Kwa wanawake walio kwenye ndoa na mahusiano please ufafanuzi!

bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,383
1,354
Hivi kwa nini mara zote mwizi wa mume wa mtu ndiye hulaumiwa,lakini mwanaume huyo anayemwacha mkewe ndani na kwenda nyumba ndogo halaumiwi kwa kiwango kile anacholaumiwa mwanamke? Utakuta mke wa huyo mwanaume anamwinda huyo nyumba ndogo utasikia nitamchinja, sijui atanitambua, sijui nitamfanyizia kama vile ndiye alikwenda kumwita huyo mwanaume wakati mwanaume huyo ndiye alimfuata na kumtongoza na labda kumdanganya kwa hadithi nyingi kuwa sina mke na blablaa kibao? Kwa nini mwanamke asimkalishe kwanza mume wake amuulize kisa gani kilichomfanya mpaka atembee nje ya ndoa kuliko kuanza kukwaruzana na nyumba mabibi wa nje wa mume wake?
 
Mwizi wa mume wa mtu atalaumiwa iwapo anafahamu kabisa kuwa huyo mwanaume ni mume wa mtu, yani wewe bornagain unajua kabisa Mr.X na mwanamama T ni wanandoa, then Mr.X anakuja kwako kukutongoza, ukikubali basi wewe ndo ulaumiwe! mbaya zaidi unakuwa watu ni majirani au hata friends mnasalitiana kwa mtindo huo.

Iwapo Mr.X atamtongoza mwanamke ambae hajui kuwa huyo ni mume wa mtu basi hapo mwanamke hana makosa ila huyo mwanaume ndo anatakiwa alaumiwe, na ndio maana wanawake mnatakiwa kuwa na subira pindi mnaposikia au kuhisi kwa waume zenu wana nyumba ndogo na mfanye uchunguzi mahususi kijua ukweli.
 
sihangaiki na mwanamke anaetembea na mumewangu, nitadili na mumewangu tu kwanini katoka nje ya ndoa then nitaangalia sababu atakayoitoa ndio nitaamua kusamehe au kubwaga manyanga potelea mbali!
 
Walimweusi wewe ni mume wa mtu, najua lkn nimekupenda. Pamoja nakukupenda sijakutongoza, wewe umevutiwa nami, nami nimefuata moyo wangu pamoja na kuwa najua sintaweza kukumiliki 100%.

Sasa kosa langu mimi ni UJINGA wa kukubali kuwa spare tyle, lkn sidhani kama kosa kufuata moyo wangu 'if to love is wrong, then l don't want to be right'. Nani mwenye uwezo wa kuuzuia moyo unapopenda, hasa pale yule umpendaye naye anataka? I am just trying to think in a line ya huyo mdada (other woman). A big fool; nakubali, mkosaji sidhani kwa mtazamo wake. "Alivyokupenda wewe ndivyo alivyonipenda", hiyo no phrase maarufu itumiwayo na wadada 'wezi wa waume za watu'.

Mwenye kosa kubwa ni wewe, ambaye umemsaliti mkeo, umevunja kiapo ulichoapa mbele ya kadamnasi.
 
Hivi kwa nini mara zote mwizi wa mume wa mtu ndiye hulaumiwa,lakini mwanaume huyo anayemwacha mkewe ndani na kwenda nyumba ndogo halaumiwi kwa kiwango kile anacholaumiwa mwanamke? Utakuta mke wa huyo mwanaume anamwinda huyo nyumba ndogo utasikia nitamchinja, sijui atanitambua, sijui nitamfanyizia kama vile ndiye alikwenda kumwita huyo mwanaume wakati mwanaume huyo ndiye alimfuata na kumtongoza na labda kumdanganya kwa hadithi nyingi kuwa sina mke na blablaa kibao? Kwa nini mwanamke asimkalishe kwanza mume wake amuulize kisa gani kilichomfanya mpaka atembee nje ya ndoa kuliko kuanza kukwaruzana na nyumba mabibi wa nje wa mume wake?

Delila alimdanganya Samsoni.... Mwanamke siku zote anauwezo wa kumkataa mwanaume. Women hold the power and the right to say NO.
 
Back
Top Bottom