Kwa wanawake: Jinsi ya kudhibiti house girl asitembee na mume wako

Kunguru hafugiki bana kama mwanaume anajiheshimu na kuipenda familia Yake hawezi kutembea na Dada wa kazi
Kma mume ni kiwembe hata ueke mambo vizuri vipi atatembea nae

Usiseme hivo jaman wana mitihani si midogo hawa wadada wa kazi wa siku hizi wanadeki na kanga tu tena mbichi. Mweeee
 
mipaka ndio kila kitu. sio housegirl aruhusiwe kingia master room au kufua nguo za baba mwenye nyumba,kosa kubwa.
 
Huyo HG anaonana na hubby less than masaa 2 weekdays. Kama ni kuogopa basi ogopa warembo walomzunguka mumeo kazini...iambie serikali iweke amri ya kukataza wadada kujiremba makazini...

Akyanani siwezi jipa pressure ziso na lazima...do me I do you...I am not that weak hadi nichukie na kuwa suspect warembo wote...
Kwanza sitakagi hg mchafuchafu mpaka mgeni ajue bila kuuliza kuwa huyu ni HG...

Na hakuna masharti yoyote nyumbani kwangu...aliye ndani ni mwanafamilia ana uhuru wa kuongea na baba au mama freely

Hapo umeongea bi mkubwa.

Dunia ya leo huwezi mchunga mtu mzima. Watoto tu tuna washindwa hao wengine utayaweza? Kama mwanaume anajielewa na kujitambua hauna haja ya kukimbizana nae...
 
"kuna watu wnafanyiwa kila kitu na wake zao lakini kila hausg anapotia maguu lazima alambe"
kuna member alisema hapo juu sasa sijui chanzo ni nini
Na ndio wengi....wewe chunguza wale wanawake wife material (kibongobongo) ndio waume zao vyupi mkononi....wanakula hg zao na kama haitoshi na wa majirani wanachanganya, mashemeji humo humo....sa sijui utaweka masharti hadi kwa majirani....huna kazi ya maana ya kufanya

ni tabia tu hainaga dawa
 
Tukumbuke kwamba Kuna wanaume hawaridhiki.hata umpe.moyo wako huwa hawarithiki..NB.......ni baadhi lakini.sio wote.
 
Tukumbuke kwamba Kuna wanaume hawaridhiki.hata umpe.moyo wako huwa hawarithiki..NB.......ni baadhi lakini.sio wote.

utampaje moyo wote mkuu... dunia hii hakuna anayependa asiyependa vitu vizuri. mke akishindwa kuhudumia,mme atatafuta huduma kwingine.
 
kumbe ndio maana wife akisafiri anampa likizo hausgel, kwann wanawake mnakuwa na mawazo ya namna hii? ni dalili za kutokujiamini
 
Hv asubuhi wewe mwanamke umeamka,umemuandalia mumeo maji ya kuoga,umemuandalia chai,umemuandalia nguo&viatu.Usiku umemuandalia chakula,hadi mikono unamnawisha,maji ya kuoga umeandaa,umeketi mezani na mumeo.Hata akihitaji chumvi wewe unasimama unamsave.....

.....kha!, mpaka mikono wananawishwa?, kwa kuwa hawana miguu?!, huyo house girl achukue tu I ain't doing all this!, thory!
 
Huyo mume amekatika mikono hadi HG aingie na kusafisha chumba? Yaani mnaishi wawili ndani ya chumba na mshindwe hata kukisafisha? Kuna mambo HG hatakiwi kuwafanyia...
Ukimtamani HG hata binti yako unaweza kumtamani, kumbuka yule ni kama binti yako hata kama ni msaidizi wenu..bado ina jukumu la kumlea!

Afadhali wewe mwanaume umesema, I think mikono yenu na miguu yenu inaacha ku function the moment mnao!, naona mpaka mnaoshwa, mnatayarishiwa nguo!, mnavalishwa?!, kilicho baki ni kulishwa halafu tukimaliza kuwalisha tutawawekea pacifier.......
 
Kuna baadhi ya watu wa kabila moja hivi nyanda za juu kusini msichana akienda kufanya kazi Za hg anaambiwa asiende kufanya kazi tu Bali atafute na mume, huyo mume anaweza akawa baba mwenye nyumba na madawa ya kienyeji ya kumzuzua mwanaume wanapewa na mama zao.

Changamoto za hg ni nyingi.

Mkuu hii hata mimi nakubaliana nayo japo wanaume nao huwa wana tamaa lakini sometimes hawa hg wanakuwa na nguvu za giza hivyo kwenye kutafuta hg lazima pia umakini uwepo msije laumiana bure kumbe tunguli inafanya kazi.
 
Hawa sichana wa kazi pia wanahitaji muda wa kupumzika na kubadilishana mawazo na marafiki, kumfungia ndani tu sio fresh, awe na muda wa kutembea na kujipumzisha aishi maisha ambayo unamp binti yako anapokuwa amekuwa kwa kuwa mwisho wa siku nao wanatakiwa kuwa na familia zao. Kumfungia ndani na kuwa na mawazo ukishindwana nae arudi kijijini sio fresh, wengi miji mikubwa tumekuja kutafuta maisha baada ya chuo au biashara zimetuleta na kupata wenzi huku kukibwa kumfanya rafiki na kumpa elimu ya afya ya uzazi na unazungumza nae maisha yake akitoka hapo, na kumtania akuoneshe mchumba sio mbaya akwa na wazo la kuwa na familia yake huku na sio lazima arudi kwao. Mwanaume akiona msichana anatoka anarudi anafuraha ana amani hatamtamani atahisi ana mtu wake, ila anapojua yupo ndani tuu ndio kwanza wanataka wajimilikishe na wanagonga bila kinga kwa kuwa wanawaamini sana mwisho wanaomba ushauri wa kukwepa mimba za madada.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom