Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

kuna season moja yakikorea inaitwa ugly alert nibomba sana. kama unaitafuta ingia YouTube search ugly alert sehemu ya 1 imetafsiliwa kiswahili nouma sana
 
005xvInegw1egn03vkueij31400p0gp4.jpg

Soo Hyun
 
mjr95 nimeanza kukuogopa kwa haya maandishi yako mawili ya mwisho ndani ya thread hii na itanibidi nikuite sunbae, tafadhali sana EMPTY dongsaeng usiniite tena sunbae kwa sababu anayestahili heshima hii ameshajidhihirisha baada ya kujificha kwenye mchicha kwa muda mrefu akidhania hatojulikana.

without discipline, order will crumble. And without order we can't fight the enemy. I would do worse to stop the order from crumbling
maneno hayo nakumbuka aliyazungumza kwenye episode ya tatu baada ya wanajeshi watatu kuamua kujaribu kukimbia kambini na ndipo akatoa amri ngumu sana ya kuuliwa na vichwa vyao kuwekwa katikati ya mji ili iwe fundisho kwa yeyote yule atakayejaribu kwenda kinyume na amri ya jeshi la majini haijalishi anayevunja amri ana cheo kiasi gani.
kwenye andiko lako umemaliza kila kitu kinachomuhusu mwanadamu huyu anayejulikana kwa jina la yi sun shin ambaye takribani vita vingi alivyopambana alikuwa na upungufu wa wanajeshi na hata huduma muhimu kama chakula,usafiri na hata dhana za kisasa za kupambana na maadui.
jaribu kufikiria joseon walikuwa wanategemea zaidi mishale na majambia wakati wajapan walikuwa na ubongo wa mzungu (bunduki) lakini bado japan aliambulia kipigo chenye kuumiza kutoka kwa yi soon shin, unajua kwa nini japan walikuwa wanashindwa na joseon?
sababu ni ndogo tu wajoseon walikuwa na mwanadamu mwenye ubongo hatari zaidi ya bunduki, wahenga wanasema ni bora unyimwe mali kuliko kunyimwa maarifa.
mjr95 nitakapofikia episode ya 10 ya hii drama nategemea kuiweka kiporo kwanza ili niivutie kasi ya kuja kuiendeleza tena.
sisi sote ni wanajeshi wenye dhambi kubwa sana ya kuwaua maelfu ya ndugu zetu ndani ya bahari hii kwa miaka 7,kama tutashindwa kuimaliza vita hii kwa ushindi basi tutakuwa tumeshindwa kurudisha furaha na amani ya wanachi wa joseon na pia tutakuwa tumeshindwa kuwafanya marehemu kupumzika kwa amani huko waliko na dhambi zetu zitaendelea kubakia, leo hii wanajeshi 16000 tunakwenda vitani huku sura zetu na nafsi zetu zina dhambi lakini kesho tutarudi huku sura zetu zikiwa na furaha ya ushindi,katu tusiache hata meli moja na mwanajeshi mmoja wa kijapani kurudi kwao akiwa mzima wa afya.
lakini maisha yote wanasiasa ndio watengenezaji na waharibifu wa nchi jaribu kufikiria jinsi gani mfalme seonjo alivyokuwa na bifu na mtumishi wake kisa ni kwamba yi soon shin anapendwa sana na watu kuliko yeye, ndio maana mimi Damushin siipendi sana siasa wala jukwaa la siasa.
duh! huku kwetu vilipotokezea vita vya kagera baadhi ya wazee niliwahi kuwasikia wakijisifia eti walikula sabuni ili wapate ugonjwa wa kuharisha na wasichaguliwe kwenda vitani, hahhahahhhahahahhhahaha chezea uhai.pumbavuuuuuuuu
 
Jamani hebu nitajieni upcoming kdrama mnazozisubiria kwa hamu.
Hahaaa Mkuu UHURU JR kuna Drama kama Tatu nazisubiri kwa hamu kubwa sana aisee.

RADIO ROMANCE
186f1e91cea39b06136a27af588e56b1.jpg
Ni moja kati ya Drama tatu ninazo zisubiri kwa hamu sana. Kinacho nafanya niisuburi kwa hamu kubwa namna hiyo ni huyo Mdada Song Geu Rim natamani nione kipaji chake kilivyo kikubwa hasa upande wa hizi drama za Romance. Nilivutiwa nae kwenye ile Drama ya While you were sleeping Mdada huyu alinivutia sana. Nataka nione humo ndani amefanya nn baada ya kuaminiwa na kupewa nafasi. Pia nataka nione Kijana Ji Soo Ho kafanya nn humo ndani baada ya kucheza kwa umaridadi mkubwa katika Drama ya Because this is my first life. Hizo sababu zinafanya niisuburi kwa hamu na shauku kubwa mno. Radi Romance itakuwa hewani kuanzia Tarehe 29 Januari na itakuwa ikirushwa kila Jumatatu na Ijumanne katika kituo cha KBS 2.

MR. SUNSHINE
6e384f28b45e22473baa76d94959f47e.jpg
Sababu kuu ya kuisubiri ni kutokana na huyo muhusika mkuu Lee Byung Hun. Huyo Mkuu Binafsi sijabahatika kutizama Drama yake yoyote baada ya ile ya IRIS 1, huenda zipo tu nyingi lakin sijataka kuzitafuta. Kwahiyo hicho kitendo cha kukaa mda mrefu bila kutizama drama yake yoyote hasa ukizingatia kwenye IRIS 1 alitulia vizuri mno ndio kinanifanya niisuburi kwa hamu nijue kaja kivip tena. Wanadai itaanza kuonyeshwa kati ya Juni ama Julai kwenye kituo cha tvN.

ARE YOU HUMAN TOO?
f788a8054ef1c0d23aa7ef571daa956e.jpg
Hahaha drama ya mwisho ninayo isubiri kwa hamu ni hiyo. Kinacho nifanya niisuburi ni jina lake. Hahaa jina lake tosha Mm linafanya niisuburi kwa hamu kubwa mno.

Mkuu UHURU JR kwangu mm hizo ndio Drama ninazo zisubiri kwa hamu na shauku kubwa. Ngoja kina Damushin Sunbae, EMPTY, aminas, Prishaz na wengineo watakuja wakujuze ni drama zipi wanazo zisubiri kwa hamu.

mjr95.

 
Back
Top Bottom