Kwa Wanasiasa: Kwanini tunauziwa viwanja bei ghali 2-8mil kwa bei ya serkali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Wanasiasa: Kwanini tunauziwa viwanja bei ghali 2-8mil kwa bei ya serkali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fikirikwanza, Jun 18, 2012.

 1. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Inasikitisha sana kuona mtanzania hana fursa nzuri ya kujenga makazi bora kutokana na dhana mbaya ya serikali ya kuggeuza ardhi kuwa mtaji mkubwa wa mapato ya kuendesha nchi, yaani haki mojawapo ya makazi kati ya nne za maji, chakula, makazi, mavazi inagandamizwa kwa kasi kubwa.

  Hebu tujiulize kwanini bei ya kiwanja iwe kubwa kuliko kipato cha mfanyakazi wa kima cha chini kwa mwaka mzima??? kweli sera za CCM zinaakili??? yuko wapi Filikunjombe, yuko wapi Makamba January, yuko wapi Mama Anne Kilango, yuko wapi Sitta yuko wapi Mwakyembe, yuko wapi Waziri anayehusika na Makazi, Yuko wapi waziri wa Ardhi, Yuko wapi waziri wa maendeleo ya jamii, yuko wapi Waziri MKUU, yuko wapi RAIS???????

  Zaidi yote yuko wapi Mbunge, ambaye tunamlalamikia kila siku kuhusu bei ghali ya viwanja, aliyeahidi kwenda kuongea matatizo yetu bungeni yuko wapi???

  Je hata ardhi ambayo mungu katupatia bure nayo inashindikana kuigawa kwa watanzania ili wajenga makazi bora, inakuwa suala la tajiri hata na hili? kulala sehemu nzuri imekuwa luxury????

  Ushauri wangu kila mtu apewe kiwanja kwa bei ya laki 1-5 tu, serikali ivunje mtandao wa ulanguzi wa viwanja; ardhi sio biashara, iweje mtu anachukua viwanja 50 ili auze kwa bei ghali, udhaifu wa serikali ukome sasa. Mbaya zaidi wakati wa magufuli alidai hata naibu wake RM alikwa na viwanja vingi vingi amejilimbikizia.

  Unyonge wetu ututoke kwanza ndo tusitahili haki. TUUNGANE KUPAMBANIA HAKI YA MAKAZI BORA
   
 2. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  vipi haya malalamiko uki PM NAPE JR.anaweza kuwa na ufafanuzi au akayapeleka kwenye vikao vyao kujadili.Kwa kweli wanatuumiza mie nilikuwa na kishamaba changu wakanilipa fidia kiduchu kupitia VALUERS wao baada ya kupima viwanja siwezi hata kununua na kifidia walichonilipa yaani ni full wizi,usanii na mateso tu kwa mnyonge.
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  well said ..... nakuunga mkono na hoja yako ya makazi bora.

  Hivi sasa kiwanja vilivyopimwa vya serikali vinauzwa kama ifuatavyo:

  Low density ........milioni 10
  medium density.......milioni 8
  high density .......milioni 5 - 6

  Matajiri wamegeza mradi wa kununua ardhi na kuuza kwa bei ya juu zaidi......

  kama viwanja vingekuwa bei ndogo hakuna ambao angefanya biashara ya maana
   
 4. K

  Kichoncho Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 13, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata kwa bei hiyo ya juu bado hakuna fair distribution wanagawana wenye nchi,kwa mfano,viwanja vya gezaulole mgao wake mlalahoi kupata kiwanja ni next to impossible
   
 5. mpenda

  mpenda JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 250
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Yaani serikali inangalie hili swala kwa upya hizo gharama ni kubwa sana kwa wananchi wakawaida ambao wengi ni wafanyakazi. Wabunge waliangalie hili na kulizungmzia PLZ!! gharama ni kubwa sana.. na bado hatujajenga. hebu PM na waziri walizungumzie hili. Mbunge wa Temeke uko wapi?
   
 6. b

  bumes Senior Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kweli serekali ya CCM yimeamua kugawa watu kwauwezo wao mana yake wanasema mtu mwenye kipato kidogo hastahiri kukaa mjini.

  Wanjua ki[ato cha wafanyakazi nahao hawana kazi, wegatafuta njia kwamba kilakundi hili linapata viwanja, lakini kwasasa hatuna serekali hiyo yina mda yakwangalia watu wa chini.

  Chaajabu kwenye TV ya ALJAZEERA jana kuna mama moja mu Greek alikuwa anasema maisha yao yatashuka KAMA WA AFRICA HAO WANAISHI KWAMSANDA.

  Vyote hivyo vinaonesha kwasi ngani wazungu wametuzarau, hata kama vogozi wetu wanashinda huko huko kutafuta misanda.

  The most painful thing is that our Governments have no planning regarding the reduction of debts from outside or time line showing how many years we expect to get this loan and then seize.

  Please let us use our education otherwize right now we are being laughed at, despitethe resources we have.
   
 7. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Well said mkuu maana huku kwetu pande za mtoni kijichi viwanja ni mil 20 hadi 40.
   
 8. s

  slufay JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  milioni 40 mbona ndogo mimi niliambiawa 50 na kundelea na zote nyingi hizo wanamiliki maafisa wa ardhi au madalali wao
   
 9. Jotojiwe

  Jotojiwe JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Hapa kwenye swala la viwanja linaponijia najiona kama mimi sio mtanzania hataivyo hata mashamba kwanini wanamwekea kikomo mtanzania mwenye uwezo wa kuendeleza aridhi kumiliki hekar 5 tu. Mi'siwaelewi chukua chako mapema.
   
 10. v

  vngenge JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Sasa uprofesa wa Tibaijuka na uzoefu wake U.N unatusaidiaje kama Taifa? Ndio usikivu wa serikali huu? au haoni tatizo?. Tanzania hatuna matatizo ya ardhi kiasi kwamba kupata sehemu ya kujenga ni shida. Hivi unamuuzia mtanzania kiwanja milioni 10 wakati unajua kipato chake hakizidi mil 2 kwa mwaka unamsaidia au unamfundisha wizi. Hki ya makaazi ni haki ya kikatiba hivyo wananchi wakikimbilia upinzani mnaunda tume kutafuta sababu nini!
   
 11. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu Fikirikwanza,

  Umegusa jambo ambalo limekuwa likiumiza kichwa changu. Ni kweli makazi bora ni haki ya kila mtanzania. Ili haki hii iweze kutekelezeka ni lazima bei ya kiwanja kilichopimwa iwe chini ili hata mtu anayepata kipato cha chini aweze kumudu.

  Tupaganie haki yetu kwa pamoja. Kwa kuanza nitampigia simu mbunge wangu ili alijengee hoja bungeni. Lakini kwa kuwa viongozi wa serikali na CCM kwa ujumla hawajali maisha ya wananchi wa kima cha chini na hakika watampuuza. Tuwasaidie wabunge wetu makini hasa wa CDM kupigania haki hii. Tuunge mkono M4C ya CDM ili 2015 tuiondoshe CCM madarakani. Wapo watakaosema hata CDM hawataweza; naamini wataweza kwa sababu wakizembea tutawaondoa madarakani. Kwa kuwajibisha vyama vya siasa kwa kutumia nguvu ya umma maisha bora kwa kila mtanzania yatawezekana.
   
 12. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Nyinyiem na Serikali yake ni wavivu sana kufikiri. Hawana sababu ya kuumiza vichwa kufikiri kwa sababu wanajua watoto wao wana vyeo serikali na benk zote, wana hodhi ardhi kubwa, wananunua kura, wanachakachua kura.

  Kuomba haki ni uenda wazimu. Haki inadaiwa kwa nguvu.

  Mtoa mada amegusa watu wengi saanaa! Ni kweli kuna ufisadi mkubwa sana katika ardhi hasa mawaziri wenyewe na maafisa ardhi.

  Kumbukeni suala la ardhi ya Burka na mpaka sasa makaburu ndo wamejaa kule na sasa kiwanha bila million 80 hupati. Wananchi walipelekwa hela zao na wakatepeliwa. Huyu naibu waziri wa ardhi mwenyewe ni mpiga dili na hawajali wananchi wake.

  Suluhisho ni nini????

  Kuendelea kupiga kelele hasa ifike kwenye magazeti. Watu kuandika makala kwenye magazeti. Iwe kampeni ili wahusike wasikie na pia wabunge wa upinzani waulize maswali bungeni.
   
 13. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimepata habari manispaa ya temeke maeneo ya Gezaulole kunauzwa viwanja 1800 lakini form za maombi zilizouzwa ni 14,000 na kila form inauzwa 30,000/=. Kwa mahesabu ya kawaida Manispaa ya temeke imeingiza milioni 400 (400,000,000)
  katika form za maombi kwa viwanja 1,800 inavyotegemea kuwauzia wananchi,

  HUU NI WIZI WA WAZI KABISA USIOPASWA KUVUMILIWA.
   
 14. m

  mgao wa umeme Member

  #14
  Jun 18, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Inauma sana. yani serikali badala ya kuwasaidia wananchi wake ile waweze kuwa na makazi bora INA WAIBIA. Form kuuzwa sh 30000 ni wizi uku wakijua kabisa kwa 90% ya walioomba watakosa. kwanini form isiuzwe sh 5000 au chini ya hapo. kwa kutoa copy ni gharama kiasi hicho. form zenyewe watu waliofika saa moja asubuhi wakaambiwa zimekwisha nikashindwa kuelewa kwa ofisi za serikali zinafunguliwa saa ngapi?
   
 15. l

  lost account Member

  #15
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa wa gezaulole sijui watatoa muda gani wamalizwe kulipwa, maana unaweza ambiwa ulipe in two months or wanyang'any'wa kiwanja.
   
 16. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Nafurahi kuwa hoja hii inatugusa wengi, actually wote maana kila mtanzania anahitaji makazi bora, kulalamika sio suluhu, kunung'unika sio suluhu hata kidogo, Je tufanye nini? maana nchi ni yetu walio na madaraka tumewapa sisi, serikali ipo na wabunge wapo.

  Naomba tuongelee tufannye nini bei za viwanja ziwe na uwiano wa kipato cha mfanyakazi wa serikali kima cha chini, Tufanye nini kuua udalali kwenye suala la Ardhi, maana serikali inauza kiwanja bei juu, fisadi wa ardhi na idara ya ardhi anajimilikisha viwanja 50, kisha anauza kwa bei juu, dalali anaweka cha juu, mzigo wote ni kwa watanzania 99.99% hiyo 0.01% ni hawa mafsadi wa ardhi. Je kupitishwe sheria inayotaja bei za viwanja kwa kila halmshauri?? hakuna ruhusa kulipa zaidi ya bei ya serikali???
   
 17. d

  decruca JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kwanza kabisa nawasalimu wana JF na naamini mmenikaribisha kwa moyo mkunjufu. Nirudi kwenye mada, hivi hili swala la manispaa ya Temeke kukusanya pesa za fomu kwa ajili ya kugawa viwanja and then wakaa kimya linakuwaje? nakumbuka nilishachukua fomu kipindi fulani na walisema ni mradi wa viwanja 20,000,matokeo yake wakagawiwa wakubwa tu kama viwanja 700 hivi. bac nikawa na matumaini kwamba labda bado wanaviandaa majina mengine yatatoka, sasa nashangaa wanauza fomu tena hivi huu sio utapeli? na si hivyo tu vya ilala navyo! basi si waturudishie pesa zetu?
   
 18. I have a dream

  I have a dream Member

  #18
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kusema ukweli bei ya kuuza viwanja kigamboni ni mbaya sana. Meter square moja ni shilingi elfu 8, niulize maskini anaweza kumudu? WAZO LANGU KWA SERIKALI, NI VIZURI MKAANGALIA HILI JAMBO VIZURI ILI WATU WAWEZE KUPATA MAKAZI BORA KWA BEI NAFUU.
   
 19. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  huwezi kupewa ardhi inaonekana wewe ni mnyaruanda
   
 20. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Maskini kiwanja cha nn? tena kiwanja kigamboni , geza beach kbsa?
   
Loading...