Kwa wapendanao: Hii inawahusu zaidi akina dada

Alvin A.

JF-Expert Member
Oct 14, 2016
2,868
3,624
Heshima kwenu wanawake na wanaume wa hapa jamvini,

Lengo siyo kupashana, bali kukumbushana.

Mada ya leo ni hii:

Inapokuja ishu ya mahusiano, kuna jambo hutokea endapo utasalitiwa na yule uliemuamini. Unaposalitiwa, ule ujasiri wa kujitoa tena kwa mwenzako hupotea, mtu unaanza kuwa na mawazo, na kujiuliza huyu mtu alikosa nini kwangu hata akaamua au ameamua kunifanyia hivi.
.
Unaposalitiwa, mtu huanza kuchukua tahadhali, hupoteza kabisa uwezo wa kuamini tena na unakuwa makini mno kwenye ishu za mahusiano. Kimsingi unapata jambo fulani ambalo wanasaikolojia wanaliita "post-trauma skepticism" ambapo mtu unapoteza imani na kuhoji kila jambo ambalo mwenzako atalifanya.
.
Pale unapoumizwa na watu uliowapenda, pale ambapo mtu uliyempenda kwa moyo wote na kumuamini anavyokuachia maumivu, hutokea, ukapata aina fulani ya hekima. Hekima hiyo ni gharama ya kuumizwa kwako na mahusiano lakini hasara yake ni kwamba, huchukua muda mrefu kuamini tena katika upendo wa kweli, kupenda tena na kumuamini mtu.
.
Anyway, nilikuwa nataka kusema kwamba, unapokabiliana na maumivu ya kukataliwa, kuachwa ama kusalitiwa, kuna Hekima unatakiwa uipate ambayo itakufungua ufahamu kwamba, sio kila mtu uliyenae anayo malengo kama uliyonayo kichwani mwako!
.
Hivyo basi, nakushauri, fanya sana uchunguzi kabla ya kumkabidhi mtu baki moyo wako!

FB_IMG_1571983883969.jpeg
FB_IMG_1571580429548~2.jpeg
 
Back
Top Bottom