Kwa wanaotafuta kazi humu

ISLETS

JF-Expert Member
Dec 29, 2012
8,121
5,332
Salamu kwenu,

Kwa vijana watafuta kazi wote, naomba niwakumbushe tu vitu vichache muhimu ambavyo naona threads nyingi havizingatiwi.

1. Personal details(taarifa binafsi), sema jina hata initial tu mfano "Melo", jinsia, umri ambapo si lazika uweke umri kamili kama hautaki kila mtu ajue mfano kama una miaka 25 unaweza andika 20s, 20-30, au

2. CV, hii si kwa wasomi tu, hata tusiowasomi, si lazima kuweka CV iliyokamilika, ila kiwango cha kitaaluma ulichofikia kwa sasa pamoja na taaluma nyingine ulizonazo. Mfano kuna watu wanaishia kusema "nina ujuzi wa computer" my friend ujuzi wa computer ndio nini, sema level gani, na kama ni ujizi wa kujifunzia mtaani basi sema pia.
Pia kama unataaluma mbili au zaidi sema pia, mfano unaweza ukawa una certificate ya basic computer application pia ni graduate labda education/ualimu.

3. Mawasiliano/contacts, weka mawasiliano zaidi ya aina moja, na epuka kusema "aniPM" au "anifuate PM" shifa yako, we kubali mchezo uishe vile mtoa dili anataka.

4. Usalama na ufalagha/security and privacy. Usijieleze kiundani sana na kuachia contacts ambazo huwa hazina usiri. Ndio maana kwenye jina unaandika initial name pekeyake, contacts unaweza weka email, namba maalumu. Jitahidi kuwa na email yenye jina zuri lakini si lako moja kwa moja mfano kama unaitwa Melo Iddi, email inaweza kuwa imelo67@gmail.com, pia unaweza kutenga namba maalumu ya kuombea kazi mtandaoni isiwe ile unayotumia kwenye mambo yako mengine ya msingi mfano kuweka pesa nk.

6. Lugha/language, maneno unayotumia, uandishi wako vina maana kwenye kutafuta kazi.
Mamna unavyojibu comments za watu hata huko PM.

7. Pambana na changamoto. Hasa comments ambavyo hazitakufurahisha, si mara zote utapata majibu mazuri, kuna wakati yatakuja mabaya, kejeli, utani, na dharau, katika yote we furahi na uchukulie kawaida kama kwamba waliandika hayo hawakuwa serious.

Hasta la vista
 
Kwa madogo wote wanaotafuta kazi waje Bunju kwenye hekalu langu siku ya juatano niwafabyie nterview natafuta kijana wa kulisha mbwa na ushababoi
 
Back
Top Bottom