Kwa wanaume: Ikikuuma potezea tu

Ph-25

JF-Expert Member
Nov 19, 2012
1,159
537
Mwanaume unatakiwa kujitambua na kujiheshimu bila kusahau kuutunza ujana wako kwa maneno yenye hekima na busara. Kama wewe ni kijana na haujaoa na una miaka 25 kwenda juu basi jua wewe ni baba pasipo mtoto jiandae kuwa baba bora na mume bora kwa matendo na mawazo bila kusahau kuitunza haiba yako ya kiume kwa mavazi safi na bora.

Mwanaume anayejiheshimu huwa hanyoi kiduku hata siku moja, kijana bora mwenye kujitambua huwa sio mtumwa wa pombe hata siku moja, kuwa na idadi kubwa ya wanawake sio ujanja bali ni utumwa wa fikra sababu unatakiwa uitawale pombe na wanawake sasa ni wakati sahihi wa kuacha ujinga a kujiaanda kuwa mume bora na baba bora.

Mwanaume anayejitambua havai nguo za kumbana mapaja, havai mlegezo wala havai nguo za kumbana makalio, mtoto wa kiume jaribu kuwa muungwana sababu neno mwanaume limebeba ubora wa utashi wa fikra na tabia. Wanawake wanapenda wanaume wenye upeo mkubwa na wanao jiamini sababu mwanaume ni kiogozi na kichwa katika familia sasa unawezaje kuwa kichwa cha familia na kiduku huku ukiwa na mlegezo?

Wewe ambaye upo chuo ujanja si kupiga selfie na wanawake au kushinda kwenye Instagram part kila weekend, badilika sasa na acha ujinga tumia chuo kama kiwanda cha maarifa na sio sehemu ya fashion show na mashindano ya kununua smart phone,kuwa mwanaume bora ili ukikutana na wanaume wenzio uzungumze kama mwanachuo aliyekomaa nasio kulamba lamba midomo.

Ongeza idadi ya kusoma vitabu na sio kuwa mashindano ya kuwa na idadi nyingi ya likes za picture za swagger na wingi wa majina yasio na tija,kumbuka Kendrick Lamar alitegeneza Brand ya jina lake na wewe tengeneza Brand name yako na sio kuiga ujinga usio na tija.

You cannot change yesterday, but you can change today and tomorrow.

# ModernGentleman
 
....hahahahaha..mi nimeishia kwenye avatar!
..ngoja nimalize kucheka ntarudi kusoma ulichoandika!.dah

110357.jpg

"Maneno yenye hekima na busara", kama kwenye avi yako sio? Basi fresh.
 
Ira mkuu tatizo riko kwa wanume wa darisarama sijui wamerogwa na nani potii nashindwa kuerewa rabda mlozi wao kafa potii karibu musoma mkoa wa mara kwa wanume wa shoka
 
Mwanaume ni Kuwahi nyumbani ili ukae na familia yako, mambo ya kukesha baa waachie Barmaids
 
yaan k
Mwanaume unatakiwa kujitambua na kujiheshimu bila kusahau kuutunza ujana wako kwa maneno yenye hekima na busara. Kama wewe ni kijana na haujaoa na una miaka 25 kwenda juu basi jua wewe ni baba pasipo mtoto jiandae kuwa baba bora na mume bora kwa matendo na mawazo bila kusahau kuitunza haiba yako ya kiume kwa mavazi safi na bora.

Mwanaume anayejiheshimu huwa hanyoi kiduku hata siku moja, kijana bora mwenye kujitambua huwa sio mtumwa wa pombe hata siku moja, kuwa na idadi kubwa ya wanawake sio ujanja bali ni utumwa wa fikra sababu unatakiwa uitawale pombe na wanawake sasa ni wakati sahihi wa kuacha ujinga a kujiaanda kuwa mume bora na baba bora.

Mwanaume anayejitambua havai nguo za kumbana mapaja, havai mlegezo wala havai nguo za kumbana makalio, mtoto wa kiume jaribu kuwa muungwana sababu neno mwanaume limebeba ubora wa utashi wa fikra na tabia. Wanawake wanapenda wanaume wenye upeo mkubwa na wanao jiamini sababu mwanaume ni kiogozi na kichwa katika familia sasa unawezaje kuwa kichwa cha familia na kiduku huku ukiwa na mlegezo?

Wewe ambaye upo chuo ujanja si kupiga selfie na wanawake au kushinda kwenye Instagram part kila weekend, badilika sasa na acha ujinga tumia chuo kama kiwanda cha maarifa na sio sehemu ya fashion show na mashindano ya kununua smart phone,kuwa mwanaume bora ili ukikutana na wanaume wenzio uzungumze kama mwanachuo aliyekomaa nasio kulamba lamba midomo.

Ongeza idadi ya kusoma vitabu na sio kuwa mashindano ya kuwa na idadi nyingi ya likes za picture za swagger na wingi wa majina yasio na tija,kumbuka Kendrick Lamar alitegeneza Brand ya jina lake na wewe tengeneza Brand name yako na sio kuiga ujinga usio na tija.

You cannot change yesterday, but you can change today and tomorrow.

# ModernGentleman
yaan ktk wanaume nenye akili ww mtoa mada n mwanaume tena mwanaume mwnye busara pia hekima! kwn nakuunga mkono kw 100% kwn mawazo yako n chanya n yana tija n pia yanelimisha jamii. n hata tkijaribu kuangalia jamii yetu y sasa vijna wengi gtumepotoka n tunaiga mambo hayana mcngi n tunaacha mambo yenye maadili n mwsho w cku tunajikuta hatuna hata tunachoambulia badala yake tunakuwa wahuni n kuishi kuwa wavuta bangi, walevi, n pia kutumia unga n vilevi mabalimbali! kiukwl nimekuelewa sn n pia nakuunga mko sn! vijana tubadilike sn!
 
Back
Top Bottom