Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kazz0

Kazz0

Member
Joined
Mar 15, 2015
Messages
48
Likes
153
Points
15
Kazz0

Kazz0

Member
Joined Mar 15, 2015
48 153 15
Kama wewe ni mpenzi wa Korean Dramas, karibu katika thread hii tupate ku share kuhusu kazi hizo hatari za mkorea.

Tuambiane;

- Ipi ni drama yako bora ya kila wakati kwako?

- Ni ya aina gani? (Wengi tumezoea kusema za 'mjini' na 'vijijini')

-Nini kinakuvutia sana katika hiyo Drama?

Pia:

- Nani ni Msanii wako Bora wa kiume na wa kike na baadhi ya drama alizoigiza?

- Nani ni sexiest Actor au Actress kwa maoni yako?

- Ipi ilikua Drama yako ya kwanza ya kikorea kuiona?

- Ni Drama gani ya kikorea unaitafuta sana na unapata wakati mgumu kuipata? (Unaweza ukasaidiwa kuipata na mashabiki wengine)

*Pia tumia thread hii kufahamishana kuhusu drama mpya zilizotoka au unayohisi ni nzuri ila haijapata umaarufu sana!!

Karibu tujumuike! Saraghae! Kumooyo!!

=========

Baadhi ya Links za Dramas mbali mbali za Korea...;

Be Strong Geum Soon

Princess Ja Myung Go

THREE DAYS (2014)

Swallow the Sun

Jumong

King Guenchoggo

=====

Links za ku-download drama za Kikorea;

- Watch Drama Online | Korean Drama | Japanese Drama | Taiwanese Drama | Hong Kong Drama | Chinese Drama
- GoodDrama.Net

======

Updated: Kwa mjadala na kubadilishana uzoefu kuhusu series za jumla za movies mbalimbali, za zamani na mpya, Unaweza pia kufuatilia UZI HUU hapa Series (Special thread)
..

Kazi kwako.. Enjoy!
 
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
2,463
Likes
8,802
Points
280
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
2,463 8,802 280
The third charm inaboa balaa
third charm ni moja kati ya poor romantic comedy project niliowahi kuiangalia ndio maana sikuendelea nayo mbele baada ya kufika episode 4.
lakini niliwahi kusoma comment yako hapo nyuma ukisema ya kwamba unavutiwa sana na drama zenye kiss scene?
third charm ni full kiss scene sielewi Numbisa kwa nini haijakuvutia?
mwanadada esom kwake yeye kumbusu mwanamme inaonekana ni jambo la kawaida, inawezekana anapiga mswaki mara 10 kwa siku.
hahahahahahahaaaaaaaa
1544108260306-png.958172
 
Numbisa

Numbisa

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Messages
111,261
Likes
485,346
Points
280
Numbisa

Numbisa

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2016
111,261 485,346 280
Aaah kuna aina za kiss bana zinakera mno,kiss tamu ni ile ngumu kuipata yaan jamaa anasota weee mpaka unajiuliza scene ya kukiss itakuwaje,kiss kama za whats wrong with secretary kim,100days my prince,heirs etc zipo amazing,yummy,awesome hahahahahaa

Bora uliishia hapo,mie niliivuta yote bila kuiangalia mwanzon khaa hasara iliyoje,story mbovu

View attachment 958172
 
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
2,463
Likes
8,802
Points
280
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
2,463 8,802 280
SKY CASTLE DRAMA
kuna wimbo mmoja umeimbwa na muimbaji fulani anajisifia ya kwamba mchumba wake nyumbani kwao ni mboga saba,basi kama yeye ni mboga saba kwenye ulimwengu huu kuna watu maisha yao ni mboga trillion 5.
kumalizika kwa third charm kituo cha JTBC wamekuja na project hii ambayo ndani yake inajaribu kuzungumzia maisha ya familia takribani 5 ambazo zina rekodi nzuri za kimafaanikio kuanzia elimu hadi fedha ambao kwa pamoja wanaishi kwenye ngome ambazo damushin anaziona kwenye internet.
 1. hizi familia kama kawaida yao wanawake ni washindani sana licha ya kuwa ni marafiki wa karibu lakini hakuna hata mmoja anayekubali kuwa chini ya mwenziwe.
 2. kuhusu watoto wao ndio usiseme maisha yao ni kama watoto wa royal family.
 3. ni washindani sana kwenye maswala ya elimu, kama mtoto ni kilaza atalazimika asome kwa lazima ili mradi familia ionekane imejaa heshima mbele ya jamii. Kibaya zaidi baadhi ya wazee wanawalazimisha watoto wasome fani wanazozitaka wao husuani fani ya udaktari eti kwa sababu babu, baba wote ni maprofessa wakubwa sana kwenye sekta ya afya.
 4. kwa upande wangu naiona ipo vizuri kwa sababu waigizaji wote wamebeba uhusika wao kwa kiwango cha PHD ya ngano. hamuna mambo ya kitoto
 
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
2,463
Likes
8,802
Points
280
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
2,463 8,802 280
Aaah kuna aina za kiss bana zinakera mno,kiss tamu ni ile ngumu kuipata yaan jamaa anasota weee mpaka unajiuliza scene ya kukiss itakuwaje,kiss kama za whats wrong with secretary kim,100days my prince,heirs etc zipo amazing,yummy,awesome hahahahahaa

Bora uliishia hapo,mie niliivuta yote bila kuiangalia mwanzon khaa hasara iliyoje,story mbovu
hahahahhahaaaaaaaa
unataka kiss scene iwe tabu kupatikana kama timu pinzani inavyotafuta mpira pindi inapokutana na barcelona ya guardiola.
kibaya zaidi unakutana na muandishi aina ya kim eun sook ambaye anakutaminisha weee mara empty kama ilivyokuwa MR SUNSHINE.
inaonekana hasira zako zilikuwa zaidi ya hasira za meok goo pindi anapokosa bakuli la wali na supu ulipokuwa unaiangalia mr sunshine.
teh teh teh teh
 
Numbisa

Numbisa

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Messages
111,261
Likes
485,346
Points
280
Numbisa

Numbisa

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2016
111,261 485,346 280
Hahahahahhaha muandishi wa mr sunshine shwainii zake kwa kweli alinikomoa vibaya mno.

Nshammiss meok goo na vituko vyake
hahahahhahaaaaaaaa
unataka kiss scene iwe tabu kupatikana kama timu pinzani inavyotafuta mpira pindi inapokutana na barcelona ya guardiola.
kibaya zaidi unakutana na muandishi aina ya kim eun sook ambaye anakutaminisha weee mara empty kama ilivyokuwa MR SUNSHINE.
inaonekana hasira zako zilikuwa zaidi ya hasira za meok goo pindi anapokosa bakuli la wali na supu ulipokuwa unaiangalia mr sunshine.
teh teh teh teh
 
kipozi

kipozi

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2015
Messages
917
Likes
865
Points
180
kipozi

kipozi

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2015
917 865 180
Ooooopppssss finally nimeimaliza Dong Yi!
Jamani nimeliaje pale alipokuja kujengewa na wale masikini? (Final episode)
Hii drama ina mafunzo mengi sana kuliko nyingine zote nilizowahi kuziangalia.
Mali sio kitu bali utu

Tuko sawasawa ktk list,nimeinjoi sana couple ya King na Dong Yi. Na naweza kusema huyu ndiye mfalme bora kabisa ktk drama zote nilizoangalia. Jumong nilimkubali ila muandishi alinikera kwa kutokuwapa nafasi Jumong na Ye Soya.
Bora hii imekuwa na happy ending.
Nipe basi suggestion ya drama nyingine kali ya historical kama hii?
mi pia jumong ilinikera mwishoni haikua na happy ending
 
mkorea

mkorea

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2016
Messages
847
Likes
1,163
Points
180
mkorea

mkorea

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2016
847 1,163 180
Aisee mkuu hiyo kitu naitafuta kwa hamu sana bila mafanikio yoyote yale. Damushin mzigo huu hapa.
Huu mzigo hauchok kuutazama maana yan kuna martial arts na panga za hatari
Kuna siku nilianza mida ya saa 4 iv usiku napiga next tu nashangaa mbona nje kweupe nan anamulika tochi natoka naona kote kweupe nachek muda saa 12 ilibd nicheke tu

Hii series naipa %150 ata ukiniambia ntaje playlists yangu
1.dae Jo young
2.dae Jo young
3.gwangaeto
4.jumong
5.emperor wang gun
 
aminas

aminas

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2015
Messages
2,615
Likes
3,138
Points
280
aminas

aminas

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2015
2,615 3,138 280
third charm ni moja kati ya poor romantic comedy project niliowahi kuiangalia ndio maana sikuendelea nayo mbele baada ya kufika episode 4.
lakini niliwahi kusoma comment yako hapo nyuma ukisema ya kwamba unavutiwa sana na drama zenye kiss scene?
third charm ni full kiss scene sielewi Numbisa kwa nini haijakuvutia?
mwanadada esom kwake yeye kumbusu mwanamme inaonekana ni jambo la kawaida, inawezekana anapiga mswaki mara 10 kwa siku.
hahahahahahahaaaaaaaa
View attachment 958172
Mi ndomana Sikujishughurisha Kuiangalia.

Encounter Damushin Yaani Encounter Hii Drama Ni Ya Kufungia Huu Mwaka Yaani.

Kusema Ukweli Sijawahi Ona Drama Ya Hye Kyo Before Descendants Na Sijaona Drama Nyengine Ya Hye Kyo Kabla Ya Hii Encounter.

Kuna Mahala Ulishawahi Andika Kuwa Joong Ki Alipandishwa Kutoka Kivuli Cha Mke Wake Sikuwa Nimeelewa Ila Baada Ya Encounter Ndo Naelewa.

Hye Kyo Ni Level Za Ji Woon Hili Nalo Sikuwa Najua Ila Baada Ya Encounter Nimejua.

Umu Ndani Bo Gum Kafunikwa Hatari, Japo Uhusika Unamueleza Aigize Anavyoigiza Ila Anaelewa Ukubwa Wa Hye Kyo Ndomna Naona Ata heshima Ndani Ya Maigizo Yao Kwa Macho Yangu Lakini.

Asoiona Aitafute Naona Inakimbizana Na Last Empress kwa Ratings.

Inastahili Heshima Kiukweli.
 
mjr95

mjr95

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Messages
5,492
Likes
6,809
Points
280
mjr95

mjr95

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2016
5,492 6,809 280
Emperor Wang Gun kitu cha hatari hicho usipime nakwambia. Hahahaha King Gwangaeto kuna baadhi ya masuala ilinifunza mpaka leo sijutii kuitizama. Jumong ndio Korea Drama kwangu kwa mda wote. Sasa naitafuta hiyo King Dae Jo Young huo mzigo nina hamu nao yaani we acha tu. Naona umesahau mzigo mmoja unaitwa The Immortal Yi Soon Shin kitu cha hatari hicho, akili nyingi mpaka unalewa. Tafuta huo mzigo kama bado haujautizama, historical Drama ndio drama bora kwangu.
Huu mzigo hauchok kuutazama maana yan kuna martial arts na panga za hatari
Kuna siku nilianza mida ya saa 4 iv usiku napiga next tu nashangaa mbona nje kweupe nan anamulika tochi natoka naona kote kweupe nachek muda saa 12 ilibd nicheke tu

Hii series naipa %150 ata ukiniambia ntaje playlists yangu
1.dae Jo young
2.dae Jo young
3.gwangaeto
4.jumong
5.emperor wang gun
 
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
2,463
Likes
8,802
Points
280
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
2,463 8,802 280
Asante.....nitaicheki
itapendeza sana kama utachukua uamuzi wa kuiangalia kwa sababu ipo vizuri sana na ni hadithi ya kweli.

hymn of death.
namuomba Mungu anijaalie nishuhudie project nyengine ya lee jong suk kabla hajaenda kutumikia taifa lake kijeshi
 
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
2,463
Likes
8,802
Points
280
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
2,463 8,802 280
mi pia jumong ilinikera mwishoni haikua na happy ending
 1. labda ulipendelea mfalme dongnmyeong jumong na malikia soseono waendelee kuwa pamoja?. historia lakini haipo hivyo kwa sababu bila ya soseono kuondoka goguryeo taifa la baekje lisingelikuwepo.
 2. labda ulitaka jumong na mke wake wakutane mapema? wahusika wakuu wa ile drama ni chumong na soseono na ndio walikuwa ni msingi wa kuwapigania wagojoseon,ndio maana hata screen time yao kati ya jumong na yesoya ili ni ndogo sana ukilinganisha na ya jumong na soseono.
 3. ninachowapendea wakorea hadithi zao mara nyingi hawapindishi ukweli kwa dhumuni la kutaka kumfurahisha mtazamaji bali wanaonyesha ukweli ili kimfundisha mtazamaji ili apate kuelewa uhalisia wa historia.
ulishawahi kuangalia emperor of the sea?
naamini mwisho wake ndio utazidi au ulizidi kukuchukiza lakini ukweli wa historia ulibaliki vile vile.
jumong haikuwa full fictious drama.
 
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
2,463
Likes
8,802
Points
280
Damushin

Damushin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
2,463 8,802 280
Aloanza kuangalia clean with passion, boyfriend, na memory of alhambra aniambie kama ni nzuri
kwa uoni wangu kwenye alama 10.
 1. boyfriend / encounter = 7.3
 2. memories of alhambra = 7, ukitoa episode za wiki hii.
 3. clean with passion for now = 6.5
 4. sky castle drama = 7.5
 5. a pledge to god = 7.5, ukiondoa episode za wiki hii.
 6. the last empress = 6.8
 7. less than evil drama = 8.
bila ya kusahau maneno yangu na uelewa wangu si sheria.
 
aminas

aminas

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2015
Messages
2,615
Likes
3,138
Points
280
aminas

aminas

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2015
2,615 3,138 280
kwa uoni wangu kwenye alama 10.
 1. boyfriend / encounter = 7.3
 2. memories of alhambra = 7, ukitoa episode za wiki hii.
 3. clean with passion for now = 6.5
 4. sky castle drama = 7.5
 5. a pledge to god = 7.5, ukiondoa episode za wiki hii.
 6. the last empress = 6.8
 7. less than evil drama = 8.
bila ya kusahau maneno yangu na uelewa wangu si sheria.
The Last Empress Naomba Iwe Ya Tatu Pleez.
Kati Ya Izo Zote Nimeangalia Nne.

Ila Naweza Sema Encounter na Last Empress Ndio Best kati ya Nne Nilizoangalia

Alhambra Nimeielewa Ila Ina type Za W, Kumbe Nikaja Jua Ni Muandishi Mmoja..

Clean With Passion Hii Ngoja Kwanza Niaangalie Tena Na Tena.
 
Forum statistics

Threads 1,238,950
Members 476,289
Posts 29,337,676