Kwa Wanayanga tu: Yanga inakata punzi kipindi cha pili au ni mbinu zao za kiufundi?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,288
12,579
Inaonekana kama vile Yanga inacheza michezo tofauti kipindi cha kwanza na kipindi cha pili. Kipindi cha kwanza Yanga inacheza soka Safi na la kisasa na kushinda mabao dakika za mwanzo za mechi.

Kipindi Cha pili Yanga inapunguza Kasi lakini wapinzani wanashindwa kuchomoa BAO waliliofungwa ingawa inaonekana kama vile Yanga haichezi vizuri, kitu kinachotafsiriwa na wengi kuwa Yanga imekata punzi kipindi Cha pili.

Ukweli ni upi, Yanga inalinda nguvu zake kipindi cha pili ili kujiandaa na mechi ijayo hasa baada ya kushinda kipindi Cha kwanza au Yanga inakata punzi kipindi cha pili?
 
Yote kheri tu, as long as hamna timu iliyofanikiwa kuifunga yanga walau goli moja hata hicho kipindi cha pili ambacho wanasema timu inachoka.

Ndipo hapo ushahidi kuwa timu inachoka unakosa mantiki.
 
Timu inakata pumzi ni pale itakapofungwa maana wachezaji watakua hawana nguvu ya kupambana.

Wapinzani hawarudishi magoli, mantiki ya kukata pumzi inatoka wapi?
 
Yote kheri tu, as long as hamna timu iliyofanikiwa kuifunga yanga walau goli moja hata hicho kipindi cha pili ambacho wanasema timu inachoka.
Ndipo hapo ushahidi kuwa timu inachoka unakosa mantiki.
Wanashindwa kuthibitisha kuwa timu inachoka. Kama ingekuwa inachoka kipindi Cha pili huenda Yanga ingekuwa inafungwa kipindi Cha pili
 
Nadhani huu mfumo wa kocha niwakubadili yaani timu ikishapata goli moja inaridhika na wakati ina nafasi yakushinda magoli mengi zaidi kitu ambachokinaweza kuathiri matokeo ya timu dakika za mwishoni
 
Sifien tu ujinga mbinu mbinu gan kutunza nguv mechi inayofuata ndio nn.. Hv vigoli ipo siku tutakuja chomolewa tutarud hapa kutukana sahv semeni mbinu tu
 
Nadhani huu mfumo wa kocha niwakubadili yaani timu ikishapata goli moja inaridhika na wakati ina nafasi yakushinda magoli mengi zaidi kitu ambachokinaweza kuathiri matokeo ya timu dakika za mwishoni
Of course. Italeta maana pale ambapo timu imeshinda magoli mawili na zaidi ila sio goli moja.

Sana sana kocha anatakiwa atumie kipindi cha kwanza kupiga magoli mengi ili wapinzani wakija kuizoea mechi na kuanza kujiamini wawe wamechelewa.

Waamuzi wetu pia kuna mahala wanakwama. Just imagine goal 🥅 mechi kati ya yanga na geita zilkua offside.
 
Ukweli ni upi, Yanga inalinda nguvu zake kipindi Cha pili ili kujiandaa na mechi ijayo hasa baada ya kushinda kipindi Cha kwanza au Yanga inakata punzi kipindi Cha pili?
ni mbinu za kiufundi, ingawa sio kwa ajili ya mechi ijayo kama ulivyosema bali kwa ajili ya kupata matokeo katika mechi hiyo hiyo husika. Ni wakati wetu wa kuvimba, anayesema tunakata pumzi anajidanganya
 
Of course. Italeta maana pale ambapo timu imeshinda magoli mawili na zaidi ila sio goli moja.

Sana sana kocha anatakiwa atumie kipindi cha kwanza kupiga magoli mengi ili wapinzani wakija kuizoea mechi na kuanza kujiamini wawe wamechelewa.

Waamuzi wetu pia kuna mahala wanakwama. Just imagine goal 🥅 mechi kati ya yanga na geita zilkua offside.
Nadhani shida sio mfumo wa kocha bali wachezaji wa Yanga kushindwa kuzitumia nafasi zinazotengenezwa. Yanga Ina uwezo wa kupata magoli 3 kwenye kipindi Cha kwanza kama nafasi zote zingetumika vizuri. Yacouba peke yake anapoteza nafasi 2 hadi 3 za kufunga magoli, Faisal 1 hadi 2, na Mayele 1. Kama watarekebisha tatizo la kupoteza nafasi mfumo huu wa Nabi utawatesa wengi. Mnafunga magoli mengi kipindi Cha kwanza na kitunza energy kipindi Cha pili ili kupunguza majeruhi na kihifadhi energy. Maana ligi bado ni ndefu sana.
 
ni mbinu za kiufundi, ingawa sio kwa ajili ya mechi ijayo kama ulivyosema bali kwa ajili ya kupata matokeo katika mechi hiyo hiyo husika. Ni wakati wetu wa kuvimba, anayesema tunakata pumzi anajidanganya
Inazishangaza timu nyingi, Yanga imekata punzi lakini goli halirudi.

Yanga inapocheza slow game kipindi Cha pili inawapa makocha wa timu pinzani mahala pa kutokea na kujitetea baada ya kufungwa. Mara nyingi utawasikia wakisema timu ilirebisha ilirekebisha makosa kipindi Cha pili hivyo hatukufungwa goli lingine. Najiuliza kama mlirekebisha makosa kwanini hamkurudisha magoli mliyofungwa kipindi Cha kwanza?
 
kwa hiyo kumbe kweli ni kukata pumzi, sio mbinu?
Hiyo ni kwa mujibu wa wachambuzi wetu wanaosema timu imekata punzi. Hawajiulizi kwanini kama timu imekata punzi timu hazitumii meanya huo kusawazisha? Huo ndio ushahidi kuwa Yanga haikukata punzi bali ni mbuni za kocha Prof. Nabi na benchi lake.
 
hiyo mbinu ya kufunga kagoli kamoko dakika za mwanzo ikishagundulika tu hamtashinda tena game nyie matopwinyo. subiri shida zenu zitaanzia mtakapoanza kutembelea mikoa ya kusini Kule mbeya. sasahiv kuna vigongo vitatu(mbeya kwanza, city na prison)vyote havipo tayari kupoteza match.
 
Utelezi huu wa Yanga tayari umeshawaangusha Simba ngao ya jamii, KMC, Geita na Kagera sugar hadi Sasa. Kikosi Chao ni kipana hatari na kinazidi kuelewana siku hadi siku. Watapigwa tu aisei.
 
Back
Top Bottom