Kwa wanaume: Mnampangia mtu aishi vipi afanye nini wewe inakuhusu nini?

MAMNYOKA

Senior Member
May 24, 2014
163
48
Habari za jioni jamani kuna tania moja kwa baadhi ya wanaume hii tania inashangaza na hata ukijaribu kutafuta maana yake hupati.

Ni hivi unakuta mwanaume mmeshaachana kitambo tu kila mtu anamaisha yake lakini kinachoshangaza ni mmoja kati yao kutokubali matokeo.

Hasa wanaume unampangia mtu aishi vipi afanye nini wewe inakuhusu nini kwa nini ukiamua ku move on usi move kweli kweli unaanza kuongea ongea Mara uchokoze watu ujue wapo kwenye mood gani hii haitakusaidia ungejua umuhimu wa huyo mtu tangu kitambo ungemjali unajifanya unajua kushauri baada ya kuachana huo ni ujinga ukiachana na mtu muache aendelee na maisha yake mda wako kwake umeshaisha.

Kudukua mawasiliano,

Kumtoa kasoro,

Kumtukana au kupanga mbinu za kumuumiza hazitasaidia,

Kama unamaisha yako endelea nayo na sikujifanya unajua sana kutoa kibanzi kwenye macho ya wengine wakati kwako vimejaa ni hayo tu kila mtu apambane na maisha yake kufatilia ya wengine hakikusaidii na hakubadilishi ukweli zaidi ya kujishushia hadhi na kuonekana mwanaume suruali.
 
Pole sana Manyoka, usijali ni mapito tu na amini yatapita na utasahau kabisa usumbufu unaopata.

Inawezekana huyo jamaa aliokuacha kaona umuhimu wako sasa na anajutia uamuzi aliouchukua, so anataka mrudiane ila kukwambia anaona aibu. Ila sio wanaume wote tuko hivo, ni huyo au hao wachache uliowahi kuwa nao ndio wako hivo.
 
Habari za jioni jamani kuna tania moja kwa baadhi ya wanaume hii tania inashangaza na hata ukijaribu kutafuta maana yake hupati.

Ni hivi unakuta mwanaume mmeshaachana kitambo tu kila mtu anamaisha yake lakini kinachoshangaza ni mmoja kati yao kutokubali matokeo.

Hasa wanaume unampangia mtu aishi vipi afanye nini wewe inakuhusu nini kwa nini ukiamua ku move on usi move kweli kweli unaanza kuongea ongea Mara uchokoze watu ujue wapo kwenye mood gani hii haitakusaidia ungejua umuhimu wa huyo mtu tangu kitambo ungemjali unajifanya unajua kushauri baada ya kuachana huo ni ujinga ukiachana na mtu muache aendelee na maisha yake mda wako kwake umeshaisha.

Kudukua mawasiliano,

Kumtoa kasoro,

Kumtukana au kupanga mbinu za kumuumiza hazitasaidia,

Kama unamaisha yako endelea nayo na sikujifanya unajua sana kutoa kibanzi kwenye macho ya wengine wakati kwako vimejaa ni hayo tu kila mtu apambane na maisha yake kufatilia ya wengine hakikusaidii na hakubadilishi ukweli zaidi ya kujishushia hadhi na kuonekana mwanaume suruali.
Tatizo hata wavulana mnawaita wanaume siku hizi.

Mwanamme anakimbia wanawake.

Wiki hii nimepigiwa simu na ma ex wanne, wote wananitafuta, mwingine ananiomba msamaha kwa mambo hata sikumbuki, mwingine anautaka muhogo anasingizia keyboard yake imeharibika nimpelekee keyboard wakati duka la keyboard analijua (nimemnunulia na kumtumia online kutoka Amazon halafu nimempotezea), mwingine analazimisha kurudiana, mwingine anaulizia nitakwenda kumuona lini.

Na wote nimewafungia vioo.

Hutanikuta nikimpangia maisha ex kwa sababu mimi mwenyewe nina mambo mengi sana maisha haya.

Sasa huyo mtu anayefuatilia maisha yako wakati mshaachana huyo nina wasiwasi ni mvulana, si mwanamme.
 
Back
Top Bottom