Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 10,326
- 6,849
Kwa wanasaikolojia na wengine wote ambao mnapenda kudadisi mambo. Kwa kawaida ili mtu aweze kufikiria, lazima tumie lugha, na lazima iwe ni lugha anayoijua, kwa sababu kwa maana nyingine, kufikiria ni sawa na kuongea mwenyewe kimyakimya, na mtu hawezi kuongea kwa kutumia lugha ambayo haijui! Kwa hiyo ili mtu aweze kufikiria, lazima atimize sifa kuu mbili nazo ni:
MOJA: Lazima atumie lugha fulani katika kufikiria
MBILI: Lugha atakayotumia kufikiria lazima iwe ni ile ambayo anaijua. Mtu hawezi kufikiria kwa kutumia let's Kisukuma, wakati hajui kuongea Kisukuma.
Swali langu sasa ni je, mtoto mdogo asiyejua lugha bado (na si yule asiyejua kuongea, maana mtoto anaweza akajua lugha ila bado akawa hawezi/akachelewa kuongea), huwa anafikiria? Na kama huwa anafikiria, huwa anafikiriaje?
Na kama huwa hafikirii, kwa nini huwa unaweza wakati mwingine ukamfanyia tendo fulani halafu akatabasamu au akacheka? Je, matendo haya ya kucheka au kutabasamu huwa anayafanya kwa kutumia instincts tu au ni vipi?