Kwa Wapendwa Wabunge wetu!

Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
906
Habari Ndugu zangu,

Kwa miaka mingi sasa nimekuwa niosikia na kuona, kama ambavyo naamini wengi mmekuwa mkiona na kusikia hii tabia ya ajabu ya waheshimiwa wabunge wetu, na sana wa CCM.

Imekuwa ni kawaida sasa (ingawa sijui kama huwa wanafikiria kweli) kwamba mbunge anaposimama kuchangia hoja ama muswada, ataanza na kuimba sifa zisizo za msingi wa wakubwa wake na marafiki, halafu ataendelea kukosoa kwa kina hoja, huku akitoa kasoro kibao na mapungufu yaliyo bayana na yasiyo bayana. Halafu humalizia bila haya kwa "kuunga mkono hoja"

Kwani hasa ni nini maana ya kupoteza muda wote huo kukosoa kitu unachokiunga mkono? huu kama siyo ujuha ni nini hasa? Na ni kwa nini Mbunge asisimame na kuunga tu mkono hoja na kukaa? What is the point kukosoa? Na hapo tunakuwa tumemsaidia nini Mwananchi kama pamoja na ubovu wote uliopo tunaishia "kuunga mkono" na kuitikia "ndiyooooo" kama vyura?

Sidhani kama kuna sababu ya kufanya huu utoto. Huu ni unafiki na usaliti kwa wananchi. Na hata kama mwananchi haelewi kinachoendelea bado siyo haki wala siyo sawa kufanya hivyo na ni Mbunge kutotekeleza wajibu wake.

Hivi kuna mtu au Mbunge yeyote mwenye sababu nzuri ya kutetea tabia hii?
 
habari ndugu zangu,

kwa miaka mingi sasa nimekuwa niosikia na kuona, kama ambavyo naamini wengi mmekuwa mkiona na kusikia hii tabia ya ajabu ya waheshimiwa wabunge wetu, na sana wa ccm.

Imekuwa ni kawaida sasa (ingawa sijui kama huwa wanafikiria kweli) kwamba mbunge anaposimama kuchangia hoja ama muswada, ataanza na kuimba sifa zisizo za msingi wa wakubwa wake na marafiki, halafu ataendelea kukosoa kwa kina hoja, huku akitoa kasoro kibao na mapungufu yaliyo bayana na yasiyo bayana. Halafu humalizia bila haya kwa "kuunga mkono hoja"

kwani hasa ni nini maana ya kupoteza muda wote huo kukosoa kitu unachokiunga mkono? Huu kama siyo ujuha ni nini hasa? Na ni kwa nini mbunge asisimame na kuunga tu mkono hoja na kukaa? What is the point kukosoa? Na hapo tunakuwa tumemsaidia nini mwananchi kama pamoja na ubovu wote uliopo tunaishia "kuunga mkono" na kuitikia "ndiyooooo" kama vyura?

Sidhani kama kuna sababu ya kufanya huu utoto. Huu ni unafiki na usaliti kwa wananchi. Na hata kama mwananchi haelewi kinachoendelea bado siyo haki wala siyo sawa kufanya hivyo na ni mbunge kutotekeleza wajibu wake.

Hivi kuna mtu au mbunge yeyote mwenye sababu nzuri ya kutetea tabia hii?



mkuu,

wabunge wa ccm huwa wanasinzia huku wakiwaza hiyo biashara,
na akiamka kuchangia anatapika utumbo kama unavyoona mkuu
 
Back
Top Bottom