Kwa wanaoona mbali, Waziri Ndalichako ni sumu kwenye mfumo wa elimu

Kwa muongo mmoja uliopita umuhimu wa elimu ulikuwa na thamani sana kwa vijana maana thamani yake iliendana na mazingira yaliyokuepo na watu wengi walitamani kupata elimu ili waweze kujikomboa kiuchumi

Baadaya ya muongo mmoja kupitia, hali iliyopo sasa KWA TANZANIA SIO DUNIANI KOTE elimu sio kitu kinachoweza kumkomboa mtu kiuchumi au kumfanya aweze kuishi maisha nzuri, kwa wengi hii ni baada ya waziri husika Ndalichako na mfumo wake kutokuendana na teknolojia

Yaani namanisha kwamba mfumo wa elimu upo nyuma sana na teknolojia ya dunia inavyotaka ndio maana kuna wasomi wengi sana mtaani na hawana pa kwenda. Hali iliyopo sasa MTU MWENYE DEGREE ANAWEZA KUWA MUUZA MAHINDI YA KUCHOMA BARABARANI AU anauza nyanya tu

Sasa unajiuliza Huyu mtu kapoteza miaka zaidi ya 16 kusotea kuuza nyanya ni UPUUZI WA Hali ya juu, wakati huo kuna mtu kaishia darasa la saba (kama yupo smart) kwa miaka hiyo kumi na sita ambayo mtu anatafuta degree utakuta maisha yake amejipanga na tayari ameshakuwa na vitu muhimu kulingana na mahitaji ya binadamu.

Hapo ndipo utakaposhangaa msomi kasota miaka yote hiyo na mtaani akirudi anaonekana hana maaana na hata akitaka baadhi ya kazi alizosomea miaka yote hiyo atahitajika awe na uzoefu wa miaka kadhaa ni upuuzi mkubwa sana na bado msomi huyu akichelewa kupata ajira na kwa bahati nzuri akafanikiwa baada ya miaka kadhaa kuipata hiyo ajira utakuta anaishi na MADENI maisha yake yote ya utumishi.

Ili kuboresha mfumo wa elimu nchini Tanzania ipo haja ya Huyu Waziri Ndalichako na kundi lake kuondolewa katika sekta hii maana ni kama hawajieliwi kwa sababu wao wanaamini katika mfumo wa kutupa wasomi mtaani na bila kujua kile walichowaandalia kina manufaa gani mtaani na kufanya thamani ya elimu kushuka kwa speed kubwa sana.

Anatakiwa kiongozi katika sekta hii awe na uthubutu wa kuvunja baadhi ya mitaala isiyokuwa na TIJA na awe na uwezo wa kutatua changamoto ya thamani ya elimu na mazingira ya kiuchumi kwa msomi atakaye kuwa yupo mtaani Kwan kwa hali iliyopo sasa ni mbaya sana.

Profesa huyu ana amini katika makaratasi yasio endana na uhalisia inasikitisha sana na kutia aibu sana ELIMU YA TANZANIA NI TAKATAKA na Ndalichako hatoshi kwenye mfumo, ukweli huu lazima usemwe ili tujenge mfumo mpya kwa vizazi vijavyo.
Tumwache

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Kitu gani mkuu unatumia kama kipimo sahihi cha kupima uthamani wa elimu?

Ajira hakuna mtu kamaliza degree anaona asikae bure bora ajishughulishe na biashara ndogo ndogo napo mnawananga akika vijiweni napo mtawananga sasa unataka wafanya nini?
nafasi zipo za kutosha ila hawatoi ajira kwa makusudi tu mbona kikwete alitoa sana. Kuna shule ina wanafunzi zaidi ya 1000 walimu wa hesabu wapo wawili shule ipo dar
 
Ushauri
1). Serikali/wizara ya Elimu iombe nafasi za kuwapeleka wahitimu wetu wa fani za u fundi na sayansi kwenye mafunzo tarajali(internship) ya miezi mitatu au sita kwenye nchi ambazo zimepiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya viwanda Kama china,Indonesia na Thailand.
2). Bajeti ya wizara ya Elimu iongezwe ( ili kusomesha vijana wengi kwenye fani za science na ufundi( kwenye vyuo vya Kati na juu)
3) wizara ya Elimu kwa kushirikiana na wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Africa Mashariki kutafuta nchi marafiki na washirika wa maendeleo Kama China au Thailand au Indonesia,ili kupeleka vijana wetu (mafundi mchundo) kwenye mafunzo ya vitendo/tarajali (internship) kwenye viwanda vikubwa na vidogo vidogo kujifunza kwa vitendo technolojia ya kutengeneza vifaa mbalimbali.
(kwa mfano wachina wanaweza kutengeneza mabati kwenye eneo dogo,kwa kutumia technolojia rahisi na kwa gharama nafuu hata eneo la buguruni).
4) Serikali iweke utaratibu mzuri na rahisi wa kupata mitaji ya kuanzisha viwanda vidogovidogo - vyeti vya wahitimu viwe dhamana (security ya mikopo) pamoja na masharti mengine.
 
Kiufupi serikai nzima kwenye suala la elimu imefeli.

Hizi pesa wanazochezea kujenga madarasa nchi nzima.

Ni bora wangewekeza kujenga vyuo vya kati na VETA nchi nzima tupate kutengeneza ajira za vijana wetu.
mkuu hata hayo mazao ya VETA mbona hayajaleta impact kwny kupungua kwa wasio na ajira? Naongelea wahitimu wa VETA.

Leo ukizunguka kwny magereji, mafundi wake wengi hawakuhitimu wala hawapajui VETA.
wamejifunza locally kwny gereji za mtaani.

Mafundi cherehan wengi bado hawatokani na veta.

Shughuli za useremala, pia wafundi wetu wanaotuuzia samani sio mazao ya VETA.

Udereva ni hvyohvyo, ujenzi wa nyumba, kuchomelea ni hvyohvyo hadi ufundi simu!

Point yangu ni kwamba bado VETA haijafanikiwa kujipambanua vizuri zaidi ya kutoa vyeti..

Wahitimu wa VETA wamefocus kwny kuajiriwa zaidi kuliko kujiajiri..
 
Uko sahihi wengine ilibidi kubadili na hayo mafani na kuanza kusoma vitu vingine upya Kisha ama kuajiriwa au kujiajiri tofauti na fani uliyosomea VETA
 
mkuu hata hayo mazao ya VETA mbona hayajaleta impact kwny kupungua kwa wasio na ajira? Naongelea wahitimu wa VETA.

Leo ukizunguka kwny magereji, mafundi wake wengi hawakuhitimu wala hawapajui VETA.
wamejifunza locally kwny gereji za mtaani.

Mafundi cherehan wengi bado hawatokani na veta.

Shughuli za useremala, pia wafundi wetu wanaotuuzia samani sio mazao ya VETA.

Udereva ni hvyohvyo, ujenzi wa nyumba, kuchomelea ni hvyohvyo hadi ufundi simu!

Point yangu ni kwamba bado VETA haijafanikiwa kujipambanua vizuri zaidi ya kutoa vyeti..

Wahitimu wa VETA wamefocus kwny kuajiriwa zaidi kuliko kujiajiri..
Mkuu hapo ndipo chenga ya ujuzi inapoanzia serikali ipo haja ya kukaa chini na kuunda mfumo wa ujuzi ambao una soko mtaani .. ndio maana watu wanatumia fursa ya kujifunza mtaani ujuzi baada ya kuona alichosoma hakina tija kwa nafasi aliyonayo mtaani
 
mkuu hata hayo mazao ya VETA mbona hayajaleta impact kwny kupungua kwa wasio na ajira? Naongelea wahitimu wa VETA.

Leo ukizunguka kwny magereji, mafundi wake wengi hawakuhitimu wala hawapajui VETA.
wamejifunza locally kwny gereji za mtaani.

Mafundi cherehan wengi bado hawatokani na veta.

Shughuli za useremala, pia wafundi wetu wanaotuuzia samani sio mazao ya VETA.

Udereva ni hvyohvyo, ujenzi wa nyumba, kuchomelea ni hvyohvyo hadi ufundi simu!

Point yangu ni kwamba bado VETA haijafanikiwa kujipambanua vizuri zaidi ya kutoa vyeti..

Wahitimu wa VETA wamefocus kwny kuajiriwa zaidi kuliko kujiajiri..
Mkuu upo sahihi kabisa asilimia kubwa ya vijana wetu hawataki maelimu makubwa ya kuwa maprofesa watu wanataka ujuzi tu wakuweza kufanya shughuli zao
Mfumo wetu wa elimu upo nyuma watu wanaozalishwa kwa sasa wengi wana amini ajira ni serikalini lakini mtaani kuna fursa kibao na ndio tunataka wizara ilink na mtaan sio kutupa wasomi mtaani ina ikibidi wafike mbali kwa kuona vyeti vya kitaaluma viweze kuzalisha ujuzi na fursa mbalimbali kwa kuwazesha mikopo na kufungua njia mbalimbali na mataifa ya nje katika kazi za vitendo ..na ndio maana nasema huyu mama hatoshi yupo kimakaratasi zaidi kuliko dunia inavyokimbia kiteknolojia
 
Kumlaumu Mama yetu kama Yeye pekee anaeza badili mfumo wa elimu tunamuonea... Lugha tuu ya kufundishia ni kizungumkuti - hivi tusimlaumu MTU mmoja wakati elimu ni suala la wanazuoni/Watanzania wrote tujadili Kwa mapana... SOKO la ajira lina mambo Mengi - watu wa hbr (upashanaji hbr) wanahusika sana .. Na tusiidharau elimu yetu ni nzurii .. Ajira na vijana waende huko na huko kutafuta SOKO la kazi ..
 
Kiufupi serikai nzima kwenye suala la elimu imefeli.

Hizi pesa wanazochezea kujenga madarasa nchi nzima.

Ni bora wangewekeza kujenga vyuo vya kati na VETA nchi nzima tupate kutengeneza ajira za vijana wetu.
Mfumo wa elimu umeharibiwa tangu zamani labda ungesema akina Ndalichako wangeanza kuuboresha. Walivipuuza vyuo vya kati na kufanya kila Chuo kitoe degree, wakajza nchi na Vyuo vikuu bila kufahamu kuwa ajira nyingi ziko huku kati kwenye viwanda na ajira binafsi ama kujiajiri. Leo hii hata ufaulu wa kwenda Chuo Kikuu umeshushwa ili watoto wengi waende Chuo na kuchukua digrii wakati ajira za kuchukua wenye digrii ni chache sana na sana sana ziko serikalini. Wangerudisha utaratibu wa kuchukua cream ndio waende vyuo vikuu na wale wengine waende vyuo vya kati kwani hata hao wahitimu wa vyuo wa sasa na digrii zao hawaajiriki kwani uelewa wao uko chini sana, yaani wako kinadharia zaidi. Elimu badala ya kuwa mkombozi wa vijana imekuwa ni janga kwani walio wengi walipofanikiwa kwenda chuo walikuwa na matumaini yaliyopitiliza kwa kupata ajira au kazi nzuri. Turudi kwenye utaratibu wa zamani ufaulu wa kwenda form one upandishwe ili cream tu ndio iende fomu one na form five na hatimaye vyuo vikuu. Waliobaki wapelekwe kusomea ufundi, kilimo na fani zingine ngazi za chini na kati. Nchi wakati huu tunapoita wawekezaji kwenye viwanda ilitupasa tuwe tumewekeza kwenye skilled labour kama nchi za wenzetu mfano China. Hii pamoja na idadi kubwa ya labour force imeifanya China kuwa rafiki wa wawekezaji toka hata mataifa hasimu wao kama USA.
 
Mfano wa CHINA nimekupata sana ..wakazi wa china wanaviwanda mpaka majumbani uchumi wao umekua kwa kasi sana..
UJUZI wa kati ndio msingi wa uchumi na maendeleo kwa taifa letu yaan kuna gap kubwa sana hapa kati kati ndio maana wajanja wengi wanalitumia gap hili kujinufaisha na sio kuendeleza taifa..
 
Back
Top Bottom