Kwa wanaume ambao mlikuwa na kazi lakini sasa hamna na wake zenu ndio wanaoendesha familia mliwezaje kutoboa?

othuman dan fodio

JF-Expert Member
Jan 2, 2018
5,657
9,043
Kichwa cha habari kinahusika, kama mnavyojua ktk maisha kuna kupanda na kushuka Leo unacho kesho huna ndio kanuni ya maisha ilivyo.

Suala la ajira limekuwa Changamoto sn kwa dunia ya leo kwa jinsia zote mbele yaani wake kwa waume lkn inakuwa maradufu kwa upande wa kiume kwakuwa utamaduni wetu hasa wa kiafrika imezoeleka kwamba wanaume ndio watafutaji na ndio watunza familia.

Back to the topics, kufuatia sera mbovu za uchumi za mwenda zake watu wengi nikiwemo mie turifurushwa makazini na kupelekea ajira kuwa changamoto sasa basi mke wng ndio alichukua jukumu la kuendesha familia ili siku zisonge.

Sio kwamba Mimi nilibaki tu hom kumsubili wife alete hapana nilikuwa naingia kitaa na mm Ku hustle ili nisikae kindezi na kuonekana mpenda kitonga, lkn kama mnavyojua kitaani sio kwa mchezomchezo kitaa kigumu kinyama,

Kila deal unalojaribu linabuma, ingia kwenye umachinga na kitambulisho changu cha elfu20 napo hamna kitu, basi maisha yakawa ni tyt ile mbaya japo mtoto wa kiume nikawa najipa moyo kwamba 1day nitatoboa tu na life litakuwa normal.

Sasa turudi kwa upande wa mke wng at first my wife wangu alikuwa ndio comfort wng akinipa moyo kwamba yupo pamoja nami na ataweza kuhandle changamoto ninazopitia, kiukweli na Mimi ni shahidi wife ali play part yake kwa kiwango fulani, maji nilikuwa nawekewa bafuni, boksa nanunuliwa, mbususu nilikuwa naichakata kila ninapohitaji, na vitu vingine vingi siwezi kuweka vyote hapa ambavyo mtoto wa kiume alistahili kupata kutoka kwa mwanamke.

Sasa wajuba naona mambo yamebadilika sio kama zamani my wife wangu ame change to the extent nahisi atakuwa amenichoka na kuniona takataka mbele ya jamii,

Kwanza ile heshima kama mume ndani ya nyumba siioni tena, maji sikumbuki Mara ya mwisho kuweka ilikuwa lini, akirudi kutoka kazini ananikuta nipo sebleni nimeshika remote, kwanza hanisalimii atapitiliza moja kwa moja chumbani akija sebleni anachukuwa remote na kuweka kipindi anachotaka yeye na anapiga bit ole wake mtu abadilishe.

Kipindi chenyewe haangalii anenda zake jikoni huko tena ataanza kufoka mbona glass haijaoshwa, kijiko kipo chini, dirisha hujafunga, chakula mbona kimebaki kidogo mtoto wa kike anafoka na uso umemvimba utasema nyoka aina ya koboko amemeza simbilisi.

Kwakuwa hatuna house girl kazi zote nafanya mie ikiwemo kufua nguo zake, hadi za ndani nafua mie, kuna wkt nikifua nakuta vitone kwenye chupi najiuliza nn hiki lkn napotezea tu yy ndio kashika mpini mm sina vyangu, mbususu sipewi na nikipewa kwa masharti mpaka yy siku hiyo ajiskie, asipo jiskia miezi inaweza kukatika na usipewe harafu nikitaka kuchepuka nashindwa sijui kaniroga huyu.

Kwa kweli mambo ni mengi na visa ni vingi ukurasa huu hauwezi kutosha kuelezea, vijembe vimekuwa ndio wimbo wa Taifa siku akiwa nyumbani ,akiwa jikoni huko mm nipo sebleni anaongea na mwenzie kwenye simu, ........ningekuwa na uwezo ningemuoa mimi, mara utaskia lipolipo tu kama ling'ombe bora ng'ombe unapata maziwa na nyama, hujakaa vizuri utaskia yaani we na mista wako couple yenu nimeikubali sn huku wakicheka kicheko chao cha umbea,

Swali kwa wanaume wenzangu je mlitumia njia gani kwanza kuwa handle wanawake wa aina hii na mliwezaje kuhandle situation hii na baadae kuja kutoboa na heshima ikarudi kama zamani, angalizo kumpenda bado nampenda kwani tuna watoto na sitaki familia yangu isambaratike,

Nakaribisha ushauri mzuri tu mbaya baki nao.
 
Nimecheka hapo ulipoeleza kwamba unakuta vitone kwenye nguo zake za ndani unapofua(nisamehe kwa kucheka)!Nimewaza mbali na mengi.

Hata hivyo,kwa sababu umeamua kuvumilia,ni vema ukatafuta kazi yako ya kujiajiri.Mimi ningeweza;
1-Udobi.Nina uwezo mkubwa wa kufua na kunyoosha nguo aina kwa aina.Hebu na weye jaribu.
2-Ufundi/urekebishaji/Ushonaji wa viatu.Utundu wa kushona(marekebisho)viatu nilijifunza tangu darasa la kwanza.Haiihitaji mtaji mkubwa.Nyuzi,sindano na vigozi vya kuunganishia palipoharibika au kuchanika.
3-Kusafisha na kung'arisha viatu.Kama upo katika mji mkubwa,usione soo!Hizi ni shughuli tumeanza kuzifanya tangu utotoni.Unasafisha raba,viatu vya ngozi na "ku-brush" vingae kwa kiwi.

NB:Hizo ni shughuli zisizohitaji mtaji mkubwa.Jaribu upate mahitaji yako ya kawaida.Kama ulizoea "ubossboss" unakwama.
 
Nashukuru kwa ushauri nitaufanyia kazi ila kwa shughuli hizo nitaweza kutoboa kweli au dharau ndio zitazidi
 
Nashukuru kwa ushauri nitaufanyia kazi ila kwa shughuli hizo nitaweza kutoboa kweli au dharau ndio zitazidi

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
Huo ni mwanzo tu. Kama upo kwenye mji au jiji kubwa,utapata kipato kizuri tu.Ni kazi zisizohitaji mtaji mkubwa wala nguvu.Nimeona umeeleza unafanya shughuli za hapo nyumbani.Basi,hiyo nguvu ndogo waweza kuitumia huku umekaa ukapata wastani wa Tsh.15,000 hadi 20,000 kwa siku.
 
Huo ni mwanzo tu.Kama upo kwenye mji au jiji kubwa,utapata kipato kizuri tu.Ni kazi zisizohitaji mtaji mkubwa wala nguvu.Nimeona umeeleza unafanya shughuli za hapo nyumbani.Basi,hiyo nguvu ndogo waweza kuitumia huku umekaa ukapata wastani wa Tsh.15,000 hadi 20,000 kwa siku.
Hapa mtaani ninapokaa wapo wanaofanya hizo shughuli za udobi na kushona lkn hawatoboi nao wanalalamika maisha magumu

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
 
Hapa mtaani ninapokaa wapo wanaofanya hizo shughuli za udobi na kushona lkn hawatoboi nao wanalalamika maisha magumu

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app is
Si lazima ufanyie mtaani kwako.Tafuta sehemu nyingine.Nimekushuri hivyo kwa sababu yaonesha hauna mtaji mkubwa wa kuanzisha ujasiriamali wowote.Kama una utaalamu,zunguka kwa wanaohitaji utaalamu wako uwape huduma.
Hapa mtaani ninapokaa wapo wanaofanya hizo shughuli za udobi na kushona lkn hawatoboi nao wanalalamika maisha magumu

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
Katafute mtaa au sehemu nyingine.
 
bila kutafuta pesa mkuu hautaweza epuka dhahma za bibie,

alaf kama chai hii, ya uvuguvugu tena
Kwahiyo unataka kusema visa vitaongezeka zaidi ya hapa as long as sina mkwanja, ila jua hii sio chai ni kweli nayapitia, tena kuna siku alirudi usiku sana alidai kuwa alikuwa kwenye kikao cha harusi lkn hakuniaga kama alikwenda kwenye kikao cha harusi,

Alirudi mida mibaya ikanibidi nimsubirie kumfungulia mlango, yy sio mnywaji wa pombe lkn niliskia harufu ya pombe kutoka kinywa chake, nilipojaribu kuhoji hakunijbu alijitupa tu kitandani na kwanza kukoroma

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
 
Hawa viumbe kuishi nao tabu sana,mnaolalamika kaeni mjue kwamba hawa hawakuumbwa waje kulisha watu nje ya damu zao hata nyie mnaokula good time siku inakuja ombeni Mungu aendelee kuwapa utulivu ktk utafutaji wenu....i mean,mf:akizaa mtoto atamuhudumia 100% uwezo akiwa nao,baba/mama yake (damu yake halisi) atawahudumia kwa 100% bila kulalamika ila kukutunza wewe uliyekaa naye kwa wema akiwa goli kipa hata miaka kumi hujawahi kumfanyia vituko hawezi.

Omba Mungu akusimamie ktk utafutaji wako ufanikiwe huyo akiendelea kuleta dharau na majivuno fukuza uanze upya siyo dhambi.
 
Back
Top Bottom