Kwa Wanawake: Zijue dalili za Mwenza anayeweza kukuua katika Mahusiano, tafakari mahusiano yako na Uchukue Hatua

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu, takriban wanawake na wasichana 47,000 duniani kote waliuawa na wapenzi wao wa karibu au wanafamilia wengine mwaka 2020.

Hii ina maana kwamba, kwa wastani, mwanamke au msichana huuawa na mtu katika familia yake kila baada ya dakika 11.

Kuna jambo linafaa kufanywa kukomesha mauaji hayo. Kwa kuanzia, wanawake wanahitaji kujua dalili za kuangalia ili kuepuka kuwa wahasiriwa wanaofuata wa mauaji.

Je, utamtambuaje Mpenzi au Mume anayeweza kukuua?

Mwanasaikolojia wa Dar es Salaam, Charles Nduku anasema, wale wapenzi possessive/umiliki wana uwezekano mkubwa wa kuua. Anasema ni kawaida kwa wanaume kuwaonea wivu wanawake wao lakini wivu wa kupindukia na kudhibiti kila kitu katika maisha ya mwanamke kunaweza kuwa hatari mara mwanamke huyo anapoamua kuendelea na maisha yake

Wanaume wenye uwezo na udhibiti hawako tayari kuona mwanamke akijiamulia mambo yake mwenyewe. Hii inawafanya kuwa na upeo zaidi na kuwa huru, uhuru ambao wanaume huutafsiri kama kukosa heshima. Ikiwa mwanamke hatakuwa mwangalifu vya kutosha kusoma reactions ya mwanamume wanapogombana, yuko katika hatari ya kupoteza maisha yake ikiwa mambo hayataenda vizuri

Vitisho ni ishara nyingine pamoja na unyanyasaji wa kimwili. Vitisho kama vile, ‘hakuna kuamua mambo peke yako,’ ‘siku moja utajuta ulichonifanyia’ vitisho kama hivi huchukuliwa poa lakini ni vya kufikirisha. Kama mtu anakupiga na kutoa vitisho waziwazi ni dhahiri kuwa ipo siku atashindwa kujicontroll

Unyanyasaji ni ishara tosha kwamba anaweza kukuua. Na inapotokea mara ya pili, unyanyasaji huwa mkali zaidi kuliko mara ya kwanza. Hii ni kwa sababu wanafamilia watahusika katika kutatua tatizo hili na mwanamume ataona aibu na hataaminika tena. Inashauriwa kuondoka baada ya tukio la kwanza la unyanyasaji lakini kutokana na shinikizo la jamii na hofu ya jinsi watu watamchukulia mwanamke, wengi huchagua kubaki na ndipo mauaji hutokea

Karoli Mabula, mwanasaikolojia nasaha katika CounselingTz Consulting, anasema kuwa kuua ni tatizo la kisaikolojia linalohusiana na magonjwa ya akili. Mtu akiua, anaamini kuwa angefaidika na kitendo hicho. Mtaalamu huyo anasema, msongo wa mawazo, mfadhaiko na upweke ni baadhi ya vichochezi vya mauaji. Ikiwa mwenzako anaendana na maelezo na hauko tayari kutafuta msaada, unapaswa kuwa mwangalifu kwani kuna uwezekano mkubwa wa kukuua.

"Watu huua wakati hawana majibu sahihi kwa maswali yao na wakati hawapati ushauri wa jinsi bora ya kutatua shida zao. Ni muhimu kuwa na mazungumzo katika ndoa na kuwatumia wataalamu pale mambo yanapoharibika. Kushindwa kufanya hivyo kutasababisha migogoro isiyoisha,” anasema Mabula

Kwa dalili hizi jiulize upo salama? Ni uamuzi wako kuchukua hatua na kujiokoa au kuendelea kuvumilia na kuongeza takwimu za waliouliwa na wenza wao.

Mwenye masikio na asikie
 
Mahusiano ya siku hizi ni kukaa mguu ndani mguu nje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom