Kwa wanaofahamu taratibu za upimaji wa ardhi / umiliki wa ardhi

Daud26

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,222
819
wasalaam, kama heading inavyojieleza ka yeyote anayefahamu hatua za upimaji wa adrhi na gharama zake. nimauliza hivi kwa sababu mimi nipo mbali na ofisi za ardhi halmashauri, hivyo kwa yeyote anayefahamu utaratibu naumba anisaidie. ahsanteni.
 
Upo mkoa gani kiongozi? Ukitaka ni PM nikupatie namba ya private surveyor makini sana atakaekufanikishia kazi yako.
 
Surveyor wengi si waaminifu,unaweza kuhitaji kazi kwa haraka wakaanza kukuzungusha kwaiyo tafadhari kama ukimpata kuwa muangalifu sana
 
Mhh mbona mi nimeanza kufuatilia nimeambiwa niende serekali za mtaa ,niende kata halafu kwa mkurugenzi ,then niende aridhi ,nimeambiwa nisije nikarubuniwa na wasanii wa mjini , Niko hatua ya mkurugenzi kwa sasa ili niende aridhi
 
wasalaam, kama heading inavyojieleza ka yeyote anayefahamu hatua za upimaji wa adrhi na gharama zake. nimauliza hivi kwa sababu mimi nipo mbali na ofisi za ardhi halmashauri, hivyo kwa yeyote anayefahamu utaratibu naumba anisaidie. ahsanteni.
1465570612361.jpg

Unaweza ukaipitia hiyo
Ila mimi mwemyewe ni surveyor
Karibu
GOLD LAND CONSULT CO LTD
tupo legho sinza
 
Hivi eneo (square area) la Tanzania walilipima kwa kutumia nini? Ni utaalamu gani unatumika?
 
HATUA ILI UWEZE KUPIMIWA KIWANJA AU SHAMBA LAKO (Ili uweze kupata hati miliki)

Ukaguzi wa eneo lako husika ili kujua eneo lako limepangwa kwa ajili ya matumizi gani, Hapa atashirikishwa mpima ardhi kwa ajili ya kufanya utambuzi wa eneo husika kujua lipo kwa ajili ya matumizi gani, Hivyo ni lazima afike site kwako na kifaa (Handheld GPS), Achukue vipimo kuzunguka eneo lako, Baada ya hapo akatafute taarifa za eneo lako halmashaur/ wizaran ili aweze kupata raman ya mipango miji.

Matokeo ya zoezi la ukaguzi wa eneo,
Eneo husika kukosa sifa za kupimika, eneo husika linaweza likakosa sifa za kupimika kwa eneo husika kutokua limeandaliwa matumizi kabisa (halina mchoro wa mipango miji), Eneo husika kuwa lipo katika matumizi ya maeneo ya kijamii mf makabuli, barabara, soko n.k

Eneo husika kuwa na sifa ya kupimika,
Eneo husika kuwa katika matumizi ambayo mtu binafsi anaweza kumili mf makazi, hotel, biashara n.k

Kibali cha upimaji,
Mteja au mmiliki halali wa eneo husika inabidi aandae barua kwa ajili ya kuomba kupimiwa eneo lake, Barua hiyo itapita serikali ya mtaa na halmashauri husika.

.Upimaji,
Hapa ni suala la kitaaluma zaidi ambapo mtaalama ataweka mipaka katika eneo lako kwa kutumia mawe (beacons), litaandaliwa file kwa ajili ya kwenda wizaran likiambatanishwa na ramani ya upimaji. Na mwishowe utarudishiwa ramani iliyo hakikiwa toka wizarani kama ramani ya upimaji.

Mteja utakabiziwa ramani ya upimaji,
ambayo utapaswa uende nayo kwenye halmashaur husika umuone afisa ardhi ili aweze kukuandalia hati miliki yako.

Gharama za upimaji zinatokana na ukubwa wa kazi yaan idad ya ekari na viwanja hivyo inaweza kuwa laki3, 5,6,7 ...hadi 2m itategemea na idad ya viwanja.

By Surveyor Aloyce
WhattsApp 0713778937
0754619189
0686087101
GOLD LAND CONSULT CO. LTD
Tunapatikana Sinza legho
 
Back
Top Bottom