Kwa wanasiasa wengi siasa ni kazi

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,605
8,744
Kuna wanasiasa wachache sana kwenye nchi zetu zinazoendelea wanafanya kazi ya siasa kama wanaharakati wa maendeleo. Wengi wa wana siasa wanafanya siasa kama kazi. Nchi zetu hizi ambazo ndiyo zina jitahidi kuanza kuleta maendeleo watu wengi wanaona wanasiasa ndiyo wenye pesa na magari mazuri. Hivyo watu wanao onekana wa maana ni wana siasa.

Mimi mfano ni diaspora naishi Texas hata mwakilishi wangu simfahamu na sio muhimu, diwani wangu simfahamu. Kwasababu huu ni mwaka wa uchaguzi ndiyo unapata pata barua na mabango ya wagombeaji. Kwa wenzetu siasa ni gharama na wito na sio sehemu rahisi ya kwenda maana kuna kazi, biashara na mambo mengine ya kuleta kipato. Hivyo msije mkashangaa hamahama ya wanasiasa ni kama kunama kazi tu.

Watanzania tumekuwa na utamaduni wa kuto kutaka kujua au hata kufikiria juzi nilimuuliza mtu anipe maana ya beberu akashidwa. Mwanasiasa ambaye anahama chama inatakiwa aweze kueleza tofauti ya kisera ya kuhama wanavyosema kuunga juhudi kwani kuna Mtanzania ambaye hataki barabara zijengwe? au hospitali zijengwe?, au shule zijegwe, au tume na mikataba mizuri. Sasa unavyosema una enda kuunga juhudi ni juhudi zipi ambazo ulikuwa huungi? na kwanini?. Kama haukuwa na sababu ya kutokuunga mkono wakati ukiwa huko je ni akili gani zimebadilika mwaka wa uchaguzi?. Lakini kwasababu Watanzania wengi wanapenda drama na ushabiki hata kuwauliza haya maswali hakuna.

Watu wengi wanasema mimi Chadema au mimi CCM lakini hawawezi hata kutueleza tofauti ya sera!. Wanasema wengine serikali inajenga barabara au inaleta maji? Je mlitaka serikali ifanye nini?. Leo hii kwenye mambo makubwa utakuta wote Chadema, CCM na vyama vingine mambo wanayo taka kimaendeleo ni yaleyale hakuna tofauti kubwa utasikia tofauti ndogo sana ambazo sio za kisera mfano watasema kampuni ya ndege wangetakiwa kukopa badala ya kununua kwa cash sasa hili sio swala la chama ni fikra za mtu binafsi.

CCM inachukua sera za upinzania na upinzani unachukua sera za CCM hivyo hakuna tofauti kubwa kisera tofauti ni personality tu za wanasiasa. Kuna wengine wanapenda vijana, wasomi na wafanya biashara. Hivyo wahamaji ni kwa maslahi ya kazi zaidi ya sera.

Cha kushangaza Tanzania kuna mbinu nyingi za maendeo tofauti ambazo sijasikia hata mwanasiasa mmoja akisema au hata kutoa maoni au upinzani au chama tawala mfano

1. Je mfumo wa elimu kuanzia madarasa watoto wanayochukua, mihulana ujenzi wa shule unaendana na nyakazi hizi za kisasa?. Mfumo wa elimu ni wa miaka zaidi ya 40 sasa lakini mabadiliko ya ushindani duniani na teknologia bado hayaja badilisha mfumo wetu wa elimu. Tusishangae tunasikia elimu inashuka kiwango ni kwasababu hatuendi na wakati na hatuwezi kushindana na wenzetu ambao wanabadilika.

2. Je mifumo ya kilimo na umiliki wa Ardhi umeleta maendeleo na je kuna mbinu tofauti? sijasikia mtu yeyeote akipendekeza mfano masoko kujegwa au kilimo cha kisasa kwa vijana.

3. Je tuna mbinu gani mpya ya kuleta ajira kwa vijana wengi nchini ambao 70% ni chini ya miaka 25. Je mbinu zipi mpya za kisera tunazo. Mfano tumetumia vipi teknologia ya siku hizi kuleta kazi nchini? India wana kazi mamilioni za kampuni ambazo haziko hata India mfano kampuni nayofanya wahasibu wapo India na wanafanya kazi bila matatizo hizi ni ajira kule India. Lakini sijawahi kusikia mbinu mpya watu wanasubiri viwanda.

vijegwe na kazi za vijeba.

Hivyo tunatatizo kwamba siasa ni kazi na hakuna ubunifu kwenye siasa.Hili sio Tatizo la Tanzania pekee hata Kenya hakuna tofauti kisera siasa zimekuwa kama vile kabila fulani haliko kwenye siasa. Hivyo Tanzania tunaenda kwenye siasa ambazo zinaitaji kujumuishwa kwenye serikali zaidi ya sera. Vyama vitakuwa mikusanyiko ya udini, ukabila, ukanda na hata ujana na uzee.

Tofauti ya siasa inatakiwa kuwa sera na kama mtu hujui kwanini upo kwenye siasa unatakiwa usiwepo. Tunamsema zitto na wengi kumshangaa kwasababu yeye pekee ndiyo anajaribu kidogo kutoa mawazo tofauti
 
..CCM hawaamini ktk USHINDANI.

..CCM hawaamini ktk demokrasia ya vyama vingi.

..CCM hawaamini kwamba chama chao kiko juu ya sheria za nchi.

..Pia chama hicho hakina sera au ubunifu wa kuwrza kuleta maendeleo na kuondoa umasikini in OUR GENERATION.

..ahadi alizokuwa akipewa Babu yangu na wagombea wa Tanu ndiyo hizohizo ninazopewa mimi na wagombea wa CCM.
 
Back
Top Bottom