Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Nina hamu kweli nijue kilicho jili baina ya hao viumbe viwili.
ISNF5vB.jpg

Kaenda Kupanda Public Trans
 
Damushin Sunbae acha vituko ndugu mi sina ujanja wowote ule wala usiniogope, mm bado ni mwanafunzi kwenu. EMPTY, aminas, UHURU JR, Prishaz pamoja na ww Damushin Sunbae nyinyi nyote kwa pamoja ni walimu wangu wala Mm siwazidi chochote kabisa. Na ninafurahi sana kuwa na walimu kama nyinyi kwa pamoja.

Hahaa Damushin Sunbae huyo kiumbe wa kuitwa Admiral Yi Soon Shin alikuwa balaa sio mchezo, maamuzi anayo chukua yanadhihirisha kweli ni General aliye stahili cheo hicho kabisa. Wale wazee wanao mchongea kwa Mfalme Seonjo ili tu aonekane mbaya kwakweli kuna kipindi natizama wanacho kifanya natamani ata niwarukie Hahaa. Inaonyesha kabisa tawala za kifalme hapo zamani hawa maGeneral walikuwa wanaogopeka sana kutokana na ile nguvu walio kuwa nayo ndicho kitu kilicho kuwa kinamuogopesha Mfalme Seonjo. Alihofia kutokana na ile nguvu aliyonayo Admiral Yi Soon Shin pamoja na watu wanavyo mpenda alihofia huenda akapinduliwa. Kumbe ata wazo hilo Yi Soon Shin hakuwa nalo kabisa yy lengo lake ilikuwa kuwafukuzia mbali Japanese.

Shauku niliyo nayo ni kujua ni vipi huyu Yi Soon Shin alijiunga na Jeshi la Majini mpaka kuwa Kiongozi wao. Maana mkuu pale historia yake inaanza kuonyeshwa toka utotoni anaonekana yupo yupo tu sasa nataka nijue ilikuwaje mpaka akapata hicho cheo kikubwa namna hiyo. Hahahaa ndio maana nikianza kutizama Drama sitaki niishie katikati huwa najitahidi nimalize kabisa. Ww ukifika hapo pumzika nitakuwa nakujuza Kinacho kuwa kinaendelea.
hili andiko lako nimelirejea kulisoma mara nne ndipo angalau nikapata cha kukujibu, kiukweli hili andiko limenifanya muda huu niitafute episode ya 11 hadi ya 15,wakati asubuhi nilisema nataka niiweke kiporo sasa kwa huu ushawishi wa andiko lako kwa nini nisikuite sunbaenim?
kiukweli nimevutiwa zaidi na urafiki wa tokea utotoni kati ya ryu seung ryong, yi soon shin na won kyun. huyu ryu seung ryong baadae anakuja kuwa na nyadhifa mbali mbali kwenye utawala wa mfalme seonjo na kwenye vita ya imjin war alishika nyadhifa ya waziri wa ulinzi na ndie aliekuwa akimpa support kubwa sana yi soon shin. baada ya kuona mfalme seonjo amekuwa na hofu na yi soon shin aliamua kuacha shughuli za kisiasa, kama sikosei episode ya 3 ya drama hii anaamua kupeleka barua ya kuacha kazi kwa mfalme seonjo.
 
hili andiko lako nimelirejea kulisoma mara nne ndipo angalau nikapata cha kukujibu, kiukweli hili andiko limenifanya muda huu niitafute episode ya 11 hadi ya 15,wakati asubuhi nilisema nataka niiweke kiporo sasa kwa huu ushawishi wa andiko lako kwa nini nisikuite sunbaenim?
kiukweli nimevutiwa zaidi na urafiki wa tokea utotoni kati ya ryu seung ryong, yi soon shin na won kyun. huyu ryu seung ryong baadae anakuja kuwa na nyadhifa mbali mbali kwenye utawala wa mfalme seonjo na kwenye vita ya imjin war alishika nyadhifa ya waziri wa ulinzi na ndie aliekuwa akimpa support kubwa sana yi soon shin. baada ya kuona mfalme seonjo amekuwa na hofu na yi soon shin aliamua kuacha shughuli za kisiasa, kama sikosei episode ya 3 ya drama hii anaamua kupeleka barua ya kuacha kazi kwa mfalme seonjo.
Damushin Kuna Kitu Nakifatilia Kuhusu Nyuma Ya Kpop Coz Hii Ndo Nimeona Watu Wengi Wanaongelea Tofauti Na Kdrama.
Kuna Madudu Sana Kwenye Hii Kitu
Kweli Kila Penye Nzuri Kuna Bays.
 
https://ondramanice.io/drama/the-book-of-corrections-jingbirok--detail
  1. @mjr95,EMPTY dongsaeng mukipata nafasi baadae muitafute na hii inayoitwa jingbirok the memoir of imjin war.hadithi yake inafanana na tutakachokiona kwenye admiral yi soon shin drama. ila ndani ya drama hii anazungumziwa ryu seong ryeong na harakati zake za kuifanya joseon inakuwa na amani kwa kujiandaa kijeshi dhidi ya uvamizi wowote utakaotokezea lakini bahati mbaya baadhi ya mawaziri na mfalme seonjo walimpuuza. aigooo siwamalizii kuwahadithia
  2. jingbirok maana yake ni kitabu cha kujisahihisha na kimeandikwa na msomi ryu seung ryong ambaye kwenye comment yangu ya juu nimemuelezea kama ni mtu wa karibu wa yi soon shin ambaye kwenye vita ya imjin ndio alikuwa muhusika mkuu wa masuala ya kijeshi na pia aliwahi kuwa waziri mkuu.Aliandika kitabu hiki baada ya kuachana na harakati za siasa chini ya utawala wa mfalme seonjo.kitabu hiki kimekuwa ni moja kati ya chanzo muhimu kinachotumika kuelezea uhusiano wa mgogoro kati ya china,korea na japan.
  3. mwaka 1969 serikali ya korea ilikichaguwa kitabu hiki kama ni miongoni mwa hazina 132 bora za utawala wa korea (National Treasures of South Korea)
  4. Ryu Seong-ryong aliandika Jingbirok ili kuwa kama ni ukumbusho wa kuzuia uvamizi wa vita kama ya imjin (1592-1598) usitokee tena, kutafakari juu ya makosa walioyafanya ya kupuuzia taarifa za japan kujianda na uvamizi,jambo ambalo lilipelekea joseon kupoteza miji yake mitatu na kusababisha vifo vya maelfu ya wananchi wasio na hatia na wengineo kutumikishwa utumwani nchini japan na hata china.
  5. kim sang joong ndiye ameigiza uhusika wa ryu seong ryeong na kim tae woo ndiye ameigiza uhusika wa mfalme seonjo
    20141217002045_0.jpg
  6. hadithi ya drama hii inaanza kabla ya vita ya imjin na vita ya noryang ambayo ilipelekea kifo cha admiral yi soon shin
  7. kama si juhudi kubwa za kidiplomasia na za kivita alizozichukua ryu seong ryeong basi tungelishuhudia joseon ikitawaliwa na japan na ming china, na pengine kwa wakati huu taifa la korea lisingelikuwepo.
  8. wakati vita ilipozodi mfalme seonjo aliamua kuikimbia nchi yake kwa kupitia mto yalu na kujificha nchini china (ming), cha kushangaza wafuasi wake wengi walikubaliana na maamuzi ya mfalme lakini ryu seung ryong alimshauri mfalme seonjo asifanye hivyo kwani kitendo hicho kingeliwafanya japan na ming (china) kuigawa joseon,licha ya kuwa ming walikuwa wakiisaidia joseon kwenye vita hiyo lakini kwenye mali hakuna udugu wala urafiki wa kudumu.
  9. ryu seung ryeong binafsi ndio alikuwa akiwaongoza yi soon shin na general kwon yun kwenye vita ya ardhini dhidi ya wajapan. ukiangalia admiral yi soon shin kuanzia episode ya 4 watatu hawa wanakuwa marafiki sana tokea udogoni mwao.
  10. baada ya vita kumaliza wapinzani wake wa kisiasa walimshinda kwenye vita chafu ya kiutawala na ndipo akavuliwa nyadhifa zote na kuamua kuondoka kwenye mji mkuu wa hanyang na kuelekea Hahoe Village, North Kyungsang Province, kwenye mji mkuu hakurudi tena ndipo akaandika kitabu hiki cha jingbirok.
  11. jina lake la utotoni aliitwa Igyeon, shuleni alikuwa akiitwa Seoae, kwenye drama ya admiral yi soon shin kwon yun anapenda kumuita yi seong ryeong jina la bookworm kwa sababu anapenda kusoma vitabu.
  12. Lee Kwang Ki (ameigiza nafasi ya Ha Ryun ndani ya Jeong Do Jeon drama) ameigiza nafasi ya konishi yukinaga na Kim Kyu Cheol ameigiza uhusika wa tayotomi hideyoshi, kwenye admiral yi soon shin ameigiza uhusika kama ni rafiki wa yi soon shin
    UHzmpGp.jpg

  13. Lee Jung Yong ameigiza nafasi ya kato kiyomasa na cha kufurahisha kwenye admiral yi soon shin drama pia ameigiza nafasi ya kato kiyomasa.hahahahahaaa bonge la zari
    55h0OAT.jpg
  14. kwangu mimi namfananisha ryu seung ryong na jung do jeon kutokana na harakati zao za kisiasa na kuwa na uchungu na maisha ya wananchi kutokana na mateso wanayokutana nayo wakati wa vita, nadhani tofauti yao ni kwamba ryu seung ryong alipambana peke yake ila jung do jeon baadae alizunguukwa na watu kama yi seong gye, yi bangwon ambapo kwa pamoja walifanikiwa kuuangusha utawala a goryeo ulioanzishwa na mfalme wang guhn ambaye naye alianzisha taifa la goryeo baada ya kumpindua goong yae.
 
aminas noona bila ya kusahau leo hii black knight drama inaendelea, nina wasi wasi humu ndani tunaangalia watu wawili tu ndio maana nimekuita peke yako.
naomba radhi kwa yeyote atakayekuwa hajafurahishwa na uamuzi wangu.
 
aminas noona bila ya kusahau leo hii black knight drama inaendelea, nina wasi wasi humu ndani tunaangalia watu wawili tu ndio maana nimekuita peke yako.
naomba radhi kwa yeyote atakayekuwa hajafurahishwa na uamuzi wangu.
Leo Silali Mpka Nione Kwanza.
Mie Tena Na Rae Won.!!
Nimeona Teaser Zake Iko Ngumu Ngumu Kidogo leo.
 
aminas hii playlist nimeshaihifadhi kwenye kimeo changu ngoja leo usiku niisikilize, si unajua mimi ni mpenzi mkubwa wa hizi melody na ballad kuliko pop. pumzika kwa amani kim jong hyun


1 - 0:00 - END OF A DAY (하루의 끝)
2 - 4:37 - I'm Sorry (미안해)
3 - 8:48 - Lonely (feat. Taeyeon (태연))
4 - 12:54 - 따뜻한 겨울 (Our Season)
5 - 16:58 - 가을이긴 한가 봐 (It Must Be Autumn) (feat. Go Youngbae)
6 - 21:04 - 1000
7 - 25:07 - 멍하니 있어 (Just Chill)
8 - 28:33 - Love Is So Nice
9 - 32:00 - 눈싸움 (Blinking Game)
10 - 35:38 - Love Belt (feat. Younha (윤하))
11 - 39:09 - Fine (그래도 되지 않아?)
12 - 42:14 - Fireplace (벽난로)
13 - 46:38 - Moon
14 - 49:22 - RED
15 - 52:35 - Suit Up
16 - 56:25 - MONO-Drama (일인극)
17 - 1:00:40 - Déjà-Boo (데자-부)
18 - 1:04:10 - Like You
 
aminas hii playlist nimeshaihifadhi kwenye kimeo changu ngoja leo usiku niisikilize, si unajua mimi ni mpenzi mkubwa wa hizi melody na ballad kuliko pop. pumzika kwa amani kim jong hyun


1 - 0:00 - END OF A DAY (하루의 끝)
2 - 4:37 - I'm Sorry (미안해)
3 - 8:48 - Lonely (feat. Taeyeon (태연))
4 - 12:54 - 따뜻한 겨울 (Our Season)
5 - 16:58 - 가을이긴 한가 봐 (It Must Be Autumn) (feat. Go Youngbae)
6 - 21:04 - 1000
7 - 25:07 - 멍하니 있어 (Just Chill)
8 - 28:33 - Love Is So Nice
9 - 32:00 - 눈싸움 (Blinking Game)
10 - 35:38 - Love Belt (feat. Younha (윤하))
11 - 39:09 - Fine (그래도 되지 않아?)
12 - 42:14 - Fireplace (벽난로)
13 - 46:38 - Moon
14 - 49:22 - RED
15 - 52:35 - Suit Up
16 - 56:25 - MONO-Drama (일인극)
17 - 1:00:40 - Déjà-Boo (데자-부)
18 - 1:04:10 - Like You

Eeeh! Mola.
Mi nimedownload Kipindi Cha Ye Huiyeol Sketchbook Special Summer Episode
Umo ndani Ameunganisha Zile Best Ballad,Akiwemo Hyoshin,IU,Taeyon, Lee Juck Ailee, Urban Zakapa,Oh hyuk Na Wengine Kibao Basi Hii Nikilala Ipo Maskioni Nikiamka Ipo Maskioni Mpka Baadhi Ya Nyimbo nimeaza Zishika.

Uyu Oh Hyuk Ana Sauti Flani Ivi Dah!!!
 
Back
Top Bottom