Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Wewe ni mwananume jasiri na mwenye elimu nzuri tena ya chuo kikuu. Kwa kuwa ulihitimu miaka 6 iliyopita ukiwa na umri wa miaka 24 na kubahatika kupata kazi moja kwa moja, ulijitahidi kuwekeza ipasavyo na kuchukua mkopo katika taasisi moja ya fedha na hatimaye umejenga nyumba yako jijini Mwanza.
Kutokana na mila, tamaduni na desturi za kabila lenu, mtu akipata kazi na kusoma licha ya kwamba unakuwa unawasaidia wazazi lakini kiu kubwa ya wazazi ni kuona wajukuu. Walikuhimiza sana uoe nawe ulimshawishi mpenzi wako uliyekuwa nae chuo ambaye ni mwalimu katika shule ya sekondari X ili mfunge ndoa nae alikubali.
Taratibu zote zilifanyika, uliposa na ulichangiwa sana maana kadi za harusi ulitembeza mno. Na kwa kuwa uko smart pia ni meneja katika kitengo cha masoko katika kampuni inayoifanyia kazi, umekodi ukumbi maarufu jijini kwa ajili ya harusi yenu na hatimaye siku ya harusi yenu ni leo na tayari binti anapambwa huko saloon maana send off yake ilikuwa juzi.
Sasa, wakati ambapo ukiwa sehemu maalumu kwa ajili ya kumsubiri huyo bibie aliyeko saloon ili mpande gari moja la kifahari kuelekea ukumbini taarifa maalumu imekuja.
MPENZI WAKO AMETOROSHWA NA JAMAA YAKO WA KARIBU ANAYEITWA NEGILE NA ZAIDI NI KWAMBA TAYARI WAPO SEHEMU Y KUFUNGA NDOA YA KISERIKALI.
Je, ungechukua hatua gani?