chonde chonde karata zako zichange vizuri dada yangu yasije yakakutokezea ya bwana jung do jeon a.k.a sambong.
Kabla hujaanza kuifuatilia historical drama nyengineyo basi itafute hii lakini bahati mbaya kissasian haipo.

JUNG DO JEON (SAMBONG) : 2014 project
View attachment 991270

 1. Jeong Do Jeon at Dramanice
ukiiangalia hii picha kwa macho yote mawili utakutana na veterani actor watupu ambao wanafahamu maana halisi ya kuigiza historical drama. kama ilivyo jing bi rok drama na humu ndani vile vile hamuna muda wa mapenzi bali ni ubabe wa wanasiasa.
kama umewahi kuiangalia six flying dragons drama na ukaiangalia na hii itakuwa unatembea mule mule ila kwa asiyefahamu six flying dragons ni project ya mwaka 2015 wakati hii ni project ya mwaka 2014.

mwandishi wa six flying dragons kwa kiasi kikubwa anatulazimisha tuamini ya kwamba shujaa aliyefanikiwa kuiangusha goryeo na kuzaliwa joseon alikuwa ni yi bang won ambaye baadaye anakuwa mfalme wa tatu wa joseon (taejong) baada ya kufanya mapinduzi ya damu kwa ndugu zake na wapinzani wake, lakini shujaa wa ukweli ni huyu jamaa anayeitwa jung do jeon(sambong)
humu ndani utaona jinsi gani sambong alivyoweza kupambana kutoka mwanasiasa asiyekuwa na nguvu hadi akafanikiwa kumshinda waziri mkuu wa goryeo na mpaka kufikia hatua ya kuiangusha Goryeo kingdom na kuzaliwa Joseon akishirikiana na general yi seong gye. Kuna tabu nyingi sana alizipitia ikiwemo kugombana na rafiki yake kipenzi jung moong jo
best historical drama na hutojutia kuitazama nakuahidi.

 1. Jeong Do-jeon alizaliwa na kufariki (1337-1398), alikuwa ni mwanasiasa na mwanamapinduzi wa ukweli nyakati hizo za goryeo hadi joseon.
 2. ndiye alikuwa bwana mipango wa general yi seong gye ambaye ndiye mfalme wa kwanza wa joseon (taejo).Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1383 maeneo ya hamgyeong.
 3. walipofanikiwa kuiangusha goryeo alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa kwanza wa joseon.
 4. wakati joseon makao makuu yake yalipojengwa hanyang, sambong ndiye aliyependekeza ikulu ipewe jina la Gyeong bokgung.
sambong alijikuta akiingia kwenye mgogoro na Yi Bang-won kwa sababu ya vita ya urithi wa madaraka ambapo sambong kiupande wake hakuvutiwa na mtazamo wa kiuongozi aliyokuwa nao yi bang won.
 1. sambong aliamini ya kwamba serikali bora ni ile inayoongozwa na watu wote wakiwa na uhuru wa kutoa mawazo yao mbele ya kiongozi mkuu, sambong aliamini ya kwamba pindi kiongozi mkuu wa nchi anapoongoza nchi kwa ushirikiano wa watumishi bora aliowachagua basi hata kama mfalme ni mediocre basi siasa ataiweza. Dhana hii kiupande fulani ilipingwa na wapinzani wake ambao waliamini ya kwamba sambong alikuwa na mpango wa kujimilikisha madaraka kwa kumtumia mtoto mdogo wa yi seong gye. lakini hoja zao alizijibu ya kwamba mfalme ndiye mwenye mamlaka ya kunichagua mimi na pia ana mamlaka ya kuniondoa mimi hivyo basi kama ataniona ni tishio basi atakuwa na haki ya kuniondoa madarakani.hivyo basi aliamini kama yi bang won atashika madaraka ataongoza kwa mkono wa chuma.
 2. yi bang won na washirika wake waliamini ya kwamba kwa kuwa joseon bado ni taifa changa basi linamhitaji zaidi kiongozi atakayekuwa na msimamo ili aweze kulivukisha mbali taifa hilo kwa sababu bado waliendelea kujitokeza wanaharakati waliotaka kuirudisha goryeo. Vita ya watu hawa wawili wenye akili nyingi ilimalizwa kwa mapinduzi ambapo yi bang won aliwaua ndugu zake ambao walikuwa hawakubaliani kimtazamo na vile vile alimuua sambong na watu wake na kumtangaza kama ni msaliti wa nchi. yale aliyoyahofia sambong ndiye yaliotokezea wakati wa utawala wa mfalme taejong kwa miaka 18 ya utawala wake kwa sababu alitawala kidikteta, japokuwa alifanikiwa kuifanya joseon kuwa taifa imara kabla hajamuachia madaraka yote mtoto wake yi do (sejong the great). Nilichowapendelea zaidi wanasiasa hawa wawili ni kwamba wote walitaka kuyapigania maslahi ya wananchi na si matumbo yao

great thinker jeong mong ju na jung do jeon walikuwa ni marafiki sana nyakati hizo wanasoma pamoja mpaka kujiingiza kwenye siasa nyakati za goryeo. wawili hao kwa pamoja walikuwa na ndoto ya kuleta mageuzi kwenye utawala wa goryeo ambao uligubikwa na rushwa na ubadhirifu wa rasilimali nyakati za mwishoni.
bahati mbaya sana wawili hao walipoteana njia baada ya sambong kubadili msimamo wake wa kutaka kuirudishi heshima goryeo hadi kufikia hatua ya kuizamisha goryeo na kuanzisha joseon.
 1. sambong aliamini ya kwamba kwa hatua iliofikia goryeo hakuna uwezekano wa kuirudisha katika njia ilionyooka kama ndoto zao zinavyowaaminisha, bali njia pekee ni kuizamisha goryeo iliotawaliwa na ukoo wa WANG ( from emperoe wangun to.....). sambong aliamini ya kwamba taifa jipya chini ya kiongozi mpya atakayekuwa chini ya wanasiasa wanaokwenda na wakati ndiyo ukombozi wa wananchi.
 2. great thinker jeong mong ju aliamini ya kwamba kubadilisha jina la taifa kusingeliondoa uhalisia wa dhiki wanazokumbana nazo wananchi, kiupande wake aliamini goryeo hii inayoonekana kuchoka kama atapatikana kiongozi bora basi wananchi watayafurahi maisha, hivyo basi alikataa maoni ya sambong na wafuasi wake mpaka kufa kwake, bwana yule aliamini ya kwamba Tanzania kuipa jina jipya la Dubai haimaanishi chochote kiuhalisia kama viongozi wake hawaendani na jina la Dubai. msimamo wa bwana huyu ulikuwa ni mwiba mchungu sana kwa upande wa sambong na wafuasi wake kwa sababu yeye aliyekuwa ndio nguzo ya mwisho ya goryeo, hivyo basi kama jeong mong jo angeliachana na mkakati wa kuipigania goryeo na kuungana na sambong basi urafiki wao ungeliendelea kuwepo kama mwanzoni.
hatimaye Jeong Mong-ju aliuliwa mnamo mwaka 1392 kwenye daraja la sonjuk na aliyeongoza mauaji hayo ni yi bang won, nyakati hizo sambong alikuwa kifungoni kutokana na harakati zake za kuiangusha goryeo.
historia hadi leo inamtaja Jeong Mong-ju kama ni mzalendo wa ukweli aliyeamua kufa kwa ajili ya nchi yake ya Goryeo. kifo chake ndio ulikuwa mwisho wa taifa la goryeo kuendelea kuwepo kwani mwaka huo ndio taifa la joseon lilipoanzishwa.

siku chache kabla ya kifo chake vita ya maneno kati ya pande mbili hizo ilizuka ila kwa njia ya ushairi

yi bang won aliandika shairi lifuatalo
What shall it be: this or that?
The walls behind the temple of the city's deity* has fallen - shall it be this?
Or if we survive together nonetheless - shall it be that?

jeong mong ju naye akajibu
Though I die and die again a hundred times,
That my bones turn to dust, whether my soul remains or not,
Ever loyal to my Lord, how can this red heart ever fade away?

KBS DRAMA AWARDS:2014

 1. Daesang awards (muigizaji bora wa mwaka) : Yoo Dong Geun ambaye pia mwaka huu amebeba tunzo hii
 2. High Excellence Award in Acting :Jo Jae Hyun
 3. Excellence Award in Acting park Young Gyu
 4. Best Screenwriter :Jeong Hyun Min
ina maana hii drama ndio ilibeba tunzo ya ubora kwa mwaka 2014, mwaka 2015 drama ya jing bi rok the memoir of imjin war ndio ilibeba drama bora ya mwaka.
kwa maelezo zaidi tembelea tovuti hii
anyeong
Kwangu Sambog ndiye Waziri mkuu bora wa Joseon master wa Hidden root
 
Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined
Apr 14, 2018
Messages
116
Likes
164
Points
60
Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined Apr 14, 2018
116 164 60
nimeyapenda maamuzi yako kwa sababu kwa hali inavyokwenda hapa nyumbani kwetu naiogopa siku nitakayotembelea humu nikakutana na taarifa ya kuhuzunisha, ni bora uendelee kuwa mwanaharakati kwa njia ya televisheni drama.
:p:p:p

umenipa heshima kubwa sana isiyoendana na uwezo wangu
Nadhani mie peke yangu ndiyo nifika mbali maana hizi historical drama zimejenga kwa kiasi kikubwa uzalendo wangu halafu Miye nimeshajifunza kikorea hivyo nazidi tu kuongeza misamiati
 
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
2,771
Likes
10,013
Points
280
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
2,771 10,013 280
jioni ya leo nilibahatika kuiangalia movie inayoitwa masquerade (Gwanghae: The Man Who Became King) ambayo muigizaji mkuu alikuwa ni lee byung hun. Ni movies inayozungumzia stori ya mfalme gwanghae ambaye anaamua kumtafuta mwanadamu anayefanana naye kisura na kumfanya kuwa mfalme kwa lengo la kujiepusha na wapinzani wake ambao walidhamiria kumuondoa madarakani.
kupitia movie hii muigizaji lee byung hun alishiriki nafasi mbili ambazo ni ya mfalme gwanghae na nafasi ya mburudishaji (clown) ambaye alifanana na mfalme gwanghae, inakadiriwa movie hii mnamo mwaka 2012 ilivunja rekodi ya mauzo ya tiketi ambapo takribani watu millioni 12 walinunua tiketi kwa ajili ya kuiangalia movie hii.

baadae ndipo nikaitafuta drama ya The Crowned Clown ambayo ni remake ya movie ya masquerade. Kupitia drama hii episode 2 za mwanzo tayari nimeshajifunza asilimia 80% ya matukio yaliotokezea kwenye movie ya masquerade, nimebaki najiuliza:
je niendelee kuifuatilia hii drama kila wiki wakati najua kitakachotokezea mbeleni?
 • nimeshajua ya kwamba huyu imposter king atajiweka karibu na malikia kama ilivyokuwa kwenye movie
 • nimeshajua ya kwamba huyu imposter king atajulikana na malikia ya kwamba ni fake
 • nimeshajua ya kwamba huyu imposter king atajulikana na wapinzani wake kutoka western faction
 • nimeshajua ya kwamba huyu imposter king atawapigania wananchi wake wasitolewe sadaka kwa ajili ya taifa la ming china na pia ataweka sheria ya matajiri kulipa kodi ya ardhi.
 • nimeshajua ya kwamba huyu imposter king baadae atakimbilia uhamishoni ili kujiepusha na adhabu ya kifo kutokana na kuigiza nafasi ya mfalme gwanghae.
sijui niifuatilie pengine itaongezeka vionjo kama vya neymar wa barcelona?
hii ndio drama pekee mpya nilioifuatilia mpaka muda huu, nimekusudia mara hii nipunguze ulevi angalau kutoka chupa 50 za mwaka 2018 hadi chupa 25 za mwaka 2019.

nashindwa kuelewa kwa nini drama zote ninazoziangalia zinazowazungumzia mfalme seonjo na mwanawe gwanghae zinawaonyesha wawili hao wakiwa na uhusiano mbaya utafikiri wa Iran na Saudi arabia.
aigoooo kuna watu walifikiri nitaitaja Iran dhidi ya Izrail mataifa ambayo tokea bibi yangu ni kigori wanatambiana ujinga utafikiri ni ngumi za jogooo.
 1. THE KINGS FACE DRAMA: mfalme seonjo alimchukua demu wa mtoto wake.
 2. jingbirok the memoir of imjin war: vita ya urithi wa madaraka
 3. yi sooon shin drama : vita ya urithi wa madaraka
 4. gu am heo jun :mfalme seonjo hakupendelea kumuona mtaalamu wa tiba heo jun akiwa na ukaribu na gwanghae.
1547159488850-png.992076
dunia na watu wake ni vitu viwili tofauti, kuna watu wanajishangaa kwa kufanikiwa kusoma vitabu 50 kwa mwaka wakati mjinga mimi najishangaa kwa kufanikiwa kuangalia drama 50 kwa mwaka 2018.
 
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
2,771
Likes
10,013
Points
280
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
2,771 10,013 280
bado munaendelea kugoma kuifuatilia sky castle drama?
leo inaendelea episode ya 15 na tukumbuke episode ya 14 iliangaliwa na asilimia 16 ya watu wanaoishi korea ya kusini. kutoka 1% hadi 15% ni hatua kubwa sana tumepitia.
JTBC hawajawahi kuonyesha drama iliovuka 13% kwa kuangaliwa nchini korea.
au na nyinyi munadanganya maisha humu ndani?
musigope bwana hakuna asiyedanganya.
 
Attachments:

Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined
Apr 14, 2018
Messages
116
Likes
164
Points
60
Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined Apr 14, 2018
116 164 60
 1. dae jo young drama = 2006
 2. king gwanggaeto drama = 2011
 3. unaposema dae jo young imechukua waigizaji kupitia king gwanggaeto utakuwa unakosea.
Pengine nilizungumza sababu King Gwanggaetto niliona kwa mara ya kwanza 2011 Dae Jo young 2012
 
Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined
Apr 14, 2018
Messages
116
Likes
164
Points
60
Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined Apr 14, 2018
116 164 60
Ki
Hizo nilizozibold nimekwisha kuzitazama, hizo nyingine nitazicheki bila shaka Mkuu.
Asante kwa mapendekezo

Sent from my iPhone using JamiiForums
Ukifika sehemu ya 15 ya King Gwanggaetto the Great njoo utupe maoni umeionaje
 
Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined
Apr 14, 2018
Messages
116
Likes
164
Points
60
Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined Apr 14, 2018
116 164 60
Kwa sasa naifuatilia Yi san ambayo inamuelezea mfalme Joeng Jo wa Joseon ambaye ni moja katika ya Mfalme bora kabisa wa Joseon dynast huyu aliachiwa Nchi na Babu yake Yoeng Jo ambaye pia alikuwa Genius na alipenda watu sana. Kumbuka King Yoeng Jo of Joseon ni mtoto wa King Sukjong na mama yake ni Constort Suk bin Choe(Dong Yi) Inasemekana alirithi U-Genius na Uzuri wa sura toka kwa mama yake Suk bin choe(Dong Yi)
 
Nifah

Nifah

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2014
Messages
26,226
Likes
25,416
Points
280
Nifah

Nifah

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2014
26,226 25,416 280

Sasa mimi nimeacha kuangalia Yi San nilishafika episode 5 ndio naangalia Gwanggaeto nipo episode 5! Lol

Ila nashukuru kwa haya maelezo yako maana sikuwa nikijua kama Yi San ni mtoto wa kipenzi changu Dong Yi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mdomo bakuli

Mdomo bakuli

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2017
Messages
1,947
Likes
2,983
Points
280
Age
97
Mdomo bakuli

Mdomo bakuli

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2017
1,947 2,983 280
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
2,771
Likes
10,013
Points
280
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
2,771 10,013 280
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
2,771
Likes
10,013
Points
280
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
2,771 10,013 280
Baada ya kifo cha Jumong Gogryeo ilipoteza ushupavu wake hasa kwa Bakje ambayo ilianzishwa na Sosono.
kuondoka kwa mtakatifu jumong kuliifanya kwanza Goguryeo ipoteze nguvu kwa Buyeo ambayo bado mfalme Daeso alikuwa ndio mtawala, tokea mwanzoni Buyeo haikupendelea kuona taifa changa la Goguryeo linakuwa na nguvu kubwa zaidi yao, hivyo basi kugawanyika kwa Goguryeo pia ulikuwa ni mwiba kwa ustawi wa Goguryeo mbele ya Buyeo, Han dynasty na makabila mengineo ukiiondoa Baekje ambayo isingelikuwa na nguvu ya kuivamia Gogoryeo kwa miaka ya mwanzoni.

Lakini baada ya mfalme Yuri kumkabidhi madaraka mtoto wake wa kiume aliyeitwa Muhyool taifa la goguryeo lilirudisha tena nguvu zake za mwanzoni, huyu muhyool alikuwa ni mjukuu wa nne wa jumong na alitunukiwa cheo cha crown prince akiwa na umri mdogo na hii ilitokana zaidi na kifo cha kaka yake Dojeol, pia alikuwa na kaka yake anaitwa hamyeong ambaye alivuliwa cheo cha crown prince na baba yake.

huyu muhyool ndiye aliongoza kampeni ya kuivamia buyeo ambayo ilikuwa onfire nyakati hizo chini utawala wa babu yake wa pili ambaye ni Daeso na kufanikiwa kumuua mfalme daeso, tukumbuke mama yake jumong aliolewa na baba yake daeso ambaye ni geumwa hivyo basi muhyool alimchukulia daeso kama ni babu yake.
huyu muhuni hakuishia hapo tu bali mataifa mengi ya jirani aliyabeba na kuitanua tawala ya goguryeo mpaka kufikia kubeba maeneno ya han china pamoja na naklang.
muhyool
kama walivyo baadhi ya wafalme wengineo alipewa heshima ya DAEMUSIN (damushin = mungu wa vita).
mpaka hapa utaona ya kwamba baekje hawakuwa na nguvu ya kusimama na Goguryeo nyakati za mwanzoni.
kutoka jumong wa goguryeo hadi geunchogo wa baekje ni miaka takribani 300 imepita.

1547252083362-png.992387
 
Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined
Apr 14, 2018
Messages
116
Likes
164
Points
60
Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined Apr 14, 2018
116 164 60
Babu
Sasa mimi nimeacha kuangalia Yi San nilishafika episode 5 ndio naangalia Gwanggaeto nipo episode 5! Lol

Ila nashukuru kwa haya maelezo yako maana sikuwa nikijua kama Yi San ni mtoto wa kipenzi changu Dong Yi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Babu yake na Yi san yule mfalme mzee(JoengJo) ndo mtoto wa Dong Yi hivyo Yi san ni kituu cha Dong Yi.
 
Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined
Apr 14, 2018
Messages
116
Likes
164
Points
60
Great Conqueror

Great Conqueror

Senior Member
Joined Apr 14, 2018
116 164 60
kuondoka kwa mtakatifu jumong kuliifanya kwanza Goguryeo ipoteze nguvu kwa Buyeo ambayo bado mfalme Daeso alikuwa ndio mtawala, tokea mwanzoni Buyeo haikupendelea kuona taifa changa la Goguryeo linakuwa na nguvu kubwa zaidi yao, hivyo basi kugawanyika kwa Goguryeo pia ulikuwa ni mwiba kwa ustawi wa Goguryeo mbele ya Buyeo, Han dynasty na makabila mengineo ukiiondoa Baekje ambayo isingelikuwa na nguvu ya kuivamia Gogoryeo kwa miaka ya mwanzoni.

Lakini baada ya mfalme Yuri kumkabidhi madaraka mtoto wake wa kiume aliyeitwa Muhyool taifa la goguryeo lilirudisha tena nguvu zake za mwanzoni, huyu muhyool alikuwa ni mjukuu wa nne wa jumong na alitunukiwa cheo cha crown prince akiwa na umri mdogo na hii ilitokana zaidi na kifo cha kaka yake Dojeol, pia alikuwa na kaka yake anaitwa hamyeong ambaye alivuliwa cheo cha crown prince na baba yake.

huyu muhyool ndiye aliongoza kampeni ya kuivamia buyeo ambayo ilikuwa onfire nyakati hizo chini utawala wa babu yake wa pili ambaye ni Daeso na kufanikiwa kumuua mfalme daeso, tukumbuke mama yake jumong aliolewa na baba yake daeso ambaye ni geumwa hivyo basi muhyool alimchukulia daeso kama ni babu yake.
huyu muhuni hakuishia hapo tu bali mataifa mengi ya jirani aliyabeba na kuitanua tawala ya goguryeo mpaka kufikia kubeba maeneno ya han china pamoja na naklang.
muhyool
kama walivyo baadhi ya wafalme wengineo alipewa heshima ya DAEMUSIN (damushin = mungu wa vita).
mpaka hapa utaona ya kwamba baekje hawakuwa na nguvu ya kusimama na Goguryeo nyakati za mwanzoni.
kutoka jumong wa goguryeo hadi geunchogo wa baekje ni miaka takribani 300 imepita.

Kumbuka baada ya Kifo cha Muyul hapa Gogryeo ilikuwa na matatizo mengi sana ndani ya Nchi na ndiyo yalipelekea kupigwa kirahisi hata kabla ya Geuchoggo kuitawala Bakje
 
Hivi kumbe Mzee Geumwa alimuoa mamake Jumong? Mbona kwenye Jumong sijaona hii? Sitaki kuamini kama nimesahau...

Ila nilitamani kama Lady Yuhwa angekuwa na Geumwa tokea mwanzo na sio Haemosou ila hata couple yao na Haemosou pia niliipenda.
Muandishi ya Jumong alijua kuniliza jamani, ajabu ndio series yangu kipenzi ya muda wote!

Umenifurahisha kwa picha na avatar ya Oppa wangu Song Il Gook.
Hivi hana/hayupo ktk project yoyote itakayotoka hivi karibuni? Nimemmiss mnoooo.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Forum statistics

Threads 1,249,905
Members 481,150
Posts 29,714,485